BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MBARAKA MWARUKA MWINSHEHE! August, 21, 2007

Filed under: Muziki — bongocelebrity @ 11:16 PM

Iwe ulizaliwa enzi za uhai wake au baada ya kifo chake, jambo moja ambalo wote tunafanana ni kwamba ukisikia muziki wake sio ajabu utatikisa kichwa, kutabasamu, kucheza au kurukaruka. Ukishaguswa na muziki huo sio ajabu ukajiuliza swali gumu; kwanini mungu akamchukua Mbaraka Mwaruka Mwinshehe baada ya ile ajali ya gari nchini Kenya tarehe 13 Januari mwaka 1979? Angelikuwa hai nani asingependa kusoma mahojiano yake? Inasemekana Mbaraka Mwinshehe alikufa kutokana na kuvuja damu nyingi na asipatikane wa kumchangia damu ili kuokoa maisha yake. Alifia hospitalini Mombasa.

 

Hayati Mbaraka Mwinshehe akicharaza gitaa na kuimba!

Uwezo wake wa kutunga nyimbo, kupanga muziki na kudonoa gitaa hauna mfano wake mpaka sasa. Ukimsikiliza leo unaweza dhani kapiga gitaa hilo juzi kumbe ni miaka chungu mbovu iliyopita. Kizuri zaidi ni kwamba upigaji wa gitaa hakufundishwa na mtu bali yeye mwenyewe. Akiwa bado kijana mdogo kabisa alicheza muziki uliokuwa unajulikana kwa jina la “kwela”(asili yake Afrika Kusini) na bendi iliyojulikana kama Cuban Branch Jazz.

 

 

 

Mbaraka Mwinshehe akimvisha mke wake, Amney Shadad, pete ya ndoa. Hiyo ilikuwa tarehe 17/3/1972 mjini Morogoro.
Mbaraka alianza kujitengenezea jina kwenye medani ya muziki wakati alipokuwa mmojawapo ya wanamuziki waliokuwa wanaunda bendi maarufu ya Morogoro Jazz kati ya mwaka 1964 mpaka 1973. Baadaye ndipo alipoanzisha bendi yake mwenyewe iliyojulikana kama Super Volcano mwaka 1973. Alidumu na kutamba na Super Volcano mpaka mauti ilipomfika miaka sita baadaye. Kuimba alijifunza kutoka kwa Salum Abdullah, mwanzilishi wa Morogoro Jazz ambaye baadaye alijiengua na kwenda kuunda Cuban Marimba Band.

Hii hapa ni baadhi tu ya miziki ya Mbaraka Mwaruka Mwinshehe ambayo inatufanya tuendelee kumkumbuka daima. Lala pema peponi.

 

SHIDA

 

 

EXPO 70’s PART I

 

EXPO 70’s PART II

 

 

Mbaraka akifanya vitu vyake huku amezungukwa na mashabiki wake.Tizama walivyotulia wakipata ujumbe.

 

Jogoo la shamba linaweza wika mjini?

Endelea kupumzika pema peponi Mbaraka Mwinshehe.

Picha kwa niaba ya Michuzi. Miziki shukrani zimwendee Steve Mugiri.

 

 

 

Advertisements
 

18 Responses to “MBARAKA MWARUKA MWINSHEHE!”

 1. gabriel Says:

  kwanza nashukuru kwa kuleta hii habri ya star mtanzania halisi ambaye alikuwa mstari wa mbele kupiga na kuendeleza muziki wenye identity ya kitanzania na vionjo (mapigo) vya tanzania originally na siyo mambo ya kikongo
  hakika tungekuwa na wanamuziki wenye moyo na vision kama ya marehemu mbaraka basi wacongo na wengine wangekuwa wanajivuna kwa kuiga mziki wetu na siyo sisi kufuata fuata wao kwa kuiga vionjo ,mitindo na mpaka namna ya uimbaji na madoido utasikia watu wanatajana majina ,mara pededjee,na ala zile za kitanzania siku hizi wanaiga za kikongo completetly tena wasivyo na aibu wenyewe wanajivuna kwamba wanapiga sebene tena sebene ya nguvu,loh!
  ukija bongo flava ndio kabisa aibu tupu
  wasanii tufuate nyayo za wazee wetu mbaraka mwishehe,mlimani saida karoli,msondo ,bima lee,washirika,chee mundugwao,maneti, na wengine wengi tuu amabao usiku na mchana waliupenda utanzania na kupiga mziki wenye vionjo vya kwetu na siyo vya kuiga mziki amabao uliweza simama peke yake na mtu wa tamaduni tofauti akiusikilza tuu anaweza kuidentify na siyo kushangaa kwamba mziki gani huu wa tanzania mbona ni kama wa kenya ,mbona ni wenge muzika hao au mbona ni hip hp ya marekanai ,au mbona ni kwaito hiyo!
  tuache kuiga ,tusijione bora kwa kuwa wenge muzika wa tanzania ,au mafikizolo wa tanzania au mariah carrey wa tanzania .ni lini jamani tutaamka na kuwa na chetu wenyewe na tjivunie !
  amkeni
  kazi ya sanaa ni creativity hata hao tunaoiga walicreate kwanza hawakuiga

 2. gabriel Says:

  mwandishi naomba uniruhusu ni toe maoni yangu kuhusu ulichosema hapao juu kwamba mungu alimchukua mabaraka mwinshee.
  hivi,naomba nikuulize haya maswali .

  ni kweli kwmba mungu anachukua watu kwa kuwaua katika ajali kama hiyo ya mabaraka ni mungu gani huyo anawapenda watu eti akitaka uende kwake anakuua? tena cha kushangaza huyo mungu amemwua mbaraka mwishehe kinyama kama hivyo ,mmh! ili tuu amchukue aende kwake

  umeshawahi kufikiri ni kwa nini mungu awachuke watu kutoka duniani (sehemu aliyotutengenezea ili tuishi)
  ili waende wapi kisha wachukua ?
  hivi doesn’t it make sense to you kwamba mungu na uwezo wake woote wa kialmity anauwezo wa kuumba kila aina ya mtu anayetaka au anyempenda yeye yaani kama ni mbaraka mwinshehe basi anaweza kuwaumba hata milioni moja kwa malengo na kazi anayotaka yeye na sioni kwa nini mungu huyo aje achukue mtu hapa duniani na hali yeye anauwezo wa kuumba,mbali zaidi anakuua kwanza kinyama halafu ndio anakuchukua,
  hivi ni kweli mungu akikutaka anakuua kwanza? je kuua ni sifa mojawapo ya mungu ?
  what sense would it make kwamba mungu alimpenda sana mbaraka mwishehe kwa hiyo akapanga ajali ya kinyama ya gari ili amwue tena kinyama kama ulivyoandika ,kisha hapo sasa ndio amchuke aende kwake

  hivi mimi sifahamu bwana mwandishi ,kazi ya mungu ni kuua? au kifo ni kazi ya mungu? kama ndio hebu nifahamishe ni nania mwenye kazi ya kuumba,kulinda,kuponya,kufariji,kuto maisha kwa wandamu.is it mungu au shetani?
  mimi nilipata kusikia mahali kwamba mtu akifa anarudi k mavumbini sijui kama una ka idea na hili? na kama hii ni kweli sasa mungu alimchukua mbaraka mwinshehe ili aende wapi huko?
  pia nilisoma mahali kwamba mungu alitengenza dunia ,ulimwengu kwa ajili ya mwanadamu aishi humo afurahie maisha na kumtukuza yeye sina uhakika kama ni kweli juu ya hili lakani kama ni kweli je ni kwa nini sasa mungu huyo aliyemtengenezea mwandamu mahali pake pa kuishi akuchukue tena nisichokielewa anakuchukua kwa staili ya ku-kuua kama maremu mabaraka sasa sijui anakupeleka wapi
  mwandishi naomaba kiungwana tuu unifahamishe only if you have a little idea of justifying kwamba mabaraka alichukuliwa na mungu
  asante sana

 3. Bob Sankofa Says:

  Hii ndiyo picha yangu ya kwanza kuiona yenye taswira ya Mbaraka. Alikufa mwaka moja kabla ya mimi kuzaliwa, nimekulia kwenye nyumba ya wapenda muziki na toka nikiwa mdogo nilikuwa nikisia sana jina la Mbaraka Mwinshehe na kusikia kazi zake lakini sikuwahi kuona taswira yake. Hii ni ya kwanza katika miaka 27. Asante Bongo Celebrity.

  Pamoja!

 4. Farida Says:

  Nadhani kuna kila sababu ya kumkumbuka Mwinshehe,muziki wake haushi hamu hata kwa watoto watakozaliwa,Wanamuziki jaribuni kuiga mfano wake siku zote mtakuwa mpo juu hata kama hamtakuwepo duniani you will be remembered by next and next generation.Thax Bongo Celebrity tumemjua vizuru gwiji la muziki.

 5. stambuli Says:

  Nashkuru kwa kutuwekea hiyo picha hapo juu,naungana na muungwana aliyetangulia kwa kukiri kwamba hata mimi ni mara yangu ya kwanza kuona wajihi wa mbaraka mwishehe,ni mmoja wa wapenzi wa nyimbo zake tangu nilipopata fahamu ktk dunia hii,huwa namfananisha na Jabali la muziki-Mar.Marijani Rajab kwa kweli uwezo wa kutunga,kuimba,kupiga ala ya muziki na kupangilia muziki ulikuwa ni wa hali ya juu.Nyimbo zao hazichuji utafikiri albamu imetoka leo.Keep it up_bongo Celebrity

 6. ndesanjo Says:

  Ukiacha muziki ambao aliuweza (kuandika mashairi, kupanga vyombo, na kudonoa hilo gitaa), nimegundua pia kuwa alikuwa anajua kuvaa. Na pia alikuwa na “jicho,” si unaona picha ya mwenzi wake?

  Asanteni kwa kutukumbusha hazina moja ya taifa letu.

 7. Ally Says:

  Ebwana ndio mi mwenyewe sijawahi kuona picha ya huyu bingwa mi sinikadhani savimbi hahaha dah baab kubwa mi namkubali sana nyimbo zake mi mwenyewe bwa mdogo lkn nazikubali kama zimepigwa jana nyimbo ujumbe bwana japo ule mdundo ukiusikia unajua tena hii kitambo!ndio mzee.

 8. kabukalilo Says:

  sijui hata nianzeje,lakini niseme tu kuwa nyinyi mna AKILI za ziada,yani mna akili pita kiasi kwa jinsi mlivyofikiria hatimaye kuamua kuitoa historia na picha za Mbaraka Mwinshehe,hakika mimi binafsi napenda na ninasikiliza sana miziki ya Mbaraka lakini sijawahi muona katika picha mana alikufa miaka miwili kabla sijazaliwa, kwahiyo hii ni mara yangu ya kwanza kuiona picha ya mbaraka,aisee!! kumbe kidogo alifanana na mzee jangala huyu muigizaji maarufu na mkongwe hapa nchini,

  nimefurahi na nimewapenda sana mzidi na mzidi,naamini kama mmeweza ya Mbaraka basi mnaweza kutuonyesha ya Nico Zengekala wa iliyokuwa Juwata Jazz

 9. Freddy Macha Says:

  Wakati nikisoma kidato cha tano Mzumbe mwaka 1973; ndiyo mara ya kwanza kukutana maso kwa maso na Mbaraka Mwinyishehe. Alikuwa na desturi ya kuja kupiga shuleni kwetu na bendi yake. Ikifika haftaim alikuwa akituachia vijana (enzi hizo nikipiga na bendi ya shule iliyoitwa “Earthquakes”) vyombo ili tujifae. Akitupa moyo.
  Mara ya kwanza kabisa, basi kupanda jukwaani na bendi, ilikuwa kwa ihsani ya marehemu Mwinyishehe, Simba wa Morogoro, msanii, asilia Mtanzania, fahari ya Wabongo. Mtunzi. Mpenda watu. Pongezi na heko kwa kutuletea habari zake…

 10. Oganzo Says:

  Ahsante sana kwa kutukumbusha mwimbaji huyu ambaye alipendwa Afrika nzima. Ningependa kusikia baadhi ya nyimbo zake. Huku nilipo, sina jinsi ya kusikia nyimbo hizi ila kupitia kwa Bongo celebrity. Pongezi na Heko!!

 11. Qasem Al-Majita Says:

  Kama alivyo Pele kwenye soka la dunia, Muhammad Ali kwenye ndondi za dunia, Shaaban Robert kwenye fasihi ya Kiswahili, Mbaraka anabaki msheherekewa (celebrity) wa nyakati zote. Alipiga gitaa na kuimba – kitu amvacho wachache wa bongo flava wanadiriki kufanya. Kwanza Bongo flava nini kama siyo maadili ya kutuelekeza kupoteza utamaduni wetu. Naungana na mdau Gabriel hapo juu anayeshauri tufuate mifano ya kina Mwinshehe, Saida Karoli, Maringo na wengineo.

  Maringo – uko wapi? Udumu (Ndolela…)

 12. Mkabahati Says:

  Jamani,
  Sijui niseme nini kuhusu huyu Super staa wetu. Well, mi nilisikia nyimbo za Mbaraka for the fist time on a long journey from Dar to Botswana tulikua kati kati ya Zambia huko. Nakumbuka i asked my dad a lot of questions about the guy..wimbo wake wa mtaa wa saba really stood out. Since then nina cds mbili za his hits which i listen to on my lazy days. Thank you so much Michuzi for bringing our Morogoro Legend back..we all miss him soo much. I bet huko aliko he’s doing live shows 24/7! By the way aliacha watoto hata..?

  Stay blessed.

 13. Mama wa Kichagga Says:

  AMA KWELI KIFO KAUMBIWA MWANADAMU! BAADA YA MIAKA 60 NA SISI WOTE HAPA BC TUTAKUWA TUMEKUFA WOTE! TUISHI KWA HAKI NA AMANI HAPA TWAPITA TU NI KITUO CHA DALADALA HIKI TUSIJISAHAU JAMANI!

  Sauti, nyimbo na maadili yaliyomo kwenye tungo alizoacha huyu shujaa wetu, Mazalendo na mwanamapinduzi Mbaraka Mwinshehe vitadumu milele na ni kielelezo cha mchango wake kwa jamii ya watanzania ndani na nje ya nchi.

  Wakati umefika sasa tubadilike wote na tufanye kazi kwa faida ya vizazi vijavyo! Naamini wapo wazalendo wengi sana Bara na Visiwani waliokuwa na vipaji hivi na ambao hatuachi kuwakumbuka mara tusikiapo zilipendwa (bado zinapendwa haswa).

  Wazo langu hapa ni uwezekano wa kuwa na MAJUMBA YA MAONYESHO MBALIMBALI (Jumba la historia ya taifa, NK NK), liwe kubwa kwelikweli na tuhifadthi mambo haya yote kuanzia mimea, wanyama wetu tulionayo, tamaduni zetu, watu maarufu.

  Shughuli zinazoweza kufanyika ni pamoja na:

  a: kwanza kabisa maeneo haya yasiwe na kiingilio ili kumpa nafasi kila atakaye kuingia/kutembelea asiwe na kikwazo

  b: watu binafsi watengewe maeneo ya biashara na walipishwe kodi ili mapato yatumike kuendeleza mradi husika

  c: Biashara za vyakula mbalimbali/restaurants, maduka ya nguo na vitu mbali mbali za KITANZANIA TU JAMANI NA SIO VINGINEVYO KWANI HII ITAKUWA NI SEHEMU YA UTAMADUNI WETU, MADUKA YA BIDHAA ZA MUZIKI, MADUKA YA VITABU VYA HADITHI NA SIMULIZI ZA KITANZANIA NA WATU MAARUFU WALIOLITUMIKIA HILI TAIFA KM BABA, MWANAMAPINDUZI, MUWAZI, MZALENDO, …………..& MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE, MWANAMKE WA SHOKA BIBI TITI MOHAMED, MBARAKA MWINSHEHE NA WENGINE WOTE WALIOTEMA CHECHE ZA MAENDELEO HAPA NCHINI NA TAARIFA ZAO KAMILI. PIA HATA WALE WALIOFANYA VIBAYA TUNAWEKA HISTORIA ZAO ILI VIZAZI HADI VIZAZI VIJIFUNZE!

  FAIDA ZA MIRADI YA NAMNA HII NI PAMOJA NA:

  1. Kubooresha utalii (sio kila mtu anataka kwenda mbugani bwana)

  2. Kuwa kama vituo vya Elimu kwa wanafunzi na watafiti, wageni

  3. Kuwa na maeneo ya kutembelea siku za week-end kwa wakazi

  4. Kutengeneza ajira (wahudumu ndani ya mradi)

  5. Kuongeza mapato – ya sekta mbalimbali km uandishi, uimbaji-kanda, watu binafsi(biashara) nk

  6. Kuwa na mahala pa mapumziko kwa kuchangamsha akili wananchi ili kupunguza “Mifadhaiko (Stress) ya maisha” na kujenga mishikamano ya familia (matembezi ya familia).

  7. Kuhifadhi historia yetu

  JAMANI NAONA NIISHIE HAPA MAANA NIKIWAZA SIKUBALIANI NA HII HALI YA UMASKINI NA MFADHAIKO WA AKILI TULIONAO KABISA.

  TUNAZO RASILIMALI NA VITU VINGI VYA KUFANYA KILA MMOJA WETU NA KIWANGO CHAKE CHA ELIMU HATA KAMA NI CHEKECHEA AKAPAONA HAPA DUNIANI KUWA NA YEYE ALITAKIWA SIO KUISHI KAMA MGENI KISA MAISHA HUWEZI KUYAMUDU!

  HEBU KILA MTU ASIMAMIE VIZURI NAFASI YAKE NA AMUWAZIE MWENZAKE ZAIDI YA ANAVYOJIWAZIA YEYE!

 14. damassan Says:

  ivyo jamani hakuna hata vidio crip ya mbaraka mwishee,kwani alikwenda japan,ujerumani ivyo haziwezi kupatikana dvd au vcd kweli inawezekana jamaani, thenk’s mr michuzi kwa picha za king of lumba bong.

 15. watubwana Says:

  siri ya mtungi aijuaye ngata.MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.

 16. joseph abbas Says:

  nawapongeza san wadau kwa kujitokeza kupongeza nyimbo za mbaraka mwinshehe,kweli zinatisha.huyu jamaa alikuwa na kipaji cha aina yake.mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,amina.

 17. joseph abbas Says:

  wimbo wake wa “shida”ndo unanipa sana hisia za kuendelea kusikiliza sana nyimbo zake.mimi nawaomba wasanii wajaribu kuziimba tena nyimbo zake kama wanavyoziimba sana nyimbo za marijani rajabu.huu ni ukweli kabisa,,,,hakuna upinzani na nyimbo hizo kwa sasa.isipokuwa nyimbo za sasa hivi ni uhuni mtupu…….afanaleki…..!!!!!!!kifo hakina huruma…………

 18. Khalid Magram Says:

  Ahsante sana kwa kunikumbusha nilikotoka. Nakumbuka huu mziiki wakati napata mloo wa mchana hapo Gerezani mama ntilie.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s