BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“TUSIBWETEKE”-FRESH JUMBE September, 23, 2007

Filed under: Muziki,Tanzania/Zanzibar,Utamaduni — bongocelebrity @ 1:12 PM

Wengi wetu tumetokea kumjua kama Fresh Jumbe ila kwa kirefu na kikamilifu jina lake ni Fresh Jumbe Mkuu Waziri Kungugu Kitandamilima.Kila mwaka ifikapo tarehe 19 mwezi wa kumi (Oktoba) husheherekea kumbukumbu ya kuzaliwa.Alizaliwa mwaka 1968 katika hospitali ya Ngamiani iliyopo katikati ya jiji la Tanga. Anatoka kwenye familia ya watoto nane, wanne wa kiume na wanne wa kike. Wazazi wake wote wawili wametokea wilaya ya Pangani mkoani Tanga.Mama
akitokea katika kijiji cha Bweni kinachoangalia mto Pangani na baba
kwenye tarafa ya Mkwaja kijiji cha Buyuni kitopeni kilichopo mpakani
kabisa kati ya wilaya ya Pangani na Bagamoyo.

 

Akiwa Tanga sehemu anayoiita nyumbani ni Makorora “Mti Mkavu” karibu kabisa na shule ya msingi Makorora ambayo ndipo alipoanzia elimu yake ya msingi kabla ya kuelekea Bakwata Sekondari kwa ajili ya elimu ya sekondari.

Hivi sasa Fresh ni mmojawapo wa “mabalozi” wetu nchi za nje kupitia muziki.Anafanyia shughuli zake za muziki nchini Japan.Lakini walio wengi bado wanamkumbuka Fresh akiwa na bendi maarufu nchini Tanzania kama vile Sikinde,Msondo,Bicco Stars,Safari Sound nk. Kwa hakika Fresh Jumbe ni mojawapo ya majina ambayo washika dau katika medani za muziki hawawezi kuyasahau.

Siku chache zilizopita,tulipofanya naye mahojiano Fresh Jumbe alitueleza mengi.Katika mengi hayo suala la muziki wa Tanzania, inaposimama bongo flava alilipa kipaumbele cha aina yake. Tunaweza kudiriki kusema kwamba Fresh ametoa changamoto ya aina yake kwa wanamuziki wenzake,yeye mwenyewe,mapromota wa muziki,wana habari na kwa ujumla washika dau wote wa muziki nchini Tanzania. Ni changamoto gani? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

PICHA YA WIKI # 2

Filed under: Photography/Picha,Tanzania/Zanzibar,Utamaduni — bongocelebrity @ 7:28 AM

 

Hii ndio picha iliyojishindia kuwa “picha ya wiki” hii. Pichani ni msanii Wanne Star ambaye ni mmojawapo wa wasanii wachache ambao wanadumisha mila na tamaduni zao. Picha na Michuzi Jr.