BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

K-LYINN: UREMBO SIO SURA NA MAUMBILE TU June, 24, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki,Urembo — bongocelebrity @ 12:06 PM

Jina lake halisi ni Jacqueline Ntuyabaliwe, nyota yake ni Sagittarius (Mshale). Wengi bado tunamkumbuka kama mrembo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2000 na kisha kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya mrembo wa dunia (Miss World) yaliyofanyikia nchini Uingereza na Visiwa vya Maldives.

 

Tofauti na mawazo ya wengi, kama anavyobainisha katika mahojiano tuliyofanya naye hivi karibuni, alianzia kwenye muziki kisha akaja kwenye urembo na baadaye akaamua kurejea katika muziki mahali ambapo ndipo alipo hivi sasa. Mwezi ujao anatarajia kufyatua albamu yake ya pili itakayokwenda kwa jina la K-Lyinn- Crazy Over You.

Ametoka wapi, nini mtazamo wake kuhusu muziki na urembo, wapenzi wa muziki na mashabiki wake watarajie nini katika albamu yake mpya, nini siri ya urembo wake na anatoa ushauri gani kwa wasichana? Hayo yote na mengineyo ameyaweka bayana katika mahojiano yafuatayo;

BC: Unaweza kuwaambia mashabiki wako kuhusu maisha yako ya utotoni? Unakumbuka nini kuhusu utoto wako?

K-LYINN: Utotoni nakumbuka jinsi nilivyokuwa nacheza na baba akirudi kutoka kazini na mara nyingi alikuwa akinipeleka kutembea jioni.Pia nakumbuka nilivyokuwa nikienda kanisani na mama.Nilikuwa napenda sana kusomewa hadithi za vitabu.

BC: Historia ya maisha yako, kama ilivyoandikwa kwenye tovuti yako, inaonyesha kwamba baada ya shule ulianza shughuli za muziki kwa kuwa mwimbaji wa Tanzanite Band. Baada ya hapo ukaingia kwenye masuala ya ulimbwende ambapo ulifanikiwa kushinda taji la Miss Tanzania mwaka 2000 na kisha baadaye ukarejea kwenye muziki tena. Nini kilivutia kwanza kuingia kwenye muziki na kisha masuala ya ulimbwende?


K-LYINN:
Tokea nilipokuwa na miaka sita au saba nakumbuka nilikuwa napenda sana kuiga na kuimba nyimbo za wanamuziki wa ulaya kama Madonna na Mariah Carey,kwahiyo nilipopata nafasi ya kujiunga na bendi ya Tanzanites kwangu ilikuwa kama njia ya kutimiza ndoto yangu.Kuhusu urembo nakumbuka kuna wakati nilikuwa natamani nipate nafasi ya kuvikwa taji na kuwakilisha nchi yangu lakini sana sana niliamua kushiriki baada ya kukutana na watu mbalimbali ambao walinishawishi nishiriki na kunipa moyo kuwa nina nafasi ya kushinda.

BC: Nini siri ya urembo wako?

K-LYINN: Kwanza kabisa mimi binafsi napenda sana kujipatia muda mrefu wa kupumzisha akili na viungo kila siku na kupata usingizi wa kutosha na ninaamini hiyo ni siri mojawapo ya urembo.Pia huwa nakunywa maji mengi na kula matunda na mboga katika mlo wa kila siku.Nikipata muda huwa nafanya mazoezi.

BC: Miaka zaidi ya sita sasa imepita tangu ulipovishwa taji la Miss Tanzania. Unaweza kutukumbusha kidogo ulijisikiaje siku hiyo?

K-LYINN: Kwanza nilitangazwa kuwa mshindi nakumbuka kuwa nilishikwa na butwaa na ilichukuwa muda kuamini ni mimi niliyeshinda na baada ya kuamini nilijisikia furaha isiyo na kifani.

BC: Mafanikio uliyoyafikia kwenye masuala ya urembo ni ndoto ya wasichana wengi sana.Je pamoja na muziki bado unajishughulisha na masuala ya urembo? Kama ndio kwa jinsi gani na kama hapana, kwanini umeacha?

K-LYINN: Kwa sasa huwa sijishirikishi sana na masuala ya urembo kwanza kwasababu kazi ya muziki inachukua muda wangu mwingi,lakini pia ni kwasababu bado hatuna kazi nyingi sana hapa kwetu zinazohusu urembo.

BC: Unaye mtu yeyote ambaye unamuona kama role model wako? Kwanini?

K-LYINN: Baba yangu ni role model wangu,ni mtu mkarimu na yeye ni daktari na amejitolea maisha yake kusaidia watu.Pia naamini ni baba mzuri sana kwasababu bahati mbaya mama yangu alifariki miaka kumi na mbili iliyopita na baba alinilea vizuri mpaka nimefikia hapa nilipo.Yeye huwa tayari kunisikiliza muda ninapohitaji kuongea nae na huniunga mkono na kunipa ushauri katika maisha yangu.

BC: Sasa naomba tuongelee albamu yako mpya unayotarajia kuitoa hivi karibuni.

Kwanini umeamua kuiita albamu hii K-LYNN?

K-LYINN: Album yangu inaitwa K-LYINN CRAZY OVER YOU,Nimeamua kuuita hivyo kwasababu napenda watu walifahamu na kulizoea jina langu na Crazy Over You ni jina la single itakayokuwepo katika album yangu.

BC: Je unatunga mashairi ya nyimbo zako zote wewe mwenyewe?

K-LYINN: Ndio,mashairi yote utakayosikia katika album yangu nimetunga mwenyewe.

BC: Watu wengi wangependa kufahamu, inakuchukua muda gani kutengeneza albamu nzima kama hii yako?

K-LYINN: Muda wa kutengeneza album huwa unatofautiana,lakini album hii imenichukuwa mwaka mmoja kuikamilisha.

BC: Itakuwa na nyimbo ngapi kwa ujumla na imerekodiwa katika studio gani?

K-LYINN: Album itakuwa na nyimbo kumi,nimefanya kazi na producers tofauti kama Said Comorian,Mwaks,Dunga na Roy.

BC: Katika albamu hii mpya utakayoitoa hivi karibuni umewashirikisha wasanii gani?

K-LYINN: Album hii nimemshirikisha Mr.Blu,Sweeza,na Noora.

BC: Wapenzi wa muziki wategemee nini kipya katika albamu hii?

K-LYINN: Wapenzi wategemee ujumbe utakaowagusa na mziki utakaowafanya waamke na kucheza.Album hii niliitengeneza kwa ajili ya mashabiki wangu.

BC: Nyimbo zako nyingi katika albamu iliyopita zilikuwa zinahusu masuala ya mapenzi. Wengi tungependa kujua, kwanini unapenda zaidi kuimba nyimbo za mapenzi? Hadithi zilizoko kwenye mashairi yako zinatokana na uzoefu wako binafsi?


K-LYINN:
Napenda kuimba nyimbo tofauti tofauti na lakini kwa sasa naamini nyimbo za mapenzi zinagusa rika tofauti na kuna mambo mengi ya kuimba katika masuala ya mapenzi na zina wapenzi wengi sana,pia katika album hii mpya kuna nyimbo isiyo ya mapenzi.Hadithi zilizoko katika nyimbo zangu zinatokana na hadithi zinazotokea katika maisha ya watu tofauti sio hadithi zangu binafsi.


BC: Mara nyingi wasanii wa muziki huwa wanakuwa na malengo maalumu katika miziki wanayotunga, kuiimba na hata kucheza. Kwa miaka mingi makundi mawili makubwa yamekuwa ni wale wanaofanya muziki kwa ajili ya kuelimisha na wanaofanya kwa ajili ya kuburudisha. Muziki wako upo zaidi katika kundi gani kati ya haya?

K-LYINN: Nafanya muziki kwa ajili ya kuburudisha na kuelimisha kwa ujumla.

BC: Nini maoni yako kuhusu muziki wa kizazi kipya ambapo katika siku za hivi karibuni umekuwa ukizungumziwa kama muziki utakaopita haraka kutokana na kukosa ujumbe wa maana?

K-LYINN: Mimi naamini mziki wa bongo flavour unaweza kufananishwa na mziki wa R&B na mziki usioweza kupita kwani aina ya mziki huu hubadilika kutokana na wakati,si kweli kwamba mziki huu hauna ujumbe kwasababu ziko nyimbo nyingi sana ambazo zina mashairi yenye ujumbe wa maana ila labda mwelekeo wa sasa asilimia kubwa ni nyimbo za mapenzi kwasababu inaonekana kuwa zina wapenzi wengi lakini msanii mwenye kipaji anaweza kubadilika na kutunga mashairi yenye maudhui tofauti inapohitajika.

BC: Ukiacha wewe mwenyewe, ni msanii au wasanii gani duniani wanaokuvutia sana na ambao ungependa kufanya nao kazi siku za mbeleni?


K-LYINN:
Namzimia sana Beyonce na Mary J Blige,kwa wasanii wa kiume ningependa

kufanya kazi na Usher Raymond,Neyo,Basta Rymes na Jay Z.

BC: Mbali ya Tanzania umewahi kufanya perfomances katika nchi gani zingine? Huwa unajisikiaje kuperfom nje ya Tanzania?

K-LYINN: Nimeshawahi kufanya performances nje na bendi,na kwa ajili ya kuitangaza album yangu ninapanga kufanya tour katika baadhi ya nchi za Africa na UK na US pamoja na baadhi ya nchi za Europe.Ratiba za shows zitapatikana katika website yangu www.klyinn.com

BC: Unatoa ushauri gani kwa wasichana wadogo wanaotaka aidha kuingia kwenye mambo ya urembo au muziki? Nini tofauti kati ya fani ya muziki na urembo?

K-LYINN: Wasichana wanaopenda kuingia katika masuala ya urembo nawaambia kuwa kwanza wasome na wasubiri kufikia umri unaotakiwa,urembo sio sura na maumbile tu bali pia ni ufahamu na mambo mengi mengine huwa yanayotakiwa.Na ili kufanya muziki ni muhimu kuwa na kipaji asilia na kama wanaweza kusomea fani hiyo wataweza kufanikiwa zaidi kwani muziki ni kama biashara ambayo kama unaifanya vizuri unaweza kuitumia kuendesha maisha.

BC: Kwa wapenzi wa muziki ambao wangependa kununua albamu yako unawaambia nini? Nani msambazaji wako na itapatikana katika maduka gani?

K-LYINN: Wapenzi wa muziki wangu watakaopenda kununua album yangu napanda kuwaambia kuwa album yangu ikishatoka watapata taarifa za mahali au maduka zitakapokuwa zikiuzwa katika matangazo na vile vile katika website yangu WWW.KLYINN.COM.

BC: Asante K-Lyinn kwa mahojiano haya na kila la kheri.

K-LYINN: Asanteni pia. 

Advertisements
 

49 Responses to “K-LYINN: UREMBO SIO SURA NA MAUMBILE TU”

 1. Tito Says:

  Dada Kylinn interview yako nzuri, lakni ningependa kukupa advice; Punguza maringo, jifunze kucheza katika video zako, tafuta walimu wa kukufundisha kucheza. Mengine jitahidi ila nasisistiza acha kuringa.

 2. Harry Says:

  Kwani mtu akiandika mwaka inakua tabu…dec 6th …..?????Watanzania tuache hizo…be proud of your age…

 3. siah Says:

  Mmh it look like u have good vision in your work Okey then work hard we are hehind you but please PUNGUZA MARINGO Coz yanatuboa mashabiki wako n try to dance in your videos plzzzzzzzzzzz,Ur good but Maringo sana so PUNGUZAAAAAAAAAAAAA.

 4. rosemary Says:

  klyinn hongera tunaisubiri album yako kwa hamu sana

 5. florence Says:

  you seem to be a strong,smart and you know your goals.keep it up,nice interview

 6. sam Says:

  Keep ur head up sis and do yo thing,maisha huwezi kukosa wapinzani lakini pata faraja kwa kujua kuwa wapo wengi wanaokutakia mema.gdluck

 7. Yvonne Says:

  It is really encouraging to see that now Tanzanian Beauty Contestants and singers are going out there, are being noticed all over the world.

  K-Lyinn, just do your thing sister…you are doing great. And if your style of music is NOT TO DANCE, so be it….and if you can incorporate a little dancing in your videos, then that’s even better.

  The important thign that you must remember is to always do something to improve yourself as a person, your music and your image. Try new things, new techniques BUT it should be something that you are confortable to do.

  Looking forwards to your new album. All the best.

 8. may Says:

  huyu dame nadhani kucheza hajui kabisa !hata disco huwa tunamuona amtafute choreographer mzuri hata kama kulipia ni kma anavyoenda gym anashindwa nini??pale fitzone centre na kwengine kibao wanafundisha dancing tena apate wa belly dancing
  kiuno kigumu sana mama huyu.cute face,gud dressing but poooooooooor dancing.hatuko kwa kina lundenga hapa alaaaaaaaaaaah

 9. Kusiti Says:

  Lady K-lynn!
  Mind the least about those who are trying to push you back. i personally like you styles. Dancing is not the only thing that makes a music beatiful! kwani mabinti wangapi wanakata mauno sanaaaaa kwenye video zao yet video yao inakuwa haina mvuto??? wasikuzingue wala nini. Sie wengine tukikuangalia na slow movement zako tuna-enjoy kichiz kuliko ungeanza kujiviringisha hovyohovyo!

  Big up lady.

 10. jitu Says:

  well,klyin is a good singer n composer,i appreciate her although at first i thought that he couldnt did well,incase of dancing,this does not matter,the important thing is that,her songs are very impressive.the voice its so nice.keep it up!!!!!!!!
  incase of biograph,its not a secret klyn u are so PROUD!!!!!!!!how much it COST u to express ur birth year,u are a role model that we are copying from u,so when u hide ur information it means u cheat the whole society that looks upon u,acha maringo bibie,hatuendi hivyo,na hata ukitangaza hiyo miaka yako haina maana kuwa TUTATANGAZA NDOA,ni hayo tu.

 11. Africanbro Says:

  Nyie watu hebu acheni hizo…acheze acheze acheze NINI…the biggest singers Whitney Houston, Mariah Carey, Christina Aguilera na Celine Dion…wanacheza wapi…they move a lil and thats it….Kwahiyo pozeni ball. K-Lynn girl no one owes you nothing other than a song. So do u..baby! anayeona unaringa akajiue…ang why shouldnt u? PEACE!!!

 12. B Says:

  Hongera kwa kujituma na kufanya kazi nzuri ambazo hupendwa na wengi.Usife moyo endelea na moyo huohuo

 13. Rehema Says:

  JALI MAISHA YAKO USIJALI WATAKAVYO WAO UNAONEKANA MREMBO SANA UNACHEZA VIZURI SI MPAKA UKATE VOUNO NDIO UONEKANE UNAJUA KUCHEZA .ANAYESEMA UNALINGA ANA LAKE JAMBO SI WATU WOTE WATAKUPENDA . USIFI MOYO ENDELEA NA MOYO HUOHUO

 14. manorizo Says:

  ah!! not so good!!! just go 2 my web…….

 15. Meg Says:

  Keep it up girl !!!!!!!!! congrats.
  Remember it is very very hard to satisfy people’s desire.

 16. Alex Kikoti Says:

  Kazi zako nazuhudu. Keep up mama.

 17. Mkenya Says:

  I just happened to stumble on the crazy over you video and wow !!! Good song, good lyrics and a knockout babe !! Nice work Klyinn.

 18. Jacqueline Says:

  Hi babe,Thats gud and nice of ya.the music is just a blast and never mind on what these idiots says.U’r looks,lyrics,the voice and that lovely shape.All is just incredible.
  Keep it up luv be strong and courageous.Am very impressed with ur slow moves and am sure thats not a band / show ure doing and i really dont expect u to do that.

  Keep it up and be blessed.

  Am your fun and will always be

 19. chesi Says:

  The girl is good, dancing or not. you dont have wriggle your bottom to be a good singer………

 20. Zahra Says:

  Hello K-Lyn big up sister! Napenda nyimbo zako nakupenda wewe mwenyewe pia, unaimba vizuri unacheza vizuri kifupi unanifurahisha, napenda sana nyimbo yako ile ya “penzi utapata ukimwacha” ni nyimbo nzuri na inanigusa kila nikiiona pia shooting yake imetulia, hongera baby unajitahidi!!!

 21. TINA Says:

  We nimrembo wakupendeza sana dia mungu akusaidie katika kazi yako yamuziki pia take care majaribu yapo kila mahali muombe mungu sana akuepushe na mambo yaulimwengu huu.

 22. miss pauline joseph Says:

  hey girl ni wimbo wako mmoja tu wa crazy over u ndo nilioupenda so unatakiwa ujitahidi sana kutukosha wapenzi wa muziki ili tukupende as dayz pass.so kaza buti mama ninaimani tutakupenda zaidi.ushauri wangu ni kwamba punguza make ups kama wewe ni mzuri ni mzuri tu wewe huoni kama siku hizi unazeeka…….why girl….

 23. tatu Says:

  KLNNY WENYE CHUKI NA WEWE WAAMBIE WAMEZE NYEMBE WAFILIE MBALI.
  KWA MIE NAKUPENDA SANA KATIKA WANAMUZIKI WANAWAKE WATZ NAWEZA SEMA UPANDE WA MAVAZI UNAFUNIKA VIBAYA TENA WEWE NI MATAWI YA JUU.

  1. UNAJUA KUPANGILIA MAVAZI
  2. UJACHUSHA TOKEA UWE MISS TZ HADI LEO UKO BOMBA.
  3. SAUTI PIA UNAYO.
  4. UNAJUA MIKAPU IPI NI YA MCHANA NA IPI NI YA USIKU.
  5. UNYWELE SASA UTAFIKIRI UMEZALIWA NAO.

  MIE NAKUOSHEA SANA M2 WANGU NAPENDA SANA NYIMBO ZAKO HASA WIMBO WA NIKIPATA WANGU DUH UNANIMALIZA KABISAAA.

  HUYO ANAYESEMA KWAMBA HAUCHEZI TENA NI MNAFIKI TATIZO LA WABONGO TUMEZOEA KUONA MWANAMZIKI AKIKATA 2 MAUNO BASI NDIO TUNAONA ANACHEZA? KILA M2 NA STAIL YAKE BANA
  MBONA WA2 KIBAO WANAKATA MIUNO LAKINI KWENYE KUIMBA BILA.

  WENYE WIVU WAJINYONGE.

  HONGERA SASAAAAAAAAAAAAAAA

  TATU KITENGE

 24. lili Says:

  well sheis good tena very good i thnk i like all of her songs keep it up girl…

 25. babyface Says:

  Hellow Lily keep it up my dear yani uko juu vbaya sana unajitahidi mimi nakupa hongera wala usiwasikilize hao wanaotaka ukatike ama ucheze kama kichaa kama wamezoeshwa viuno na RC basi wamfute hata nyumbani kwake akawakatikie wajinga wakubwa hao,watanzania bwana hivi hawajawaona biggest singers kama mariah carey,celine dion,tony braxton,whitney houston na wengine wengi maarufu wanacheza taratibu just slow motion hisia kali hivyo ndio vitu vinavyotakiwa bwana acha kuwasikiliza hao washamba na malimbukeni waliozoea viuno

 26. scope Says:

  jaq wewe ni matawi ya juu,HAURINGI ILA WANAOKIUONA WANABABAIKA WENYEWE NA KUDHANI UNA RINGA.KAZA BUTI MAMA.ILA BOY FRIEND WAKO ANAFAIDI!!!!!!

 27. pakamafia Says:

  MTU ANIFAHAMISHE NINI MAANA YA KUPIGA UK NA EUROPE,DADA HUYU HAPO KUNA DALASA.?????KASEMA ANAPENDA KUPIGA UK NA EUROPE.DOMM.

 28. Mama wa Kichagga Says:

  Jack,

  Hongera sana! Endelea kufanya vitu vyako. Wapende sana maadui zako na waombee Mungu waishi maishi marefu ili unapozidi kufanikiwa wajionee kwa macho. Kwa wale wanaokuponda wajiulize mara mbili mbili wao wamefanya nini kwenye jamii hata kikaonekana? Tuache tabia mbaya ya kukwazana. Siku zote tutiane moyo ndipo tutapata maendeleo. Jamani watanzania tuamke. Kiuno kipo ndani sio kwenye majukwa! Lini hongera sana mdogo wangu. Nakutakia kheri uwe juu kila siku zinavyosogea. Kama kiuno ni mali basi Wachagga tungekoma, ila ndoa zetu ziko juu na imara tena bila kiuno. Big up Dear.

 29. SAMIBOY Says:

  Gal you look good..Keep it up girl !!!! always target your goals and not what people say
  Remember it is very hard to satisfy people’s desire.

 30. mweusi Says:

  nina furahi sana kusikia maendeleo mazuri ya dada huyu,lakini vile vile ningeomba watu kama yeye wasiache kabisa kujishughulisha na mambo ya urembo kwa sababu angalau wao wana upeo na masula haya

  wawe wana rekebisha makosa yanayo fanywa na kamati ya miss tanzania kwa kutoa maoni yao na si kukaa kimya.

  ndugu wananchi msije mkashangaa siku moja kamati ya miss tanzania ikamchagua mchina kutuwakilisha kwenye miss world.

 31. mweusi Says:

  nina furahi sana kusikia maendeleo mazuri kuhusu dada huyu.

  lakini warembo kama hawo ambao wanaupeo wakutosha kuhusu masuala ya urembo ningeomba wasijitoe kabisa kwenye masuala hayo.

  wawewanatoa maoni yao kuhusiana na makosa yanayo fanywa na kamati ya miss tanzania na si kukaa kimya.

  ndugu wananchi msije mkashangaa siku moja kamati hiyo ya lundenga ikamchagua mchina kutuwakilisha kwenye miss world.

 32. Reg Miserere Says:

  Mtu hazuiwi kutoa maoni yake, …lakini kumsemea mtu sivyo ndivyo hiyo siyo.

  We Tito/ siah;

  Kulikoni? Ni maringo gani mnaongelea? kukata kiwil wili???

 33. U mrembo,
  mbona watu wanalalamika sana kwamba unamaringo?
  nashindwa kuelewa wanakutafsiri au wanakuelewa vizuri?
  sometimes wa2 huchanganya maringo na upole!
  Mimi siwezi kusema lolote japo pia uliwahikuniudhi siku moja nilipokusikia kwa masiko yangu ukitamka kuwa nyimbo za msanii mwenzio Ben Kinyaiya zinakuboa na hajui mziki. Ulisahau hata wewe ni moja kati yao (wasiojua) Hivi unachokiimba wewe na wenzio baadhi kitazame, kipindue, ukigeuze alafu niambie kama umeona kinaalama yoyote inayoonyesha kama huyu ni msanii kutoka Tanzania?!
  Poleni sana mziki sio kupiga makelele!
  kmobango@yahoo.com

 34. Mama wa Kichagga Says:

  Kasambula,

  Kama ulimsikia ulimuuliza? Na kama ulimuuliza na kumalizana sidhani kama HAPA ni mahali pake! Waonekana kuwa na chuki, kiburi na mkosanishi wa watu wewe? Ningekufahamu unakoishi ningekuzukia huko huko tupeane ushauri wa namna ya kuishi na binadamu. Hivi unafahamu kumsemea mwenzio vibaya namna hii ni zambi? Usisahau kuitubu maana hii unayo ndugu tena iko hapo kifuani na usoni!

  Wee mkubali tu Jack hata kama hutaki maana kama kakutangulia hata hatua moja inaletaga maana kwenye mashindano.

  KUNA MSEMO USEMAO UKISHINDA KUMPIGA ADUI YAKOOO, BASI UNGANA NAE! HAPA NAKUSHAURI UNGANA NA JACK ILI UKUZE KIPAJI CHAKO.

  ACHANA NA TABIA MBAYA YA KUPENDA KUHUKUMU, BADALA YAKE JADILI MADA NA PENYE KAZI NZURI USIACHA KUPATIA MOYO KAMA IPO TATIZOOO, BASI KOSOA KWA BUSARA ILI UJUMBE UWEZE KUMFIKIA MLENGWA, VINGINEVYO UTAKUWA UNABWABWAJA HOVYO TUU! NA KISHA KUPOTEZA MUDA.

 35. julieth Says:

  hapana hujanikosea ninalia kwa furaha, mapenzi unayonipa sijawahi kupata……………………………
  i really like that song more than any other song that you ve ever sang, see you were very young, and that innocent look on your eyes. yani it was juz waooooooooohhhhhhhhhh!!!!!!!!

  thumbs uo babe aluta continua,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, baby gallllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllll………………………..

 36. virgoeyes Says:

  She’s got a sweet voice, that matches her look. Kenyan artist have a lot to learn from Bongo Flava. keep it up K-Lynn

 37. manka nkya Says:

  ooooooooops huyu dada me namfagilia kwasababu anajua kupangilia pamba,kuimba halafu hana maringo wanayasema ana maringo wana lao jambo, so my sister kaza buti pull youre sox ucwasikilize wanaadamu hawakosi la kusema.
  swala la kucheza ni kawaida kila mtu ana style yake, mbona unacheza vizury
  hawaoni famous singers kama mariah carey, whitney houston na wengine wengi hawachezi lakini kazi zao ni very attractive so don wory keep it up dear

 38. mukrim Says:

  jaribu kubadilisha mavazi nashanga sana kuona msani kama wewe unatakwia kuonya na sio kuaribu so nguo zako kwa kweli hazifurahishii

 39. jamy Says:

  Nakufagilia kiujumla kaza buti ssiter mambo yako makubwa.

  big up!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 40. senator Says:

  DADA KLYNN MIMI NI MREMBO KAMA WEWE LAKINI NIMETOKEA KUKUPENDA SANA UNAONAJE TUKIWA WAPENZI.naitwa naomi aka OMI

 41. samwel mdalingwa Says:

  mmh you look so cute,I real admire your work .so keep it up with more efforts.
  SAM frm tegeta mbweni masaiti

 42. MAMII Says:

  Punguza kuimbia puani then jifunze kucheza….Japo watu wanakufagilia but bado hujamfikia ray.c

 43. reenaa Says:

  u r gud k- lyinn. do whatever u like people always they like that u r good mama

 44. annie Says:

  i guess ur missind jawa,she was the only one who could do ur hair bt u still ;look fine,

 45. impala Says:

  jakilini acha uyungu,mariah carey kaanza imba mwaka 1990.sasa wewe mwaka huo ulikua na miaka sita-saba,hukua unakaribia kuondoka nyakahoja wewe?muwe mnajistukia sa’zingine bana!!

 46. amy Says:

  she is my favourite of all.. I love her style…can listen and her watch any time…she’ll get much much better with time…love u girl..dont mind them people..keep doing what u r doing…

 47. mpagamaY Says:

  we uko juu ccta,

 48. kundani Says:

  I love her. I not been in Tanzania in ’bout 2 years now lakini i really miss it. And i love her songs!!
  Peace.

 49. doreen Says:

  you are beautiful in nature ilove you so much.mwaaaaaaaaaa


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s