BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI September, 16, 2007

Filed under: Photography/Picha,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 1:19 PM

 

 

Upo msemo usemao picha moja huongea au ni sawa sawa na maneno elfu moja. BongoCelebrity tunakubaliana na hilo na hivyo katika jitihada za kuhamasisha ukuaji wa sanaa ya upigaji picha au photography nchini Tanzania na kwingineko walipo watanzania, tumeamua kwamba kuanzia leo, kila jumapili tutakuwa tunatoa kitu kinachoitwa “Picha ya Wiki” ili kuwapa nafasi wapiga picha professionals (weledi/wa kulipwa) na hata wale amateur (ridhaa au wanaojifunza) kuonyesha kazi zao kupitia hapa. Kwa hiyo kama wewe ni mpenzi wa sanaa ya upigaji picha, tunakukaribisha kututumia picha zako kwa kutumia e-mail yetu bongocelebrity at gmail dot com. Picha inaweza kuwa ya rangi au black and white na ukubwa usiopungua urefu 420 px na upana 600 px.

Picha ya wiki hii imepigwa hivi karibuni wakati wa tamasha la Fiesta na Ahmad Michuzi (Jr). Pichani ni mmojawapo kati ya wanasarakasi wa kundi la Wanne Star akifanya vitu vyake. Karibuni.

Advertisements
 

4 Responses to “PICHA YA WIKI”

 1. Tom Makori Says:

  Wazo bomba sana hili BC.Nimeipenda sana picha hii.pongezi kwa mpiga picha Ahmad.

 2. Dinah Says:

  Wow! hiyo picha bab kubwa!

 3. muddy Says:

  Si shangai kwa picha nzuri kama hii kwani familia ya Michuzi nayo imebobea kwenye fani hii ya upigaji picha kama zilivyokuwa familia za kina Manara,Mwakatika,Kiwelu,Zimbwe,watoto wa marehemu Omar Mahadhi Bin Jabir kwa kusakata kabumbu.
  Ahmad songa mbele!!!

 4. Bob Sankofa Says:

  Muddu umesahau familia ya kina Matumla pia.

  Ukitazama picha hiki ndio utagundua nguvu moja ambayo hakuna kitu kingine chochote katika ulimwengu wetu kinaweza kufanya isipokuwa kamera, kitu hicho ni KUSIMAMISHA MUDA. Ni kitu hiki pekee ndicho kinanifanya nipende sanaa ya fotografia.

  Ulimwengu unakwenda kasi sana, inapendeza unapokuwa na uwezo wa kuusimamisha ndani ya vipande vya sekunde, Michuzi amefanikiwa kwa hilo.

  Picha safi, wazo safi.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s