BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MUNGU IBARIKI TANZANIA! September, 6, 2007

Filed under: Soka,Taifa Stars — bongocelebrity @ 9:01 PM

 

Wote kwa pamoja, kama unavyowaona pichani ni celebrities. Majina yao hivi sasa ndio yametawala vinywa vya wapenda michezo, watanzania kwa ujumla. Wengine wamediriki hata kusema “utaifa” uko mabegani mwao hivi sasa.

Jumamosi hii kuanzia saa tatu usiku, timu yetu ya taifa ya soka ambayo inajulikana kwa jina lisilo rasmi la JK Boys, watateremka dimbani kukabiliana na majirani zetu kwa upande wa kusini, Msumbiji, katika mchezo muhimu wa mwisho katika kuwania tiketi ya kucheza katika fainali za mataifa ya Afrika 2008 zitakazofanyikia nchini Ghana mwakani. Mchezo huo utafanyikia katika uwanja wa taifa mpya na wa kisasa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000.

Mara ya mwisho Taifa Stars ilishiriki katika fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 zilizofanyikia nchini Nigeria. Je vijana wetu watatutoa kimasomaso hiyo jumamosi? BongoCelebrity inaungana na watanzania wote popote walipo, kuitakia kila la kheri timu yetu ya taifa. Go Go Taifa Stars!

Advertisements
 

6 Responses to “MUNGU IBARIKI TANZANIA!”

 1. Tenga Says:

  Naungana na watanzania wenzangu kuwatakia kila la kheri vijana wetu.

 2. stambuli Says:

  Timu ikipangwa vizuri,substitute za maana zikafanyika pale itakapoonekana kuna udhaifu,wachezaji wakacheza JIHAD, washangiliaji wakashangalia kama WENDAWAZMU Ushindi utapatikana Come rain come Shine.Tupo Home kwanini TUSISHINDE Kila kitu Chetu.Tupeni Raha TAIFA STARS.Mwisho Wacheni Choyo na Ubinafsi ukijiona umekaa sehemu huwezi kufanya cha maana toa pasi kwa mwenzio afunge mambo ya anao anao yamepitwa na Wakati.
  Na mambo ya kumwingiza mtu zimebaki dakika tatu tuyaache ,dakika tatu atafanya nini,Meck mexine alionekana mechi na uganda haendi na kasi ya mchezo kocha amwangalie sana akionekana mzito ampumzishe.Canavaro na Swedi mkipangwa pamoja mtulie msiwe na papara chezeni kama VICTOR COSTA.BIASHARA ASUBUHI JIONI WATU WANAHESABU MALI.

  Stambuli(jam Stam)

 3. I believe we can win the match.But we have to make sure that our defenders are well organized and they shoudn’t panic.Also the foward line must be active in order to score many goals.If we believe we can achieve.

 4. nachey Says:

  TFF VIPI? MPAKA SASA TICKET ZIMEISHA MANAKE NINI? SIJUI LINI WATU WATAKUA WASTAARABU BONGO

 5. Salim Simba Says:

  Boban,Nizar,Maftah na Babi!macho yetu kwenu Team work ndio siri ya mafaniakio!

 6. mwalimuzawadi Says:

  Sijui neseme nini…. roho zetu, mioyo yetu… mawazo yetu… fikra zetu na uzalendo wetu woote ni kwenu vijana wa Taifa Staaaz…enendeni mkaitende ile kazi mliyotumwa na watanzania kwa ushujaa…tuko tayari kwa matokeo yoyote na hatutawalaumu kwa chochote…mpaka sasa tunashukuru angalao mmetutoa aibu katika medani ya soka la kimataifa… gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooh!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s