BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

koffi olomide atinga ofisi mpya za Clouds fm 88.4 leo June, 9, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 9:45 AM

1Mwanamuziki nyota kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Koffi Olomide ambaye pia ameteuliwa kuwa balozi wa Malaria ametua jijini Dar leo kwa ziara ya siku mbili chini ya shirika la Umoja wa Kimataifa linalohudumia Watoto la UNICEF,Koffi Olomide  kesho atafanya mkutano pamoja na kwenda kutembelea mji wa kihistoria wa Bagamoyo uliopo nje kidogo ya jiji la Dar,pamoja na ziara yake fupi pia alipata wasaa wa kuzitembelea ofisi mpya za redio ya Clouds Fm 88.4 ( Clouds Media Group) zilizopo Mikocheni,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.Pichani Koffi Olomide akizungumza na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bw.Joseph Kusaga leo jioni kwenye chumba kilichoandaliwa maalumu kwa ajili ya kukutana na wageni mbalimbali.