BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ALFRED TIBAIGANA October, 1, 2007

Filed under: Jeshi,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 3:50 PM

 

 

Pichani ni Afande Alfred Tibaigana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar-es-salaam. Ungepata nafasi ya kuhojiana naye ungependa kumuuliza maswali gani? Picha kwa msaada wa Haki Ngowi.

Advertisements
 

12 Responses to “ALFRED TIBAIGANA”

 1. Chriss Says:

  Ningemuuliza kwamba yeye alikuwa kwenye safu ya Omari Mahita ambaye alikuwa mwizi na mla rushwa mkubwa hapa Tanzania. Hakuwahi kujiudhuru wala kusema lolote. Kipi kinaweza kutufanya tuamini kwamba yeye hakuwa anakula rushwa na hasa ukizingatia kwamba Mahita alikuwa akiwatumia vibaraka walioko chini yake. Kipi kitatufanya tumwamini?

 2. Dinah Says:

  Mngetukumbusha majukumu yake ingetusaidia kuibua maswali….Ngoja nijaribu haya machache ambayo huninyima amani nikifikiria Polisi Tz.

  1-Ni wazi kwamba Raia wengi hawajui haki zao hali inayopelekea kuwaogopa Polisi badala yakuwakimbilia kwa msaada, yeye kama kamanda wa polisi analizungumziaje hilo na je Polisi kwa ujumla wanampango gani wa kuweka wazi haki za raia ili wasinyanyaswe na Polisi?

  2-Jinsi ya kukabiliana na wahalifu au watuhumiwa aliyetoweka/toroka/jificha. Vijana wako (Polisi) wanatabia ya kumuweka ndani mke, mtoto, rafiki au ndugu wa mtuhumiwa ili kuisaidia Polisi na hivyo wampate wanae mtafufa (mhalifu).

  Swali:(a)-Je hamuoni kuwa huko ni kuwanyima haki watu hao ambayo pamoja na ukaribu wao na mtuhumiwa hawana uhusiano wowote na vitendo vyake vya kiharifu.

  (b)-Ikiwa Polisi wamepatiwa mafunzo ya kutosha na wanafanya kazi kwa kufuata taaluma inakuwaje wanatumia njia za mkato(kuweka mtu mwingine ndani ili wampate mtuhumiwa). Wewe kama Kamanda una lipi la kutetea kuhusiana na uzembe, uvivu nakutojituma kwa vijana wako?

  3-Unampango gani wa kukabilianana Polisi wenye miili mikubwa/wanene? Usicheke, ni wazi kuwa hawatoweza kumkimbiza mhalifu kutokana na uzito wao……Huenda ndio sababu ya Polisi kukiuka haki za binaadamu kwa kuweka ndani wake au watoto ili kumpata mtuhumiwa?

  4-Je Polisi hupewa mafunzo ya jinsi yakukabiliana na watu (People skills) na kubaki “calm” nakufanya kazi yake hata kama anarushiwa matusi au kutishiwa?

  5-nimeasahau………
  Ni hayo tu kwa sasa.

 3. Dinah Says:

  oh nimekumbuka.

  5-Anampango gani wa kukomesha tabia ya Polisi kupiga raia ovyo?

  6-Nasikia kuna nchi ambazo wanautaraibu mzuri sana wa kumlinda raia au kukabiliana na uhalifu, kwamba raia ukihitaji msaada wa Polisi unawaita kwa kutumia # yao(911), wakifika kwenye tukio lakini wakashindwa kukabiliana nalo huwaita SWAT n.k.

  Swali: Je kwa hapa nyumbani nikipiga # (955 vile?) mkaja lakini mkashindwa kukabilianana tukio mnawaita nani? Natumaini sio FFU!

  Kila la kheri ktk utendaji wako wa kazi.

 4. Pius Pius Says:

  Jiji la Dar ni moja kati ya majiji ambayo si salama kwa wageni, tumeshuhudia watalii wakiporwa mitaa ya Posta hasa Samora mchana kweupe, tumeshuhudia wabadilisha fedha wa pale Empress wakiwaibia wageni mchana kweupe na cha kushangaza matukio mengi hufanyika hata Polisi wakishuhudia, je ni changamoto gani anapata kwa malalmiko kama haya akiwa kama Mlinda amani mkuu wa kanda nzima ya Dar Es Salaam.

 5. Amandus Mugaya Says:

  NAungana na Bwana Pius hili tatizo linatakiwa ufumbuzi kwa kweli inasikitisha sana hasa tunapojinadi kuwa nchi yetu ni ya Amani na unasikia kila siku Watalii wanaibiwa na vibaka tena katikati ya jiji!!! Hawa Mdudu mdudu, Pangusa, Chokoraaa ni wezi wamezoeleka, nani mjini asiye mjua Mengi (Mwizi Maarufu pale Posta, anakidonda mguu cha miaka nenda rudi) ndiye muuza Camera na Simu za wazungu mkubwa, Ni mara ngapi tunaona Laptop za wazungu zikiuzwa ilihali zinakuwa na Data za watu masikini za muda mrefu, Mheshimiwa alitolee majibu hilo, Heko kaka Pius ulipotelea wapi na mbona hauandiki siku hizi?

 6. maya65 Says:

  nchi za wenzetu ukimuona polisi unakuwa na hali ya kujisikia salama na polisi anakuwa ni kama rafiki lakini polisi wa bongo…mhhh ukimuona unaanza kuogopa na ukifika kituo cha polisi wanaanza kukujenga hofu hata kama si muharifu!!!!
  hivi hii ni kwa nini? je hatuwezi kuwa na jeshi la polisi linalothamini haki na kuheshimu raia? mishahara ya polisi ni kutokana na kodi zetu ina maana sisi ndio tunaowalipa mishahara ,sasa kwa nini wawe wababe kwetu badala ya kutunyenyekea sisi raia tunaowalipa mishahara?
  hebu afande tibaigana litafakari hilo!!!!

 7. Mshauri Says:

  KWA NINI UNAPOZUNGUMZIA SUALA LOLOTE KWENYE VYOMBO VYA HABARI UNAONGEA KIBABE SANA?

 8. TanzanianDream Says:

  Duuh wacha na mimi niulize langu,sina ndugu wala rafiki polisi lkn hali yao pia inaniumiza

  Yeye akiwa kama polisi wa cheo cha juu bila shaka anapata mshahara afueni je anawajibika vipi katika kushawishi mishahara iongezwe kwa polisi ?

  Simaanishi ni kazi yake kuongelea hayo bali ana nafasi kubwa ya kufikisha kilio chake kuliko Polisi wa Kisiju…

 9. Mpendakeroro Says:

  Aroooo,Arooooo,Arooooo… Ni hayo tu miyee…

 10. Dinah Says:

  7-Utaratibu gani unatumia ili kuthibitisha kuwa aliye kamatwa ni mtuhumiwa kweli?

  8-Watu wanauwawa kila siku, je mnatumia mbinu gani kuwapata wauwaji? Na mtuhumiwa wa uuwaji anapofikishwa mahakamani huwa mnathibitisha vipi kuwa yeye ndie kweli ameua?

  9-Je kuna utaratibu wa kupimwa akili kwa wale wanaokili kuua lakini ktk hali halisi hawajaua bali wanasikia uchungu kwa vile wanahisi kuwa ni makosa yao kuwaacha “wapendwa” wao peke yao mpaka wakauwawa na watu wasiojulika?

  10-Nini kifanyike ili Raia wawaamini vijana wako (polisi) na kuwakimbilia ikiwa wanahitaji kulindwa/kuwa salama?

  11-Mwananchi wa kawaida akiwa na sherehe yake akaomba Polisi kama 8 hivi wamsaidie kwa ulinzi mahali pa shughuli hiyo je atapaswa kuwalipa?

  12-Je mafaili yenu mnayahifadhi? Pia mnakabiliana vipi na “Cold kesi” zile zilizokufa baada ya rushwa au baada ya kukosa ushahidi?

  13-Kuna swala la kuwekwa lumande kwa zaidi ya masaa 96 kwa vile tu huna mdhamini, wewe unafikiri ni haki kwa mtuhumiwa?

  Ni hayo tu kwa sasa.

 11. Matty Says:

  mi naona tungeongea kihaya tu!

 12. phinias bashaya Says:

  Nasikia ametangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Muleba Kusini,siasa ni mchezo mchafu uliojaa chuki uzushi na malumbano je yuko tayari kuhimili yote haya??

  Kabla ya hapo aliwahi kushiriki siasa au anaingia kama mwanafunzi?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s