
Hasheem Thabeet (pichani),mtanzania ambaye wengi wanamtarajia kuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi maarufu ya mpira wa kikapu nchini Marekani(NBA), ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji 21 walioteuliewa kuchezea Timu ya Taifa ya mpira wa kikapu nchini Tanzania kwa upande wa timu ya wanaume.Pia wanawake 20 wameteuliwa kuunda timu ya taifa kwa upande wa wanawake.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Tanzania(TBF),Lawrence Cheyo, timu hiyo ya wanaume itakuwa chini ya makocha Bahati Mgunda na Evarist Mapunda wakati ile ya wanawake itakuwa chini ya makocha Salehe Zonga na Pascal Nkuba.
Majina ya wachezaji walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni; Frank Kusiga, Ashraph Harun, Edward Robert, Paschal Nsana, Abdallah Ramadhan Dulla, Francis Mlelwa, Frank Augustino, Sudi Abdallah Razak, Mohamed Ally Dibo, Oswald Maboko,Amon Semberya, Kafashe Abdallah, Tarimo George, Juma Kissoky, Mgindi Mkumbo, Amiri Muhidini, Batungi Gilbert, Alphonse Kusekwa, Jije Makani, Hasheem Thabeet na Alex George.
Kwa upande wa wanawake walioteuliwa kuunda timu ya taifa ni; Annosiata Anthony, Agnes Simkonda, Jabu Shabani,Grace Daud, Grace Peter, Fraja Malaki, Evodia Kazinja, Elizabeth Masenyi, Naima Boli, Mary Meshack, Nipaeli Kessy, Amina Ahmed, Neema Emmanuel, Monica Aloyce, Zakia Kondo, Dajda Ahmed, Dolita Mbunda, Hadija Kalambo,Lucy Sangu na Lucy Augustino.
Timu hizo zipo chini ya udhamini wa kampuni ya Barrick Tanzania na zinatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyikia nchini Rwanda.