BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

AMINA CHIFUPA HATUNAYE TENA! June, 26, 2007

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 3:37 PM

                     

Hivi punde BongoCelebrity imepokea habari za kusikitisha sana kwamba aliyekuwa mbunge wa vijana, Amina Chifupa (pichani) amefariki dunia muda mfupi tu uliopita. Mauti imemkuta katika hospitali ya jeshi Lugalo alipokuwa amelazwa. Chanzo cha mauti bado hakijatolewa rasmi.Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa update zozote zitakazopatikana.

BongoCelebrity inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki popote walipo na pia watanzania wote kwa ujumla.Mungu ailaze pema peponi roho yake.

Advertisements
 

60 Responses to “AMINA CHIFUPA HATUNAYE TENA!”

 1. Halima Says:

  Jamani jamani,duh imekuwaje tena masikini Amina???
  Mungu ilaze roho yake mahali pema peponi.Amen

 2. laila Says:

  Duu hii nu nyuzi mbaya sana. Yaani ilivyoniuma, hii inaonyesha jinsi tunavyojisikis celebrities wetu wakifa. Poleni sana familia ya Amina. Mungu amlaze mahali pema.

 3. Inno Says:

  poleni sana familia ya Amina Chifupa. Tulikutegemea sana bungeni. Mungu akusamehe makosa yako na kulaze mahali pema peponi. Duu sijui Mpakanjia anajisikiaje sasa hivi.

 4. Mabula Says:

  Hapa Toronto, Canada. Poleni sana.

 5. Evaline Says:

  Pole sana Watanzania wote kwa ujumla, na familia ya Shifupa.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Mungu awajaze amani na awafariji familia yake, mume wake na mtoto wake.

 6. Kidanka Says:

  Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake, sisi tumemsamehe yote ila alikuwa si mtu wa kutuwakilisha bungeni sisi vijana kwani wote tulikuwa tunaonekana wenye kashfa tele. Sasa tushike hatamu kumpata mwakilishi anayetufaa. Amen na sote tutakuwepo kumzika huko Njombe.

 7. SIAMINI KAMA AMINA , HATUKO NAYE TENA . MBUNGE MDOGO MA
  WAZO YAKE MAZURI TAIFA VIJANA WA TANZANIA TUMEPOTEZA KIONGOZI.MUNGU AILAZE ROHO YA AMINA MAHALI PEMA PEPONI.

 8. SIAMINI KAMA AMINA , HATUKO NAYE TENA . MBUNGE MDOGO MA
  WAZO YAKE MAZURI TAIFA VIJANA WA TANZANIA TUMEPOTEZA KIONGOZI.MUNGU AILAZE ROHO YA AMINA MAHALI PEMA PEPONI.
  columbus,oh

 9. jirani Says:

  oh my godness jana tu tupo naye leo hayupo duu its a pity Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amen dont mock the dead guys its not good for us to judge others let it be gods judgement

 10. King B Says:

  Kwa kweli sasa watu wameaanza kuelewa ubaya wa haya magazeti ya shigongo kwani kwa kiasi kikubwa tu ndio yamechangia kifo cha amina chifupa! Mungu ailaze roho ya marehemu Amina
  Sasa shigongo tafuta mtu mwingine wa kuua maana umezidi sasa na hizo habari zako….umeleta ukabila mpaka ulithubutu kusema wewe ulitoa hela ili Vicky Kamata apite lakini sasa ni wakati wa ko wa kufikiri kilichotokea ili iwe fundisho kkwako… mlokole wewe shigongo mnafiki sanaa…..

 11. tania Says:

  Duu nafurahi kuona upeo mkubwa wa Watanzania hasa Vijana, kweli Shigongo na rafiki yake Nchimbi ndio mwanzo wa matatizo ya Amina. Lakini malipo Duniani mtalipa tu hata kama mnatawala Dunia yote. Shigongo tunakushauri usifanye siasa kwenye maisha binafsi ya watu, na hizo picha za utupu unazotoa kwenye magazeti yako hatuzihitaji, kifupi aandika hadithi au mambo ya maendeleo.

  Shigongo na Nchimbi jirekebisheni.

 12. John Says:

  Naimani Muda huu si wa malumbano, tumwombee tu mwenzetu apumzike kwa amani na ndugu zake tuwape moyo hasa katika kipindi hiki kigumu kwao.

 13. SHECHE Says:

  Kweli kazi ya mungu Haina Makosa, Kalale pema peponi shujaa wetu AMINA CHIFUPA.

 14. cpie Says:

  R.I.P Amina ull olwayz be loved.

 15. Neema Says:

  Nawaombea sana familia ya AMINA waweze kumaliza salama wakati huu mgumu kwani haya yote ni mapenzi ya mungu, kazi ya mungu haina makosa mungu alitoa na mungu ametwaa kazi ya bwana ishukuriwe. Tutamuombea sana Amina ulale salama mahali pema peponi. Kazi yake mungu aliyomtuma akafanye mungu aliona kuwa ameshamaliza hapa duniani. Hili ni pigo kwa watanzania wote wakubwa na wadogo

 16. tom l Says:

  hivi hiyo hospitali ya lugalo ina nini? pepo mpaya au? nakumbuka hata girl friend wangu alikufa hapohapo mwaka 2000!!!!
  any way..imekuwa ghafla sana kwa binti huyu kufariki, midomo mibaya ya ya watu au?

 17. Yasmin Simba Says:

  Amina was my role model & a hero to me.Namchukulia Amina kama mwanajeshi aliyefia vitani. It hurts kwani she was soo young to die!! Ila aliyoyaacha viongozi wajitahidi kuyaendeleza..Mungu amlaze mahali pema peponi,AMEN.

 18. Prisca Says:

  Tunamshukuru MUNGU kwa yote, tumepoteza kijana ambaye tulitarajia siku za usoni angafanya mamabo makubwa zaidi. Angalizo kama kuna mkono wa mtu ajue kwamba MUNGU wa sasa hivi ni kijana analipa hapahapa duniani.
  Inaniuma sana sijui kwa nini..MUNGU ailaze roho ya Amina peponi. Amina

 19. Rehema Says:

  kwakweli Nona SHIGONGO amefanya sherehe nyumbani kwake maan alitaka AminaAFE ILI YEYE ALITHI HUO WADHIFA HAYA CHUKUA NA UFURAHIE VYEMA yaani unaandama maisha ya mtu mpaka unatamani hata pumzi yake uwe unampa wewe
  Utaua wangapi kwa maneno yako na chokochoka zako Sinta alitaka kujiua sababu ya maneno yako Nora Aamekuwa na wazimu sababu yako mbona wanaume wenzio huwaandiki unaogopa mkong’oto eee sasa mpeleke mkeo akaolewe na mpaka njia na wewe uende bungeni badala yake tumekuchoka tulikupenda sana mwanzo kwa hadithi zako lakini huo umbea mnaoufanya na timu yako ni ungobya nina mengi ya kusema maananinauchungu sana na wewe Shigongo FURAHI SASA

 20. Esther Says:

  Kweli ni habari za kusikitisha sana.
  Tunatakiwa tushukuru kwa kila jambo, ingawaje kibinadamu ni vigumu sana..kwa hiho tuwe tayari wakati wowote.

 21. ray Says:

  AMINA MUNGU AKUBARIKI HUKO UENDAKO .POLE FAMILIA YA AMINA SANA .NANYIE MNAO UWA UWENI HADI MCHOKE ILA MKICHOKA NANYIE SAFARI MTAWAKUTA MLIO WATANGULIZA.

 22. tom lee jones Says:

  hivi marehemu ilikuwaje hata akapelekwa hiyo hospitali ya lugalo? hivi toka lini wanajeshi wakawa madoctor? mbona hospital bigwa zipo nyingi tu…..hivi ilikuwaje mimi sielewi!!!!!
  naomba mnijibu watau!!!

 23. Mang'era Says:

  Ama hakika binadamu akiandamwa sana inakuwa noma. Yawezekana kabisa akafa kafa “natural death” ila sasa hao kina Eric Shingongo na wenzake lazima lawama ziwafikie kwa namna moja au nyingine! Sasa Shigongo sijui ataweka unafiki gani……….Maana hachalewi kujifanya naye eti anasikitika kwa msiba!

  Tunategemea watu kama kina Shigongo wafanye SHEREHE sasa! Maana walichokuwa wanakitaka kwa AMINA, wamekipata

 24. diana Says:

  Mwenyezi Mungu ilaza roho yako mahali pema poponi amina.

 25. MAKALA Says:

  MAY YOU REST IN PEACE GIRL FRIEND,SHIGONGO AND NCHIMBI YOU GONNA GET YOURS!!

 26. Angela Says:

  kutoka ,JAPANI,
  MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI BI AMINA JAMANI,
  NAMUOMBEA AMANI RAHMANI NA BABA YAKE,
  MAMA NA BABA WA AMINA POLENI,

 27. lilian Says:

  Dada yeyu mpendwa, mengi yamekwishasemwa na kila mdau, kwa kifupi tunakutakia mapumziko mema, kwani kazi ambayo Mungu alikutunuku katika umri wako mdogo sana imeshakamilika hapa duniani..utabakia kuwa mwanga kwa vijana na kina mama wote ulimwenguni. Umekuwa changamoto mahiri katika maswala ya kutetea haki na kuzungumza ukweli bungeni…daima utakumbukwa kwa ucheshi na maneno yako ya dhati kwa walengwa..
  Bwana amekupenda zaidi na hatuna budi kumshukuru kwa kila jambo. Pole kijana Rahmani, pamoja na familia nzima ya marehemu..
  Raha ya Bwana umpe daima Amina Chifupa apumzike kwa amani. AMINA!

 28. mboni Says:

  kama alikosea basi wangemfuta ubunge sio kumuua, i hate politics, i hate all the people in one way or onether who caused this death, i hate you killers, you gonna pay for this death,wote mtakufa vifo vibaya tu,you will pay for this, it pains
  rip amina sina raha kabisa hapa nilipo, mnasababisha mpaka nichukie nchi yangu kwa haya matendo jamani, ndio maana wat hawarudi huko, siasa ni uzushi mtupu

 29. Musika.N.V Says:

  Dearst Amina ,I didnt know you will die before I meet you and talk to you face to face.You are the voice of Tanzania youth.I wanted to discuss with you on how best we can help Tanzanians youth. Now you are no longer there!!Im very very sad.Goodbye Tanzanian hero who knows why you are leaving us the time when we need you most.I pray that someone else will take over and make sure all the good things you did for Tanzanians youth do not perish
  Poleni sana Watanzaia wenzangu

 30. Kilandu Says:

  There is no need of speculation. I am not sure that shigongo even writes ll those nonsense in his daily tabloids, I think Amina died from stress. May be there is a need of giving a statement of her previous histrory with diabetes. Also its possible she started feel weak early, but sometimes busy people ignore the symptoms because of their schedules. May be she seeked medical attention to late. But a combination of things might have caused her death.

  Lets wait and see if there is going to be a report. Is there anyone who has any idea of why she has to be rest in Peace. Is it because she was married to Mpakanjia. Is she from there. If its because of her husband, it does not make sense since they had some sought of divorce/ separation.

  Lets wait patiently to hear what would be said after the report.
  RIP

 31. mariam Says:

  Nimesikitishwa sana na kustuka kwa msiba wa amina, lakini jamani watu wen=ma hawana maisha huo ndio ukweli , mungu huwaleta duniani ili kuwapasoma watu wengine nini, cha kufanya, amina aliingia bungeni kutoa changamoto kwa wabunge wote, na alionyesha wazi pamoja na udogo wake wa umri, na elimu yake ndogo, lakini akili na wajibu wake kwa aliowawakilisha haukuwa mdogo,
  Amina pumzika salama dada, kazi yako imekwisha hapa duniani. japo umekwenda lakini somo kwa wanasiasa limefika kazi kwao kufuata nyao.

 32. dj tom in japan Says:

  it doesnt make sense to that a young girl of 1981 dies because of maralia and diabetes!!!!
  huu ni uongo, hii haiwezekani kwa sababu katika uhai wake hatukusikia hata siku moja kwamba eti amina alikuwa na kisukari!!!kama ilivyoelezwa katika barua ya mdau mmoja katika michuzi blog, huyu dada alikuwa anatoa taarifa za wauza madawa ya kulevya, sasa je serikali ilikuwa na mpango gani wa kumuwekea ulinzi? alihitaji protection, any way hiki sio kifo cha kawaida, kuna mkono wa mtu….naomba serikali ichunguze!!!!!!

 33. Fatma Says:

  Inauma sana kifo cha Mpendwa wetu mdogo wetu Amina. Inabidi tumuombee kwa Mola apumzike kwa Amani.

 34. bridget Says:

  R.I.P Amina kipenzi chetu sisi tulikupenda lakini mungu alikupenda zaidi kweli uyu shigogo na nchimbi wafanye party kila kitu wanataka wapate wao haya tutawaona kwanza nimefurai jamaa alizani atauza vijigazeti vyake kachemsha wwengine ndo wamefaidi nani atasoma kiu na ijumaa leo HUNA JIPYA

 35. liz Says:

  Sasa nani atamdhiri AMINA HILO NDILO TUNATAKA NA KUONA UNAFIKI WA WATU!!!! PIA UVCCM UNANINI KWANI IPYANA ALIKUFA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA JE KUNAMKONO WA MTU AU???? HEBU UNGANISHA MAZINGIRA YA TALAKA YALIVYOTOLEWA, JE MPAKANJIA HAKUTAKA KUSIKILIZA KAULI YA MKEWE NA KUPATA UHAKIKA KAMA KWELI ZITO ALIKANDAMIZA??? BY THE WAY.. NI WANAWAKE WANGAPI MPAKANJIA ALIONAO NA AMINA AMAVUMILIA??

  jack

 36. Formula Says:

  “Amina was a soldier till the end of time”.people should keep in mind that alwayz “Good Die Young” n’ Amina has proven that!
  may Allah put her soul rest in peace,Amina!!!!!!

 37. BongoSamurai Says:

  Duniani hajawahi kutokea binadamu aliyemkamilifu.Kila mtu ana kasoro zake ila kwa tabia zetu mbaya huwa tunapenda kuona mabaya tu yanayotendwa na wenzetu!!Mie ningependa kumuuliza bwana Shingongo je Amina hakuna zuri hata moja alilotenda kama binadamu hadi ukafikia hatua ya kumuandama kwa kila hatua aliyokuwa anapiga?? Pili je wewe ni malaika na hauna baya lolote ambalo umeshawahi kulitenda?? Umefikia wakati wa inabidi ukae chini na ujiulize au ujichunguze ni nini ambacho ulikuwa unafanya au umefanya katika maisha yako ili kuielimisha jamii kupitia magazeti yako ya udaku na sio kuandamana watu kwa sababu zako binafsi!Amina alikuwa na mazuri mengi tuu na katika msiba na mazishi yake yote yamejionyesha maana wengi tulimlilia na bado tunamlilia na hatuamini kama hayuko nasi tena!Amina, lala pema peponi kamanda wetu, wote tuu njiani tunakuja natumaini utakuwa mwenyeji wetu siku ambayo Mungu atatuita kwenye makao ya milele.

 38. Matilda Says:

  Dada yetu kipenzi,Rafikiyetu Mpendwa,Ndugu,aunt,Ma mdogo nk.Hatunae tena,Tunakumbuka mengi sana umeyafanya hapa duniani na sito sahau pale ulipo sema NIPO TAYARI KUFA KWAAJILI YA VIJANA WOTE HAPA TZ,kusu madawa ya kulevya na umekufa siku ya madawa ya kulevya kwani kuna mkono wa mtu? kama ndio Mungu ata muonyesha na yeye,Tunajua sote tupo njia moja ila naona kama Amina kwake ni mapema sana jamani maana bado ndoto zake hazijatimilizika vile,ila huwezi jua ya mungu.rest in peace,Amina!!!!!!

 39. Nerra Says:

  Sisi kama wanawake na vijana tumejifunza vitu vingi kutokana na kifo cha Amina! na nasema Tanzania kamwe hatupata maendeleo yeyote kwa hali hii, mie naona kila mtu aishi anavyoweza lakini maswala ya kujitoa kwa ajili ya wengi kwa nchi ni adithi,jamani nina hasira!!!!!………………………??? Mpaka lini???

 40. salvatory Says:

  najua its not only polioticians in this but the drug dealers in this why u people ????????? this isnt a natural death of coz and why u Amina and on the same date of ur fight againts drugs u must be god sent to save Tanzanians from politicians am wrighting this in so much pain that its unexplainable i hate politics an never politics in this Tanzania . amd u shigongo u had a hand in this shez away are u happy with that every where on ur papers its her u killed ha 2 i hate u man DADA AMINA REST IN PEACE WE TANZANIANS SHALL ALWAYS REMEMBER U FOR UR CHARITY AND GOOD TAKE CARE FOR THE YOUTH WE SHALL MISS U BYE

 41. tumaini lema. Says:

  Tulikupenda sana ila mungu kakupenda zaidi amina.
  Mwenyenzi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi.

 42. Tulinagwe Says:

  Its not good to talk bad things about dead people,huu ni utamaduni wa kiafrika,ila ukweli na uwazi ni muhimu,kuna mzee mmoja wa kigamboni ambaye binti yake ilidaiwa aliolewa na Mpankanjia alisema Amina na mmewe lazma wamwombe radhi la sivyo maafa makubwa yatawapata,ajali ya gari ya Mpakanjia ilikuwa mwanzo tu makubwa yatafuatia.kwa sababu amemshtakia mungu kwa kumsema yeye muongo mbele ya jamii.

 43. Tulinagwe Says:

  Mwanamasanja Banzastone aliimba hujafa hujasifiwa,ni mteja wa madawa lakini aliimba kitu cha maana,kilichomuua Amina ni aibu ambayo iliyokuwa mbele yake,atasema nini mbele ya watanzania kwa kuachwa na mpakanjia mwanaume ambaye alikuwa anajisifia kila kukicha hatomuacha!hadi akaanzisha kundi la aliloliita la Al Qaeda kupambana na wezi wa waume za watu!wauza madawa ya kulevya wamuue wa nini hakuwa na ushahidi wala hakuwahi kumtaja hata mmoja.Shock depression ya talaka,that is all

 44. Mwaju Says:

  mshtuko aibu ya talaka na albadiri au yamini ndiyo the most reasonable explanations ya kifo cha Amina hakuna jingine la Nchimbi,Shigongo wala wauza madawa ya kulevya.magazeti yalikuwepo kabla ya talaka na Nchimbi alikuwepo kabla ya talaka

 45. Collins Says:

  Ni dhambi kumuongelea mtu aliye mbele ya haki (hasa kwa mabaya)kama alivyofanya huyu ndugu yangu “kathiku” sijui nani!
  hata sijui huyo m2 kama ana dini,halafu at da end unakuja kuomba msamaha,so tell us was it a joke what you had tell us from ur first comment!?.
  nafikiri ulitaka tu uone wa2 watakavyorumbana “that’s it!”
  basi sio to da dead p’ple,for GOD seak!!!.
  mungu akusamehe!
  R.I.P dear sister AMINA.

 46. The Truth Teller Says:

  Kila kitu tumuachie Mola jamani.Hivi na sisi tuliokaa kimya tukianza kueleza Ulimwengu kuhusu siri za Shigongo tutalaumiana?Nilikasirishwa sana na Shigongo alivyotuabisha wanaume kusema kuwa alifuatwa na marehemu…….Kwanza kama ulitongozwa kudos…at least kuna mrembo alikutaka…!Mambo kama hayo wanaume huwa hatumwagi hadharani jamani….aaaaaha nimesahaaau…Shigongo ni…………?!!!!Mdomo mdomo huo….!!Nilikuwepo na nilikuona….ha ha ha ha…What goes around, comes around…..now it’s your turn…..BOOOM…!!!

 47. erwin Says:

  FROM SOUTHERN INDIA
  ROHO YA AC ILALE PEMA PEPONI..AMEN POLENI SANA FAMILIA YA AC

 48. Meg Says:

  Msihukumu msije mkahukumiwa,
  MUNGU alize ya AMINA mahala pema peponi. AMEN

 49. Meg Says:

  Msihukumu msije mkahukumiwa,
  MUNGU alize ROHO ya AMINA mahala pema peponi. AMEN

 50. mamii Says:

  Rest In Peace Amina! you were a woman and a half, na uliwatikisa vya kutosha! you are a hero, that’s obvious!!
  Kusema eti Amina kafariki kwa ajili ya aibu ya talaka ni makosa! what is TALAKA??? i don bilieve this! wangapi wameachwa kwa talaka and they are still surviving?
  kusema magazeti na some owners wamechangia ni kweli coz, kama angeachwa na kila gazeti likaendelea na habari tofauti na sio kumuandika yeye day in, day out ni dhahiri maisha ya Amina yangeendelea kama kawaida!
  naunga mkono kuwa magazeti yamechangia kwa kiasi kikubwa depression yake na hata kifo chake.
  haya she is no more, let us see their creativity now!
  AMINA WE LOVED U SO MUCH, HONESTLY, U WERE MY ROLE MODEL! LALA SALAMA KIPENZI CHA MACHO YANGU

 51. glory Says:

  rest in peace mt role model

 52. salma Says:

  Nilikupenda sana Amina lakini mungu kakupenda zaidi.

  yaaani siasa ya bongo haifai nawasihi na kuwaasa vijana wote ikiwezekana wasijihusishe kabisa huko ! Amina masikini anataka kufungua tu mdomo wamemziba mojakwamoja!!! anyways hata wao ipo siku wataelekea huko! kwakweli iliniuma sana na kunisikitisha !

  Nchimbi hongera sana wewe na mpakanjia malengo yenu yametimia bila kumsahau mshiri mkuu mwenzenu Eric shigongo.

  Mungu akulaze mahala pema peponi . Amina Chifupa

 53. kirayas Says:

  Hoi
  sasa hii ni mitengo! Badaada ya Drama iliyo pita tena imeingia ingine! hivi ni kweli Mpakanji Kafariki na Wema ama kuna mmkono wa mtu? hivi tunaelekea wapi watanzania jamenii? anyway mungu amlaze marehemu Mpakanjia mahali pema peponi.Condolly from Holland.

 54. ukende Says:

  No one wuld eva explain how it feels, But lets accept the fact thats she is nat with us anymore…what we can do better for is to inherity oll the good things that she initiated.wat i lent frm her,that she neva know to givup.may Almight GOD rest her in peace. amen

 55. Ray. Says:

  Mwenyezi mungu akupumnzishe mahali pema peponi amen. mungu anajua yote kila anayekuongelea mabaya mwenyezi mungu atakusimamia kwa kutuma malaika wa kheri ili wakuzibe amina.

  rest in peac friend.

  Rafikiyo.

 56. bertha Says:

  pole family ya AMINA.

 57. neema mhando Says:

  So young… so beautiful…..
  RIP.

 58. Matty Says:

  RIP AMINA! nothing gonna change but it pains!

 59. Kila nafsi itaonja umauti haijalishi utakufa vipi! Kila msiba una namna na sababu zake! Kikubwa zaidi ni dhambi tu ndizo ambazo zinatukuwa mavuno yetu tukianza kutafuta nani anahusika na msiba wa Amina. Tumshukuru Mungu kwa kuonyesha uwezo wake basi!

 60. Nuru Maluyo Says:

  Imeniuma sana kupata taarifa ya msiba wa Mh Amina yaani sina hata la kusema!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s