BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“MENGI YASEMWAYO NI UONGO”-RAY C July, 23, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki — bongocelebrity @ 11:53 PM

Inasemekana ndiye msanii wa kike mwenye mvuto kushinda wote Afrika Mashariki. Jina lake halisi ni Rehema Chalamila. Wapenzi wa muziki wake wanamtambua zaidi kwa jina Ray C. Ndio kwanza una umri wa miaka 25. Jina lake lilianza kuvuma alipokuwa mtangazaji redioni kabla hajaamua kuingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki,sio tena kama DJ bali muimbaji/mwanamuziki. Ingawa anasema angependa watu wausikilize na kuucheza muziki wake zaidi ya kuongelea uchezaji wake awapo jukwaani(viuno), ukweli unabakia kwamba Ray C ni mmojawapo wa entertainers wazuri jukwaani.Hivi karibuni BongoCelebrity ilifanya naye mahojiano yafuatayo. Katika mahojiano haya Ray C anazungumzia historia yake kimuziki toka utotoni mpaka alipo hivi sasa,mipango yake ya baadaye na kama lengo la BongoCelebrity anatoa ushauri kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye fani ya muziki.Pia anaweka wazi swali je alishawahi kuolewa? Na nani?

BC: Wengi tunafahamu kwamba historia yako ya muziki ilianzia ulipokuwa unasoma katika shule ya Kabojja iliyopo nchini Uganda.Lakini kwa vyovyote vile hukuanza kuusikia muziki ulipokuwa nchini Uganda bali tangu utotoni.Unakumbuka ni wanamuziki gani uliwahi kuwasikia aidha sifa zao au muziki wao ulipokuwa mdogo? Je walikuwa na mchango wowote katika uamuzi wako baadaye wa kuingia kwenye muziki?

RAY C: Kama mtoto mwingine yeyote anayezaliwa nchini Tanzania, nilipokuwa mdogo nilikuwa napenda kusikiliza muziki. Wanamuziki wa hapa nyumbani ambao nakumbuka nilikuwa napenda kuwasikiliza ni wengi lakini wanamuziki kama Bi.Shakira (mwimbaji wa taarabu) na Remmy Ongala nilikuwa napenda zaidi kuwasikiliza.Nilikuwa napenda sana kumsikiliza Bi.Shakira kwa sababu nilikuwa napenda sana miziki yenye mahadhi ya taarabu hivi.

Lakini pia nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo za kihindi na pia kuangalia sinema za kihindi. Nakumbuka utotoni nilipokuwa nikitoka tu shule nikifika nyumbani ni kuweka mikanda ya sinema za kihindi. Nilikuwa sio msikilizaji mzuri sana wa redio kipindi hicho. Nakumbuka nilichokuwa nakifanya wakati nikiangalia sinema za kihindi ni kwamba wanapofikia tu sehemu ya kucheza (unajua tena movie za kihindi,kila baada ya action fulani,muziki unafuata) nachukua kalamu na karatasi naandika wanachoimba kwa kiswahili,kama ninavyosikia. Ilifikia mahali ikawa mtu akiniambia niimbe wimbo fulani wa kihindi nauimba wote lakini bila hata kuelewa maana yake.Ingawa sikujua wakati huo,kumbe ndio taratibu nikawa najifunza uimbaji.Nadhani ndio maana hata hivi leo,ukisikiliza vizuri baadhi ya nyimbo zangu utasikia zina baadhi ya vionjo au mahadhi ya kihindi hivi.

BC: Kabla hujaamua kuwa mwanamuziki ulikuwa mtangazaji redioni au DJ. Huwa unamiss kazi yako ya utangazaji? Kama ndio unamiss nini?

RAY C: Ni kweli, wakati mwingine namiss utangazaji.Pengine simiss utangazaji kama kazi lakini namiss ile kuwa studio na kupiga nyimbo fulani fulani ninazozipenda. Pia namiss ule uhusiano unaokuwepo baina ya mtangazaji na wasikilizaji wake. Kama unavyojua baadhi ya wasikilizaji huwa wanatokea kupenda kipindi fulani kutokana na aidha aina ya miziki inayopigwa au mtangazaji mwenyewe. Kama utakumbuka wakati huo mimi nilikuwa ndio DJ pekee mwanamke nchini Tanzania. Kwa hiyo wakati mwingine namiss utangazaji lakini sema tu kwa sababu muda unakuwa hakuna na mambo ni mengi hivyo inakuwa hakuna jinsi.

BC: Ulipokuwa mtoto uliwahi kuota kwamba siku moja utakuwa msanii maarufu kama ulivyo hivi leo?

RAY C:Hapana sikuwahi kabisa kuota. Lakini nadhani kwa ujumla uanamuziki ndio ilikuwa ndoto yangu maishani ila nilikuwa sijui tu nianzie wapi. Hii inatokana na ukweli kwamba nilikuwa napenda sana mambo ya muziki kama nilivyosema hapo juu.Yaani mimi mwenyewe kuna wakati nashangaa kwamba nipo hapa nilipo hivi sasa.

BC: Kuna mtu yeyote unamkumbuka alikushawishi uingie kwenye muziki?

RAY C: Kuna watu wawili watatu ambao walinishawishi kuingia katika muziki.Lakini sana sana ni Ruge Mutahaba ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa meneja wangu pale Clouds FM. Nakumbuka mara nyingi kila baada ya kumaliza kufanya kipindi changu redioni alikuwa akinisikia nikiimbaimba kwenye corridors za pale ofisini na ndipo akanishauri kama ninapenda kuimba na ningependa kurekodi basi nifanye mazoezi zaidi ya uimbaji, nitafute mtu aniandikie wimbo au niandike mwenyewe niingie studio kurekodi japo single moja kwanza na kisha kama itakuwa nzuri basi yeye angenisaidia kurekodi albamu nzima.

Mtu wa kwanza kuniandikia wimbo akawa ni Patricia Hillary wa JKT Taarabu,yeye ni mwanamuziki wa taarab. Nilikuwa nataka niingie kwenye viwanja hivyo .Aliniandikia wimbo wa Mapenzi Yangu ambao ndio ulikuwa wimbo wangu wa kwanza kutoka kwenye albamu yangu ya kwanza. Wakati huo Ruge tayari alikuwa na kampuni ya Smooth Vibes ambayo ilikuwa na wasanii kama vile Banana Zoro, Lady Jay Dee na wengineo.Huo ndio ukawa mwanzo wa safari yangu hii ya muziki.

BC: Urembo ulionao ni mojawapo ya mambo muhimu katika fani ya muziki.Nini siri ya urembo wako?

RAY C: Hamna kitu chochote kwa kweli.Kwanza mimi ni mvivu sana wa mazoezi.Sipendi kabisa mazoezi ingawa inabidi kwa sababu miaka inaenda kwa hivyo inabidi kufanya mazoezi ili nijiweke fiti. Pengine mazoezi ya viungo yatokanayo na mazoezi katika choreography na pia kujitahidi tu kutunza afya. Lakini muhimu labda ni ndivyo nilivyozaliwa tu.

BC: Jamii mara nyingi huwa inakuwa na tafsiri yake juu ya msanii yeyote ukiwemo wewe. Tafadhali chukua nafasi hii tafsiri yako binafsi kwa namna unavyojiona mwenyewe.

RAY C: Kwa watu ambao wanaonijua na hata wale wasionijua, mimi bado ni Rehema.Ray C ni jina nililolitunga tu.Jinsi nilivyozaliwa na jinsi nilivyokuwa na mpaka nilivyo hivi sasa hamna kilichobadilika. Umaarufu haujanibadilisha,mimi ni mtu wa kawaida sana, binadamu wa kawaida tu tofauti na ambavyo watu wengi wanaweza kudhania au wanavyofikiri.

BC: Kama msanii kuna wakati inakuwa vigumu kueleweka katika jamii. Unadhani hiyo huwa inatokana na nini na je wewe ishawahi kutokea ukahisi jamii haikuelewi?Ilikuwaje?

RAY C: Kwa kawaida, kama msanii kuna wakati utaandikwa vizuri na kuna wakati utaandikwa vibaya. Hali kadhalika kuna wakati hutoeleweka. Kwa upande wangu nahisi asilimia 80 wananielewa na 20 iliyobakia ndio hawanielewi. Najua kuna wakati watu wanataka sana kujua jinsi mimi nilivyo na mambo kama hayo.Naelewa. Zaidi najitahidi kufuatilia zaidi kazi yangu ya muziki ambako nadhani wengi wananielewa na ndio maana wanaukabali na kuupenda muziki wangu. Nipo kwenye kazi zaidi ya mambo mengine.

BC: Vipaji viwili vikubwa ulivyonavyo na vinavyotambulika hivi sasa ni kuimba na kucheza. Kati ya hivyo kipi unakiona ni kigumu zaidi kukiendeleza; kuimba au kucheza?Na kwanini?

RAY C: Hapa ningependa kuweka wazi jambo moja muhimu. Mimi ni mwanamuziki na sio mcheza show.Show ni sehemu tu ya kazi yangu.Kwa maana hiyo ningependa zaidi kujulikana kama mwanamuziki na sio “kiuno bila mfupa” kama ninavyojulikana miongoni mwa wengi.Hiyo imetokea tu kwa sababu I am an entertainer.Kwa hiyo nimebuni tu vitu vyangu ili kuboresha kazi zangu na kwa sababu najua huwezi kusimama tu kwenye stage kama mti. Ningefurahi zaidi kama watu wangesikiliza na kucheza zaidi nyimbo zangu kuliko kuconcentrate zaidi kwenye viuno. Kwa hiyo nadhani vipaji vyote ni muhimu.

BC: Katika baadhi ya mahojiano uliyowahi kufanya siku za nyuma ulikaririwa ukisema mambo yafuatayo; huna rafiki wa karibu (best friend) na kwamba unapendelea zaidi kukaa peke yako. Ukizingatia kwamba miaka kadhaa imepita tangu ukaririwe ukisema hivyo, mashabiki wako wangependa kujua bado una msimamo ule ule au mambo yamebadilika?

RAY C: No comment. Kwa sasa sidhani kama ningependa kuongelea mambo yangu binafsi mbele ya kadamnasi.

BC: Waandishi wengi wa habari wamekuwa wakilalamika kwamba hupendelei kuongea na vyombo vya habari na zaidi kuongelea habari zako binafsi mara kwa mara.Kuna ukweli wowote katika hilo?Kwanini?

RAY C: Unajua kama mwandishi akinifuata kwa habari za maana nitamsikiliza. Lakini akinifuata kwa habari ambazo hazina uhakika na hazina maana, siwezi kufanya naye interview.Kwa hiyo wanaolalamika wanajua wanachokifanya na ndio maana sipendi kufanya interviews nao. Interview za kazi naweza nikazifanya.Lakini interview zenye vitu ambavyo ni binafsi, vya ndani vitu ambavyo hata yeye mwandishi vingekuwa vinamhusu yeye asingethubutu siwezi kuzikubali.Kwa hiyo muda mwingi nakataa kwa vitu ambavyo nahisi havifai. Kama ni kazi, kuhusu kazi yangu nitaongea,siwezi kukataa kwa sababu najua hiyo ni sehemu ya promo kitu ambacho ni muhimu kwa msanii yeyote yule.

BC: Ukitizama nyuma, tangu ulipoingia kwenye fani ya uimbaji muziki, kuna mabadiliko yoyote katika muziki wako, mashairi yako na ala unazotumia katika muziki?

RAY C: Yeah kidogo naingia kwenye ujana zaidi.Unajua mimi nilianza na nyimbo za zouk zouk hivi yaani za watu wazima. Kwa hiyo sasa nachanganya zaidi,yaani kuna ujana kidogo na utu uzima pia.Kwa mfano katika hii albamu yangu ya Sogea Sogea ukiisikiliza kuna nyimbo kama tano hivi zenye hadhi ya kiutu uzima halafu kuna nyimbo za clubs (club songs) mahsusi kwa vijana. Kwa hiyo nimebadilika kidogo na kuchanganya ili kuburudisha watu wa rika zote au kuweka kwenye mahadhi tofauti.

BC: Umaarufu ni jambo linalopita. Wakati mwingine huwa unapita kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa. Leo uko juu kesho uko chini. Je ukweli huu hukutia woga wakati mwingine na unafanya nini ili kuendelea kuwa hapo ulipo?

RAY C: Mimi kwangu umaarufu haunipi shida sana. Ninachoangalia zaidi ni kufanya kazi nzuri ili watu waipende na iweze kuuzika vizuri. Nasema hivyo kwa sababu nadhani ni muhimu zaidi kwa msanii kuwa na kazi nzuri ili hata umaarufu ukipita, vizazi na vizazi vitakavyokuja viweze sio tu kulikumbuka jina lako bali pia muziki wako kama ambavyo imekuwa kwa baadhi ya wasanii wa zamani ambao bado kazi zao zinapendwa na zinasikika hata baada ya wao kustaafu au hata kuaga dunia.

BC: Je tangu uanze shughuli za muziki imeshawahi kukutokea ukajuta kwanini ulijiingiza kwenye masuala ya muziki? Kama ndio nini kilitokea kufanya ujute au utamani usingekuwa mwanamuziki?

RAY C: Siwezi kutumia neno “kujuta”, kwasababu, kuna watu ambao wana vipaji, kama nilichonacho mimi na ambao hawajatoka ingawa wangependa kutoka na kufikia sehemu niliko mimi. Lakini kwa namna fulani kuna freedom fulani unaipoteza unapokuwa msanii au mtu maarufu.Unajua zamani nilikuwa free zaidi kufanya kitu chochote ninachokitaka tofauti na hivi sasa ambapo jamii inakuangalia na kufuatilia kila unachokifanya. Kama binadamu yeyote kuna muda kama unataka kutoka hivi na rafiki zako ama mtu wako ili uienjoy na mambo kama hayo lakini mapaparazi wanakuwa wamekuzunguka kila sehemu.Unafanya kitu leo kesho kishaandikwa gazetini.Uko sehemu umekaa tuu labda unapiga story kesho ipo gazetini.Kwa hiyo mara nyingine unakuwa na uwoga fulani hivi ambao saa nyingine unaboa kwa kweli.Kwa ujumla unakuwa huenjoy kama ambavyo mtu wa kawaida anavyoweza kuenjoy.Lakini ndio maisha.

BC: Wanaume walio wengi hutamani sana kuwa na mpenzi kama wewe. Kwa maana hiyo vishawishi vingi huelekezwa kwako. Je huwa unakabiliana vipi na vishawishi hivyo?

RAY C: Vishawishi vipo, lakini kwa mtu kama mimi katika umri wa miaka 25 nilionao tayari ni mtu mzima, hivyo najua ninachokitaka na ninajua vishawishi vibaya na vizuri. Kwa hiyo vitu kama hivyo vinapita, tumeshazoea ni maisha ya kawaida tu. Ila Mimi sipendi mtu anifuate kwa ajili ya umaarufu wangu. Ningependa mtu yeyote anichukulie kama Rehema tu.Mapenzi ya kweli sio tena kwa ajili ya umaarufu ingawa hiyo ipo sana tu na ndio maana wakati mwingine mtu unaamua tu utulie peke yako, maana unakuwa huna uhakika mtu yuko serious ama?

BC: Wakati mwingine mashabiki huwa kama vichaa kwa furaha na hamasa. Unaweza kutuambia kama uliwahi kukumbana na mshabiki ambaye alikuacha hoi bin taabani kwa “ukichaa” wake? Ilikuwaje?

RAY C: Matukio kama hayo mara nyingi yanatokea.Siwezi hata kuanza kuviorodhesha. Kwa mfano kama hapa Tanzania unakuwa unazunguka sehemu mbalimbali na kuna watu wengine wanakuwa wanakuona kwenye screen lakini wakikuona mtu live wanakuwa kama hawaamini. Lakini tumeshazoea kwa sababu hata ingekuwa mimi nikimuona msanii ninayemzimia live ningekuwa na furaha.Ila mtu kama mimi vitu kama hivyo havinisumbui sababu ni najua hao ni mashabiki(fans) tu na sisi bila mashabiki hatuwezi kuwa tulivyo na ndio tunaowategemea wao zaidi.Kwa hiyo wakija wafurahi, ili mradi mtu asikuumize au asikujeruhi. Shabiki akija kwenye show mna enjoy mnaongea, piga picha nk.Hivyo ndivyo vitu tunavyofifanya kila siku.

BC: Msanii mara nyingi huwa ni kioo cha jamii inayomzunguka. Kwa hiyo siku zote anatarajiwa awe mfano wa kuigwa (role model). Unaliongeleaje suala hili?

RAY C: Kwa kweli kama msanii, kama tulivyoongea hapo mwanzo, ni kioo cha jamii. Kwa hiyo huwezi kufanya vitu vya ajabu ajabu kwani watu wanakuangalia, kuanzia watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwa hiyo kwa upande wangu najitahidi sana kuepuka vitu vya ajabu ajabu mbele za watu kwasababu najua kwamba macho yote yanakuwa yananiangalia mimi ninapokuwa sehemu yeyote ile.

BC: Tangu utoe albamu yako ya kwanza mpaka hivi leo ni mambo yepi matatu muhimu ambayo umejifunza? Una ushauri gani kwa vijana wasichana ambao wangependa kufikia hapo ulipo hivi leo?

RAY C: Mambo matatu ambayo nimejifunza katika fani hii ni kwanza uvumilivu.Unajua wakati unaanza fani hii, watu wengi sana wataongea. Wengine watakuambia hujui kuimba, wengine watakuambia hili na lile ilimradi tu kukukatisha tamaa.Kwa hiyo ni uvumiliivu tu. Cha pili ni personality. Kama msanii ni lazima uwe na good personality kwa watu wote ili uweze kama msanii kuuza kazi zako na uweze kukubalika kwenye jamii. Namba tatu ni usikivu.Wasikilize mashabiki wako,wakubwa zako, DJs na wadau mbalimbali wa fani ya muziki.

Kwa hiyo kama kuna vijana wenzangu kama wana plan ya kuingia kwenye muziki ni muhimu wazingatie hayo mambo matatu hapo juu bila kusahau kuweka mawazo yao yote kwenye muziki.Watafanikiwa.

BC: Mwezi wa nne mwaka huu ulitoa albamu yako mpya iliyokwenda kwa jina la Sogea Sogea. Wapenzi wako na mashabiki wako wengi wameshapata fursa ya kuinunua na kuisikia, wengine bado hawajapata nafasi hiyo na hivyo wangependa kujua nini kipya katika albamu hiyo? Umewashirikisha wasanii gani na kama albamu hii ina ujumbe maalumu ni ujumbe gani na ina nyimbo ngapi? Wasambazaji wa albamu hiyo ndani na nje ya Tanzania ni kina nani?

Kama nilivyosema hapo juu katika albamu hii kuna mabadiliko katika aina za miziki, midundo nk.Album yangu ina nyimbo 11.Wasanii niliowashirikisha ni TID katika wimbo Nilikutamani, Dgritty(mdogo wake Loon wa Marekani) katika wimbo Siangalii nyuma, Pfunk katika wimbo Kama Wanipenda,na Nako 2 Nako katika wimbo Kwa Ajili Yako. Wasambazaji wanaosambaza kazi zangu ni Mamu Stores wa hapa Tanzania.

BC: Nje ya nchi ya nchi kama Marekani,Canada na Ulaya je?

RAY C: Huko bado hatujapata msambazaji anaeaminika, naenda kwa ajili ya Tour tu.

BC: Wewe ni msanii ambaye umeshafanya ziara (tour) za kimuziki sehemu nyingi duniani, ndani na nje ya Tanzania, nchi kadhaa za Afrika, Ulaya na Marekani. Unaweza kutuambia umejifunza nini katika ziara zako zote hizo?

RAY C: Kitu nilichojifunza ni kuwa wasanii wa hapa Tanzania inabidi tupeleke kazi zetu huko nje kwa sana tu.Nasema hivi kwa sababu watu wengi sana ambao wanakuja kwenye show zetu wanakuwa hawana original copies za kazi zetu. Wachache sana wanakuwa wana original copies ambazo mara nyingi wanakuwa wametumiwa na ndugu zao. Wengineo wengi wanakuwa wana fake copies,wengine wanazitoa nyimbo kwenye internet tu na mambo kama hayo.Kwa hiyo kama tungeweza kupata wasambazaji wa kuaminika sehemu hizo ingetusaidia sana sisi wasanii na pia kukuza muziki wa Tanzania.

BC: Hivi karibuni unatarajiwa tena kuanza ziara yako ya nchi za nje ambapo kwa mujibu wa taarifa tulizonazo unategemea kuzuru nchi za Ulaya na Marekani. Unawaambia nini mashabiki wako wanaopanga kuja kwenye maonyesho yako katika nchi hizo?

RAY C: Mimi naweza kuwaambia kuwa wakae tu tayari. Kwa wale ambao wananijua na ambao hawanijui na wanataka kuona kazi , kusikiliza kazi zangu, nawashauri waje kwenye shows. Tour inaanza tarehe 28th July 2007 nchini Norway.Itakuwa ni tour ya miezi mitatu ingawa tunaweza kuongeza siku kwa sababu kuna sehemu mbalimbali mashabiki wamekuwa wakituma maombi. Baadhi na nchi Ulaya nitakazo tour ni Uholanzi, Sweden, Ujerumani na UK. Kwa upande wa Marekani mashabiki wangu wa Boston, Washington DC,Ohio, Houston, Dallas, Atlanta, New Jersey na kwingineko wajiandae.

BC: Ungepewa nafasi na kuchagua mwanamuziki yeyote, kutoka sehemu yoyote duniani ambaye ungependa ushirikiane naye kimuziki katika siku za mbeleni ungemchagua nani? Na kwanini?

RAY C: Sasa hivi ambaye namfeel ni Rihana wa nchini Marekani. Napenda jinsi alivyo tu na jinsi anavyoimba. Naamini kwa sababu hizo haitakuwa vigumu sana kushirikiana nae. Mwingine ni Ciara pia wa Marekani.Huyu napenda anavyocheza.

BC: Maisha kama msanii au mtu maarufu mara nyingi huwa yanaenda na wakati mwingine kuvumishiwa au kusingiziwa mambo ambayo siyo ya kweli. Je hivi sasa kuna jambo lolote linaoongelewa hivi sasa au liliwahi kuongelewa siku za nyuma kuhusu wewe ambalo ni la kuzusha tu na pia ungependa kuchukua nafasi hii kukanusha?

RAY C: Kwa kweli asilimia kubwa ya vitu vingi wainavyoongelea, kama hakijatoka kwangu mwenyewe, sio vya kweli hata kidogo.Au tunaweza kusema katika mia, ishirini tu ndio vya kweli na vilivyobaki ni vya kutunga.

Kwa mfano mimi sijawahi kuolewa hata siku moja.Uhusiano wangu niliokuwa nao na Mwisho Mwampamba ulikuwa ni uhusiano wa boyfriend na girlfriend tofauti na ambavyo vyombo vingi vya habari na watu wengi walivumisha.Huo ni mfano mmoja kati ya mingi sana.

BC: Unapokuwa mapumzikoni unapendelea kufanya mambo gani zaidi ya kusikiliza muziki jambo ambalo ni wazi si rahisi kwako kuliacha?

RAY C: Kwa sababu wakati wa kazi za muziki nakuwa napata muda kidogo sana wa kulala,niwapo mapumzikoni huwa napendelea sana kulala na kupumzisha akili.Huwa napenda pia kusafiri au kutembelea sehemu mbalimbali just for leisure.

BC: Nini mipango yako ndani ya miaka mitano ijayo?

RAY C: Kuwa na video production company, studio na pia designer’s clothing line.

BC: Asante kwa fursa hii, kila la kheri katika kazi zako.

RAY C: Asanteni bongocelebrity.

Advertisements
 

84 Responses to ““MENGI YASEMWAYO NI UONGO”-RAY C”

 1. Neema Says:

  Ray C kwa kweli umependeza sana ulivyovaa especially the shoes are the bomb. Very good interview, reading about you in here sure answered a lot of questions. Good luck in your ventures and may God bless you and keep bringing all the the good music to us. Welcome to North America, and I’ll try to be in your concert.

 2. Habiba Says:

  Ray c nakupenda sana,na napenda sana nyimbo zako mno hasa wimbo wako wa “uko wapi nikufate” huwa unanikumbusha mbali sana na pia napenda unavyovaa japo sometime kuna nguo hazifurahishi sana but its all good.ila nakuzimia mno kuliko unavyoweza kuhisi hapa bongo ni wewe na Jide ndo wasanii wa kike ninao wazimia.Safari njema katika tour yako

 3. Farida Says:

  MUSIC IS YOUR JOB.KEEP IT UP.AND TAKE CARE OF YOUR SELF.

 4. Eusebio Hillary Says:

  Kwakweeli Kaazi ipo!

  Mimi mwenyewe binafsi na wadau wezangu,twazipenda sana nyimbo za huyu mwana dada tena big up sana . But style yake ya mavazi inatuonyesha ni jinsi gani ukosefu wa nizamu unavyomsumbua huyu mwana dada,ili na liweka wazi na atakae mindi poaa bali ukweli ndio unao itajika kwasasa ili tumuokoe mtu huyu na wengine wenye tabia kama yake.Jamani tunatakiwa tufanye kazi sana kwakuonyesha vipaji vyetu ipasavyo,kwani hivyo ndio vitatuweka kwenye ramani ya kukumbukwa muda mrefu na hata kunyanyuka kimapato na si kukaa uchi,au kutuonyesha maumbile yako. Jamani kumbuka kuna wazazi,wadogo,kaka na hata dada zake wanaoangalia hizi picha zake za nusu uchi zilizo tapakaa kila sehem,je! anataka tujifunze nini toka kwake?
  Jamani hapa ni bongo kwenye utamaduni uliostaarabika na ninaomba nifagilie ilo,sasa hawa watu wa magharibi wametoka wapiii?? Kwakawaida msichana hasiye kuwa na aibu kwa wakubwa na wadogo zake kwa mila zetu za Africa ni kituko!!!! Tujieheshimu jamani ili tueshimiwe wakina dada na wakina kaka,sisi ndio tunatakiwa kuziendeleza mila zetu zile zilizo bora na si kuleta ma mila ya kishenzi umu ndani kutuaribia.

 5. Isack Maruma Says:

  Ray C,you are a very beautiful woman and I love your songs.You know how to dress too,so sexy,uh uh uh.Umejitahidi pia kuyajibu maswali kwani nadhani hawa jamaa wa bongocelebrity nao kwa maswali tu hawajambo.Big up guys,tuleteeni pia celebrities wanasiasa kama kina Zitto Kabwe,Emmanuel Nchimbi na wengineo.

 6. Dj,bob Says:

  sema mtoto Rehema kwa kifupi unanipagawisha sana, nakupa hongea bint mzuri sana, ila naomba kujua kama umeolewa tena wa bado , uko single baada ya kuachana na jamaa poa midazz

 7. Dj,bob Says:

  mimi naomba nijibu tu swali langu, kama umeolewa tena au bado, kama vip nijibu hata kwenye email,. Rehema

 8. Dj,bob Says:

  EUSABIO,HILLAR,
  wewe acha bifu na RAY,C dada mimi nakupa big up tunaenda na dunia wewe mchamba wawapi bwana , Rehemu, mnyalu mwenzangu wewe achana na wabongo hawajui kusifu wanajua kuponda wewe keep, up miss,
  nguo,nguo hivi umemuona Ray C bas mbona mamisi kibao wanatembea stejini na vichupi ila umeuchuna kwa kuna video gani ambayo RayC kaonesha maumbile yake kama picha za ufukweni na kina Nance, Sepetu,Fraviana na wengine wengi ambao siwezi kuwataji, Isitosha hata wengine ni ndugu zako dadazako au wanao, Utajiju na wivu wako, Dada Rehema tuko , pamoja wacha waseme wabongo umbea ni kazi yao tu hasa mtu anapopata mafanikio , Nenda kawaseme Mamiss na mamodo, , UTAJIJU BWANA

 9. Eusebio Hillary Says:

  Dj,bob

  Hapa hakuna swala la ushamba wewe,hawa dada zetu ni raisi sana kupokea kila kitu bila kutazama maswala ya kulinda heshima zao,nafikiri ungekuwa muelewa ungaligundua niliyoyaandika awali,hii ni kwaajili ya yeye na wengine wenye tabia kama zake inamaana nimejumuhisha adi hao uliowataja hapo juu.Hakuna cha big up na uvaaji wake!! jamani huu ni utumwa wa akili ambao wapokeaji wake ni vipofu,Serena mcheza tennis maarufu kaanza kupiga picha za utupu sasa na nyinyi igeni sasa maana si kwenda na wakati uko!
  Vijana tuamke.

 10. queen Says:

  Ninakufagilia bint mrembo unaekwenda na wakati. Wewe ni mwanamuziki unakuwa stejini watu wakikuangalia unahitaji uwe na mvuto kwa wengi.Napenda kumweleza huyo anaejadili nguo zako,hazimuhusu wewe unavaa nguo zinazoendana na kazi yako na mwili wako.Kila nguo inamahala pake pa kuvaliwa.Anataka uvae nguo ya kanisani kwenye stej? au nguo ya sokoni kwenye steg? acha hizo ni ukosefu wa maendeleo! Usimkwaze dada wa watu anapendeza sana kwa wengi keep it up Ray C.

 11. kibaso Says:

  RAY C BINT VIUNO!!!!!!kamatia hapo hapo wewe ni mojawapo wa wasanii wanao peperusha bendera ya bongo kwa mziki wa kizazi kipya “BONGO FLAVA”
  Moyo wako wa kizalendo na jitahidi sana !sana hadi ufikie kiwango cha kimataifa na utafanikiwa mungu yupo pamoja nawe
  BIG UP

 12. Mtoa Mada Says:

  Huyu dada siku zote mimi nimetokea kumpenda kwanza jinsi yeye alivyo, pili nyimbo zake ambazo kwa kweli nyingi huwa nazizimia kupitab kiasi, kama ule wimbo wa umenikataa…
  i like your hair dos and the way you dress up yaself..i admire you, you have a glamorous look, you are so beautiful and keep glowing!
  Zidi kupeperusha bendera ya nchi yako popote pale ulimwenguni na mwenyezi Mungu akuzidishie maisha marefu..
  Kwa wale niliowaudhi kwa mawazo yangu hapo juu, am sorry ila hayo ndio maoni yangu na mtazamo wangu..
  Big up ma sister….

  Mtoa Mada…

 13. Dj,bob Says:

  QEEN,KIBASO, MTOA MADA’
  mmesema point za mwaka kazanane kula karanga, sana , hehehe, Ray C wewe piga bao ila swali langu naomba unijibu

 14. Mimi K Says:

  I think ur so talented but the dresses doesnt define you.

 15. Prince M Says:

  Kwa kweli Ray C anajitahidi sana na nyimbo zake nazipenda. Nikiwa kama Producer/Director wa filamu nafikiri anaweza pia kuwa actor mzuri hasa akicheza filamu za love story na ningependa kutengeneza naye filamu nikirudi huko bongo lakini pia nafikiria kumwalika aje acheze huku huku ughaibuni.

  Na niko tayari kkkumsaidia hata mawazo atakapo taka kuanzisha studio yake maana huko ndio kwenye fani yangu hasa so namkaribisha kwenye fani.

 16. Matile Says:

  Rehema mpenzi wangu, wabongo midomo ni mali yetu hatuilipii VAT wala nini! Wewe kaza buti acha nao hao wazushi! wanataka uvae hijabu stejini? au ujifunge khanga mbili? kwani unaenda msibani? Piga vitu mwanangu! wewe ni msanii bwana na sio sister Magdalena!

 17. Bob Chura Says:

  Hongera sana kwa kuperform miziki mizuri sana Rehema. Wewe pamoja na wafuasi wako mnapendeza sana. Hebu niambie Rehema safari yako ya Marekani utakuja na NINA KIMARO?

 18. REBBY Says:

  Dear Ray C; Kwanza nakupenda sana, unanivutia kuanzia wewe mwenyewe, mavazi, nyimbo zako ndo usiseme kabisaa, kuna watu wengi sana wanakupenda, wajinga wajinga achana nao hao hawakosekani kwenye jamii, songa mbele dada mzuri, natamani sana siku moja niwe kama wewe, nitahitaji sana ushauri wako wakati fulani. Kila la heri beibe.
  NB: Hongera sana, maswali hayo umeyajibu vizuri sana, akili yako imetulia mami.

 19. papa wemba Says:

  achana na mabo ya wabongo wasio elimika wewqew ni mwana mziki, mie nipo houston nakuzimikia sana unapo kua jukwaani ukifanya mambo yako,vile vele waimbaji wa marekani ulio wataja ni wazuri jitahidi ukija wasiliana nao ili wakupe mavitu.mnyalukolo tuinulie bendera wanyalu wenzio.ukifika houston ni e- mailie ili tuonane kwa mazungumzo nz ushauri zaidi. weenye wivu wajinyonge, mimi papa wa h town

 20. Innocent Peter Mosha Says:

  Ray, dada yetu kweli muziki wako nimtamu sana na unamgusa kila mtu; Kwangu binafsi ni hivyo bali nina wasiwasi na maisha yako ya baadaye; mi naona fanya mziki kwani nia fani yako ila swala la heshima ni la msingi sana tuangalie zaidi utamaduni wa nyumbani kuliko huo wa ughaibuni”””” jamani hao tayari wametupita miaka 100 mbele nasi tunakazana kkuwafikia na kila siku wanafanya njia ya kutuangamjza TUJIJENGE HOME KWANZA KWA WAKUBWA NA WATOTO” NA MAJINA YETU YATADUMU MILELE kwani waswahili wanasema MCHEZA KWAO UTUZW: Eusebion Hillary naungana na wewe hakuna swala la ushamba tusiige mambo yasiyo na msingi.

 21. maureen Says:

  Ray C kwa kweli u binti mrembo kila idara umekamilika, Mwenyezi Mungu kweli kaumba na kafanya kazi yake bila kukosea, nawe pia kazi zako zote za mikono yako ni nzuri sana na zimebarikiwa thats why zinakubalika kila kona ya dunia ILA kitu kimoja unapswa kuelewa japo kwa fikra za utu uzima ni RESPECT. na heshima ya mtu haipatikani dukani ama sokoni inaanzia kwa mhusika mwenyewe jinsi alivyo na anaishi na anaVYOJITUNZA. PLS SANA JITAHIDI KADRI UWEZAVYO UBADILISHE BAADHI YA MAVAZI YAKO ILI KAMA MWANAMKE UWE NA STAHA DUNIANI. BADILI ANGALAU HATA 20% YA NGUO ZAKO. MENGINEYO KWA KWELI UKO FIT

  BIG UP

 22. meddy Says:

  I like this interview, kwa kweli ni mahojiano yaliyotulia kuanzia kwa Ray C mwenyewe na mhusika wa bongo celebrity! You really know how to express basic ideas.
  Big uuup guys!!!

 23. renee Says:

  For real gurl’! u came a long way, and now ur doin’ it big!! keep up the good work, and dont listend to them’ haters who gon’ keep hatin’ on u. All they gon’ do is make u stronger!! u look great! ur music is great!! ..

  Out..

 24. Noneed Says:

  anailitka kujua kama juyu binti ana wazazi wake wanaoangalia muziki wake. Je anajua maana ya neno “Nasty” alilovaa kwenye nguo zake? Ana miaka 25 na tayari anaweza kukachaa uchi wakati huo huo anatumia maneno kama “role model” ameishawahi kuwa shule au ndio wale wale?

 25. Noneed Says:

  Tanzania yetu hii!!!! Aibu tuu. Kwa kweli wizara ya Utamaduni inahitaji kufanya kazi, duuuu

 26. Wilson Says:

  Big up moderate girl.Life is an existence of so many challenges.You have succes when a lot of pain has already pierced your heart.Keep it up.Being an artist is different from being a politician.You neeed an atraction for your fans to get closer to u everyday and also to pop your music high in the sky the issue of ‘vinguo’ hope is nonsense for the time being,kwa sababu hata wanakwaya kanisani wana mavazi yao kwa ajili ya perfomance.Unless hizo nguo unazivaa mtaani hapo siwezi kukutetea.
  One small thing,
  I always like your songs but will be much happy if one day I attend your great stylistic shows at least with people around you who play it lively.
  Make huku kuimba ka cd sio kuzuri sana na ndio maana mnaibiana bit kwa sababu zinatengenezwa na maproducer walewale.
  Kip it up mrembo,piga kazi tuko na wewe.

 27. shac Says:

  Mh hapana kwakwel we bint unaitia aibu wizara ya utamaduni na michezo kwani nakumbuka hata mavazi ya ajabu yalishapigwa marufuku even mamiss na wanapendeza kama ilivyopendekezwa.
  Hivi hujui kama unamtia aibu hata mama/baba yako aliyekuzaa akiwa na watu wake waheshima? na ndugu zako je? maana wanyalu wanajulikana kwa nidhamu wewe je?Na je kanisani/msikitini waenda? Mbali na hayo huoni kama unamkosea mungu wako?ndio umzuri ila sio vya ivyo hebu vaa nguo za kawaida tuone kama utaonekana hivo(uzuri)unazidisha kujitia mvuto dear?
  For sure nakupenda sana dada etu na unaimba vizuri ila mavazi hayo na (UNYALU) wapi na wapi?Jitahd bwana

 28. dj tom in japan Says:

  hebu acheni hizo,yaani mmemuona ray c tu ndio anavaa mavazi yasiyo na heshima? yeye ni mwanamuziki lazima aendane na mavazi ya fani yake na watu wanampenda kwa ajili ya mavazi yake hayo hayo, nyie mlitaka avae kaniki akiwa stajini?

 29. Ken Says:

  Ray C mambo yako bomba kichizi! uimbaji unao, uzuri wa sura unao, uzuri wa umbo unao, akili timamu,Mungu akupe nini.
  hao wanaozungumzia mavazi wanakosa kuelewa kuwa kuna mavazi tofauti kulingana na kazi na mahali mtu alipo. Kwenye muziki ukiingia na tenge la mama UWT hata uimbe vipi utakuwa unaboa! We endelea na mambo yako mamaa waseme yaliyo mioyoni mwao, wakiimba wao watinge na hijab na kanzu tuone.
  Good luck in your endevours!

 30. Eusebio Hillary Says:

  KAMA HUJUI ULIPOTOKA,HUTOJUA UNAPOKWENDA HAKIKA!

  Kwakweli tu vipofu wa mambo bado na watu wengine wataendelea kunufaika kwa ufinyu wa mitazamo na akili zetu sisi watu wa kizazi cha Dunia ya tatu.Nafikiri watu walipota kuangalia kile kipindi cha BABA -T cha roots jana jumapili 29th July ndani ya channel 5, angeelewa na kukubaliana na mimi kabisa nilicho kiandika hapo awali.Kwa kifupi walionyesha mambo ya utumwa na dhana kamili iliyoadhisha uchezaji uchi au nusu uchi juu ya majukwaa ya mziki.Walionyesha video kabisa jinsi dada zetu wakati wa utumwa walivyo kuwa wakichezeshwa nusu uchi uku ngoma zikipigwa ndani ya soko la watumwa, ambako wanunuzi walifika na kununua mtumwa waliopendezwa nao,na vigezo vikiwa maumbile yao(kama sehem za kifua,makalio na miguu),vile vile hiyo video ilionyesha hizi video za kisasa za hawa dada zetu wanaocheza nusu uchi na nyinyi mnashabikia ni fasheni, wakasema ndio mambo yale yale ya kale yaliozalilisha dada zetu na ndio yanayoendelea hivi sasa.Je! ikiwa kama hawa jamaa wa First World wanapinga haya mambo je! sisi wana wa dunia ya tatu watu wa kuiga tuu tufanyeje?? Najua vigumu kukubaliana na hivi kutokana na upeo wetu wa mambo lakini ukweli ni huu, inabidi tubadilike kwani tunakopekwa siko tunakotakiwa twende.Ndio dunia imekuwa ya kibiashara zaidi sasa,lakini tusidhalilishe utu wetu jamani kwaajili ya fweza na hii dhana ya kudanganywa kwenda na wakati. huu ni utumwa unaokuja kwa njia nyingine mpya kabisaaa kwa wale wenye hisia za mbali watakubaliana na mimi. Kwakuongezea, kwa wale waliomsikiliza Emmanuel Nkulila mtanzania ambaye anayeendesha shughuli zake za mziki marekani aliojiwa juzi na redio moja na akaongelea mambo haya haya ya kucheza nusu uchi stagini yanavyopingwa kwasasa na wamarekani wengi wakidai ni uzalilishaji wa mwanamke. Je! wewe unasemaje?

 31. Brother Hugo Says:

  Ray C kwakeli umependeza. Unajiamini wala huna wasiwasi na wanaokuzungumzia. Nijuavyo mimi ukweli unao mwenyewe, hata kama huyo Mwisho alikuwa Bfriend wako ni wewe unajua mwenyewe.
  Na kikubwa zaidi hao wanaokusema wanafanya bonge la branding na matangazo yao ni zaidi ya nyimbo zao redioni au kwenye TV.
  Big up ma mdogo na ikibidi toka na Baba zao.

 32. Kiriki Says:

  Rehema kweli nakubali umekua na ubongo wafanya kazi vilivyo, umeenda saafi na alokuhoji na nakukubali kwa kumudu interview, wengi wa celebrities hawaelewi ama maana ya kuhojiwa, au umuhimu wa utu wao kwa public, Kwa kweli muziki wako ni bomba mno tena mno
  Kuwa mwanamuziki au mwanamitindo haimaanishi uvae wakati wote kama uko jukwaani, we una mvuto na hata ukivaa hijabu mbnona utawateka wengi, Nguo yeyote utakayovaa itakupendeza na hakika utapendeza jaribu kubadili style sister.
  Malengo yako ni thabiti kwani akina Ritha wa benchmark, Beatrice na wengine waliaanzia wapi???

  BABIE DEVELOP YOUR IDEA AND MAINTAIN YOUR CARRIER pia tuko nyuma yako ukitaka support wasiliana nami upande wa PRODUCTION za video

 33. Sia Says:

  Ray C mimi nilikuwa nahitaji album yako mpya na ya zamani kununua niko UK je nitazipataje?original copies

 34. Eusebio Hillary Says:

  Haswaaaaaaaaaa!

  Naona sasa mwanga kwa mbali unakuja,nimefurai akika, watu mnaanza kutambua nini nilichokuwa nakisema hapo juu! Big-up sanaa,together we will stand apart we will fall.Thanks wazalendo!

 35. Yvonne Says:

  I do think that Ray C is quite something to talk about – In a good way. I have learned that you cannot please everyone…just do what you feel natural to do. Kuna washamba kati yetu ambao bado wako kwenye dunia ya 19, ambao wanakosoa kila kitu. Hivi mnataka RAy C aende kufanya tour huko UK na huku USA akiwa amevaa nini?? Sketi ya kutambaa chini jamani? Blauzi ya mikono mirefu??? Si atachekwa jamani? Hivi mnawaona ma-celebrity wa Holywood wanavyovaa kwa kwenda na wakati? Mie sijaona kama amevaa kitu chochote cha kupita kiasi…I think she’s just perfect! I’m looking forwards to yout concerts…Go girl, Keep it up!

 36. rasheed mkilalu Says:

  wewe ni kioo cha jamii jaribu kuifundisha jamii mambo meme ninauakika watakusikiliza

 37. Glory Says:

  Min nafikiri tusimlaumu Ray C ktk mavazi yake, ni vigumu mno kukubalika katika muziki wa bongo na mavazi ya magauni marefu au vitenge, hata mashabiki wa bongo wenyewe wanapenda wakione kiuno cha Ray C, sasa akiingia amekificha mwanawane unafikiri itakuwaje?………

 38. BongoSamurai Says:

  Big up Ray C, unawakilisha.
  Napenda sana nyimbo zako.Tour njema.

 39. Zahra Says:

  Ray C, mimi unanifurahisha sana nyimbo zako na uwapo stejini sio siri unanifurahisha,Big up lady wanawake na maendeleo!!!!!

 40. chill Says:

  First impression matters a lot dadangu.ur so talented but u dont know how to behave.ur have 2 behave like an african girl not like an american bitch.by the way ur very beautiful and i hope u can do it!kip it up girl!napenda kazi zako!

 41. lulu Says:

  we chill?? na wengine wote!!!!! lol hamuoni haya kupoteza muda wenu kwa vitu visivyoukua vya msingi? eti american bitch? lol unajua maana ya neno bitch wewe ama waandika tuu? msipende kumjaji mtu kutokana na mavazi mavazi ni kitu cha kawaida,pili isitoshe kwani ray c sio binadam? kama yeye ni binadam kama wewe basi muacheni afanye roho yake inamtuma au mawazo na fikra zake.utamaduni wa kitanzania? aaaaah wangapi mnafata maneno ya vitabu vya mungu vilivyosemwa? hakuna hata mmoja dunia wote sisi ni wadhambi.sasa kama tunashindwa kufata maandiko ya mungu ambayo tunajua mwisho wetu ni jehanam itakuaje watu washindwe kutofata utamaduni? jamani muacheni huyo dada kama alivyo,ray c anafanya kazi nzuri na anajituma akiwa stejini.mbona hamuwapondi madaktari au maprofessa wanaofanya uhuni na wanafunzi huko vyuoni.mnakaa chini na kuanza kumkosesha raha dada wa watu.. kama hamana cha kuandika tulieni na familia zenu au marafiki na kuliwazana hapa kuandika vitu ambavyo haviwezi kubadilika kamweeeeeeeeeeeeeeeeee….

 42. Talaht Says:

  Rehema I really feel you,kazi zako zimesimama na una mvuto wa hali ya juu.you’re so beautiful kila sector na pia unapendeza sana.nisingependa kukufundisha au kukuchagulia nguo za kuvaa ila if I were you nisinge vaa nguo ambazo ni too revealing like the way you sometimes dress up.Pamoja na kazi yako ya uanamuziki I believe unaweza kijisitiri na bado ukatoka bomba asikwambie mtu kizuri ni kizuri tu and thats what you are.Ila kumbuka the choice is yours and its your life so you got the right to choose how you wanna live it.I still fancy you though.
  Talaht

 43. sinzia Says:

  dear Ray C,
  nimehudhulia show yako jana Norway (Bergen)…kweli umetukata kiu manake show ilikuwa imefana kupita kiasi
  Sinzia.

 44. anny mwiya Says:

  big up ray c mambo yako super sana nazizimia sana nyimbo zako na mavazi yako ni bomba sana achana na wabongo …. kaza buti BIG UP KWA SANA TUU………TAKE CARE GIRL…

 45. TINA Says:

  ukweli Ray c ni mzuri pia maisha si muziki tu jaribu kutafuta mwenza wakaribu mwowane ueshimike kama Lady j Dee.

 46. TINA Says:

  Dia we mzuri sna tu dia maisha si mziki jaribu kutafuta mwenz uolewe ueshimike kama Lady J Dee.

 47. stambuli Says:

  Mnashindwa kuelewa jambo moja kila kazi inataratibu zake na miiko yake,pia kuna kachumbari kwenye kazi ambayo inendana na aina ya wateja wa kazi yake.Ray C amegundua kitu kimoja nacho ni kwamba wanaume wanapenda kuangalia akina Dada wanaokaa nusu Uchi,mate huwatoka(sisemi wote isipokuwa asilimia kubwa)hivyo basi naye akaona ili aongeze chachandy kwenye kazi yake ni akaweka mtego huo ambao midume mingi mikware imeingia kuangalia matiti,mapaja na nyonga ya Ray C.wanasikia Raha.Lakini wanaume haohao ukiwambia na wao dada zao wakae uchi tuwangalie wanakuwa wakali kama pilipli kwa sabababu asili ya maumbile ya Binaadamu anapenda kufanya jambo baya kwa mwengine akifanyiwa yeye ankuwa mbogo.Utamkuta hodari Kukamatia dada za wenzake yeye dada zake wakishikishwa ukuta bila kufuata taratibu anakuwa mbogo? Ndio maana steji show wanaokaa uchi ni dada zetu wanaume stage show wanavaa vizuri,Je wao hawapo kazini?Jibu ni lile KUVUTIA WATEJA.Na ray C anapofanya hivyo anavutia Wateja Yupo Kazini.Kwani si Umemuona changu doa kavaa kanga au gauni anajiuza anavaa nguo staili ya akina Ray C.wote wapo kazini isipokuwa huyu mmoja anotoa huduma ya macho tu na huyu changudoa yeye anotoa zote mbili kuangalia na Kuuchezea mwili wake unavyotaka,huo ndio ukweli.Kwa ujumla Ray C.tunampenda nyimbo zake nzuri lakini anatuuzia biashara nyingine tusiyoihitaji Mwili wake.Kuna bendi moja ya kongo inaitwa Extra Musica hawana stegi show mwanamke katika bendi yao waimabji na wapigaji ni wanaume wanavaa suti zao freshi na mziki wanaoporomosha we acha si mchezo.wao wameona hakuna haja ya kuwadhalilisha dada zetu.Sasa watu wanapoingia kwenye show kwa mfano.Twanga wengine wanachofuata pale ni Miuno ya AISHA MADINDA NA WENZAKE na siku Twanga watakapoondoa stege show wakike wanaweza kukosa asilimia kubwa ya wateja..
  TUKUMBUKE DUNIA NI MAPITO PUMZI ISITUFANYE TUKUFURU TUFANYE MAMBO YANAYOMPENDEZESHA MUNGU.Fuateni nyayo za watu kama STARA THOMAS.
  JAM STAM

 48. Prof. Says:

  ray c na mwisho si walifunga na ndoaaaa?na wakati ule ikisemwa saana ray c u mjamzito hadi kashauriwa kuacha kukata mauno stejini ile mimba iliishia wapi?na ka ni kujifungua je baba ni upi???

 49. Proster Says:

  Nakuzimika mno Ray C kuliko wasanii wengine keep it up and pull up your sox Girl.

 50. robert Says:

  dear uko poa sana

 51. Reg Miserere Says:

  My dear Ray C….
  Kuna kitu unaokota hapa????

  Au hawa wazawa wenzio wanao kushauri ujaribu kuenzi utamaduni wako wanataka kukupoteza?? Binafsi sidhani hivyo.
  Sema tu wasi wasi wao wanaokufagilia kuhusu mavazi wanataka kukupiga chabo tu…sidhani kama kuna lingine….

  Nguo hizo si nzuri sana kipenzi……..

  Kazi ni nzuri dada

 52. mamanye Says:

  My dear sister,you are soo cute but the way you wear is not our culture.what do u expect our young sister to learn from you.On top of that your are a muslim.I would like to see changes from you this year.

 53. zawad haji Says:

  HI!!!!!!!!!!!!! natumai wote mu wazima wa afya tele,jamani nataka kujua kama Rehema ana mtoto ama la! coz nimewahi kusikia tetesi kama ana mtoto.kwa upande wa music yuko bomba ile mbaya , but, ajitahidi kidogo kwanye mavazi yake yeye ni mrembo tu hata akivaa nguo refu atavutia zaidi.

 54. mkundu mavuzi Says:

  ray c ww mtoto wa kiswahili tena sana maanake umechukuwa damu ya kiswahili nd by da way u luk hot

 55. mchana mrembo kama ww ni mzuri sana ambayo una ni faa mie…. luv ya xxx n u rock wen u perform ur sngs.. ama keli unifanya chizi

 56. khadija Says:

  hey girl i just love your songs girl u rock keep doing what u do pleace e-mail me back at prittyprincess19@yahoo.com becouse i want u to meat u’r biggest fan ever

 57. jomaeli Says:

  we hadija unajifanya unaandika kizungu halafu hamna kitu…..ni meat au meet?makubwa na hiyo because yako iangalie vzr

 58. Safia Says:

  Rehema,,,,,,,,,nice muslim name but u dnt value that,totally i dnt support u on anything, punguza kuwaza dunia sana, akhera inakungoja na ndio yenye kudumu, many people will hate this BUT ITS THE TRUTH n the truth always hurts.

 59. 17th the king Says:

  hey rehema, how is going? i stongly believe everythings is better so far. i was wonder if you wanna mail me back i will love that more. pease non’t forget maybe.

  have a great one.

 60. Isaac Says:

  Hi Ray C.Lyk ur work…keep it going.Ur a very hot lady n da way i see it,u got potential in all aspects of ur life.Keep it real n plz email me?I’d be honoured 2 talk 2 u personally.

 61. mankya nkya Says:

  youre so cuteeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kaza buti maneno weka mgongoni achana nao hao ndo wabongo. big up and pull youre sox

 62. myenzi NAZA Says:

  Kaza buti mtu wangu usisikilize maneno ya wazushi.

 63. jamy Says:

  Kazi ni nzuri sana lakini mi da angu nakushauri upunguze kuvaa nusu uchi, kwani kama ni kupendwa utapendwa tu, hayo ni maoni yangu naomba mtu yeyote asinikosoe.

 64. zaina seif Says:

  Big up Ray C. me nishabiki wa music wako unajitahidi dada yangu. wewe unaesema nusu unawajuwa wanao kaa nusu uchi kweli!? nakufagilia sana Ray C good job

 65. binti-mzuri Says:

  big up!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! mdada namfeel!…beyonce akivaa kikaptura watu wanashangilia,akivaa ray c ooh yukoo uchiii.. na awe uchi basi,kama unaona aibu si usiangalie..LOH..mwacheni mtoto wa kihehe, sura bomba,umbo bomba,sauti bomba… tunasonga mbeleeh!

 66. kemmy Says:

  HI! RAY C!
  its implesing me to meet you and talk with you even a single in minute.nakupenda lkn nikiwa dar nakua very buzy na mambo yg.
  Hi!its real that your a nice lady and very attractive,And this is not only the thing l can comment in you,
  ur songs touching much in the whole sociaty not only in guys but in all type.
  plz keep on with your fun.tallent,

 67. kim Says:

  heee! makubwa taratibu na hicho kiingereza jamani!

 68. MAMII Says:

  Wow ray c,ulitupa burudani tosha uku oslo,norway…nakufagilia saaana tu…but nahitaji album yako ya kwanza kama unayo please…

 69. u so talented .dont care abt what people say just go on ur so beautiful my dear.ilv u

 70. echo Says:

  ray uko safi ni bint mzuri ambaye ni ndoto kwa kila jicho la mwanamume lakini sio moyoni mwao, uzuri wako usiwe tu kwa ajili ya maungo yako binti jaribu kujiheshimu kama mwanamke wa afrika la sivyo utishia kumegwa tu.

 71. Dadi Says:

  si dhani kama we mzuri kiufupi mi sikukubali kabisa, unalazimisha! na kwa upofu na ufinyu wa akili zao wamemekukubali…..mzuri anajulikana tu hata akivaa hijabu ataonekana tu.,nguo za kuonyesha maungo si siri ya urembo bali ni kujirahisi na kujionyesha ni jinsi gani ulivyo kicheche.

 72. Matty Says:

  Hey! camonnnnnnnnnnn guyz kwani kuna nini hapa?? si avae nguo inayoziba kidogo magoti, tumbo n.k nyimbo zitauzika tu unless otherwise there is something under the carpet!

 73. maasai boy Says:

  u look good and sexy but plz dont 4get our culture mamaaeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 74. sweet bady Says:

  mie namsifu sana tena tunamsubiri uk na nampenda sana macho yake watu wache walonge midomo wame pewa free huzi kuzuwia mtu asiseme wangapi wamesemwa nawakowapi? mtu akishakuwa msanii lazma aende na wakati kila kitu kina vazi lake kila kitu kimajaaliwa lake kwahiyo maneno sio sumu kwako ok baby ray c nakutakia kila lakheri wao wenyewe yao hawayajui wapo tuuuuuuuuuuuuuuuu.

 75. sweet bady Says:

  usjali ray c nichoyo tu hawana lolote wasitubabaishe kila mtu anakusifu mashallah mpaka dubai unasifika hapo mtu anatamani awe dada ao ajinate choyo izo mie nachosema jamani muache sema yawatu mtu kwanza huangalia lake bado hatujafika mwisho tunasafari kubwa huko kwahiyo haifai mwacheni msimtie husda mie ray c namtakia kila lakheri nampenda sana miziki yake na naanavyocheza mashallah.

 76. leonard Says:

  yes ray c

  asikuzingue mtu kila kitu ni chako yaani mali yako kama vipi jiachie lakini tukumbuke na sisi watoto wa kiswazi

  nyc tym its m myself and i

  simba mzee

 77. hope Says:

  mwanangu kaza buti, uko juu sana kwawasanii wa
  kike

 78. hope Says:

  kweli bwana uwezi vaa nguo za kanisani kila sehemu kuna mavazi yake bwana.uko juuuuu mwanangu

 79. frank Says:

  tia bidii wangu mie nakukubali mnoooooooooooooo toka nairobi kenya

 80. watubwana Says:

  siri ya mtungi aijuaye ngata,ishi upendavyo na si wapendavyo.hongera mama.maisha ni safari,usikate tamaa,utampata mwenza na usiwe na papara.jiheshimu uheshimiwe.

 81. newayne Says:

  ah mi nakukubali bwana…ukisikiliza sana ya watu utaona maisha machungu.kip it up mpendwa…only God knows the real you..wengine mashahid tu.go on gal….

 82. ngetu Says:

  big up my only aunt dont trust on pplz cauz thr jealous i miss ur and love ur

 83. SAMMY/ SAM Says:

  Bigups Ray c;ur voice is good.KIP UP AND DONT LOOK BACK.UR VOICE IS BEING LISTEN BY MANY OUTSIDE THE WORLD.AM IN MIDDLEEAST (IRAQ)WE ALL NEED U.THANK U FOR GOOD SONGS. SAM FROM KENYA.

 84. ALI MPEMBA Says:

  Ray: Biashara inahitajia kutangaziwa ili wateja tuiyone so poa 2 lipuka hadi zaidi ya madona, atakae weza anunue na walalahoi waumwe roho.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s