BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BONGO FLAVA NI CULTURE,HUWEZI KUIPOTEZA-AY June, 14, 2007

Filed under: Bongo Flava — bongocelebrity @ 6:48 PM

 

Ahadi ni deni. Kama BongoCelebrity ilivyoahidi hivi karibuni, majuzi tumefanya mahojiano na mwanamuziki mahiri wa muziki wa kizazi kipya AY au Mzee wa Commercial kama ambavyo anajulikana pia.

Jambo moja lililo wazi ni kwamba AY ni mwanamuziki ambaye kila kukicha anajaribu kutunga na kuimba nyimbo zenye ujumbe mahsusi. Iwe anaongelea ubinadamu, maisha, mapenzi au starehe msikilizaji atapata ujumbe kamili. Hivi karibuni wimbo wake ujulikanao kama Usijaribu ulimwezesha kushinda Tuzo ya muziki bora wa Hip Hop nchini Tanzania kutoka kwa Kili Tanzania Music Awards.

Wakati habari zake binafsi (alizaliwa wapi,akakulia wapi nk) zinapatikana katika tovuti yake, yafuatayo ni mahojiano tuliyofanya na AY; Pichani juu (kulia) ni AY akipokea tuzo ya Kili Music Awards kwa wimbo bora wa Hip Hop wa mwaka hivi karibuni.

BC:Turudishe nyuma kidogo… ulianza lini shughuli zako za muziki na je
unakumbuka siku ya kwanza kabisa ulivyopanda jukwaani kama mwanamuziki? Ilikuwa wapi na ilikuwa vipi?


AY:Ilikuwa poa sana,nilihisi nina jukumu kubwa mbele,ilikuwa Dodoma NK DISCO

BC: Kabla hujatoka kama solo artist tunakukumbuka kama mmojawapo ya
wanamuziki waliokuwa wakiunda kundi lililojulikana kama S.O.G kabla
hujatua East Coast Team. Unalo lolote la kusema kuhusu wenzako mliokuwa
nao S.O.G na pia East Coast Team?Je bado mnawasiliana mara kwa mara?


AY: Sisi tushakuwa ndugu, mambo mengine yanatokea ni kuangalia maisha jinsi
unavyoyatafuta. Kwa hiyo napenda kuwaambia siri ya mafanikio ni kujituma bila
kuchoka na kupenda kujifunza mazuri toka kwa wengine.

BC: Kipi unapendelea zaidi kati ya kucheza/kuimba/kupiga muziki moja kwa moja (live performance) na kurekodi muziki ndani ya studio?

AY:
Napenda yote tu kwa ujumla inategemea na vile upo wakati huo.

BC:Je huwa unamiss kuwa na wenzio wa zamani kama wale mliokuwa nao S.O.G?Kuna mategemeo au mipango yoyote ya kurudiana na kuunda tena S.O.G?

AY:
Tupo wote siku zote so mabadiliko hata kama nafanya kazi mwenyewe hakuna
mabadiliko

BC:Je unaye mwanamuziki au kundi lolote la muziki wa bongo flava ambaye
unamuona kama mshindani wako? Kama ndio ni nani au kina nani?

AY:
Sifanyi muziki kwa ushindani na wasanii ila nafanya ushindani na maendeleo
ya kila siku ya muziki.

BC: Unajisikiaje kuwa solo artist mpaka sasa? Nini faida na hasara zake?

AY: Najisikia poa sana,nafanya kazi kwa uhuru zaidi.Ukiwa solo si rahisi kuwa na
migongano kama utaweza kujicontrol

BC: Umaarufu na hela inasemekana huwa zinabadilisha sana watu. Je unasemaje kuhusu hilo?Unadhani vitu hivi viwili vimekubadili?

AY: Si umaarufu wala pesa au chochote kikubwa kinachonitokea katika maisha
yangu kitaweza kunibadili.Mara zote naona kama kitu kipo kipo tu.ndio
maana naishi na watu vizuri siku zote.

BC: Nini ugumu wa kuwa MC siku hizi ukilinganisha na zamani ulipoanza?

AY
: Kila siku kuna ugumu kwa hiyo mimi naona ni jambo la kawaida katika biashara.

BC: Hivi karibuni kumekuwa na mazungumzo mengi sana kuhusu muziki wa kizazi kipya. Wengi wanasema muziki huu utapita kama zilivyopita aina zingine za muziki. Pia kuna lile suala zima kwamba nyimbo za bongo flava zinatamba kwa muda mfupi sana. Unadhani ni kwanini na nini maoni yako kwa ujumla kuhusiana na muziki wa kizazi kipya au bongo flava?

AY
: Bongo Flava ni culture na huwezi kuipoteza culture ila watu ndio watapotea
na kuibuka wengine. Kwa hiyo maoni yangu ni kuwa watu wasikurupuke kutoa nyimbo na wawe makini katika kuandika nyimbo zao.Pia studio zisiangalie sana pesa
waangalie zaidi vipaji vikali.

BC: Wewe ni mwanamuziki ambaye umeshirikiana na wanamuziki kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda kuliko mwingine yeyote.Umejifunza nini katika kushirikiana na wanamuziki kutoka Kenya na Uganda? Je ni kweli kwamba wenzetu wapo mbele kutushinda?

AY: Nimejifunza kuwa si kipaji pekee kitafanya muziki wako upendwe katika
jamii na wasanii wenzako ila pia jinsi ya kuishi na watu kiujumla. Kimauzo
ya album Tanzania inaongoza ingawa bado hatupati kile kinachohitajika kupatikana. Kimalipo ya shows kwa wasanii wakubwa uganda wanaongoza,wanalipwa poa sana.

BC:Kimataifa ni mwanamuziki au wanamuziki gani ungependa kushirikiana nao kisanii katika siku za mbeleni?

AY:
Akon,Dr.Dre na Timberland.

BC: Hivi karibuni kulikuwa na habari kwamba Akon alisema kwamba angependa sana kufanya kazi na wewe. Kuna ukweli wowote katika hilo na kama ndio, ukweli ni upi?

AY:
Ukweli upo.Mwaka jana nilishasign contract naye na kumpa ruhusa yeye
apromote video yangu ya Mademu Watafutaji na kama wiki moja sasa amerudia
tena kunitaja akiwa South Africa katika MTV Base katika kipindi cha
Worlwide Thing.Nimeomba copy ya kipindi hicho tola MTV Base na wakinitumia
nitaiweka katika website yangu. Akon ni binadamu kama binadamu wengine
anaweza kupenda muziki wa msanii wa tz hata kuliko msanii wa Senegal nchi
alikotokea hivyo kwa upande wangu nilijisikia faraja na furaha kubwa.

BC: Ni mtu gani ambaye ulishafanya kazi naye ambaye alikuvutia sana na
hutomsahau?

AY:
Wote niliowahi kufanya nao kazi.

BC:Mashabiki wako wangependa kujua lini wategemee albamu mpya kutoka kwako?

AY
: Nitawajulisha lakini mambo makubwa yanakuja.

BC: Tutarajie nini kipya au tofauti katika albamu yako ijayo baada ya
ya kuwa kimya kidogo?

AY:
Watu watarajie kiwango kingine kikubwa, collabo za kufa mtu.

BC: Huwa unasikiliza miziki ya aina gani kama achilia mbali ya kwako
mwenyewe? Ni mwanamuziki gani katika albamu ipi unayemsikiliza hivi sasa? Na je unasikiliza pia miziki aina nyingine au wewe ni rap/hip hop tu?

AY
: Nasikiliza sana za wasanii wenzangu wakubwa kwa wadogo. Hiyo inanisaidia pia
kufanya kazi zangu vizuri. Nawasikiliza pia wanamuziki kama Dr.Dre Chronic
2001,Sade,Morgan Heritage,Abba,Black Eyed Peas na wengine wengi.Mara
nyingi nasilikiza pia Latino Music,Kwaito na Sweety Reggae.

BC: Nini matarajio yako katika miaka mitano ijayo?

AY
: Kufanya biashara kubwa zaidi.

BC:Mwisho kabisa mashabiki wako wa kike wanataka kujua kama umeoa au
tayari una mtu? Kama bado je wanaweza kukutafuta? Na je unapochagua
mchumba au mwanamke unaangalia vigezo gani au kama tayari unaye wako huwa unatoa ushauri gani kwa marafiki zako wanaotafuta?

AY: Niko single kwa kipindi hiki na itachukua muda kupata mwingine ambae tutaendana kimapenzi na kirafiki pia.Wasinitafute atakuja tu mwenyewe automatically. Napenda msichana ambaye si mwingi wa habari pia tutakayeeelewana katika mambo mengi.

Kwa mshkaji wangu, kwa rafiki zangu sipendi kuwalimit kila mmoja anauhuru
wake.

BC: Asante AY na kila la kheri katika kazi zako.

AY: Pamoja sana man!

Advertisements
 

16 Responses to “BONGO FLAVA NI CULTURE,HUWEZI KUIPOTEZA-AY”

 1. Tunu Says:

  Good interview lakini nasikia huyu jamaa naye kajiengua kutoka ECT.Mkifanya naye tena mahojiano muulizeni tafadhali,chanzo nini?Beef?

 2. Majid. Says:

  AY nakuzimia ile mbaya, Nimefurahi kusoma interview yako. Kazi nzuri sana Bongo celebrity endeleeni hivyo hivyo.

 3. phina Says:

  ay ni mwanamziki mzuri sana napenda hana maringo ,n gud company kwa kweli olwaiz tukiwa nae tunamuombea kwa mungu akaze buti tu,gud interview kaka kuwa na moyo huo huo ,one luv

 4. msangimdogo Says:

  Nimepita hapa kuwasalimu na kuwapongeza kwa kuanzisha blogi hii. Kazi nzuri na nawatakia kila lakheri katika safari yenu ya kuelimisha jamii

 5. sophy Says:

  good interview,keep it up,thumb up!

 6. ukende Says:

  hey ay,enterview ni nzuri nime admire lifestyle yako.i like the way ur open and confident. keep it up boy.

 7. Dinah Says:

  Bongo sasa inawasanii wenye vipaji, navutiwa na wasanii wengi na AY anachukua # one. Kijana kazi nzuri, BC mnawakilisha vema kabisa.

 8. ANNA ULOMI Says:

  YAP!GUD INTERVIEW.I LIKE HIS WORK IS NICE.HE IS ALSO CONFIDENCE I LIKE THAT.KEEP IT UP.GOD BLESS U AND ALL THE BEST.BRAVO!

 9. Reg Miserere Says:

  BC Mzee kingunge yuko wapi?

 10. norasco c.nyimbo Says:

  AY NAKUKUBALI MTU WANGU.KWNZA UMETULIA KATIKA KUCHANA MISTARI.UJE IRINGA HAPA MKWAWA UNIVERSITY UFANYE MAMBO.BIG UP 2U MAN.

 11. lightness Says:

  Kazi zuri kaka.
  keep it up

 12. amanda Says:

  he is lying about being single si anamchukua dada yetu amanihuyoooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!

 13. samwel mdalingwa Says:

  BIG UP BROTHER !! YOUR music is so thrilling so keep up the same spirit!!1
  it’s me SAM frm tegeta mbweni masaiti.

 14. bonitha Says:

  hoya nakufagilia kichizi mtu wangu hasa nyimbo yenu ya habari ndo hiyo.

 15. abdul Says:

  HOYA MAZEE NASIKIA HARUFU YA ANKRA KWENYE TRACK HIIYA AMIBII. AU SIO MTU WANGU NAKUFAGILIA SANA ILE KINOMA YAANI ILE KICULTURE EEBWANA [AY]NAKUFILISANA ULIVYO PANDA CHATI NI NOMA.

 16. GLORY MTUI Says:

  nakupend sana AY kwakweli unatisha sna


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s