BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“SIWEZI KUACHA KUIMBA”-BI. KIDUDE August, 10, 2007

Filed under: Muziki,Taarab — bongocelebrity @ 12:56 PM

Kama binadamu anaweza kufikia kupewa heshima ya kuwa “taasisi”(institution) katika jambo fulani basi Bi.Kidude anaweza kuwa mmojawapo. Ukiiweka mezani historia ya muziki wa taarabu na tamaduni za unyago visiwani Zanzibar ni wazi kwamba katika meza hiyo pembeni yake ni lazima aketi Bi.Kidude. Uzoefu na uelewa alionao katika idara hiyo hauna mpinzani. Inaaminika kwamba ndiye mwanamke,mwimbaji mkongwe kupita wote Afrika Mashariki na Kati.

Picha hii ni kwa hisani ya Marcel Mutsaers aliyompiga Bi.Kidude wakati wa Tamasha lijulikanalo kama Festival Mundial kule Tilburg-Uholanzi mwezi June mwaka 2006.

Umri wake halisi haujulikani. Kinachojulikana ni kwamba ana umri zaidi ya miaka 90 na hivi sasa sio ajabu akawa ameshafikisha umri wa miaka 100! Amekuwa muimbaji tangu miaka ya 1920 akiwa ni mfuasi wa Sitti Bin Saad mmojawapo wa waimbaji wa mwanzo kabisa wa taarabu visiwani Zanzibar.

Hivi leo anatambulika na kuheshimika kama malikia wa taarabu na mambo ya unyago asiye na mpinzani. Alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo katika familia ya watoto saba. Jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa ni Fatuma Binti Baraka kabla jina maarufu la Bi.Kidude halijashika baadaye alipoanza kuwa maarufu katika uimbaji.Wazazi wake walikuwa ni wafanyabiashara ya kuuza nazi enzi hizo za Zanzibar iliyokuwa chini ya utawala wa wakoloni.

Katika mahojiano mbalimbali aliyofanya na vyombo tofauti tofauti vya habari ulimwenguni Bi.Kidude anasema alianza kuimba akiwa na umri mdogo wa miaka 10. Anasema uimbaji alijifunza kutoka kwa Sitti binti Saad tena kwa kujificha nje ya nyumba na kumsikiliza Sitti binti Saad akiwaimbia wageni ambao mara nyingi walikuwa wakipelekwa pale na yeye Bi.Kidude.

Akiwa na umri wa miaka 13 tu hakuwa na jinsi bali kukimbilia Tanzania bara(Tanganyika enzi hizo) ili kuepuka kuozeshwa kwa nguvu. Akiwa Tanzania bara alizunguka kila kona ya nchi akiwa muimbaji katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarabu likiwemo lile maarufu la Egyptian Musical Taarab. Baadaye alihamia nchini Misri kwa kifupi kabla hajarejea kisiwani Zanzibar mahali ambapo anaishi mpaka hivi leo.

Mbali na uimbaji Bi.Kidude pia ni mfanyabiashara.Anauza “wanja” na “hina” ambazo anazitengeneza mwenyewe. Pia ni mtaalamu wa dawa za mitishamba lakini zaidi ya yote yeye ni Mwalimu wa “unyago” ambapo anacho chuo chake mwenyewe huku akijivunia rekodi kwamba katika wanafunzi wake wote hakuna ambaye ameshawahi kupewa talaka na mumewe. Pengine hii ndio sababu mwaka 2004 ulipozuka umbea kwamba Bi.Kidude amefariki dunia wakati alipokuwa katika ziara ndefu ya kimuziki Ulaya na Mashariki ya mbali, kila mtu kisiwani Zanzibar alishikwa na butwaa na majonzi! Kwa bahati nzuri habari za “kifo” chake zilikuwa ni uzushi tu.

Picha kwa niaba ya Issa Michuzi.

Mwaka 2005 huko Gateshead, Newcastle nchini Uingereza,Bi.Kidude alipokea tuzo yenye heshima kutoka World Music Expo (WOMEX) kwa mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar. Katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda wanamuziki mahiri kama Peter Gabriel, Miriam Makeba na wengineo. Bi.Kidude anasema hawezi kuacha kuimba mpaka siku atakapoiaga dunia kwani akiimba anajihisi kuwa binti wa miaka 14!

Mwaka jana, kampuni ya nchini Uingereza iitwayo ScreenStation kwa kushirikiana na Busara Promotions walitoa documentary iitwayo “As Old As My Tongue-The Myth and Life of Bi.Kidude” inayoelezea historia nzima ya maisha yake. Unaweza kuona dakika kama saba hivi za documentary hiyo hapa chini.Anasema yeye anakunywa na pia anavuta,lakini zaidi ya yote anaweza kuimba bila hata kutumia spika ya mdomo yaani microphone.


Advertisements
 

12 Responses to ““SIWEZI KUACHA KUIMBA”-BI. KIDUDE”

 1. Mkongwe Says:

  This is wonderful! Bongo celebrity naona mnajua kazi yenu. Je Bi. Kidude amekwisha andika kijitabu juu ya mambo ya unyago? Anaye msaidizi/wasaidizi watakaoendeleza chuo chake atakapokuwa hayupo? Wengi wetu tungependa kujua siri kubwa ya kutunza ndoa kwani duniani maisha wawili wawili***

 2. Lizzie Says:

  Respect bibi kidude tunakupenda

 3. Kidds Says:

  Big up Kidude, I salute you and you will leave to be remembered for a very very very long time.

 4. kazuba Says:

  mambo ya bi kidude

 5. ChrisK Says:

  Bi Kidude is legendary!
  long live Bi Kidude! Hata watanzania wa usukumani imebidi tuseme shikamoo bila a kuelewa kila anachosema! Furaha ya wzanzibari kumwelewa inafurahisha peke yake..

 6. Bob Sankofa Says:

  Niliona performance yake live kwa mara ya kwanza pale Ngurudoto Lodge, Arusha mwaka huu mwezi wa sita. Bibi tunaambiwa ana miaka 95 lakini bado yuko na nguvu kwelikweli. Niliweka picha na habari kidogo ya onesho lile bonyeza http://mwenyemacho.wordpress.com/?s=Bi+Kidude+Noma ucheki balaa alilofanya. Nashukuru Bongo Celebrity kwa kutambua mchango wa bibi yetu hasa katikak ulimwengu wa muziki wa pwani

 7. Farida Says:

  Bi Kidude unatisha kaza uzi uendelee kuwafunika vijana.Jamani tumuenzi mzee wetu.

 8. BIG J Says:

  SHE IS THE FIRST EVER PERSON TO RAP IN SWAHILI….NO ONE IN THE WORLD CAN QUESTION ABOUT THAT….I’VE READ ABOUT HER ON DAILY MAIL AND THE GUARDIAN HERE IN LONDON….I’LL LOVE TO SEE HER LIVE PERFOMANCE….HOPEFULL NEXT YEAR WHEN I VISIT TZ

 9. miss pauline joseph Says:

  bibi sasa umechoka,kwanini usipumzike au unakimbia kulima?

 10. Freddy Macha Says:

  Aliyesema kuwa sasa Bi yetu Mkubwa Kidude, fahari ya nchi yetu, kachoka; eti apumzike (“akakimbilie kulima”) hajui kuwa wasanii na wachapa kazi kwa jumla huwa hawapumziki? Hata wakishafariki, bado kazi zao huendelea kufurukuta, kugagata, kusereketa, kukarakata, kukata kata na kung’ata ng’ata.

 11. Mkereketwa Says:

  I love bi kidude. Yaani inaonekana enzi za ujana wake alikuwa si mchezo huyu.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s