BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

USIPIME July, 17, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki — bongocelebrity @ 7:29 AM

 

Miaka sita iliyopita wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania walianza kuisikia sauti yake redioni na baadaye kumuona kwenye luninga. Single yake ya kwanza iliyomuingiza kwenye ulimwengu wa muziki iliitwa “Sogea Karibu”. Hivi sasa anatambulika kama Black Rhino aka The Dan Dada.

Black Rhino ambaye pia ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Sokoine mjini Morogoro akisomea shahada ya kwanza katika masomo ya biashara ni mdogo wa kuzaliwa wa msanii mwingine maarufu wa bongo flava, Professor Jay ambaye tovuti hii ilifanya naye mahojiano hivi karibuni.

Ndani ya mwezi huu wa saba, anatarajia kuingiza sokoni albamu yake ya kwanza itakayokwenda kwa jina USIPIME. Itasheheni nyimbo si chini ya kumi.Wasanii aliowashirikisha ni kama Dully Sykes, Noorah,Hard Mad,Fatma,Q Chief,Chidi Benz,Producer Lucci,Enika,na wengine wakali kibao. Albamu imetayarishwa kwenye studio za Mandugu Digital chini ya producer Ambrose kwa kiasi kikubwa. Baadhi ya miziki imepikwa katika studio za Bongo Records.

Hizi hapa baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hii mpya;Wa kwanza ni Usipime wa pili Mistari.

Advertisements
 

7 Responses to “USIPIME”

 1. k Says:

  Well Kijana kwa kweli ana Talent!!!

 2. Moses Kaale Says:

  Mimi sio mpenzi sana wa bongo flava kusema kweli.Lakini jinsi ambavyo hii website inaandika habari zake inanifanya niupende muziki huu.Nimeusikiliza huo wimbo usipime kwa makini na nakiri kuna mantiki sana ndani yake.Asanteni bongocelebrity,tafadhali endeleeni hivyo hivyo.

 3. Kimanumanu Says:

  Big up kijana ila punguza pozi ma’ke tangu uuhisi usupastaa unaona umepanda sana bei we komaa na shule bongofleva itakujengea jina tu ila hailipi kwa muda mrefu we si unawaona akina Mr.N..e walivyochoka leo wakati ni juzi tu jamaa alikuwa juu balaa na kujiona ameliteka soko na anawezafanya lolote kazi yake ikakubalika.Komaa na shule mdogo wangu ndo maisha yako yapo hapo.

 4. Nerra Says:

  Nasisitiza ujali na utumie muda wako mwingi kusoma kuliko muziki ingawa ni fani yako lakini msanii bila elimu baba ni kazi bure, unaonaje ukiwa na PHD yako alafu ni msanii unayewika utakua juu mshikaji sio mchezo.

 5. Chinga Says:

  Safi sana Kijana ..Big Up Rhino!!!

 6. kenge Says:

  Black Rhino’s USIPIME is one of the best bongo flava rhymes ever. This guy is seriously talented and would like to hear more hits like USIPIME

 7. SNIPER Says:

  unafanya vema but unaonekana kama muuza sura fulani tofauti na profjize he is talented yaani bila huyu wewe tusingekujua”cyoishu”napenda hii track yako ya kula maisha nimeipenda sana sababu hata mimi nikichaluka nikikumbuka vimeo nilivyokula peku aaaaaaaaaah naponda maisha tu nakamua hata m kwa wiki.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s