BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ALUTA CONTINUA-PROFESSOR JAY July, 2, 2007

Filed under: Bongo Flava — bongocelebrity @ 1:22 PM

 

 

“Jina langu limevuma, Kwenye mitaa.Jina langu lina hadhi ya ki-superstar.Jina langu…..” Hayo ni maneno kutoka kwenye wimbo Jina Langu wa msanii mahiri wa Bongo Flava, PROFESSOR JAY au Prof Jiizeh. Hakuna ubishi, jina lake limevuma na ni kweli ana hadhi ya ki-superstar.

Alizaliwa jijini Dar-es-salaam tarehe 29 December 1975. Ni mtoto wa sita kati ya watoto tisa wa Mzee Leonard Steven Haule na Mama Rose Majanjara. Baadaye akasoma Ukonga Primary School kabla hajaelekea mji kasoro bahari(Morogoro) kusoma Kigurunyembe Secondary na baadaye Mbeya Lutengano High School.

Ana tuzo za muziki zisizopungua 25 ambazo amezikusanya ndani ya miaka 15 ambayo amekuwa kwenye game. Hivi karibuni BongoCelebrity iliketi chini na msanii huyu ambapo alifungua milango ambayo hajawahi kuifungua kabla. Katika mahojiano haya nadra, Professor Jay anazungumzia kwa undani shughuli zake za muziki, siasa za nchi,ushauri kwa vijana, role models, vilio vya wasanii kuhusu kazi zao na mzunguko mzima wa muziki. Pia anatoa ushauri makini kwa Raisi Kikwete, anabainisha mtizamo wake wa kisiasa na mengi mengineyo. Yafuatayo ni mahojiano kamili;

BC: Karibu sana katika BongoCelebrity na shukrani nyingi kwa kukubali kufanya mahojiano nasi.

PROF.JAY: Asante Sana na najisikia faraja sana kupata fursa hii ya kufanya mahojiano nanyi kwani itakuwa ni nafasi nzuri ya kuwajulisha mashabiki wangu kuhusu mustakabali wa shughuli zangu za kimuziki

BC: Unaweza kukukumbuka ni lini ilikuwa ndio mara yako ya kwanza kupanda jukwaani kama mwanamuziki huku umati wa watu ukisubiri uwape burudani. Ilikuwa wapi?

PROF.JAY: Yeah nakumbuka ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka 1992 nikiwa pamoja na mshkaji wangu KILLA B pale Chuo Kikuu cha Dar es salaam ukumbi wa UDASA. Nakumbuka watu walikuwa kibao nanilikonga sana nyoyo za mashabiki wa muziki huu kwa style yangu ya enzi hizo ya TONGUE TWIST.

BC: Mara nyingi wanamuziki wengi huwa wameanza muziki kutokana na kupata ushawishi (influence) fulani hivi. Unaweza kutuambia nini au nani alikushawishi kuingia katika masuala ya muziki?

PROF.JAY: Nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo za akina RUN DMC na PUBLIC ENEMY kwa kuwa walikuwa wanaimba nyimbo za kupigania na kutetea haki za mtu mweusi. Kwa hiyo nikawa nazikariri na kuziimba shuleni na pia nikawa najaribu kuongeza maneno yangu na mwisho nikawa taratibu na mimi natunga mashairi yenye ujumbe tofauti tofauti kwenye jamii yangu iliyonizunguka.

BC: Ulipojitokeza rasmi katika ulimwengu wa muziki ulijulikana kama Nigga Jay, kisha yakafuata majina kama Jay wa Mtulinga, Mti Mkavu nk.Baada ya hapo majina kama HeavyWeight MC, Professa Jay na hivi sasa Daddy yakaibuka.Nini chanzo cha majina yote haya?

PROF.JAY: Ha hah hah mbona umeyaacha mengine mengi kama vile mchawi wa Rhymes ,Mr President,Mc Shupavu,Jay Tunakuzimia, Jay Arosto, Heavy Weight Mc,Prof Jiizeeh,Jiizeh for President, Madini mtoto wa mjini, na sasa hivi wananiita SAUTI YA HELA. Hayo yote ni majina ambayo napewa na mashabiki wangu kila mmoja wao ananitunga jina lake kutokana na anavyotafsiri muziki wangu na kwa kweli na mimi huwa nayapokea kwa moyo mkunjufu kwani naamini ni hao mashabiki wanaonifanya nikubalike kote.Siwezi kuwa PROFESSOR JAY bila wao.

BC: Baadhi ya ndugu zako kama vile Mr.Teacher (anayeishi na kufanya kazi zake nchini Marekani), Simple X, Black Rhino na Kolihombi nao ni wanamuziki. Je wazazi wenu nao walikuwa wanamuziki au hivi vipaji vinatoka wapi?

PROF.JAY: Wengi sana wanajiuliza hilo swali, maana hata dada yetu anayeitwa VIOLAH HAULE naye alikuwa ni kiongozi wa waimbaji wa kwaya ya shule tulipokuwa tunasoma sekondari kiasi kwamba watu walikuwa wanamuita Equalizer. Ukweli ni kwamba baba yetu alikuwa anapiga gitaa kwa kujifurahisha tu alipokuwa kwenye mapumziko yake na mama hakuwahi kuwa mwanamuziki, mimi naamini hizi ni karama tu za mungu katika familia yetu kwa kutujaaalia vipaji visivyochuja tangu enzi na enzi.

BC: Prof. kumekuwepo na malalamiko kadhaa kutoka kwa wasanii wanaojaribu chipukizi (underground artists) kwamba ni vigumu sana kwa wao kuchanua.Wanalalamika kwamba Djs wanawabania, studio ni gharama sana nk.Nini maoni na ushauri wako katika hilo?

PROF.JAY:Sio kwa wasanii chipukizi peke yao bali hata kwetu sisi wakongwe. Hilo tatizo lipo na linatukera sana , kwani wenye studio bongo hawapo serious na kazi zao wanaifanya biashara ya muziki kama biashara ya kuuza mapera.Wanafanya wakitakacho tofauti na mlichokubaliana na kwa wakati wanaotaka wenyewe sio unaotaka wewe na radio djz wamehalalisha hongo kwamba ukirelease wimbo lazima uambatanishe na takrima ili waweze kujikimu, kitu ambacho sio sawa na kinadumaza vipaji vya wasaniii bora na kuwapa nafasi wenye senti wasio kuwa na vipaji timilifu.

BC: Kwa upande wenu ninyi wasanii wenye majina makubwa tayari, malalamiko mengi yamekuwa kwamba ‘wadosi” hawako fair katika malipo mkilinganisha na jasho mnalolitoa katika kuandaa albamu nk. Ninyi kama wasanii mmefanya nini mpaka hivi sasa kukabiliana na hali hiyo?

PROF.JAY: Kitu cha msingi hapa ni kuwashawishi watu wenye uwezo na wenye nia nzuri na sanaa hii wawekeze katika muziki huu na sio kulalamika tu wakati hakuna dalili zozote za kupata tiba mbadala. Ni kweli wengi hatufurahishwi na mpangilio wa mauzo ya kazi zetu, je dawa ni kutopeleka kazi kwa wahindi? Hapana, wakijitokeza watu wakawekeza kwenye distribution naamini kabisa kwamba kutakuwa na challenge wao kwa wao so huyu usiporidhika nae unakwenda kwa huyu tofauti na sasa wapo wachache na ni marafiki.Ukimzunguka huyu anampigia simu mwenzake kisha inakuwa 4*4-16 = 0 .Hii sanaa ni kama kivuli chetu hatuwezi kuikimbia na dawa ya tatizo ni kulikabili sio kulikwepa.

BC: Sifa yako kuu sio tu kwamba unajua kurap bali pia ni mtunzi mzuri sana wa mashairi (lyrics) kwa ajili ya nyimbo zako. Unaweza kutuambia jinsi unavyoanza kuandika mashairi yako mpaka kufikia kuyaweka kama muziki?

PROF.JAY: Swali zuri, huwa naanza kwanza kufanya research na kujua nini ambacho jamii inahitaji na ni kwa muda gani, kisha natafuta topic ambayo watu wa rika zote wataielewa ipasavyo. Baada ya hapo naanza kunote down mwongozo wa mambo ya msingi ninayotaka kuyazungumzia mwisho nakuja kuoanisha pamoja na kufanya mtiririko unaoeleweka vema kwa HADHIRA.

BC: Tukiwa bado kwenye suala la uzuri wa mashairi, katika baadhi ya nyimbo zako zilizotamba sana kama vile Ndio Mzee na Siyo Mzee na collaboration kama uliyofanya na Juma Nature katika wimbo CCM na CUF, umezungumzia zaidi masuala ya siasa. Je una mpango wowote wa kuwa mwanasiasa siku za mbeleni? Na je nini maoni yako kuhusu utawala wa raisi Jakaya Kikwete hivi sasa?

PROF.JAY: Bado ni mapema mno kuongelea kama nitakuja kuwa mwanasiasa au lah. Nasema hivyo kwa sababu naamini siasa ni wito na unatakiwa uwe umejiaandaa kuwa mwanasiasa kabla ya kuingia ndani ya siasa.

Kwa mheshimiwa raisi Kikwete kwa kweli anajitahidi sana kutoa nafasi na mwongozo bora kwa vijana na pia kuzingatia sana la ajiri kwa vijana. Pamoja na hayo namuomba atuwekee msingi thabiti sisi wanamuziki maana inaeleweka bayana kwamba sanaa inatoa fursa ya ajira kwa vijana kwa asilimia kubwa sana hapa Tanzania hivi sasa. Kwa maana hiyo sanaa ya muziki itakapokuwa ajira ya uhakika basi itakuwa imemsaidia sana mheshimiwa raisi katika harakati zake za kupambana na matatizo ya ukosefu wa ajira, utumiaji wa madawa ya kulevya, dimbwi la ujambazi na matatizo sugu ya ukahaba yanayochangiwa sana na vijana waliokata tamaa ya maisha na kupelekea kujiingiza katika makundi hayo yanayorudisha sana nyuma maendeleo ya taifa letu tukufu na hivyo kuongeza umasikini, vifo na matatizo sugu kama kuongezeka kwa wagonjwa wa UKIMWI na watoto yatima nchini kwetu.

 

BC:Kwenye albamu yako ya J.O.S.E.P.H katika baadhi ya nyimbo uliongelea masuala muhimu sana ya kijamii kama vile ajira kwa watoto,elimu, ukimwi nk. Nini unadhani kifanyike ili kurekebisha hali mbaya katika sekta hizo? Na je wewe binafsi una mtoto au watoto?

PROF.JAY: Asanta sana , hapa nadhani kitu cha msingi kwanza ni kuzijenga familia bora, tukiwa na familia zilizokulia kwenye maadili ya kidini,ustaarabu na malezi bora ina maana suala la matatizo ya watoto hayatakuwepo au yatapungua kwa kiasi kikubwa. Pili watoto wapewe haki zao za msingi kama vile ELIMU,AFYA,MALEZI BORA, na pia wapewe uhuru wa kuchagua na kufanya kile anachokipenda. Pamoja na hayo yote wazazi lazima wawe wanawaeleza ukweli watoto wao kuhusu kuhusu mabadiliko ya dunia hususani kuhusu ugonjwa huu hatari wa UKIMWI, maambukizo yake na madhara yake na jinsi ya kujiepusha na ngono zembe na kufanya mapenzi katika umri mdogo.

Ndio mimi nina mtoto mmoja wa kike ana umri wa miaka miwili na nusu na anaitwa LISA.

BC:Tukija kwenye muziki wa kizazi kipya, nini maoni yako kuhusiana na tuhuma kwamba muziki huu ushapoteza muelekeo na huenda ukapotea hivi karibuni?

PROF.JAY: UNAJUA MUZIKI WETU UMEFANIKIWA NA BADO UNAENDELEA KUVUKA MIPAKA na kuteka mashabiki lukuki ndani na nje ya Tanzania kila kukicha.Kwa hiyo ni wazi kuwa kuna baadhi ya watu hawafurahishwi na mafanikio hayo na kukesha wakiomba muziki wetu ufe au upoteze mwelekeo kwa sababu wanazozijua wenyewe.Napenda tu kwaambia hao wenye vimtimanyongo na viroho papo kwamba hii milango ya muziki wetu imeshafunguka na tutazidi kupasua anga na kama hawataki waende JUU kwa mungu aliye hai WAKAZIBE.

BC:Umekuwa kwenye muziki kwa takribani miaka 15 sasa. Kwa maoni yako, nini tofauti ya muziki wa kizazi kipya wewe ulipoanza na hivi sasa?

PROF.JAY: Duuh hili swali limenikumbusha mbali sana,unajua huu muziki wetu ulivyoanza watu tulikuwa tunauchukulia kama hobby tu, ukienda maskani unaimba nyimbo za kucopy za kina ICE T za mamtoni na watu wanakuona na wewe mjanja na pia tulikuwa tunakwenda kwenye matamasha ya mashule tofauti na hata unalipa ili uingie disco na unabembeleza na kuomba kinoma watupe mic ili tuchane kisha tunapata maujiko ya kumwaga kutoka kwa wanafunzi na mademu wa hapa na pale huku tukiwa na mapunk kama ya kina KID N PLAY nk. Hivi sasa mambo ni tofauti, muziki sasa ni ajira tena ni ajira inayoheshimika na vijana wengi tunaendesha maisha yetu kwa kutegemea muziki. Nadhani hiyo ndio tofauti kubwa.

BC:Katika maisha yako ya uanamuziki umetembelea nchi nyingi zikiwemo za Afrika na Ulaya. Nini umejifunza kutokana na ziara hizo?

PROF.JAY: Cha msingi nimegundua kuwa muziki wetu unakuwa kwa kasi na watu wa sehemu tofauti duniani wanavutiwa na sanaa yetu.Pia nimejifuza kuwa muziki ni muziki hata ukitumia lugha gani watu watakuelewa na wataupenda kwani nimekwenda sehemu nyingi na nimekutana na watu wengi wa mataifa tofauti na kusema ukweli watu wote tulikuwa kama tunaongea LUGHA moja ambayo ni muziki.Cha msingi ni kuboresha zaidi ubunifu na ushirikiano zaidi na watu mbalimbali ili tuweze kubadilika na kwenda na wakati na kuwa na ladha tofauti tofauti ili tuweze kulikabili soko pana la kimataifa

BC: Nini faida na hasara za kuwa mtu maarufu au celebrity?

PROF.JAY: Faida ni nyingi tu ila cha msingi inakusaidia kufahamiana na watu mbalimbali wakubwa na wadogo, masikini na matajiri na pia watu wa mataifa mbalimbali. Sasa kama unavyojua ukifahamiana na watu wengi hata maisha yanakuwa rahisi kidogo kwani unaweza kupata watu wakusaidiana nao kwenye pilika za kila siku kwani si unajua tena maisha hayana gurantee leo unacho na kesho huna. Kwa upande wa hasara labda kuwa sometimes nazinguliwa tu na pia nakuwa nafuatiliwa kwa kila ninachofanya yaani unakuwa hauna siri mambo yako yote watu wanataka wayafahamu ila ndio hivyo tumeshazoea na ndio maisha niliyochagua kuishi.

BC: Kama mtu maarufu(celebrity), jamii huwa inakuangalia wewe kama kioo chake. Je, wewe kama msanii wa muziki wa kizazi kipya huwa unafanya nini kuhakikisha kwamba unakuwa mfano mzuri wa kuigwa (role model) hususani kwa watoto?

PROF.JAY: Pamoja na kuwa celebrity najielewa kuwa mimi ni role model na pia ni activist (mwanaharakati).Kwa hapa nchini nimekuwa nikitumiwa na UNICEF kwa ajili ya kutembelea watoto yatima sehemu tofauti tofauti na kutoa misaada na pia kuwapa ujasiri wale wote waliokata tamaa, kuimba nao na kujadiliana nao na kujua mambo gani ya msingi waliyonayo na yapi yanahitaji wasaidiwe. Pia nilipelekwa ETHIOPIA Kwenye mkutano wa AFRICAN DEVELOPMENT FORUM ambao mheshimiwa KOFFI ANNAN aliutumia kuja kuwaaga na kusema asante kwa waafrika kwa kumsupport. Nilikuwa mmoja wa wasanii waliopeform katika bunge la Afrika mbele ya viongozi wakuu wa Afrika akiwemo Mr.Annan.Pia nilipata nafasi ya kujumuika na vijana wenzangu wa Afrika katika kongamano lililoitwa PAN AFRICAN YOUTH FORUM lililofanyika mjini Nairobi- Kenya na mgeni wa heshima kuwa Rais mstaafu wa Zambia, Keneth Kaunda.

Hivyo basi kutokana na hayo yote naamini kwamba kama mwanamuziki nahitaji kujifunza mara kwa mara na pia natumia nafasi nizipatazo kujumuika na wenzangu kuonyesha uwezo wangu na kuchukua mema yafanywayo na wenzangu. Jitihada zangu bado zinaelekea zaid ktk vita dhidi ya unyanyaswaji wa watoto,wakinamama, ajira kwa vijana na vita kali dhidi gonjwa hatari la ukimwi.

BC:Hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa wasanii wengi wa Bongo Flava kujiingiza pia katika uigizaji wa filamu (actors na actresses). Je una mpango wowote wa kufanya hivyo pia? Nini maoni yako kwa ujumla kuhusu wasanii kuwa pia waigizaji?

PROF.JAY: Nimeshauriwa na watu mbali mbali kujiingiza katika masuala ya uigizaji wa filamu ila bado natafakari maana sipendi kufanya maamuzi kwa kukurupuka. Kwa hiyo bado sijaamua kujiingiza huko. KINGINE ni kuwa kama una vipaji ni vyema ukavionyesha inaweza kukusaidia kuongeza kipato zaidi. Unaweza ukawa kwenye uigizaji ni mzuri zaidi kuliko kufanya muziki, huwezi jua. Angalia watu kama ICE CUBE, WILL SMITH au STICK FINGAZ kwa sasa wanafanya vizuri zaidi kwenye filamu kuliko muziki. Kwa hiyo nigependa na wasanii wa Bongo wajaribu. Kama mtu anajiona ana uwezo wa kufanya muziki na uigizaji atuonyeshe kiwango. Pia uchezaji wa filamu umeonekana kufanya vizuri kwa sasa na kwa kweli naamini huko mbele watakwenda mbali zaidi kwani kwa sasa hata mimi binafsi wameniteka na kuwa mmoja wa mashabiki wao na mwangaliaji mkubwa filamu za kibongo. Hata hivyo, jambo moja ambalo ningependa kuwashauri ni kujenga umoja zaidi kwa kushirikiana na wasanii wenzao wa mataifa mbalimbali.Pia wajitahidi kupigania haki zao, na mwisho waongeze ubunifu zaidi ili waweze kuongeza changamoto zaidi katika sekta hii ya uchezaji FILAMU.

BC: Kama msanii ratiba yako kwa ujumla ni ngumu kwa maana ya kwamba mara nyingi upo safarini (tour), studio ukirekodi, ukitunga mashairi, kufanya mahojiano kama haya nk.Huwa unapata muda wa kuwa na familia yako?

PROF.JAY: Suala la ratiba kwa wabongo bado ni tatizo kubwa maana unaweza ukapanga muda kupumzika ukajikuta unaitwa kwa kazi sehemu au ukawa na kazi sehemu promota akakwambia wameisogeza mbele au nyuma. Kwa hiyo suala la kupanga mambo linakuwa gumu ila hivyo hivyo inabidi twende na mazingira yetu. Kwa kweli inafikia kipindi huioni familia yako hata kwa miezi sita kitu ambacho kwa kweli kinaumiza sana hasa ukizingatia mwanangu mpenzi LISA bado mdogo na mara kwa mara hamwoni baba.Anyway, ndio maisha.

BC: Unatoa ushauri gani kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye masuala ya muziki au kufikia ulipo wewe hivi sasa?

PROF.JAY: Uvumilivu ndio siri kuu ya mafanikio, nadhani wanakumbuka hata ROMA haikujengwa kwa siku moja.Naamini kama unacho kipaji unacho tu hata wafanye nini na riziki ya mtu haipotei labda itacheleweshwa tu ila kama ipo ipo tu.Kwa hiyo kama kweli wana vipaji wasikate tamaa na waongeze juhudi ipo siku isiyo na jina milango yao itafunguka tu wafanye kazi zao kwa ufanisi na malengo pia wazingatie ushauri wanaopewa na waliowatangulia naamini watafanikiwa tu.

BC: Nini mtazamo wako kuhusu Bongo Flava kama chanzo cha ajira kwa vijana?

PROF.JAY: Hili lipo wazi kama vazi la kahaba. Nadhani wengi wetu tunaelewa kwamba hivi sasa tuna vijana wengi tu ambao kwa sasa ni wanamuziki wa bongo fleva ambao hapo kabla walikuwa wamepotea kabisa kimaadili. Wengine walikuwa wazururaji, wezi, na hata majambazi. Lakini muziki huu umewaokoa na hivi sasa wengine wamekuwa wazazi na walezi bora kabisa wa familia zao. Wengine wanawasomesha na kuwatunza ndugu zao na wengine wakijisomesha wenyewe na kufungua miradi mbalimbali ya kuendeleza gurudumu la maendeleo. Kumbuka kuwa ndani ya bongo fleva kunatoka ajira kwa wanamuziki wenyewe,mameneja wao, madj, wachoraji wa banners,wabandikaji wa matangazo, walinzi wa milangoni(bouncers), wacheza show,wahudumu wa ukumbini na mapromota. Pia kumbuka kuwa waandaaji wa matamasha ya bongo flava wanachangia sana kodi kwa kulipa vibali kadha wa kadha manispaa zinazohusika na kuchangia pato la serikali yetu katika kila tamasha linalofanywa nchini.

BC:Je una mipango ya kutoa albamu hivi karibuni? Kama ndio lini na mashabiki wako watarajie nini kipya ndani ya albamu hiyo?

PROF.JAY: Ndio, nimekamilisha kurecord album yangu ya nne inayokwenda kwa jina la ALUTA CONTINUA nikiwa na maanisha kuwa mapambano bado yanaendelea. Ni album iliyojaa maneno ya kimapinduzi na kuwapa watu CHAKULA CHA UBONGO. Ina nyimbo 14 na inategemewa kuingia sokoni mnamo mwezi wa nane mwanzoni, nimeirecord studio tofauti ili kuweka ladha tofauti ikiwemo Wow pow records ya Holand, NO End entertainment ya Uganda, Musyoka – Kenya, mandugu Digital – Kenya, 41 records- tz, Kama Kawa records-tz, Mj production-tz na Bongo recods. Pia nimewashirikisha wasanii mbalimbali kama vile Nonini wa Kenya, Cleptomaniac wa Kenya, Jose Chamilione wa Uganda, kwa Tanzania wapo Juma nature, Salu T, Fid Q, na mdogo wangu wa mwisho KOLIHOMBI. Inatisha kwani ni album niliyoipika ikapikika watu wakae mkao wa kula kwani kengele imeshalia.

BongoCelebrity info: Ndivyo Sivyo ni single ya Professor Jay inayotamba hivi sasa.Imo kwenye albamu mpya anayotarajia kuitoa.Amemshirikisha Jose Chameleone kutoka Uganda.

 

BC: Kama binadamu yeyote kuna wakati unafikia unahitaji mapumziko.Wewe hupendelea kufanya nini unapokuwa mapumzikoni?

PROF.JAY: Mimi napendelea sana kusikiliza muziki, kucheza basketball, Football na Boxing.

BC: Usingekuwa mwanamuziki unadhani ungekuwa nani hivi sasa?

PROF.JAY: Ningekuwa somewhere tu nikifanya kazii za halali kabisa ili niweze kuisaidia serikali yangu katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya taifa langu tukufu.

BC: Asante sana Prof Jay na tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.

PROF.JAY: Big Up BongoCelebrity.Ahsanteni sana.

Kwa habari zaidi kumhusu Professor Jay unaweza kutembelea www.professorjay.net

Picha zote kwa niaba ya Ahmad Michuzi wa michuzijr.blogspot.com

Advertisements
 

30 Responses to “ALUTA CONTINUA-PROFESSOR JAY”

 1. D.A Says:

  Nice Interview !!!
  Prof Jay, I still think he is the King of Bongo Flava… Lazima hawa rappers wengine wajifunze ku-Rap vizuri (in terms of rhyming) na kuongelea mambo ambayo yanaeleweka… Maana hawa rappers wengine huko Bongo hata sielewi wanachokiimba ??
  Keep up the good work Prof…..

 2. Lulu Says:

  Hi This is nice interviw. Jay is one of my favourite rapper in Tanzania. He is really and I love about that. keep it up Professor Jay.

 3. Latembe Says:

  Profesor jay good interview keep it up.

 4. kokoriko Says:

  Duu hii ni ukweli mtupu. Asante sana Jay kwa kusema ukweli, inabidi hawa ma dj waambiwe ukweli kwani sisi underground hapa tunapata taabu sana na hawa madj. Asante kwa ku present.

 5. kaka Says:

  Hii ni best interview ya hapa. Maswali ya Jay yametulia sana na ameyajibu vizuri sana. Mti mkavu unafanya kazi nzuri sana ya kuelimisha jamii. Nakuzimia ile mbaya. Sifa yako inayojulikana sana Bongo ni Kinywaji, vipi unafikiria kupunguza??? Kwani kinaweza kukuaribia kipaji chako bure.. keep it up. good job Dady.

 6. peter Says:

  Hii interview imenifundisha mengi sana kuhusu muziki wa Tanzania, sikujua kama wahindi tuu ndio wanao distribute muziki wa bongo flavour, na hawa madj ni dj njaa, poleni sana wanamuxziki wetu. Na mimi nasisisitiza sana watu kama kina Kinje mnajulikana mna pesa, jaribuni basi mjaribu kunyanyua huu mziki kwa ku invest in it. Na kwa Kikwete, unatafuta wawekezaji nchini jaribu kuangalia kam kuna watu wangependa ku invest in music, kwani watasaidia vijana wetu.

 7. Kibure Says:

  professor Interview yako bomba, lakni ningependa kukupa ushauri mmoja tu, najua wewe ni mtu mwenye kipaji, na unakitumia vizuri kipaji chako, tunaelewa kwamba mnataka kuwa kama kina Jay Z, P didy na wengine, ila tu tofauto ni kwamba mnaimba kiswahili, sasa ushauri wangu mimi unakuja hapa, jaribu sana kuwashauri wenzako wajaribu kuvaa nguo zetu, watumie madi signer wetu na utamaduni wetu, kama vile kuweka ngoma katika nyimbo zetu na kucheza michezo kama vile sindimba ili tuweze kudumisha utamaduni wetu. Sasa ninyi ambao mnaweza ku present Tanzania nchi za nje mnaimba na kuwaiga watu wa nje, je hawa watu wa nje watataka kweli kuja kwenye perfomers zenu kama unakuja pale kuimba kama Jay Z? si Bora nikamuone Jay Z. Na kwa wale ambao hawajui hata kiswahili, kwanini waje kuona P didi wanna Be instead of the real P didy? Sasa jaribu sana mtu wangu kuburisha utamaduni. Una power hiyo prof kama hujui.

 8. BongoSamurai Says:

  Profesor Jay aminia mtu wangu.Kweli ALUTA CONTINUA.Interview yako bomba sana umetumia maneno kama mwana falsafa halisi.Endelea kuelimisha jamii na hasa vijana ambao ndio kizazi cha bongofleva.Kazi yako imeonekana na sasa hata wazee wanaikubali bongofleva.Binafsi ni ule wimbo wa CCM na CUF unanikuna sana.Nasubiria kwa hamu your new album.
  Big up ma men.

 9. Miss. Says:

  Bongo celebrity kazi nzuri. Professor unaonekana ni mtu mwenye hekima ana una akili zako. keep it up. Tunaomba na wewe ujaribu kujiingiza kweny siasa ili vijana waweze jusikika na vilio vyao. Amina ndio tushampoteza tena, tunaitaji watu kama nyinyi bungeni.

 10. deo cashmoney Says:

  Well I don”t know much PJ music,but I saw one song from him about Ukimwi.nazani nyimbo inasema hapa nilipo niko kitandani,starehe zimeniweka matatani.thats shit hot.I think his okey.

 11. omary mussa Says:

  jay the best lyrical MC to bless bongo ever excluding nobody. hands down

 12. maombi kisenya Says:

  bro mambo yako makubwa kaza msuri kaka

 13. amina Says:

  mi namwambia jay apunguze kula kitimoto pale baa ya kivulini kijitonyama….uso unameremeta hivyo mh

 14. Kells Says:

  Sup jay!
  Nakukubali mtu wangu,Interview imetulia.IQ yako babu kubwa, the way umejibu maswali ina impress.
  Keep it up Bro

 15. majaliwa obeid Says:

  hi prof…i love your song so sick i wish we can raper together

 16. majaliwa obeid Says:

  Nakwambia mizizi yako iko fresh sio kama yawengine the part i like is when you puts the stories is song. Uwe na amani kirasiku

 17. kYARO Says:

  meeen u hit, no doubt,
  u have scored me.
  keepitup

 18. shefa Says:

  prof tupo pamoja aminia!! Sagwa investments inamalizia taratibu za tour yako ya USA. USIKONDE

 19. Yannick Boris Says:

  Ebwana ee nimefurahi kusikiliza interview ya msaani wa east africa me mtoto wa Kigali tazama mberre bbabba yangu tuko pamoja aata na mimi nakungoja am sure even akon will buy your CD like you do!

 20. james Says:

  this man is not!yaani namaanisha kwamba anatisha,ujumbe aliyoutoa kwa wasanii wa kubwa pamoja na wanaochipukia ni mzuri kwa sababu unawajenga ili nao wafikie ilipofika yeye(DADY)kama anavyoitwa na madhabiki,big up to you moderetor for give us this interesting interview of THE HEVY WEIGHT MC

 21. Tamim Says:

  I know u daddy, u,ve got big IQ. keep it up. Also dont forget to meditate.

 22. Chentro Says:

  Hi my Brother?

  my name is Chentro
  from Rwanda
  Prof. Jay i love you so much!!!!!!!!!!! and your song!!!!!!!!

  Thanky you very much

  Cheers

  Chentro

 23. max mushy Says:

  yeah man,jay you are the best raper in tanzania.There your songs in your album J.O.S.E.P.H you didnt release them like wapi nimekosea and nisamehe.I really love these songs.About your interview kaka huwa hukosei coz you got big IQ KEEP IT UP.I will the first to buy your album Aluta continua.Stay blessed bro.

 24. Chego Says:

  You r the winner m2 wngu we nimkali na umesmama aachana na wa2 wa majungu.keep it p m2 wngu.

 25. samwel mdalingwa Says:

  Moja kati ya wasanii wa bongo ambao kila wakitoa kazi au albam kwa ujumla lazima nidake original copy ni wewe,keep it up bro. with more efforts I really feel your music,
  it’s me SAM from tegeta mbweni masaiti.
  ONE LOVE

 26. peter Says:

  nakupongeza kwa burudani nzuri jiahidi man wanasema wa kwanz atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakua wa kwanza g.day.

 27. jose watano Says:

  nakukubali mtu wangu toka ablam yako ya kwanza mpaka hii ya sasa ushauli kaza buti na kama vipi achia wimbo wako wa naahidi ulioimba na mez b kwani mkali kinoma mtu wangu ni hayo tu jay forever

 28. Matunda Edo Says:

  ni me itwa kwa jina la Matuda Edo jani niko mwana shule la kuu mudji kuu kinshasa,

  Na furayi sana kuhona Si te ya Professor Jay , yani mimi ni ko mucongomani na fataka sana musiki la professor jay kwenie internet lakini tu ko na lazima sana ya ma lyrics za ma wimbo kama (sio – mzee, ndio mzee na zengine.)

  akisanti

 29. HAKUNA UBISHI JAY UNATISHA WENGINE WANAIGA KWAKO

 30. abdul Says:

  prof. wee ni noma yaani unatisha ile mbaya kama hip hop wendiye uliye kubalika sana endelea na makamuzi hayo kasi ile ile yaani kama usemavyo wewe mwenyewe kwamba alta continous mapambano yanaendelea


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s