BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SHEIKH YAHYA HUSSEIN. October, 10, 2007

Filed under: Tanzania/Zanzibar,Unajimu/Utabiri — bongocelebrity @ 9:44 PM

 

 

 

 

Iwe ni uchaguzi, mechi kubwa ya mpira au chochote kile chenye mvuto au gumzo la kitaifa, Sheikh Yahya Hussein (pichani) atakifanyia utabiri bila kusita. Kitu chochote kikitokea pia iwe ni ajali mbaya, mafuriko nk, Sheikh Yahya atakitolea maelezo pia akiweka sababu za kutokea kwa kitu au tukio hilo. Hivi leo anabakia kuwa mnajimu au mtabiri maarufu kupita wote nchini Tanzania. Amekuwa akifanya hivyo kwa miaka chungu mbovu mpaka hivi sasa.

Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-salaam. Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo kilichojulikana kama Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo. Baada ya kuhitimu alielekea nchini Misri alipoendelea kusomea masuala ya dini katika chuo kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.

Alirejea nchini mnamo miaka ya mwanzoni ya 60 ambapo alianza kazi yake ya utabiri . Sheikh Yahya Hussein ndiye mtabiri wa mwanzo kueneza utabiri wa kila siku katika magazeti mbalimbali ya Afrika Mashariki enzi hizo. Jina lake lilivuma zaidi alipokuwa akitoa utabiri kupitia radio kuhusu mashindano ya mpira kati ya nchi tatu za Africa Mashariki yaliyojulikana kwa jina la Challenge Cup au Gossage Cup.

Advertisements