BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TUMESHINDWA! September, 8, 2007

Filed under: Michezo,Soka,Wachezaji — bongocelebrity @ 5:47 PM

Pichani Raisi Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na wachezaji wa Taifa Stars na makocha wao alipowatembelea kambini kwao katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar hapo juzi.

Pamoja na kuungwa mkono na kila mtanzania, timu yetu ya taifa ya soka, Taifa Stars, imeshindwa kututoa kimasomaso katika iliyokuwa kampeni nzito ya kutaka kutupeleka nchini Ghana hapo mwakani kwenye fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Matokeo ni kwamba Taifa Stars imechapwa goli moja kwa bila (1-0) na timu ya taifa ya Msumbiji,(Mambaz). Kwa maana hiyo kampeni zetu kuelekea Ghana ndio zimefikia kikomo kwa mwaka huu.

Unadhani nini kimetokea? Kwa maoni yako kwanini Taifa Stars imeshindwa? Nini kifanyike kwa siku za mbeleni? Unauongelea vipi utaratibu mzima wa shirikisho la soka la Tanzania (TFF) katika uuzaji wa tiketi za mchezo wa Taifa Stars na Msumbiji? Ungepata nafasi ya kumhoji kocha mbrazili wa Taifa Stars, Maximo au raisi wa shirikisho la soka la Tanzania, Leodgar Tenga, ungependa kumuuliza swali/maswali gani? Tunaomba maoni yako.

Advertisements
 

8 Responses to “TUMESHINDWA!”

 1. Ally Says:

  Bud luck coz team yetu tulikuaka kwenye hali mbaya kutoka kwenye kichwa cha uwendawazim mpaka kwenye hii hali tuliokua nayo ya kwenda ghana ni mafanikio kiasi fulani tukae chini tuangalie tunafanya nn tena tuangalie wale vijana wamechaguliwa under 17 wakomazwe waje wafanye maajabu lkn tukitaka hawa ambao washakua wanajiona masuper star kila siku ndoto zetu zitakua za mchana,tff wajizatiti sio kila siku inakua story tuu watu wote bongo tunapenda mpira sasa kial siku wakitufanya hv tunasikitika sana yangu ni hayo.

 2. mweme Says:

  Nawapongeza kwa hatuwa waliofikia. Ushahuri wangu ni kuwa sisi kama Taifa, tuweke mkazo kwa soka la vijana wadogo, (tuwe na socca academy) ambazo ndio zitatupa wachezaji wazuri wanaofundishika kwa kila hali.

  Wachezaji tulionao wanakuwa ni ”wazee” hata kupokea mafundisho inakuwa vigumu. kwa wachezaji tulionao sasa Nisawa na umchukuwe kijana ambaye hakuwahi pitia shule kabisa na uanze kumfundisha hesabu za kiwango cha chuo kikuu. Je unatarajia atafahuru mitihani?????

 3. bernadeta Says:

  Congrats Taifa Stars, mimi nadhani timu yetu ni nzuri tu wala haina mashaka hata kidogo. Kufungwa kwa timu si hoja ya udhaifu wa timu ila game ndivyo lilivyo. Nina hakika tungeshinda sisi hilo game hata kama timu ingekuwa imecheza vibaya kila mtu angesema timu imekomaa.
  Nilikuwepo ndani ya wanja la taifa kushuhudia mechi. Kulikuwa na udhaifu wa hapa na pale lakini timu yetu ilicheza vizuri on average despite conceding early goal.

  Muhimu tff muendelee kuiimarisha hii timu ili ijenge confidence na maelewano zaidi kiwanjani nina hakika tutafika mbali. Wachezaji waliopo wala si vikongwe ni watoto tu na wanahitaji uzoefu zaidi. Kuhusu timu ya vijana hiyo iwe ndio mipango ya muda mrefu ya kuibua vipaji lakini kwa sasa bado timu yetu ina uwezo wa kufanya vizuri tu ikisimamiwa ipasavyo.

 4. TRII Says:

  bwana eee mmejitahidi,BIG UP,makosa madogo dogo tu yakujirekebisha,mlivuta washabiki tz nzima,hata wakina mama.next time you will go high.

 5. Bob Sankofa Says:

  Hatujashindwa, tumeteleza. Naifurahia grafu ya maendeleo ya mpira wa Bongo. Si mbaya kufungwa kwa sababu siku hizi hata sisi twashinda, si kama zamani tulikuwa tunafyrahia sare.

  There’s always next time. Maximo ashasema, lengo kuu halikuwa kwenda Ghana, bali kuirudisha Bongo kwa ramani ya mpira.

 6. salma Says:

  Hongera stars
  Tupo pamoja ,nyinyi niwazuri tuu kwani siku hizi tunasema kulikuwa na makosa pale na pale tofauti na zamani tulikuwa tukisema timu mbovu. Mpira ni mchezo wa makosa na namuamini Maximo atarekebisha tuu,
  Mi nafikiri hao wanaongea utumbo si wanasoka na ni mahamnazo kwani hawajui hata kama mpira unamatokeo ya aina tatu nikiwa na maana ya kushinda ,kushindwa na droo.
  Bwana stars mmejitahidi na tupo pamoja na tutaendelea kuwa pamoja kwa wabongo twapenda soka.
  Thanx to Maximo umetubadilishia timu .na umetupandisha mzuka ! hongereni sana jamani
  TUPO PAMOJA

 7. gvm Says:

  Hongera, Tanzania, Hongera Taifa Stars!

  Tumejitahidi kwa kweli, tofauti na siku za nyuma ambapo tulikua tunatoka bila point kwenye group, kumbukeni lile grupu nalo si la kubeza ohooooooooo…

  Point 8 si mchezo, amini usiamini watu wa Cameroon, Senegal, Nigeria na nchi nyingine za Africa zenye kiwango cha mpira wanaiongelea TZ kwasasa, na tukiwa huku na sisi tunapata kuchangia mada za michezo, sasa si tunafahamika? Heh, tunajivunia ati!!

  We huoni maendeleo ati mechi ya mwisho ndio inabaini nani anaenda GHANA 2008, tofauti na zamani,pengine tungeshajitoa zamani na 0 point at the bottom of the table.

  Cha msingi tushikamane na moto huu, na jitihada zielekezwe kwa vijana wadogo wakati na wakubwa wote wote tu, na rais aendelee kusupport nasi tupo pamoja.

  Tutawini tuuuuu

 8. tatu Says:

  Hongera sana Taifa stars pia hongera sana mh.JK bila wewe kutilia mkazo 2singefika hapo 2lipo Mungu ibariki Tz wabariki na wa2 wake.

  Taifa stars
  oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
  Tatu kitenge


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s