BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KWAHERI AMINA CHIFUPA! June, 27, 2007

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 10:09 PM

Hizi hapa chini ni baadhi ya picha kutoka kwenye msiba wa Amina Chifupa ambaye kama alifariki dunia jana usiku. Kwa sababu alizaliwa tarehe 20 Mei 1981 amefariki akiwa na umri wa miaka 26 tu! Pamoja na kuwa na umri mdogo namna hiyo Amina Chifupa atakumbukwa kwa mengi achilia mbali historia ya kuwa mbunge mdogo kuliko wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania lililopo hivi sasa. Vita dhidi ya madawa ya kulevya aliyokuwa ameianza kabla mauti haijamfika inamfanya awe sio tu shujaa bali mwanamke na kijana jasiri kupita kiasi. Daima tutamkumbuka kwa hilo.

Sauti yake kama mtangazaji wa Clouds FM, MC katika shughuli mbalimbali, kama mbunge, mtetezi wa vijana na wanawake daima itabakia masikioni mwetu sote.

Anatarajiwa kuzikwa leo huko wilayani Njombe mkoani Iringa. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amina.

Sheikh mkuu wa Tanzania Issa Shabaan bin Simba akiongoza ibada.

Sehemu ya umati uliofika nyumbani kwa wazazi wa marehemu mheshimiwa Amina Chifupa, Mikocheni jijini Dar-es-salaam. Kulia aliyesimama ni Muhidini Issa Michuzi, celebrity na mpiga picha maarufu.

Luiza Mbutu Nyoni na Jessica Charles pia walikuwepo kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mheshimiwa Amina Chifupa.

Picha zote kwa niaba ya Ahmad Michuzi wa michuzijr.blogspot.com

Advertisements
 

18 Responses to “KWAHERI AMINA CHIFUPA!”

 1. Tuzie Says:

  Pole kwetu sote watanzania,ndugu,jamaa na marafiki.Pumzika salama Amina.Inapendeza pia kuona jinsi celebrities walivyojitokeza kumuaga mwenzao.Udumu upendo na ushirikiano katika shida na raha.

 2. Robert B. Mujuni-Tabata Says:

  Amina Chifupa, uliletwa duniani kutuonyesha vijana tunatakiwa kupigana vipi na maisha, kwa umri wako na uliyofanya ni dhahiri kazi uliyotumwa na Muumba umeimaliza, sasa kazi kwetu vijana, sio kujionyesha na kulalamikia kwapani na kuona kila kitu ni kazi ya kiongozi au Serikali, ni wajibu kila Mwananchi hasa sisi vijana. Siku zote nabii hakubaliki kwao. Ila leo ushuhuda ni huu kuwa kazi imekwisha kwako na sasa sisi ni zamu yetu.

  Mungu ailaze mahali pema peponi roho yako Amina

 3. Prosper Minja Says:

  Tulimpenda Amina, ila Mungu alimpenda zaidi!

 4. DELROY Says:

  AMINA SHOSTI, PUMZIKA KWA AMANI MUNGU ATAWALIPIA HAO WALIOKUTANGULIZA NDOTO ZAO NAO ZITAZIMWA KAMA WALIVYOZIMA YA KWAKO

 5. BongoSamurai Says:

  AMINA REST IN PEACE.KAZI ULIYOTUFANYIA VIJANA WENZIO TUMEIONA NA TUTAIENDELEZA.

 6. Matilda Mashoko Says:

  We loved you Amina Chifupa,But God loved you more,may God your soul in Peace.Matilda

 7. Rose Says:

  MUNGU IALAZE PEMA PEPONI ROHO YA AMINA, YOTE YANASEMWA LAKINI HATUNA JINSI YA KUMRUDISHA AMINA ILA WANAOHUSIKA NA KIFO CHAKE WATALIPA, YOU WILL PAY FOR THIS NA YA KWENU ITAKUA MBAYA ZAIDI, HAMNA HATA HURUMA?! WE LOVE U AMINA AND YOUR SON TOO.

 8. Fatma Says:

  TUNAKUOMBEA MDOGO WETU AMINA UPUMZIKE KWA AMANI.

 9. JABIR Says:

  AMINA WAS SALE FISH WOMAIN LET HE LEAVE IN JAHENEM

 10. gabriel Says:

  tutakukumbuka milele!!

 11. Monica Says:

  Natoa pole kwa Mzee Hamis Gabriel Chifupa pamoja na familia yake.
  Kama binadamu yeyote anahusika na kuuondoa uhai wa kipenzi chetu mwenyezi Mungu(SW) awamulike haswa.

 12. Monica Joel Andrew (Arusha) Says:

  Nawapa pole Watanzania wote hasa vijana kwa kumpoteza aliye simama kidete kupinga madawa ya kulevya nchini.

 13. Nusura Jambo Says:

  Mungu amalaze mahali pema peponi mdogo wetu Amina Chifupa wa Mpaka Njia.

 14. mariam H Says:

  Tulikupenda lakini Mwenyenzi Mungu kakupend zaidi wote tunaenda kumoja ila inauma tunavyo ondoka kila mmoja kwa wakati wake M/Mungu akulaze mahali pema peponi amina

 15. amina Says:

  rest in peace wajina

 16. Matty Says:

  RIP AMINA!

 17. data-protection Says:

  jabir!lah!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s