BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“TAJIRI WA SAUTI” October, 8, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki,Sanaa/Maonyesho,Tanzania/Zanzibar,Utamaduni — bongocelebrity @ 5:30 PM

Mkasa wa maisha yake sio wa kipekee. Ni mambo ambayo yameshatokea na yangali yakitokea kwenye jamii zetu na pia ulimwenguni kote. Kinachoufanya mkasa wake uwe wa aina yake ni uwazi alioupa na pia uwezo wake wa kuusimulia kupitia sanaa kama ya muziki. Sauti yake ni kitu kingine ambacho kinasadia sio tu kusisimua wasikilizaji wa muziki wake bali pia kufikisha ujumbe anaotaka na anapotaka kuufikisha.

 

 

 

Hivi leo haimbi tena kusimulia kisa cha kusikitisha cha yeye kutelekezwa na baba yake mzazi tangu akiwa kichanga (baada ya mama yake mzazi kufariki) kwani anasema hayo yamepita. Leo anasimama kama mmojawapo kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya anayekubalika na kupendwa na mashabiki kibao.Bado mashairi yake yamesheheni visa vya ukweli hususani kwenye mambo ya mapenzi na mahusiano. Jina lake ni Abubakari Shaaban Katwila ambaye wengi hii leo tunamjua kama Q-Chilla ingawa bado jina la Q-Chief halijamuacha aende.

Albamu yake mpya ameiita “Tajiri wa Sauti”.Ipo sokoni hivi sasa. Lakini anasemaje kuhusu alipo hivi sasa kisanii na kimaisha? Uhusiano wake na baba yake mzazi ukoje hivi sasa? Q-Chilla pia ana habari za bendi yake anayotarajia kuizindua rasmi hivi karibuni ili aweze kuwapa burudani wapenzi wa muziki “live”.Unajua ameipa jina gani na kwanini? Kwa hayo na mengine mengi, soma mahojiano haya tuliyofanya naye hivi karibuni; (more…)

Advertisements