BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JIJI LETU October, 5, 2007

Filed under: Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 9:01 PM
Tags: , ,

Zamani paliitwa Mzizima. Inasemekana kilikuwa ni kijiji kidogo tu cha wavuvi. Mwaka 1862 Sultan Seyyid Magid aliyekuwa mtawala wa Zanzibar akapependa kisha akapabadilisha na kupaita Dar-es-salaam yaani “Bandari ya Salama”. Baadaye wenyewe tukapaita “Bongo”. Leo hii nchi yetu inajulikana sana kwa jina hilo ingawa sio jina rasmi.

 

 

Mara nyingi ni vigumu sana kuzungumzia watu maarufu wa Tanzania(bongo celebrities) bila kulihusisha jiji la Dar-es-salaam kwa njia moja au nyingine. Wengi wamejipatia umaarufu wao wakiwa jijini Dar. Wengine wanadiriki hata kuliita New York ya Tanzania.

 

Ndilo jiji kubwa kupita yote na pengine tajiri kupita yote pia nchini Tanzania. Ni mojawapo kati ya majiji yanayokua kwa kasi sana duniani. Mpaka mwaka 1996 ndipo yalipokuwa makao makuu rasmi ya nchi yetu kabla ya kuhamishiwa Dodoma ingawa mpaka leo safari ya kuhamia Dodoma haijakamilika!

Zitazame picha hizi na uone kama unaweza kuyatambua baadhi ya majengo au mitaa. Kama upo nje ya nchi hivi sasa unakumbuka nini kuhusu Dar-es-salaam?

Picha zote kwa ruhusa na hisani kubwa ya Brian McMorrow.

Advertisements
 

MwanaFA YU HAI(?)

Filed under: Bongo Flava,Muziki — bongocelebrity @ 11:57 AM

 

Habari zilizokuwa zimeenea katika mitaa ya jiji la Dar-es-salaam katikati ya wiki hii kwamba msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinjuma a.k.a MwanaFA(pichani), amefariki dunia ziliwashtua wengi. Bahati nzuri ni kwamba MwanaFA hajafariki dunia,yupo hai, anadunda mitaani. Nini kilitokea? Unaweza kupata undani wa habari hii kwa kumtembelea Bob Sankofa kwa kubonyeza hapa.

 

KARUBANDIKA

Filed under: Muziki,Utamaduni — bongocelebrity @ 12:13 AM

Ni ijumaa tena. Mwaka 2007 unazidi kuelekea ukingoni. Kwetu sisi ni wakati wa jadi mpya.Ni wakati wa kutuliza kichwa na kufanya tafakuri ya wiki. Leo tunao Maquis Original na wimbo wao maarufu Karubandika. Hivi kama unampenda kwanini usimueleze ukweli? Unaogopa nini? Atakukataa? Ijumaa Njema!