BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

THE NGOMA AFRICA BAND July, 6, 2007

Filed under: Muziki — bongocelebrity @ 7:32 PM

 

Kila wanapotokea jukwaani katika maonyesho yao mbalimbali, mashabiki hulipuka kwa mayowe, miruzi, makofi na vigelegele. Wanapoibuka huwa wamevalia mavazi ya kiafrika bila kusahau bling bling kibao za kutoka Afrika. Wamekuwepo kwenye medani ya burudani kwa zaidi ya miaka 14 sasa. Wanasema wawapo jukwaani kazi yao huwa ni moja tu; kuwapa wapenzi wa muziki burudani isiyo na mfano jambo ambalo huwatia kiwewe wahudhuriaji wa kila onyesho lao.

Hawa si wengine bali watanzania, The Ngoma Africa Band,bendi maarufu barani Ulaya yenye makazi yake huko Oldenburg nchini Ujerumani. Wamekuwepo kwenye medani ya muziki huku wakitingisha katika majukwaa ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 14 sasa.

Kiongozi wa bendi hii ni mwanamuziki nyota Ebrahim Makunja a.k.a Ras Ebby Makunja au kwa jina lingine maarufu Bwana Kichwa Ngumu mwimbaji na mtunzi mchokozi.

 

Hivi karibuni walifanikiwa vilivyo kuzikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliposhiriki na kufanya onyesho la kufa mtu huko Hamburg, Ujerumani katika tamasha maarufu lijulikanalo kama Africa Market.

 

Wakati maonyesho ya Saba Saba (7-7-2007)yatakapokuwa yanafikia kilele nchini Tanzania, The Ngoma Africa Band wao watakuwa wakifanya vitu vyao katika sehemu maarufu ya mabwanyenye “WOYTON” .Baada ya hapo tarehe 11th August 2007 watakuwa jijini Frankfurt ambako wamealikwa katika tamasha maarufu la “African and Carribean Music Festival”.

Katika picha mwenye rasta ndiye kiongozi mkuu na muasisi wa The Ngoma Africa Band, Ebrahim Makunja a.k.a Ras Ebby Makunja au Bw.Kichwa Ngumu (mtunzi na lead vocalist). Mwenye kilemba cha njano ni Said Vuai a.k.a Prince Jazbo Vuai.(mpiga bass guitar). Mwenye shati jeupe la maua ni Christian Bakotessa a.k.a Chris-B (mcharaza solo guitar). Mwenye shati la njano, mnene kidogo ni Musa Boujang a.k.a Al-Hajj Musa (mpiga tumba {drum}.

Unaweza kusikiliza baadhi ya nyimbo zao katika www.myspace.com/thengomaafrica

Una swali ungependa kuwauliza The Ngoma Africa Band? Tuandikie bongocelebrity@gmail.com

Shukrani Msema Kweli wa pale Bremen kwa taarifa hizi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements
 

8 Responses to “THE NGOMA AFRICA BAND”

 1. Teri Mashaka Says:

  This is the way to go guys.Whenever I see Tanzanians representing our country, our culture,traditions and our humanity, my heart is filled with joy!Big up The Ngoma Africa Band.

 2. Hassan Says:

  He!eh Naona sasa kazi hipo!jamaa wamejitaidi kiasi kikubwa,naukubali mdundo wao ni mzito na sio mziki wa kitoto

 3. Vicky Mwaipopo Says:

  The beat is to hot!Make crzy!but I very proud to see
  guys like this,may other musician’s will follow suit

 4. Vicky Mwaipopo Says:

  The beat is to hot!make me crazy!but I am very proud to see guys like this……

 5. Janet Kimario Says:

  Hii!!!!!!!Tamu!!mmmm!!!!!mziki wa bongo mtamu jamani!!!hivi beat zao !!mbona kali sana vichaa wetu,kazi kubwa wameifanya!nakubali beat zao sio mchezo

 6. Kulwa Says:

  HIVI?WANAMZIKI UWA MNALALA SAA NGAPI?AU NDIO HALIKI ZENU ZIMEDATA KUTOKANA NA KUKOSA USINGIZI,MAANA NIMEJARIBU KUWAFATILIA NAONA LATIBA ZENU !MNAPELEKWA MCHAKA MCHAKA NA MAPOROMOTERS KAMA KISHADA?

 7. Kulwa Says:

  HIVI?WANAMZIKI UWA MNALALA SAA NGAPI?AU NDIO HAKILI ZENU ZIMEDATA KUTOKANA NA KUKOSA USINGIZI,MAANA NIMEJARIBU KUWAFATILIA NAONA LATIBA ZENU !MNAPELEKWA MCHAKA MCHAKA NA MAPOROMOTERS KAMA KISHADA?

 8. Mzee wa Holland Says:

  Washikaji zangu mie nawazimia sana
  mlivyo litangaza jina la Tanzania kimziki moto wenu makali


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s