BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DR.ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO. September, 29, 2007

Filed under: Bunge,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 5:43 PM

Tarehe 1 Februari mwaka 2007 ni tarehe ambayo Dr.Asha-Rose Mtengeti Migiro hawezi kuisahau kirahisi. Hii ndiyo siku alipokabidhiwa rasmi ofisi na majukumu ya unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa cheo ambacho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 kilikuwa hakijawahi kushikiliwa na sio tu na mwanamke yeyote mweusi bali pia mwafrika yeyote. Kwa maana hiyo Dr.Asha-Rose Migiro ndiye mwanamke wa kwanza mweusi kushikilia wadhifa huo na pia mwafrika wa kwanza. Mwanamke mwingine ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kushikilia cheo hicho alikuwa ni mzungu raia wa Canada Louise Frechette ambaye alianza kukitumikia cheo hicho mapema mwaka 1998.

 

Dr.Migiro anayo historia nyingine ya kujivunia. Yeye ndio alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2006.

Hivi leo Dr.Asha Rose Migiro ambaye ni mke wa Professa Cleophas Migiro na pia mama wa watoto wawili wote wakiwa wakike, ni fahari ya Tanzania. (more…)