BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“TAJIRI WA SAUTI” October, 8, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki,Sanaa/Maonyesho,Tanzania/Zanzibar,Utamaduni — bongocelebrity @ 5:30 PM

Mkasa wa maisha yake sio wa kipekee. Ni mambo ambayo yameshatokea na yangali yakitokea kwenye jamii zetu na pia ulimwenguni kote. Kinachoufanya mkasa wake uwe wa aina yake ni uwazi alioupa na pia uwezo wake wa kuusimulia kupitia sanaa kama ya muziki. Sauti yake ni kitu kingine ambacho kinasadia sio tu kusisimua wasikilizaji wa muziki wake bali pia kufikisha ujumbe anaotaka na anapotaka kuufikisha.

 

 

 

Hivi leo haimbi tena kusimulia kisa cha kusikitisha cha yeye kutelekezwa na baba yake mzazi tangu akiwa kichanga (baada ya mama yake mzazi kufariki) kwani anasema hayo yamepita. Leo anasimama kama mmojawapo kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya anayekubalika na kupendwa na mashabiki kibao.Bado mashairi yake yamesheheni visa vya ukweli hususani kwenye mambo ya mapenzi na mahusiano. Jina lake ni Abubakari Shaaban Katwila ambaye wengi hii leo tunamjua kama Q-Chilla ingawa bado jina la Q-Chief halijamuacha aende.

Albamu yake mpya ameiita “Tajiri wa Sauti”.Ipo sokoni hivi sasa. Lakini anasemaje kuhusu alipo hivi sasa kisanii na kimaisha? Uhusiano wake na baba yake mzazi ukoje hivi sasa? Q-Chilla pia ana habari za bendi yake anayotarajia kuizindua rasmi hivi karibuni ili aweze kuwapa burudani wapenzi wa muziki “live”.Unajua ameipa jina gani na kwanini? Kwa hayo na mengine mengi, soma mahojiano haya tuliyofanya naye hivi karibuni;

BC: Kwa faida ya wale ambao hawafahamu historia ya maisha yako,unaweza kutuambia ulizaliwa lini,wapi na ukasomea wapi?

Q-CHILLA: Jina langu kamili ni Abubakar Shaaban Katwila, nimezaliwa tarehe 18 Mei mwaka 1984 huko wilayani Muheza mkoani Tanga. Kwa maana hiyo nimezaliwa mwaka 1984. Kwa upande wa shule nilikuwa nahama hama sana kwa hiyo nitakutajia mbili tatu ambazo nilikaa muda mrefu zaidi. Nilianzia Muheza shule ya msingi kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu.Baada ya hapo nikahamia Dar-es-salaam ambayo ndio yakawa makazi yangu ya kudumu. Sikukaa sana ikabidi niende kusoma kwa mama yangu mkubwa nchini Botswana katika jiji la Gaborone. Pale nikasoma mpaka darasa la sita ambapo kwa bahati mbaya mama yangu huyo akafariki dunia. Baada ya hapo ndio ikabidi nirejee nchini Tanzania nikisindikizana na mwili wa marehemu. Baada ya kurudi nikajiunga na shule ya msingi Olympio kwa darasa la sita hadi la saba. Sekondari sikusoma sana kwani nilishindwa kuendelea na masomo kwa ukosefu wa ada.

BC: Unakumbuka nini kuhusu harakati zako za mwanzo kuwa mwanamuziki?

Q-CHILLA: Kwa uhakika kabisa mimi nashukuru mungu kwamba kwenye muziki sikupata sana tabu kuingia. Nadhani naweza kusema hii ni kutokana na kipaji nilichokuwa nacho na ujumbe uliokuwemo kwenye nyimbo zangu.Wimbo wangu wa kwanza ulihit na ndio ukawa mwanzo. Kwa hiyo matatizo ambayo wasanii wengi huwa wanayapitia kama vile kukaa nje huku mvua inanyesha au jua kali kumsubiri producer nk mimi mambo hayo hayakunipata sana.

BC: Mwanzoni ulijiita Q-Chief na hivi sasa unajiita Q-Chilla. Nini chanzo cha majina haya na kwanini ulibadilisha kutoka Q-Chief kwenda Q-Chilla?

Q-CHILLA: Jina la Q-Chief mwanzo wake ni mama yangu.Nilipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kuniambia kwa kunitania “you are so cute”. Sasa nilipoanza muziki nilitaka kuadopt ile “cute” lakini ikawa ngumu kidogo. Kwa hiyo kiusanii ndio nikaiweka Q badala ya C. Na Chief ilitokana na kwamba babu yangu alikuwa ni Chifu enzi hizo kwenye kabila la wabondei

Q- Chilla ni jina ambalo nilipewa na msanii mwenzangu Papii Kocha “Mwana wa Mfalme” wakati huo ilikuwa ni kabla hajafungwa jela.Hivi sasa yuko jela ambako anatumikia kifungo cha maisha. Kabla ya hapo tulikuwa tunaimba wote na tulifanya tour ya albamu zetu za mwanzo pamoja.Kwa kweli alikuwa ni msanii mwenye kipaji sana. Kwa hiyo yeye alikuwa anapenda kuniita Q-Chilla badala ya Q-Chief. Alipofungwa maisha nikaamua kulichukua jina hilo kama njia mojawapo ya kuendelea kumkumbuka.

BC: Naomba nikuulize swali ambalo hatujawahi kumuuliza mtu mwingine yeyote tuliyewahi kufanya naye mahojiano. Unadhani kwanini wewe hivi leo ni mwanamuziki na sio labda kwa mfano polisi,daktari,mwanasheria nk.Kwa maneno mengine kwanini uliamua kuwa mwanamuziki?

Q-CHILLA: Mambo mawili ya msingi nadhani ni kwamba kwanza nina kipaji na pili ni mapenzi ya mungu. Isitoshe bila elimu ni wazi kwamba ingekuwa ngumu sana kwangu mimi kufanya kazi labda za kiofisi au kwa mtu mwingine yeyote. Kwa hiyo nadhani mwenyezi mungu alishanipangia kwamba riziki yangu itatokana na muziki. Namshukuru mungu kwa hilo.

BC: Mojawapo ya mambo yaliyofanya muziki wako ukakubalika kwa haraka sana ni sauti yako.Pamoja na hayo kisa cha kweli cha kuzaliwa kwako na jinsi baba yako mzazi alivyokutelekeza kilivuta hisia za wengi sana. Uhusiano wako na baba yako ukoje hivi sasa?

Q-CHILLA: Mimi na baba yangu hivi sasa tuko okay. Ningali najifunza kusamehe, kusahau na kusema asante. Kwa hiyo mimi nimemsamehe na yeye pia amegundua kosa lake lilikuwa wapi. Pia nadhani ni vigumu sana kwangu kujua nini kilitokea wakati huo. Kwa hiyo cha muhimu ni kusameheana na kuendelea mbele.

BC: Sasa kwa sababu wewe mwenyewe ni baba pia, unadhani hiyo imekusaidia kidogo kumuelewa baba yako zaidi?

Q-CHILLA: Kweli kabisa. Hiyo pia imenisaidia na inaendelea kunisaidia. Naelewa zaidi nini mzazi anaweza kufanya na nini hawezi kufanya wakati mwingine.

 

Q-Chilla na msanii mwingine maarufu wa muziki wa kizazi kipya,TID.

BC : Tukirudi kwenye suala la sauti yako. Unafanya nini ili kuhakikisha kwamba sauti yako inabakia kuwa hivyo ilivyo?

Q-CHILLA : Kusema ukweli hakuna cha ziada ninachokifanya kuhusiana na kuhakikisha sauti yangu inabakia hivyo. Kama nilivyosema hapo mwanzo, naamini sauti na uimbaji ni kipaji kutoka kwa mwenyezi mungu kwa hiyo namuachia yeye zaidi katika kunilindia vipaji hivi.

BC : Msanii siku zote anategemewa au inasemekana ni kioo cha jamii. Kwa sababu hizo yapo mengi ambayo hayategemewi kutoka kwake au kumtokea. Mojawapo ni kupelekwa mahakamani au kutuhumiwa kwa vitu kama wizi nk. Wewe umewahi kutuhumiwa na pia kufikishwa mahakamani. Nini kilitokea? Una ujumbe gani kwa jamii kuhusiana na shutuma hizo? Kesi imeisha?

Q-CHILLA : Kilichotokea ni kwamba wakati huo mimi nipo Mombasa kwenye shughuli zangu za kimuziki, nilikuwa nimewaachia marafiki zangu gari langu. Lakini kabla sijaendelea labda nikwambie kwamba mimi nimezaliwa na kukulia « in the hood ».Huko naishi na kila aina ya watu na ambao kila mtu ana utashi na shughuli zake. Ninapoishi mimi nimezungukwa na kila aina ya watu; wengine ni wezi,mateja, majambazi, polisi, maimamu, mapadri nk. Watu walionizunguka ndio wanajamii wangu,wengine ndio marafiki zangu nk.

Sasa bila mimi kujua kumbe baadhi ya wale marafiki zangu kazi zao ni wizi, ikatokea kwamba wakawa wameenda kwenye eneo la tukio wakitumia gari langu. Na wala sio kwamba walienda kufanya wizi mkubwa wa benki au sehemu kama hizo.Nadhani hawa walikuwa ndio kwanza wanajifunza kwa sababu walienda kuiba vitu kama vioo vya magari,power windows nk…yaani vitu vidogo vidogo tu. Kwa hiyo kesi ilipoenda mahakamani ilikuja kuthibitika wazi kwamba I had nothing to do with it zaidi ya gari langu kutumiwa na washkaji.Kesi ikawa imeisha hivyo.

Ninachoweza kuongezea labda ni kwamba media nayo ilichangia sana kuikuza kesi yenyewe hususani ilipobainika kwamba jina langu limehusishwa kwa njia moja au nyingine. Nadhani kuna baadhi ya waandishi wa habari walikuwa wamepania kunimaliza.Nashukuru mungu kwamba walishindwa. Kwa hiyo ninachoweza kuwaambia wana jamii ni kwamba wakati mwingine wasiamini kila kitu wanachokisoma au kukisikia.Wachuje kama chujio la nazi linavyochuja tui la nazi.

BC : Tatizo la wanamuziki wa ki-Tanzania kutouza muziki wao kimataifa bado ni changamoto kubwa inayowakabili. Kwa maoni yako, unadhani ni kwanini bado kuna ugumu kwenu wasanii wa muziki Tanzania kuuza muziki wenu kimataifa?

Q-CHILLA : Ukweli ni kwamba tunajitahidi kufanya hivyo.Kama ulivyosema ni changamoto nzito.Yapo mambo kadhaa yanachangia,masuala kama lugha nayo yanatutatiza kiasi fulani.Ndio maana hivi sasa najitahidi pia kuimba kwenye lugha zingine kama kiingereza nk. Nia ni kujaribu kutanua masoko ya muziki wangu.

Halafu kuna ile kubaniana miongoni mwetu watanzania. Kwa namna fulani hatusaidiani.Hii ni tofauti na wenzetu kwa mfano wakenya ambao wanasaidiana sana.Naweza nikaja mahali kama hapo Canada ukashangaa watanzania wakaja 12 ukumbini. Sasa kama tusipopeana support sisi kwa sisi kwanza,hao wageni watatupa vipi hiyo support? Pia mimi ningependa kutoka kwenda kuperform nchi kama hizo za mbali kwa maana halisi ya kuperform na kutengeneza hela na sio kuja kushangaa magorofa tu. Muziki ndio kazi yangu na nina majukumu ya kulea wanangu kutokana na kazi hii hii ya muziki.

BC : Nyimbo zako nyingi ni kuhusu mahaba au mapenzi. Ni kwanini unapenda zaidi kuimba nyimbo za namna hiyo? Ikitokea rafiki yako akakuomba ushauri kuhusu mwanamke gani aoe, ungempa ushauri gani?

Q-CHILLA : Ni kweli kabisa. Nyimbo zangu nyingi ni za muelekeo huo ingawa kuna wakati huwa naimba pia nyimbo zinazoelezea mambo mengine kama vile watoto wa mitaani nk. Nyimbo kama « Ninachokipata » ni mfano mzuri. Lakini kujibu swali lako moja kwa moja ni kwamba naimba sana nyimbo za mapenzi kutokana na personal experience ambapo kuna mwanamke mmoja aliwahi kuniumiza sana moyo wangu. Kwa hiyo bado nina mengi ya kuzungumzia katika mambo hayo.

Kuhusu ushauri ambao ningempa rafiki yangu;cha kwanza ningemshauri aoe mwanamke ambaye ana msimamo na maisha yake na pia anayetambua thamani yake kama mwanamke. Pili awe ni mwanamke mwenye msimamo na ambaye sio cheap. Vitu kama uzuri na mengineyo yanakuja baadaye ingawa ukweli ni kwamba wanawake ndio mapambo ya dunia yetu.Bila wao dunia ni tupu kabisa.

 

BC : Hivi karibuni tulipofanya mahojiano na mwanamuziki mkongwe na anayefanyia kazi zake za muziki nchini Japan,Fresh Jumbe alikutaja wewe kama mmojawapo wa wanamuziki wa Bongo ambao angependa kufanya nao kazi. Unasemaje kuhusu « offer » hiyo?

Q-CHILLA : Kwanza nimefurahi sana kusikia hivyo.Nadhani Fresh alishawahi kuona show zangu hapa nchini kama mbili tatu hivi. Ningefurahi pia kufanya naye kazi.

BC : Tangu umeingia kwenye fani ya muziki umejifunza mambo yepi matano ya msingi na unatoa ushauri gani kwa vijana wengine ambao ndio kwanza wanataka kuingia kwenye fani?

Q-CHILLA : Kama nilivyosema hapo mwanzoni katika kuelezea mahusiano yangu na baba yangu kwenye muziki pia nimejifunza mambo hayo hayo na mengine ya nyongeza. Kwa hiyo naweza kusema nimejifunza kwanza kusamehe, pili kusahau, tatu kusema asante, nne kumshukuru mola kwa unachokipata na tano kuwa mvumilivu. Lakini pia ningependa kuwaambia kwamba kwenye muziki kuna vikwazo vingi sana.Wakizingatia hayo niliyoyataja hapo juu watafanikiwa.

BC : Hivi karibuni imeripotiwa kwamba upo njiani kuanzisha bendi yako.Mipango hiyo inaendaje na utaiita jina gani bendi yako?

Q-CHILLA : Ni kweli kabisa kuhusu hilo. Mipango imeshakamilika, vifaa vimeshawasili na watu wapo mazoezini hivi sasa. Mara tu mwezi mtukufu utakapomalizika, mambo yataanza rasmi.Mimi nimeiita bendi yangu « Atomic ». Kama unakumbuka kwenye historia ya dunia bomu la atomic lilipopigwa huko Hiroshima na Yagasaki lilileta madhara makubwa. Ndio hivyo hivyo itakavyokuwa Atomic ikianza kazi rasmi. Kuna bendi zingine zitakufa, watu wengine watapata presha….ahahaha (natania). Pia kama utakumbuka msanii gwiji,jabali la muziki, Marijan Rajab, aliwahi kuwa na bendi yenye jina hilo zamani sana.Nimeamua kulichukua jina hilo kumuenzi.

BC : Hivi karibuni pia pamekuwepo na habari kwamba una mpango wa kujiingiza kwenye shughuli za uigizaji sinema. Je habari hizo ni za kweli? Kama ndio nini kimekuvutia katika fani hiyo?

Q-CHILLA : Habari hizo sio za kweli. Sijawahi kufikiria kufanya hivyo ingawa sanaa ya uigizaji wa sinema ni jambo ambalo nitalikaribisha endapo nafasi itajitokeza. Navutiwa na jinsi waigizaji wa Tanzania wanavyojitahidi na pia jinsi wanigeria wanavyozidi kutamba na movie zao.Ila kwa hivi sasa sina mpango huo.

BC : Wiki iliyopita umeingiza sokoni albamu yako ambayo umeiita « Tajiri wa Sauti » hivi karibuni. Lini kwa uhakika itakuwa sokoni? Kwanini umeiita « Tajiri wa Sauti »?

Q-CHILLA : Nimeiita Tajiri wa Sauti kutokana na performance nzima ya sauti ndani ya albamu hiyo.Mtu yeyote atakayepata nafasi ya kusikiliza nyimbo zilizomo kwenye albamu hii atapata maana kamili ya utajiri wa sauti uliomo. Nimeimba sana katika albamu hiyo.

Editor’s Note: Mojawapo ya nyimbo za Q-Chilla zilizomo kwenye albamu yake hiyo ni huu hapa uitwao Uhali Gani.

BC : Itakuwa na nyimbo ngapi na umewashirikisha wasanii gani? Nani msambazaji wako?

Q-CHILLA : Nimewashirikisha wasanii kama Chameleon, Nonino, Domokaya na wengine wengi. Ina nyimbo 15.Wasambazaji wangu ni Long Street Entertainment kutoka Kenya.

BC : Siku yako ya kawaida unapokuwa mapumzikoni ikoje?

Q-CHILLA : Ya kawaida tu. Sana sana napenda kufanya mazoezi ya viungo na pia mazoezi ya kimuziki.

BC : Nini mipango yako katika miaka mitano ijayo?

Q-CHILLA : Mipango yangu ni kuwa international artist. Nimejiwekea miadi kwamba mpaka hapo nisipofanikiwa katika hilo naachana na muziki.Tungoje tuone.

BC : Baadhi ya mashabiki wako wa kike wamesisitiza kwamba tukuulize swali hili.Je umeoa au una mchumba?

Q-CHILLA : Sijaoa ila nina mchumba.

BC : Una lolote ambalo hatujakuuliza na ambalo ungependa kuwaambia mashabiki wako?

Q-CHIEF : Sina la ziada sana zaidi ya kuwaambia washabiki na wapenzi wa muziki kwamba wawe focused na wasiyumbishwe sana na mambo yanayoandikwa na vyombo vya habari.

BC : Asante kwa muda wako Q-Chief

Q-CHILLA : Asanteni BongoCelebrity.

Picha zote kwa niaba ya Ahmad Michuzi Jr.

Advertisements
 

27 Responses to ““TAJIRI WA SAUTI””

 1. beutness Says:

  Maskini Mungu atakusaidia na atakujalia mengi mazuri maadamu umemsamehe baba yako.

 2. Dinah Says:

  Wow! Samehe, Sahau, Sema asante, Shukuru Mungu na Uvumilivu. Mahojiano ni babu kubwa na majibu yake yametulia, yaani nahisi huyu Kijana ni mwenye good manners……

  Nakumbuka kwa mara ya kwanza niliposikiliza ule wimbo wa “si ulinikataa” nilitokwa na machozi lakini at the end nikatamani nimwambie msamehe tu kwani ni baba yako na sehemu ya u-“Q”ute utakuwa umetoa kwake.

  Chilla, unabusara, umetulia, unavutia, unachekesha (funny), muwazi, unapendeza, umejaaliwa sauti nzuri ambayo sio ya kujifanya (act), huna kiburi (angekuwa mwingine angemtosa baba’ke kwa vile tu ni Star) pia una moyo mkubwa wa kusamehe.

  Nakutakia kila lililo jema ktk shughuli zako na maisha yako kifamilia.

  BC keep it tight!

 3. TanzanianDream Says:

  Vyombo vya habari bwana!,kwanini vikimsifia msanii na kumjengea Fanbase ni vizuri lkn vikieleza ubaya wa msanii ni vibaya….?

  Wasanii nao naona wanakuwa kama wanasiasa tu…

 4. TanzanianDream Says:

  Dinah naona comments zako zipo too personal ni hayo tu au?

 5. Kenny Says:

  kwa kweli huyu ni mmoja wa wasnii ninowazimia kwa saut yake. Hunaonekana uko humbel sana, endelea hivyo, wengi wanasema una maringo lakini ktk interview hii unaonekana una akili na unajua na kutambua kwamba kipaji unacho. Good job BC. fagilia Q chief..

 6. beutness Says:

  Anakula kitimoto lakini.

 7. ssssssi Says:

  “YAGASAKI” sio sahihi bali NAGASAKI

 8. Dad Says:

  Kijana kwa umri wako una watoto zaidi ya wawili na hujaoa–hiyo ni SOOOOOOOOOO. Any way na hao watoto watakusamehe kama nawe ulivyomsamehe baba yako–Maji ufuata mkondo.

 9. kinono Says:

  Q- CHILLA:Mimi naona hata wewe una tabia yakutelekeza kwani hao watoto kila mmoja na mama yake au niwa wa mama mmoja? una takiwa kuoa sasa maana ukiendelea hivi wengine uta waterekeza.

 10. Dinah Says:

  Kinono, kwani kuoa ndio mwisho wa kuzaa? Mimi nafikiri aache kuzaa kwani kama ni zaidi ya 2 basi inatosha kha!

  Kafunge.

 11. kinono Says:

  Dinah, sasa kama kila mtotto na mama yake hujuii hapo ndio mwanzo wa kutelekeza wengine akioa anaweza kujizuia kidogo lakini watoto wa 2 nje na akioa je?

 12. shabiki Says:

  inaonekana huyu kijana ana busara sana, nimesoma interview za macelebrity wa bongo, and this is one of the best, keep it up Chilla, kuringa ni kawaida ya ma-celebrity, hata huko ma mtoni ma-star wanaringa sana tu.

 13. emanuely lwilla a.k.a CHOMA P Says:

  KAZA MWENDO KAKA

 14. Chantell Says:

  I LOVE U Q-CHILLAH

 15. Doreen Says:

  Kwani nyie wadau mmesahau lile neno lisemwalo Ipo damuni?Kama alikataliwa basi na yy anaweza ingawa sio lazima kukataa kama alivyofanyiwa na Baba yake mzazi.
  Ila ule wimbo wa siulinkataa unatia uchungu sana.Keep it up Q chilla.

 16. DUTCH MASTER Says:

  i used to dis him.. for his voice but this nigga is cool,,after i read his interview with bc,, cheai got him.. this dude is fantastic..man of honor for tht i salute you q chilla…though i hav made sum underground tracks dissin this boi and the rest of upanga cruew.. man this dude i know for sure where he head at.. bless q.. (((xl.. d master..another tz nightmale))))

 17. Lina Says:

  Big up Q-Chilla! wewe ni mkali, sauti umejaaliwa kaza but mazee. Naomba umshirikishe Abu Bakar Mzuri katika nyimbo zako. Nina imani mtatoa kitu bomba sana, na mnafanana ile mbaya. Ni hayo tuu mazee wangu.

 18. zaina seif Says:

  Q-chilla big up, but nivizu kama utajitahidi kuchek weight umeongezeka sana mchumba.

 19. Mshkaji unaimba vizuri,unasura nzuri yakuwadanganyishia dada zetu,lakini tabia yako we na washkaji wako wamagomeni,inshu mnayoifanya sio fresh.Ngoja siku muingie choo cha kike.mnajifanya wajanja wa magari

 20. sabrina ahmed Says:

  i really lyke ur songs.keep it up and pull up ur socks.dont care abt what people say abt u,u rock,ur on the top. if iwill be given achance 2choose a worldsuperstar iwill choose u coz u derserve it.may god bless u,u truly rocks,much love and respect.

 21. keep it up,u truly rocks,u a on the top.i used 2see him ireally love him.god will help u it is good that u 4give ur dad ibelieve u will achieve something good. u a superstar don care abt whwat people say just go on with ur lyfe.

 22. i love u more than my self.

 23. if u hv tyme pls find me iknow u know me but u hv forgetten we met twice at ur place.iam sabrina.the 1who is ready 2die 4u iwillgv u my contact in privacy ihv ur no but iam afraid 2call u we used 2talk on the 4one.

 24. tom Says:

  kijana bado hujafika ila unaelekea kaza buti Mungu yupo utafika.Cha msingi ishi ndani ya malengo yako ndipo utakapofanikiwa vinginevyo utaishia njiani kama akina fulani

 25. happy Says:

  Kwa kipaji unacho kaka na kuhusu maisha au kwa kukaytaliwa ni moja ya sehemu ya maisha, lkn yote inabidi umuachie maula.

 26. happy Says:

  uko juu ile mbaya ila tu inabidi upunguze maringo kidogo maaana tunashindwa kukuelewa uko upande gani!

 27. Ariane Says:

  i luv ur songs ur awesome man!!!!!!!
  cn u email me on arianeu94@hotmail.com
  plz!!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s