BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“WATANZANIA WENZANGU WANIUNGE MKONO”-RICHA September, 18, 2007

Filed under: Fashion,Miss Tanzania,Tanzania/Zanzibar,Urembo — bongocelebrity @ 11:59 AM

Takribani wiki mbili tu zilizopita, Richa Adhia (pichani) alitwaa taji maarufu la Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2007. Maswali mengi na majibu mengi yaliibuka kufuatia ushindi wake. Bado ni gumzo linaloendelea huku kila mmoja akiwa na maoni yake. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake bila tu kuvunja sheria, kumkashifu au kumtukana mtu. Hiyo ndiyo misingi ya ustaarabu.

 

Jambo moja muhimu ambalo sote hatuna budi kukubaliana nalo ni kwamba Richa Adhia ndiye atakayetuwakilisha watanzania wote katika mashindano ya urembo ya dunia (Miss World) tarehe mosi(1) Desemba mwaka huu huko Sanya nchini China.

Hivi sasa anapojiandaa kuiwakilisha Tanzania huko nchini China, tulipata fursa ya kufanya naye mahojiano mafupi kuhusiana na maandalizi yake na ujumbe alionao kwa watanzania na wadau wote wa masuala ya ulimbwende. Yafuatayo ni mahojiano kamili;

BC: Richa kwanza hongera sana kwa ushindi wako wa Miss Tanzania 2007. Ulijisikiaje baada ya kutangazwa mshindi siku ile pale Leaders Club?

RICHA: Asante nashukuru. Nilipotangazwa kuwa mshindi nilishikwa na butwaa na kwa sekunde chache niliona kama ni ndoto.

BC: Watu wengi wametuandikia wakiomba tukuulize swali hili. Kwa maoni yako unadhani ni kwanini majaji wa Miss Tanzania 2007 walikupa wewe ushindi na si wenzako mliokuwa mkichuana? Nini kilikusaidia? (more…)