BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TOP THREE September, 3, 2007

Filed under: Fashion,Miss Tanzania,Urembo — bongocelebrity @ 11:35 AM

Pichani ni washindi watatu wa shindano la hivi majuzi la Miss Tanzania 2007 .Baadhi yenu mmeomba kuwaona warembo hao katika picha za karibu zaidi kama hizi. Queen David alishika nafasi ya tatu, Lilian Abel ya pili, na Richa Adhia kuibuka Miss Tanzania 2007. Mahojiano nasi bado aliposhinda taji la mrembo wa Kinondoni bado yanapatikana hapa.

 

Queen David

 

Lilian Abel

 

 

 

Richa Adhia

Picha zote kwa hisani ya Michuzi.

Advertisements
 

53 Responses to “TOP THREE”

 1. Bob Sankofa Says:

  Naomba kuongeza kuwa haya mashindano mshindi huwa hapatikani kwa point za jukwaani pekee bali ushindi huanzia toka siku mtu anapochukua fomu za mashindano ya vitongoji.

  Point huendelea kunyakuliwa katika kambi wanazoweka dada zetu. Huko watu hawaangalii rangi ya ngozi tu kuna vitu kama unashirikiana vipi na wenzako, mawasiliano yako, kujituma (Maana kuna wengine hata kuamka asubuhi ni lazima waamshwe).

  Sasa nadhani Richa ameshinda kwa minajili kama hiyo. Hakushindia stejini peke yake ambako wabaguzi walio wengi walidhani ushindi unapatikania pale. Watu tumesahau kuwa kuna uzuri wa ndani pia, tunawehuka na rangi ya ngozi ya mtu.

  Mimi imenikera sana hii ishu ya kumbagua dada wa watu kwa rangi yake. Ilitakiwa tulalamike iwapo dada hakuwa Mtanzania lakini taifa linamtambua kuwa ni Mtanzania. India hawana raia anayeitwa Richa Adhia, Tanzania inayo mtu huyo.

  RADHIA NI MISS TANZANIA! Wabaguzi hameni nchi.

 2. Huu ubaguzi mbaya sana Bob.Nimefatilia hii kwa siku hizi 2 naona watanzania tunakwenda mbali.Tunavuka mpaka wa utu na kupendana aliotuachia baba wa taifa.Inasikitisha sana

  Nimeandika kirefu.

 3. Ruta Says:

  Bob umenena mwanangu!!! vichaa bado wengi nchi hii. Hawa ndo wale ambao watoto wao wakipata sifuri shuleni basi midomo mireeeefu kwa walimu ohhh kwa nini mwanangu hakuchaguliwa kidato cha kwanza. wakati anacheza wao aaa!

  Haya mambo ya utanzania yanakujaje? nani kati yetu aliomba azaliwe hapa na asizaliwe nchi nyingine? si imetokea tu by chance? hiyo mipaka ya nchi hii aliichora nani? karne mbili tu zilizopita wala haikuwepo. jina Tanzania wala halina zaidi ya umri wa nusu karne. Lakini watu watafanya ishu kuuuubwa ya kumbagua mtu kwa rangi yake utafikiri wao wamepewa hakimiliki ya nchi hii.

 4. Edwin Ndaki Says:

  Ila kweli ndugu zangu kweli leo hii tanzania tunaanza kuongelea masula ya rangi?

  kitakacho fuata hapa ni ukabila na udini.Inasikitisha shana.

  RICHA AMETANGAZWA MSHINDI CHA MSINGI TUMUUNGE MKONO.NAKEMEA KWA NGUVU ZOOOOOOOOOTE PEPO LA UBAGUZI NA LILEGEE!LISHINDWE KABISA

  Ene wei ni hayo tu naomba kuwasilisha

 5. dj tom in japan Says:

  ni wetu asingekuwa wetu tungeshamtimua kama yule miss arusha!!!

 6. Cindy Says:

  kwa hizo picha hapo juu Richa ametoka mrembo angalieni macho yake? hao wengine ni wa kujiremba na vipodozi hawajanivutia sana kwa kweli. Ubaguzi hauna maana wajemeni muacheni dada wa watu apeperushe bendera she dezevu it lol sio lazima ashinde mweusi muhimu ni vigezo jamani kaaa

 7. babygirl Says:

  asante BC kwa picha za karibu. Jamani ukiangalia pic zote hapo juu hata hao wa 2 na 3 yaani tuwe wakweli hawana la zaidi. Richa she is beutifu jamani no make up yoyote hata mascara kwenye jicho hamna. Ngoja tusubiri miss worl anaweza fanya maajabu hivi hivi. Watu wanpiga kelele kisa rangi sasa hao weusi wenyewe mbona wa kawaida tuu yaani mi sijaona kabisa. Siku nyingine wadau mtupatia hata videos kabisa za mckato mzima sie tulioko mblai tuone hata shughuli yenyewe ilikuwa vip ktk stage. Ni hayo tu namtakia kila la heri Richa ktk mashindano ya dunia.

 8. NDAKI Says:

  WADAU MLIFAHAMU HII KAMPENI YA WAHINDI WALIOIFANYA??
  MIMI SIKUJUA HEBU SOMA HIYO MAIL WALIOKUWA WAKISAMBAZIANA.alafu ndio mpate nafasi ya kujua nani wanafanya ubaguzi hapa tanzania.

  TATIZO LETU TUNAKIMBILIA JUU JUU TUANGALIE NANI KABAGULIWA.JE NI RICHA KABAGULIWA AU WAKINADADA WAZAWA NDIO WAMEBAGULIWA.

  LENGO SIO KUJUA NANI MCHAWI LENGO NI KUKEMEA KWA NGUVU ZOOTE AINA YOYOTE YA UBAGUZI

  SIPO TAYARI KUWEKA HEWANI MAJINA YA WADAU WALIOKUWA WAKIONGOZA HII KAMPENI HATA MKINITISHA KUNI-SAADAM HUSSEIN(KUNINYONGA)NGOMA INAANZA KAMA IFUATAVYO.

  To All Goans, My Family & Friends,

  Please vote for “RICHA” help her win the Vodacom Miss Tanzania 2007. She is No.6

  “Richa”- Rachel is born to a Goan Mum (Sakasia Fernandes) and Hindu Dad in Dar Es Salaam. She is the first Goan/Asian ever to participate in such a competition in Tanzania. With your help, she can go on to become an Ambassador, representing Tanzania at Miss World. Who knows she may even go on to winning Miss World!!!.

  Vodacom customers simply have to send an SMS with the number 6 to 15500. The contestant receiving the highest number of votes will become Vodacom Miss Popularity 2007 and will win Tsh 5 million. The customer who sends the highest number of votes overall for the winning contestant will win Tsh 10 million along with two VVIP tickets for the final show. The top 1000 voters – those who send the most number of votes for the winning contestant will each win two standard tickets to the final show.

  For the very first time, Vodacom customers have the opportunity to vote for their favorite contestant in the top 26 Vodacom Miss Tanzania finalists. The contestant receiving the highest number of votes will become Vodacom Miss Popularity 2007.

  “The aim of the Miss Popularity voting promotion is to give our customers an opportunity to get involved in the beauty pageant and select their very own Tanzanian beauty queen. The best part is that both the pageant contestants and voters win big prizes,”.

  The profiles of all the 26 contestants are detailed fully in local newspapers as well as on TV to allow voters to familiarize themselves with the beauties and thus appropriately choose their Miss Popularity.

  The Miss Popularity SMS voting promotion will close at midnight on August 26th, 2007.The winners of the competition will be announced through local newspapers on August 28th. Vodacom Miss Popularity 2007 will be crowned at the final show.

  “Each SMS costs Tsh 150, a small price to pay considering you can win Tsh 10 million! So start sending in your votes and increase your chances of winning big with Vodacom,”.

  VOTE VOTE VOTE FOR 6

  Please please vote for Richa No.6

  Many thanks and kind regards,

  (JINA NIMELIHIFADHI LA MUONGOZA KAMPENI)NI MDOSI.

  NANI HAPA NI MBAGUZI?
  KAMA WAO WALIKUWA WAKIPIGA KURA KUTOKANA NA UGOHA HUO SIO UBAGUZI?
  TUPAMBANE NA UBAGUZI NI HATARI SANA KWA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU

  NAOMBA KUWASILISHA

 9. kibanga Says:

  Mwe… yoyote ni miss tu. Ila Ni lazma tanzania ipanue mipaka na dar es salaaam ipewe kanda.. washiriki 9 wakitoka dar hamna ushindani. Richa.. hongera na uwe mfano kama ma miss South africans. We mtanzania mwenzetu tu!

 10. safisha Says:

  Hii ni burudani sana… ni kichekesho! comedy! Nakufa mbavu!!! hawa mabinti wa kibandu na huyu muhindi ni vitu viwili tofauti kabisaaaa, wala si vya kulinganisha. hawa wabantu wana uzuri gani kumpita huyo muhindi? HAKUNA!na Huyo mhindi anauzuri gani kuwapita hao wabantu? HAKUNA! Jamani hii ni comedy…! Ni kichekesho! Uzuri wa kihindi ni wa kihindi, Uzuri wa kibantu ni wa kibantu. Kati ya hao mabinti2 wa kibantu unaweza kutafuta mzuri zaidi ni yupi, lakini sasa huyu muhindi yuko peke yake ilitakiwa kuwe na muhindi wa 2 ili nao walinganishwe. Wenye kufikiri kwa mapana wamenielewa.

 11. naomi Says:

  miye sina hata cha kucomment naona bob kasema wabaguzi wahame nchi na kama wabaguzi hawapo nchini ila inawakera sasa itakuwaje? ila watu mlitegemea nini kamati nzima ya mamiss kuanzia majaji walikuwa kina kemcho. ofcoz lazima kemcho mwezio awin kila mtu huvuta kamba kwao. so hatuna la ziada zaidi ya kuukubali ushindi.. mwaka 2010 utasikia rais wa tz ni patel tu. mh jamani miye sio mbaguzi richa mzuri na anasitahili kushinda ila watz tufungue macho sio kwa mamiss tu bali hata kwa wabunge.

 12. Ubaguzi kitu cha ajabu sana!Unakihisi kikikulenga wewe, lakini ukimlenga mtu unasahau maumivu yake.Mkuki kwa nguruwe, AU?Ubaguzi wa aina yoyote ni noma , nukta

 13. Kinono Says:

  Mimi napinga kwa nguvu zote ubaguzi wa kila aina.
  Ila kwa upande mwingine siwalaumu sana hao wanaompinga RICHA. Hii inasabishwa na sababu za kihistoria na ndugu zetu wenye asili ya asia kutojichanganya na wa bantu asili.Nakumbuka wakati Mzee wetu Makamba alivyokuwa Mkuu wa Mkoa wa DAA aliwalazimisha washiriki na wanachanganye na wengine ktk tukio fulani la kitaaifa pale DAA. Aliwaambia waache kukaa kwenye viota vyao na wajichanganye na wenzao.

  Aidha ndugu zetu hawa wao ndio wanaoanza ubaguzi. Wanashule zao pale DAA ambazo ni za wahindi watupu.(GEREZANI). Kweli kuna shule nyingine kama Mzizima kuna wa bongo wa chache sana.Ila ujue kipaumbele ni wao na kama nafasi ikibaki ndio mbongo. Mimi nina mfano halisi wa mbongo aliyeambiwa waziwazi kwamba kama nafasi ikibaki ndio atapewa. Kwa hiyo sera yao ni wahindi kwanza mbongo baadaye.

  Lakini hii si sababu ya kumukumu RICHA, ila tumpe suport 100% labda ndio itakuwa mwanzo wa wahindi & wabongo kujichanganya. na wahindi acheni kubaua watu wasio na asili yenu na muache manyanyaso.

  HONGERA RICHA TUPO NYUMA YAKO PEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA.

 14. kasrea Says:

  NYIE WOTE MNAOMUUNGA MKONO HUYO MISS TZ HAMNA MAANA YAANI HAMUONI MBELE.TATIZO SIO RANGI TATIZO NI KWAMBA HII KITU ILISHAPANGWA TOKEA MWANZO NA NDO KWA MARA YA KWANZA TANGU MASHINDANO YALIPOANZA 1994 KULIKUWA NA WAHINDI WENGI KULIKO HATA WAZAWA WENYEWE. WHY IS THAT? WALISHAJUA NINI KINAENDELEA. QUEEN DAVID NDO ANGEPASWA KUWA MISS TZ KWA SABABU ANA SIFA ZOTE ALIZONAZO HUYO MISS WENU MWENYE DUAL CITIZENSHIP LABDA TU SIO “COLORED” KAMA MNAVYOTAKA. LOOK AT THE BIG PICTURE HERE SIO TU MNAROPOKA….
  concerned tza from kansas city

 15. Lisaraye Says:

  Richa, Has beauty and brains!
  Cut all the craps, racism and all stupidness….
  She has what it takes to be Miss Tanzania.
  Remain blessed and ol the best darlin.

 16. mkereketwa halisi Says:

  walioko ulaya na wabaki ulaya. ila give her a break kwasasa

 17. TanzanianDream Says:

  Ubaguzi Ubaguzi Ubaguzi,
  Asie mbaguzi aseme hapa yeye sio,au ubaguzi ni wa rangi tu????
  Personally sikubaliani na miss tanzania kuwa gabachori,huo ndo msimamo wangu kama unaona mi mbaguzi endelea kuona hivyo….nenda india kagombee huo umiss uone chance hiyo kama utapewa huwezi wakilisha kitu u dont reflect to….wenye uchungu wakiongea eti ubaguzi….
  ULiedhani hakuna ubaguzi wa rangi na dini unakosea sana the fact is everybody is racist,its only some admit n’ some dont hiyo ndo fact pekee kwahiyo acheni kufanya unafki hapa….

 18. mvumilivu Says:

  jamani people for the love of ya country give her a break maana haman tena che kufanya ndo hivyo kishatokea basi tukubaliane hata kama tuna uchungu na nchi yetu, we have to accept the fact that miss kabachori ni miss tz hata tufanayaje. so jamani tujikaze kwa sasa

 19. mvumilivu Says:

  we malangalila unashida gani jamani nimekuambia nchi huru hii wacha watu waseme kama umeoa mwindi basi pole sie tupo huru.. we ndo ukafe mbele huna hata aibu na utakuta mtu mzima ovyo kama kimekukera sana watu kusema wanachojisikia then usiingie huku huna haya.. kalale mbele

 20. nei Says:

  PEOPLE ONE MORE TIME GET A LIFE kama mngekuwa mnajitahidi na maisha yenu kama mnavyoshinda kwa compter kukandia watu basi i think nji yetu ingekuwa mbali sana na maendeleo by now. watu mko tayari kupata sugu za mikono just kumponda mtu mtajiju GET OVER IT

 21. Gloria kiama Says:

  huyo miss hafai kuwa mtanzani ni muindi piua lakini kwavile tume zoewa kutawaliwa kila siku nyie hamta shanga sasa akienda nchi za nje ataonyesha nembo gani ya tanzania? na nyie mfikirie

 22. nei Says:

  gloria get a life ameshachaguiwa kashachaguliwa mashindano hayarudiwi. hata miye naumia ila ndo hivyo too late to catch the train sasa train lishaondoka

 23. BEABIANKA Says:

  ivi lakini jamani tunadumishaje utanzania miss tanzania anatakiwa awe mtanzania halisi atumbagui wala ata chembe ila uko andapo atajulikana katoka tz au india mmmm apa kuna kazi ila tusubiri finally na mungu amsaidie apite.ila kwa kweli ingetakiwa awe real tanzanian hapa hatuzungumzii rangi ila !!!!!!!!!unationality hilo tui mimi naona niko tofati na wenza ngu ila hatumbagui kabisa tena twampenda sanaaaaaa!!!!na pia twampngeza ni mrembo na ana kila sababu lakini wahusika warejee tangu mwanzo wa compitation ili kusiwe na lawama mbona wengine hatusemagi?ila hili limegusa wengi kazi njema .

 24. Gloria kiama Says:

  narudia tena hana chembe hata kidogo ya kuwa mtanzania huyu acheni ujinga na kubana nafasi za watu maskini nyie.Hamna endelea kamwe kwasababu ya rushwa.

 25. FLORA Says:

  naomba turudi nyuma tukumbuke mamiss wetu wa miaka ya nyuma wakina jauquelin,nancy,wema na wengine wengi heeeeeeeeee!!!!!!!!!tudumishe utanzania bwana ela zote izo na gari.its ok next time tuwe makini maji yakimwagika hayazoleki,chonde,chonde,chonde,watanzania dumisha mila,

 26. mnzava Says:

  we gloria usituletee hapa we utatuthibitishiaje kama wewe una chembe ya huo utanzania si ajabu baba yako kazaliwa kongo au pengine malawi huko au si ajabu ni mkimbizi wa kihutu, usituchanganye hata kidogo na mambo yako ya chembe ya utanzania we unajua maana ya utanzania?

 27. Freddyjoe Says:

  Mnzava, huna haki ya kuwaita wenzio Paka.
  Tujadiliane/ debate kwa hoja siyo kashfa na matusi.

 28. nei Says:

  jamani hii miss tz imekuwa vita baina yetu? loh ebu watz tuacghe ujinga..tusije tukangoana meno bure jaamni kisa umiss

 29. mnzava Says:

  freddyjoe naomba radhi kwa kumuita jamaa paka ulimi hauna mfupa samahani sana.

  Ila unajua watu wengine kweli wanatia hasira bwana kwa maneno yao ya kibaguzi mpaka mtu unapitiliza. Na kwa upande mwingine freddyjoe nadhani neno paka is much more linient kuliko kumuita mtanzania mwenzio muhindi na kadhalika. Bora tuitane paka na mbwa kuliko maneno ya kibaguzi kama haya ya muhindi na mengineyo kesho keshokutwa watu wataanza hapa hape kuitana we muhaya we mchaga we muhehe n.k na hiyo ni sumu kubwa kuliko hili nililosema mimi. Nevertheless i apologize once again to you and to the person to whom i directed to.

 30. Mansu Says:

  Hongera sana Richa! Ni matumaini yetu
  kuwa utafika mbali kutokana na vigezo
  ulivyokuwa navyo.Wale wabaguzi wa rangi
  waendelee kulia tuu.Mbona hawaku-kupinga
  tokea unaanza kushiriki mashindano haya.
  Wanaamka wakati mechi imekwisha.

  Tofauti ya ushindi wako na waliokufuatia ni
  kama MBINGU NA ARDHI. “Keep It Up”

 31. Me naona hakuna mjadala wa kujadili, hata kama hatukubali Richa kuwa miss tz, ukweli unabaki kuwa hatutaweza kumvua taji hilo. Na lingine ni kuwa kwann hamkumtoa huko miss kinondoni? Tumwache Richa apeperushe bendera ya tz, najua kwa jinsi alivyo ataipeperusha vyema bendera yetu, au je kama atashinda Miss World hatutampokea kwa nderemo na shangwe kisa si mbongo? Tuachane na ubaguzi jamani. Namkubali Richa kwa nguvu zote.

 32. Noel (Paris) Says:

  Richa really did not deserve to win this. It is not about Race. It is about MERIT. Hata kwenye maswali hakuwa convincing at all.Lilian Abel answered the questions well and to my opinion alistahili kushinda.
  But anyway congradulations May it be the FIRST and LAST time….

 33. jennifer Says:

  hehehehehehe noel umenichekesha eti first na last time. we subiria mwakani atakuja mchina na utasikia wazazi wake wamezaliwa tz. miye yangu macho tu

 34. TanzanianDream Says:

  Kama Nyerere angekuwepo huu upuuzi usingefanyika ila kwa sababu nchi imeshikwa na wapuuzi ndo kila kitu HEWALA BWANA…No siwezi kumpokea mhindi kisa kashinda Miss World hata ashinde kitu gani siwezi acha kusema hastahili thats the KEY…Kama hajastahili mwanzo kwanini akishinda astahili…Nancy was crowned Miss Africa kwa kuwa Miss SA alikuwa mweupe naona muda umefika wa kuacha kusema hatubagui wakati tunabagua..Ok on the point Richa hastahili kwa sababu hana asili ya Tanzania kwisha kazi,hata huo Uafrica hana mnampa uTanzania kweli watu hatuamki….

 35. yasmin Says:

  Anaehoji uraia wa Richa angeanzia Bungeni,mwacheni dada wa watu.Hao mnaowaita raia hawana lolote hata wakipewa ushindi huutumia vibaya.Lakini Richa yupo kwenye modelling muda mrefu na hana skendo mbovu wala majivuno, she talks to every body!!sio hao mnaowaita raia vikipata umaarufu tu hujiona matawi…HONGERA RICHA ASIYEKUTAKA AHAME NCHI.

 36. jizzo j Says:

  Maana ya ambassador ni Mwakilishi ambaye ataonyesha to the world jinsi watanzania tulivyo sasa huyu Jamani sio watu wanaweza kuthania labda Tanzania ni jimbo fulani la India( Lahore or Bangalore) Mbona wasichana warembo weusi wapo wengi sana hatujaishiwa kiasi cha kuwakilishwa na mdosi, Mbona sijawahi kuona Miss India Mwenye Asili Ya kitanzania sisi ndio tunawahindi kwani Mbona hakuna miss Nigeria au Miss Kenya Muhindi wenzetu hao wanajali Uzawa zaidi si longolongo au kenya hakuna wahindi.

 37. jizzo j Says:

  Yeye angeenda kugombea Bombay au Kashmir Kwa bongo kweli kachemsha hata kama atakuwa miss world bado Tanzania haitapata sifa yoyote ile kwa sababu huyu aonnyeshi Utanzania wowote wazazi wote wahindi nafuu hata mmoja angekuwa Ngosha poa hivyo tusinge pinga Mbona Angela Damas alikuwa amechangany’a na haikuwa noma mbona Klynn pia the same bwana huyu si wetu ni wa Ramesh Patel

 38. jizzo j Says:

  Mi hapa naamuunga mkono Huyu Tanzania Dream Kweli Richa Hastahili kuwa ambassador wa tanzania labda ni Mrembo sana lakini Hawakilishi Utanzania wowote sasa kule watu watajuaje kwamba huku kwetu almost 90% kama zaidi ni weusi jamani tusitupe asili yetu kwa rushwa wahindi hawa hawa ndi waliopewa tender za Radar, Ndege ya Rais sasa wameshahonga mpaka Tutuwakilisha miss World Tumekwisha Kwanza Richa Mwenyewe Eskimo Mpeni Queen David atuwakilishe muda wa maandalizi bado unatosha

 39. mwanamapinduzi Says:

  Jizzo,

  Hebu tulia ukae ufikiri ikisha ndio useme, sio unaropokaropoka ovyo tu kama kwamba umekunywa maji ya chooni mwezi wa ramadhani.

  Kama unasema wahindi watoa rushwa basi wanaopokea rushwa ni viongozi wa nchi ambao sio wahindi. Kama ni tender za radar, ndege ya rais au hata kama ni barrick goldmine basi waliopokea rushwa ndio wameiuza nchi na ndio wa kulaumiwa – mbona huthubutu kwenda kuwalaumu? ingelikuwa hao viongozi wana msimamo na kukataa rushwa basi asingethubutu mhindi, mswahili, mwarabu au mzungu kuiteteresha nchi. Mbona nchi za wenzetu ulaya wahindi wala kabila lolote lile hawawezi kufanya wanayoyataka kwa kutoa rushwa? jiulize kwanza.

  Swala la Richa, basi ni mrembo mzuri tu na anaweza kuiwakilisha nchi yetu vizuri tu. Mbona miaka yote kulikuwa hakuna zogo mara hii tu? akija na ushindi basi wewe utaukataa na kusema uende India? hata siku moja – utakwenda kumpokea u/ndege. Ubaguzi umekujaa na kama ni hivyo basi unaelekea pabaya just shut up na unga mkono

 40. Ally Says:

  Watu bwana wanaongea sana bila kufkiri huyu ni mtanzania mwenzetu bwana na kuhusu cjui nani alipewa miss africa kwa sababu miss south africa alikua mzungu pale wamekwenda kugombea miss world not africa mbona south kisha chukua miss world na mzungu hamuoni?!big up richa

 41. Mpasua Jipu Pwaaaa! Says:

  queen david nadhani alistahili kuwa miss tanzania kwa maka huu 2007 maana vigezo vyote anavyo si mnancheki.na kwanza huyo miss tanzania richa siku ile alochaguliwa asilimia 99 walimponda palepale wakainuka na kwenda zao na nyie wala hamlioni hilo na hamjistukii kubwabwaja hapa katika blog orr rich ndio anastahili..hamjui lolote wengine kzi kufanta mkumbo tu..huyo lundenga hana la kusema kabaki hana la kujibu mara anajitetea ooh tumeona miss world wanaangalia vigezo vingi ambavyo richa anavyo..vigezo gani kama sio huo weupe na nyele za singa mpaka matakoni..msiwe mnabwabwaja tu na mambo hamyajui.

 42. Mansu Says:

  Mijadala mingine inabidi ijadiliwe kwa hekima.Namsikitikia huyu Tanzanian Dream
  anaongea kama vile kakatwa kichwa!

 43. jizzo j Says:

  Kama hayo ndio mapinduzi wewe mwanamapinduzi umefuka kama sio kuchemka Hivi huoni hata Binti kama Queen David angekuwa miss Tz hata inapendeza ni mrembo ana vigezo vya kutosha bonge la colour real African real Tanzanian akifika china huna haja ya kuanza kuuliza ohh mbona miss Tz ni mdosi mbaya kabisa ohh ohh nakuambia this time tutachekwa huko usiombe yeye Richa Eskimo Embu mcheki toto Queen may be na wewe umeolewa na mdosi or umeoa mdosi thats why unatetea au sister nini au wewe mdogo wake na Ramesh Patel nendeni kwenu India Kashmir kwani huko hakuna Umiss this time apokewi mtu U/ndege kwani amekuwa Nancy Sumari?

 44. jizzo j Says:

  Lets just stop debating then miss Tanzania ibadilishwe jina iitwe Miss LUNDENGA or Miss Ramesh Patel naona wameshawachoka mademu wa kibongo kuwafanya vimada ili wanyakue mataji this time wamejipatia demu wao wa kidosi nyie mnalumbana wenzenu may be this time wanakula uroda wa Richa hatujui kwanza mi nipo Arusha huyo Richa labda awe Miss Dar imekuwa kero

 45. mwanamapinduzi Says:

  Jizzo J

  Unatakiwa uende shule ukasome, maana chuki na ubaguzi unakufanya usione hata mbele. Kama unazungumzia uzuri wa richa haufai basi zungumzia kwa vigezo hivyo – sio kwa misingi ya ubaguzi. kama ni MERIT basi yeyote yule ambae angelichaguliwa basi kungelikuwa na mjadala kwani kila group la watu lina mtu wao… naona kama hufahamu wewe.. kama ni misingi ya ubaguzi basi si mada hata yakuzungumziwa kabisa – nyinyi wabaguzi hatima yenu itakuwa kama ya Uganda enzi ya Iddi Amin alipofukuza wahindi ikisha baadae wakaitwa – eti warudi kuchukua mali zao kumbe nchi iliwashinda… na wewe hasama zako hizo achana nazo – tafuta maisha maana una njaa tupu.

  Hakuna mhindi atakae kwenda India – ndoto zako hizo za kibaguzi zitabaki kuwa ni ndoto tu!!!

  richa ni Ms. TZ – hata kama atakwenda kwenye mashindano ya Ms world huko pana watu walioendelea na wanaofahamu “multicultural community” na hakuna atakaeshangaa kwamba ni mhindi – labda kama ungelikwenda wewe basi ungalibaki kushangaa tuu eti huyu mweusi mbona anatoka ufaransa au huyu mzungu anatoka namibia.. usije ukenda huko ukachekwa ukatuaibisha – baki huku huku –

 46. Ally Says:

  Hahahah safi sana mwana mapinduzi maana huyu mtu anaweza akamuona tiery henry akakataa kama ni mfaransa au akamuona mark fish akasema huyu sio msouth africa ni kutofaham mambo tuu huyu mtu hajui kama waziri wa pesa wa kwanza tanzania alikua mzungu hahahahha.

 47. andejohn Says:

  hakyamungu mi sielewi ilikuwaje kuwaje miss tz ni mhindi lakini naelewa kuwa now watz ni kila sura,kabila na colour.now iam not saying that iam happy that out tz miss is lighter skin iam just happy that they have chosen someone young to represent so big p miss thing i root 4 u!

 48. anny mwiya Says:

  HI BABY BIG UP!!! DTN MIND BLA BLA JUST DO IT..I AM PRAYN FOR INSHALLAH GOD HE WILL GOING TO HELP YOU!!!! KEEP WELL… FROM ANNY……………….

 49. Chiki Says:

  NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!! SAUTI HII ILISIKIKA SIKU ILE ALIPOTANGAZWA GABACHOLI KUWA NDO MISS TZ. NA MIMI NARUDIA KWA NGUVU NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!
  NYIE MNAOMTETEA HUYU MHINDI WOTE NI VIJAKAZI WA WAHINDI, MTAKE MSITAKE. WOTE MNAITWA BOIIIII ( AU POIIIIIIIIII) THATS WHY MNAMTETEA. MBONA WATZ NI WAZURI SANA NA WALIJIBU VIZURI TUU!! ??? RICHA NNNNOOOOOOOOOOOOOOO!!! HATUKUTAKI, HASWA MIE NDO KABISA WANIPA KICHEFUCHEFU!!NOOOOOOOOOOOOO!! NA NYIE MNAOWATAWAZA WAHINDI NDO MNATETEA NYAMBAFU ZENU!!

 50. Nancy Mnzava Says:

  hako kahindi kenu sio wala nini inawezekana vp watanzania 2kawakilishe na mhindi hata kama ni katz lakini sio wa ukweli ukweli mtu mhindi kabisa,au kwa vile alikariri salamu ya kisukuma?!yaani hakyamungu huyo hata top 50 haingii.. mmeawaacha watoto wazuri kama kina lyilyi na queen kwanza majina ya baba zao yanaashiria ubantu sio huyo mhindi wenu mmetubore ile mbaya!

 51. Happy Says:

  Hata mimi na shangaa sana au hizo nywele na huo weupe ndio unawa changanya sija ona hata kigezo kimoja hakuni shawishi kuwa yeye ni mbantu hapo naona tume pigwa changa la macho.

 52. sexylicious Says:

  if we could turn back the tym,anyway Lundenga and yo fellaz i dont kno wat yu did,bt i hope yu wont repeat the same mistake,

 53. sexylicious Says:

  are you realy patriotics ama ni uzushi


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s