BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DAR-ES-SALAAM! June, 17, 2007

Filed under: Muziki — bongocelebrity @ 6:18 PM

 

Kama wewe ni mpenzi wa muziki wenye midundo ya reggae au michanganyiko ya reggae na aina zingine za muziki kama zouk,african jazz nk uwezekano ni mkubwa sana kwamba umeshawahi kumsikia au kumuona jukwaani Ras Nas au kwa jina lingine Nasibu Mwanukuzi. Ras Nas ni mtanzania anayefanya kazi zake za muziki nchini Norway ndani ya jiji maarufu la Oslo.

Jambo moja ambalo pengine wapenzi na mashabiki wake hawajui ni kwamba Ras Nas ni mwanasheria kitaaluma. Alisomea sheria katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam. Pia ni mtunzi na mghani mzuri wa mashairi.

Kwa wapenzi wa muziki wa reggae hususani Kaskazini mwa Ulaya, ukitaja jina la Ras Nas hawatokuuliza maswali mengi. Muziki wake unaongea, mashairi yake yanazungumza lugha inayoeleweka.

CV yake inaonyesha kwamba ameshiriki msururu wa matamasha kama vile Norwegian Wood – Oslo,Bergen International Music Festival – Bergen,Verden i Norden – Oslo,Oslo Mela Festival – Oslo,Zanzibar International Film Festival – Stone Town, Zanzibar, Festival of Performing Arts and Music – Lahore, Pakistan,Radio concert – Norwegian Broadcasting Corporation NRK P2 na mengineyo.

Mwaka huu anatarajiwa pia kushiriki tamasha maarufu la Oslo Mela Festival jijini Oslo. Lakini kabla ya kulipanda jukwaa mwaka huu Ras Nas atakuwa ameshatoa albamu mpya ambayo ameipa jina la Dar-es-salaam hivyo kuendelea kuwa “balozi” wetu mzuri huko Ulaya Kaskazini. Kama hujawahi kuzisikiliza baadhi ya nyimbo za Ras Nas basi unaweza kuanza sasa kwa kubonyeza hizo links hapo chini. Ukitaka kuona anapokuwa jukwaani anakuwa mtu wa aina gani bonyeza hapa.Ukitembelea tovuti yake utajifunza mambo kadhaa.

Sweet Rhythms

Guantanamo

River Nile

Kwanini aliamua kuachana na taaluma yake ya sheria na kujikita zaidi kwenye muziki? Nini kipya katika albamu yake mpya? Ana mipango ya kurejea Tanzania na kuendeleza kazi ya muziki? Ameshirikiana na wasanii gani kutoka Tanzania katika albamu yake hii? Hayo na mengineyo yatakujieni hivi karibuni BongoCelebrity itakapofanya mahojiano rasmi na Ras Nas.Stay tuned.

Advertisements
 

4 Responses to “DAR-ES-SALAAM!”

 1. Ras Kenku Says:

  Raha sana kuona jinsi wabongo wanavyorepresent,Big Up Ras Nas,muziki wako nimeukubali.

 2. Kiki. Says:

  Jamani watanzania tunajitahidi. Sasa huyu jamaa ni lawyer na anafanya mambo ya muziki. hii inaonyesha umuhimu wa muziki. nasubiri sana interview ya huyu jamaa. Naomba mmuulize anaona vipi kuhusu bongo flavour?? na anaweza vipi kuwasaidia vijana wa nyumbani waweze kujitangaza na kuja huko?? Na anauonaje muziki wa nyumbani ufanyaje ili uweze kupokelewa sana na watu wa majuu.

 3. Ilmolelian Says:

  Ras Nas kweli umenigusa sana na reggae yako ‘Guatanamo’ kwani kama unaweza kuwaona waandaaji wa London Carnival hapa London The United kingdom of Great Btitain unaweza kuongeaza kufahamika kwa muziki wako wa roots reggae hapa London. London carnival hufanyika kila msimu wa summer kuutukuza utamaduni, mila, desturi na sanaa na muziki hususan wa reggae na na mingine toka carribean(soca-rumba).
  kwa mara nyingine hongera sana kwa muziki wako wenye ujumbe mzito na bora.

 4. Ras Nas Says:

  Aisee Ilmolelian ahsante sana kwa uchambuzi wako!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s