BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DJ SEYDOU August, 29, 2007

Filed under: DJs,Muziki — bongocelebrity @ 3:56 PM

 

Kunako miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90, majina ya Ma-DJ yalikuwa makubwa kama ilivyo kwa wanamuziki wa kizazi kipya na cha zamani hivi sasa. Mojawapo ya majina hayo ni DJ Seydou(pichani). Yeye na DJ mwenzake aliyekuwa anajulikana kama DJ Yaphet Kotto walitamba sana na disco lao la RSVP Discotheque pale Mbowe (siku hizi Club Billicanas). Enzi hizo vijana walikuwa waende wanakokwenda usiku unakuwa haujakamilika kama hawatofika Mbowe kupata ladha kutoka kwa DJ Seydou na mwenzake.Jina lake halisi ni Saidi Mkandara.

Tofauti na Ma-DJ wenzake wa enzi hizo, yeye alikuwa sio muongeaji sana. Badala yake yeye alisifika sana kwa uwezo wake wa kupangilia miziki. Akianza vitu vyake alikuwa hakai mtu kitini mwanzo hadi mwisho. Uwezo wake wa kusoma ukumbi na kujua aweke muziki gani ulikuwa unawastaajabisha wengi.

Isitoshe DJ Seydou alikuwa akisifika kwa kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote mwingine enzi hizo. Kila jumamosi alikuwa hakosi kuibua kibao ama vibao vipya kutoka kona mbalimbali za dunia.

Hivi sasa DJ Seydou ni mshauri wa muziki wa sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Club Ambience ya Sinza na Sanaa Pub. Hazina ya muziki wa zamani na wa sasa aliyonayo haina mfano. Uliwahi kuhudhuria disco la DJ Seydou? Tupe kumbukumbu zako kwenye sehemu ya comments.

Pichani DJ Seydou akiwapa vijana historia ya burudani nchini Tanzania tangu enzi hizo mpaka sasa. Hiyo ilikuwa hivi karibuni wakati wa matukio ya WAPI pale British Council jijini Dar-es-salaam.

Baadhi ya miziki ambayo Seydou alikuwa akiipiga enzi hizo ni kama huu hapa uitwao Get Down on It wa Kool and The Gang. Asante msomaji wetu Daniel kwa kutukumbusha tune ya wimbo huu. Pia unaweza sikiliza vibao Midas Touch kutoka kwa Midnight Stars, Don’t StopTill you Get Enough kutoka kwa Michael Jackson, A Night To Remember kutoka kwa Shalamar, Kleer- Intimate Connection…


 

 

 

 

 

 

 

Picha zote kwa niaba ya Bob Sankofa. Kwa picha zaidi za matukio ya WAPI unaweza kutembelea blog ya Bob Sankofa http://mwenyemacho.wordpress.com

Advertisements
 

24 Responses to “DJ SEYDOU”

 1. michuzi Says:

  Hapa Bongocelebrity mmegota ikulu ya disko, yaani hata sijui niongezee nini. ngoja nijaribu..

  Enzi hizo ukienda Rungwe Oceanic Beach Resort ya Mzee Mwakitwange ulikuwa unakuitana na majina kama vile DJ Ngomely, DJ Pop Juice na wengine. Ukiosea jirani na hapo Rungwe, yaani Silver Sands, unakutana na kina John Peter Pantalakis, Choggy Sly na Kalikali ambaye baadaye alihamia YMCA.

  Ukienda Africana ulikuwa huangalii simba aliyekuwa anafugwa hapo, bali pia DJ Mehboob, wakati ukishuka mjini hususan Motel Agip na baadaye New Africa hotel ghorofa ya saba kulikuwa na DJ Emperor (huyu Joseph Kusaga bosi wa Clouds 88.4 fmunaemjuea), Boniface kilosa a.k.a Bonny Love na DJ Jesse Malongo (wa Club Afrique, London).

  Baadaye kidogo ikaja Space 1900 iliyoanzia hoteli ya Mbowe na kuhamia YMCA, na kuleta ushindani mkubwa kwenye fani ya muziki ambapo disko lilifunika kabisa muziki wa dansa. Vile vile ikazuka New Vision ambako DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela walitengeneza majina sio kawaida, huku wakimpa darasa DJ Young Millionaire ambaye sasa anatamba Star TV ya Mwanza akiwa na jina lake halisi ya Jacob Msungu, kwenye kipindi chake cha TV cha Roving DJ.

  Baada ya Space 1900 discotheque kuhamia YMCA, disko la RSVP Discotheque likazaliwa Mbowe na Ma DJ wake walikuwa mkongwe Saidi Mknadara a.k.a DJ Seydou, akisaidiana na DJ Yaphet Kotto.

  Kwa ufupi, pamoja na kwamba DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis wa hoteli ya Keys mtaa wa Uhuru walikuwa juu kwa vyombo vya kwanza vya kisasa vya disko, lakini ni DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto ambao ndio walikuwa vinara pale RSVP Mbowe. Yaani baada ya kuruka majoka kila sehemu uijuayo, lakini vijana wote wa Dar walikuwa wanakwenda Mbowe kumalizia usiku kwa DJ Seydou na DJ Kotto.

  Kwa ufupi huyu ndiye aliyekuwa baba wa disko Dar, sio pekee kwa uwezo usio wa kawaida wa kupanga muziki tu bali pia ngekewa ya kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote nchini.

 2. Ebbie Janson Says:

  Yes!..
  Michuzi hapa patamu lakini kidogo nikupe somo la huyu mkongwe wetu.
  DJ Seydou alianza shughuli hizi pale Sea View enzi za Sansui miaka ya katikati 70…akipewa muda mfupi sana kwani enzi hizo Afro 70, Safari Trippers walikuwa ndio ngome ya jiji ktk muziki. Maneno yote yalikuwa Princess pale mnazi mmoja.
  Nakumbuka mwaka 1980 Dj Seydou akishirikiana na Eddy Sally na Choggy Sly walianzisha disco pale Key’s Hotel hapo mjomba hakuna YMCA wala Msasani isipokuwa Mbowe Dj akiwa Gerry Kotto (sio Yafet Kotto), Africana na Seaview.
  Nakumbuka walifanya mashindano ya kucheza na mshindi alikuwa Golden hair (Abdallah) na Mosi Ally yule mkimbiaji wetu wa mita 100.
  Mwkaa mmoja tu walisambaratika! Choggy na Eddy Sally walikwenda Silversand na Seydou pamoja na Gerry Kotto waliungana kuunda kikundio kipya cha Space 1900 pale YMCA. Hapo ndipo Joe Janson na Kalikali walikuja ibuka hata ilipofika mwaka 1982, Space 1900 walihamia Mbowe. Kule YMCA wakawa wanapiga disco la mchana kwa vijana wadogo. Space wakafungua tena sehemu mbili New Africa na huko Moshi pale YMCA ama Moshi Hotel..
  Mwaka 1982 kweli madisco yalifunika kabisa miziki ya magita!.Msasani, Rungwe, Slversand,Italian club (clouds), Keys Hotel, Motel Agip, New Africa, Twiga Hotel, Dar Institute na sehemu nyingine kibao ambazo siwezi kuzimaliza.
  Seydou alikuwepo Mbowe hadi 1985 wakati Freeman alipoamua kufungua RSVP kuwaondoa Space 1900 ambao walihamishia makazi yao sewhemu mbili New Africa Hotel na Pale Maggot.
  Toka wakati huo Seydou hakuwa na mahala maalum kwani Space 1900 ilivunjika kutokana na matatizo ya ndani. Hata hivyo jina Space 1900 liliendelea kutumika na ndio vijana wengine akina Super Deo,Young Millionea wkaibuka.

 3. Bob Sankofa Says:

  Shule hizo mbili zilizotangulia hapo juu ni historia tosha. Lakini BC, nitafurahi zaidi mkiweza kumtia DJ Seydo mkononi na kumpiga mahojiano, tusikie toka kwa perspective yake.

  Kutokana na wachangiaji wawili hapo juu inaonekana wegine tumezaliwa katika kipindi ambacho Disco lilikwisha poteza ile ladha ya “disco”, au naona hivyo labda kwa sababu sikuishi wakati halisi wa Seydo? Wengi siku hizi tunakwenda sana disco lakini hatuwajui ma-DJ wetu kama mnavyowafahamu wa kipindi kile. Maana kuwa na historia ya mtu fulani sio mchezo.

 4. danieli Says:

  I’ve received this news with a mix of nostalgia, sadness and gratitude. Ni furaha kumuona huyu icon wa enzi zetu za disco bado anadunda–wengi waliokuwa kwenye fani ile walishadedi shauri ya fast life. Nostalgia kwa kutajwa hizo kumbi ambazo ukiingia ndani beats zinaubox moyo wako directly–wao,man gedanonit, geddannonit, whwatyagonado ifyoudon’wanna dance bystannndin’ on the waaall!Sadness kumuona seydou amekuwa kinyume sana na yule shupavu mkandamiza-santuri, ningependa kumuona pamoja na umri lakini yuko yuko kama trade ilivyo, kama mzee syke tumuonavyo na li-bike lake na hereni shingoni, get me?

 5. Shukrani kwa Michuzi na Ebbie Janson kwa historia ya kuvutia ya disco Tanzania.

  Kama kuna mtu hajaelewa Daniel anaongelea nini ni kwamba tune ya muziki alioutoa hapo ni ule wimbo maarufu wa kundi la Kool and The Gang ujulikanao kama Get Down On It.Unaweza kuusikiliza muziki wenyewe na mingineyo mwishoni mwa habari ya Seydou.Asante Daniel.

 6. Juma Maringo Says:

  Ee bwana hapa BC mmeniacha hoi kwa furaha.Hiyo miziki imenikumbusha mbali sana.Enzi hizo ukisikia disco ni disco kweli.Habari na miziki namna hii poa sana.Keep it up guys!

 7. muddy Says:

  BC ‘keep it up’ baada ya DJ Seydou tupeni pia vitu vya Ma Djs wengine wakali wa enzi hizo wapo wapi na wanafanya nini kwa sasa!

 8. fidelis m tungaraza Says:

  fidelis m tungaraza Says: August 31st, 2007 at 6:46 am
  Mlionitangulia asanteni kwa michango yenu. Nami naomba nichangie kwa sababu disco era ndiyo ulikuwa wakati wa ujana wangu. Na ndiyo kilikuwa kipindi cha disco haswa kuanzia New York (Saturday Night Fever). Kati ya mwaka 1978 na 1985 baada ya hapo Break Dance baada ya Break Dance sijui la kusema…

  Safu ya Madj wa wakati huo kwa ninaowakumbuka miye walikuwa kina Justin Kussaga (SANSUI hadi BIRIBI/CLOUDS toka Sea View mpaka Italian Club). Eddy Sally(FM Disco), Gerald-Gerry Kotto- (Mbowe au kwa jina la utani wa wakati huo CHOONI), John Bure(Rungwe), Mehboo na Clemency/t?(Gogo Disco na Floating Bar, Africana), Abby Sykes(Blowout Disco, YMCA), Ebonite WooJack(Uptown, Disco YMCA)baada ya haya madisco mawili ndipo Sudi Mwarabu akaleta Space 1900 YMCA, Madj Gerry Kotto na Seydou. Madj hawa wawili walikuja na staili mpya kabisa ya kupiga chapati (santuri) na dawa za mbu (kanda) huku wakidansi behind the Dj desk. Kwa mtakao kuwa mnakumbuka mtakumbuka ndiyo waliokuwa madj wliokuwa wanachoreography dansi zao na wanaovaa sare ya kazi maovaroli. Jamaa walikuwa watamu sana.

  Ok Tuendelee, Msasani Beach lilikuwepo disco la Marehemu? Nassoro Born City (Nasikia alifariki mwaka jana sina uhakika). Hapa ndiyo walipoingia kina Choggy na John Peter na baadaye Nigger J na Kalikali. Au siyo?

  Kama sijakosea mwaka 1982 au 83 likavuma JeSet Disco na Dj Rusual na Baadaye Young Omar, Msasani Beach Club. Ninaweza kusema mpaka sasa hivi katika historia ya burudani ya muziki hakuna disko wala bendi lililowahi kutengeneza matangazo makali kama JetSet Disco. Kwa mnaokumbuka mtaweza kukubaliana nami. Nadhani kazi ile ya matangazo ilikuwa ni ubunifu wa Mzee Fred Jimmy Mdoe na mwenziye Bwana Bakari Omari. Jet Set hawakuwa na miziki mizuri lakini walijua kutengeneza aina ya wateja na mashabiki.

  Wakati wote huo Princess hotel kulikuwa na Parliament Disco la kina Joe na Eddo. Nilichokuwa nakizimia Parliament Disco ni mafunk beat waliyokuwa wanayabaruza. Halafu lilikuwa disko la watoto wa mjini sina maana mbaya katika hili lakini lilikuwa ni disco la watoto wa mjini kwa maana ya watoto wa mjini kweli.

  Bila kusahau Pango Disco, Rex Hotel Clock Tower na lile la Continental Hotel, Nkrumah Street.

  Zama ninayoizungumzia hapa mahoteli ya ukanda wa pwani ulikuwa bado umeshikwa na mabendi isipokuwa Rungwe Oceanic kwa Dj John Bure.

  Yakaja madisko ya maghorofani Motel Agip na New Africa Hotel. Madisko haya ndiyo yaliyokuwa ya mwisho mwisho na wateja wake zaidi walikuwa vijana wapya wapya, sina maana mbaya kwa kuwaita wapya wapya. Walikuwa wapya kwa sababu hawakuwa maaluatani wa jiji wengi wao walitokea mitaa ya ushuani na attitude za kiushuani. Kweli si kweli?

  Bendi zilizotamba wakati huo: Brass Construction, Con Funk Shun, Earth, Wind, and Fire, The Isley Brothers, The Jacksons, Osibisa, Ross Royce, Soul Brothers, Lakeside, Kool and the Gang, Commodores, Orchestre Veve, Super Mazembe, Le Mangelepa, TP Ok Jazz, The Parliament, Fela Ransome Kuti and Afro 70, Simba Wanyika, The Wagadugu, Bunny Mack, Third World, Zappow. Jamani, nisaidieni nimezeeka kumbukumbu inavia. Madisko ya wakati huo miziki ilikuwa mchanganyiko lakini miziki ya Kimarekani ilikuwa ndiyo inatawala.

  Mziki iliyotamba You can do it, Kulukuni, Moni afinda, Shakala, Sina makosa, Let me love you, Sweet mother, Easy dance, Ladies night, Sail on, Why you wanna try me, You give me fever(Love to love you darling), What you waiting for, Shake your body down to the ground, Lift up the roof, Holding on, Love’s got me dancing on the floor,This is reggae music, Night fever, Staying alive, na mingineyo mingi.

  Asante sana kwa kutukumbusha mbali.

  F M Tungaraza.

 9. julius. L Says:

  Kweli huyo mtaalam wa hapo juu, F M Tungaraza, amesema na mimi nimemsikia. Kwa kifupi kamaliza yote, “BC” mnatukumbusha mbali sana, kumbukumbu zenye kuleta furaha, na zile za majonzi kwa wakati ule “nilivyokuwa natoroka nyumbani kwenda Disko, mfukoni nikiwa na pesa ya kiingilio tu, sina pesa ya soda na wala sijui nitarudi vipi nyumbani” na nikifanikiwa kurudi nyumbani kwa kudandia lifti za washikaji, najitayarisha kupokea viboko kutoka kwa wazazi.
  Keep it up BC Mnafanya kazi ya Pongezi.

  JL

 10. Ebbie Janson Says:

  Tungaraza, inabidi tuwasiliane..maanake umemaliza darasa zima la ma disco, duh mozo weee!
  MD ukiwataka hawa jamaa wote wasiliana na mtu mmoja anaitwa Kim and the boyz at 255-78715560 Mtoto wa mjini atakupa data zote.

 11. zungu Says:

  ningependa kukumbushia list kamili ya clouds enzi za motel Agip,bahari beach nk.MOTEL AGIP djs walikuwa DJ EMPEROR(Boss wa CLOUDS FM),DJ BABYFACE (Boss wa CLUB AFRIQUE LONDON)na DJ JT (Julius Tandau)BAHARI BEACH walikuwepo ma djs BONNY LUV pamoja na ALEX SHABA

 12. f m tungaraza Says:

  Ebbie Janson,

  Umenistua na hiyo “..Mozo weee!..” Hiyo Mozo wee wape pia wakongwe wengine wa madisko kama kina Justin, Gamba na Joseph Kussaga, Super Deo, Deo Kiuno, Machumu Spear aka Alhadji Sulemain Ladha, Mkandaras i.e.Seydou, Siri,na Abdallah, Ray Mtimba, Kidai, Pius Ntare, na Bonny ‘Luv’ Kilosa wataielewa.

  Nilipomaliza kuandika nikakumbuka pia kulikuwa na Studio 55, Dj Ali Kayaya na baadaye Cool Joe. Halafu lilikuja Airbone disko la mafundi ndege au marubani wa ATC walitoka Holland kusoma lilikuwa pale Forodhani Hotel.

  Nikakumbuka pia JetSet nilisahau kumtaja Dj Ibrahim Killer. Gerald, Killer, na Karl(Mzungu) Maboblish walikuwa na show zao ya viatu vya magurudumu.

  Halafu madisko ya maghorofani lilikuwepo XTC Disco la kina David Kiango na Eddy Jackson Twiga Hotel. Hili lilikuwa disko la kibillahtiih haswa!

  Kumradhi, Julius L wewe Julius L yupi? Nikikupa hint ukazipatia basi tuwasiliane. Ok, wakati wa halftime Uliwahi kula chips dume na maembe ya Mzee John? Kunywa chai na chapati Girl Guide? Tangawizi na maandazi nje ya fensi ya shule? viazi mbatata vya Mzee Machale? Na aisi krimu za vifuko za kwenye madeli na chachamawa?
  Nyumbani kwenu kulikuwa pale kona? Marehemu Juma mlikuwa mnaishi mtaa mmoja. Marehemu Adili mtaa kabla ya wa kwenu ukitokea shule? Kama ndiwe na ungependa tuwasiliane chukua mawasilano yangu kwa moderator BC.

  PS/ KUNA JAMBO NASHINDWA KULIELEWA..HIVI KWA NINI HADI HII LEO CLOUDS DISCO, MSONDO NGOMA, IKHWAN SAFAA NA THE TANZANITES HAWAJAPEWA TUZO YOYOTE KWENYE KILIMANJARO AWARDS KWA UTUMISHI WA MUDA MREFU KATIKA FANI YA MUZIKI TANZANIA? SANSUI-BIRIBI-CLOUDS DISCO WANAFIKISHA TAKRIBANI MIAKA 35, MSONDO MIAKA 45, THE TANZANITES MIAKA 40, IKHWANI SAFAA MIAKA 101, MIAKA MIA MOJA NA MOJA! NAWAOMBENI WAZEE MLIOKO UWANJA WA NYUMBANI HAMASISHENI HILI SUALA!

  F M Tungaraza.

 13. zungu Says:

  JAMANI MSIMSAHAU DJ PAILONGA MZEE WA PAMBA MOTEL AFRIQUE JIRANI YA VISION

 14. dj tom in japan Says:

  mhhh niko form one pale forodhani sec school,natoroka nyumbani na kurudi home kimya kimya tena kwa kuruka ukuta,dingi akinistukia basi halali na ananisubili the whole night akiwa na zana zote za kivita!!!!
  unacheza disco pale maggot huku uliangalia saa usije ukalimiss UDA la mwisho,na likija limeshajaza lumbesa toka huko lilikotoka !!! mambo yenyewe ni kunin`ginia mlangoni kwenda mbele, mabasi ya UDA wakati ule yalikuwa hayana mlango wa kufunga ni open door style, konda akija unatoa kitambisho cha mwanafunzi kumbuka time hiyo ni saa tano usiku basi usubili vagi la konda!!!!!!
  wee acha tu hayo ni mambo ya 80’s bwanaaa!!!!

 15. Isaac Kibodya Says:

  Fidelis asante sana kwa kumbukumbu nzuri, kwa sababu nimezisoma habari zote za mwanzo na kuzifagilia sana ila moyoni nikawa nasononeka kwa kuto ona habari za Disco Parliament. Hili hasa lilikuwa disco la watu wawili Eddo (baharia)mtafutaji na Joe Shawa mhangaikaji yeye hakusafiri alibaki nchi kavu kutesa.Wakati Eddo alipokuwa akija nchini basi alikuwa anashika shika vyombo na yeye lakini shughuli hasa ilikuwa ya Big Joe na DJ Slaughter!
  NA wala hukukosea Fidelis pale uliposema hili lilikuwa disco hasa la watoto wa mjini kwani hata Fabulous Four wakina Sabrina wakitoka Rungwe lazima wapite Parliament kabla ya kwenda kulala! Na hili ndilo trupu la shoka kwani Joe alikuwa na wasaidizi wengi na wote watu wa shughuli hasa hasa magorofani Lumumba na wasichana wote waliokuwa wakija Princess.

  Man! mmenikumbusha mbali mno..nami bado mwana Parliament ndani ya moyo wangu!

 16. stambuli Says:

  Nawafagilia washkaji wote(Vijana wa Nyerere) waliotupa History ya huku nyuma kwetu ni somo tosha kwa sisi vijana wa(Mzee Ruksa),ama kweli mli enjoy ujana wenu,Naona kama ndio ukimwi ungekuwa umeshika kasi kama kipindi hiki asingebaki mtu,watu wangepukutika kama senene,kwa maana nasikia Disco lilikuwa halinogi bila totoes pembeni.

  By Stambuli(Jam Stam)

 17. LAF Says:

  Wakongwe kuna hawa ma-dj wa siku nyingi Chris Phabby na Rachy Kutty (Rafa). Nakumbuka Rachy Kutty alikuwa JetSet Disco kule Msasani Beach Club. Inabidi kamati ya Kilimanjaro Music Awards ianzishe zawadi ya watu waliotoa mchango mkubwa katika fani ya disko na muziki Tanzania.

 18. Kikolo Says:

  Wachangia hoja mmenifurahisha sana kwani ma – Dj hawa walipokuwa wakivuma, vijana wa sasa wengi walikuwa wadogo. Wengine tulikuwa tukitoroka hata shule kwenda kwenye disco kwa Kalikali, Seydou na wengineo bila hata kuwajua sawasawa! Michuzi umenifurahisha sana kwa kusema Young millionaire ndiye Jacob Usungu wa Star Tv Mwanza.Endelea kutupa historia kama hizo.

 19. majaliwa Says:

  i am so embarased to get you blood asia, y not represent your country ?, you think one day miss india will com from tz ! if never in earth y you represent our country ? , 1st you dont know anything about our tz culture, u must feel shame (Stupid)

 20. Exuperius Says:

  Yaani,wadau mmenitoa chozi kwa kutukumbusha hayo ma-disco na ma-DJ wa enzi hizo za ujana wetu.Unatamani kama kungekuwa na uwezekano kurudisha wakati nyuma ili kwenda kuyarudi ma-funkies tena lakini wapi!!
  Tunashukuru kwa kutukumbusha tulikopitia.

 21. Kamala Says:

  Sasa ndugu zangu mmenipatia changa moto ambayo imenisimua ile mbaya kwa kunikumbusha enzi za ma DJ wa wakati ule. Pale Mbowe kulikucha na haswa akina DJ Seydou na wenzake walipokuwa wanatoa ngoma kama ile ya CHAKA KHAN (Ai’t No Body); basi stage ilikuwa inafurika kwa namna yake. Tusisahau na ngoma 3 za kupakatiana (Blues)na hapo Seydou alikuwa ni hodali kwa kukutangazia kwamba asiye na mwana aeleke jiwe. Doo! kweli ulimwengu ni mdogo!! Nakumbuka I used to admire Dj Seydou’s hair dooo (Afro). Keep up a work BC.

 22. Kamala Says:

  I meant! Keep up a good work BC. Regards

 23. Mossy Says:

  Jamani leo nimefika mbali sana au kwa kifupi nimekumbuka siku za nyuma.jamani enzi za Dj Seydou zilikuwa mwisho yaani enzi zetu,jamani vijana wa sasa naomba muige au mtafuteni mpate ushauri wake.Mimi nilikuwa sikosi enzi hizo disco.Nimefurahi sana kwamba bado anatambulika na kuheshimika.Si mwingine ni mie mpenda disco,Mossy.

 24. gasto Says:

  BWANA MDOGO FIDE TUNGARAZA NAONA HUJAMBO KWA HISTORIA, ILA UMESAHAU KAMA MBOWE KABLA YA KUJA SPACE 1900 DISCO KULIKUA NA DISCO AMBALO SIKUMBUKI JINA LAKE NA LILIKUA HALITANGAZWI GAZETINI WAKATI HUO BIRIBI LIKO MOBILE NAMAANISHA LILIKUA MARA LINAPIGA MUHIMBILI PARAMEDICAL NA NURSING PALE MBOWE KIPINDI HICHO ALIKUEPO MTU MZIMA DJ FRACO UKIPENDA UTAMWITA FRANCO SAFARINO B, BIRIBI IKAFIFIA IKAZILIWA CLOUDS DISCO PALE SALEDER BRIDGE,NDIPO SPACE 1900 IKAJA MBOWE MA DJ WAKIWA SEYDOU NA GERALD(JERRY KOTTO) KABLA HALIJA GAWANYIKA MZEE SEYDOU AKACHUKUA SPEAKER ZAKE NA KWENDA KUANZISHA DISCO LAKE AKIPIGA PALE CBE, NA SUDI SPACE AKAUNDA NEW SPACE PALE MBOWE MA DJ ALIKUWA GERALD NA JOE IKAJA VISION PALE USHIRIKA CLUB(MAGOT)


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s