BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SHEIKH YAHYA HUSSEIN. October, 10, 2007

Filed under: Tanzania/Zanzibar,Unajimu/Utabiri — bongocelebrity @ 9:44 PM

 

 

 

 

Iwe ni uchaguzi, mechi kubwa ya mpira au chochote kile chenye mvuto au gumzo la kitaifa, Sheikh Yahya Hussein (pichani) atakifanyia utabiri bila kusita. Kitu chochote kikitokea pia iwe ni ajali mbaya, mafuriko nk, Sheikh Yahya atakitolea maelezo pia akiweka sababu za kutokea kwa kitu au tukio hilo. Hivi leo anabakia kuwa mnajimu au mtabiri maarufu kupita wote nchini Tanzania. Amekuwa akifanya hivyo kwa miaka chungu mbovu mpaka hivi sasa.

Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-salaam. Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo kilichojulikana kama Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo. Baada ya kuhitimu alielekea nchini Misri alipoendelea kusomea masuala ya dini katika chuo kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.

Alirejea nchini mnamo miaka ya mwanzoni ya 60 ambapo alianza kazi yake ya utabiri . Sheikh Yahya Hussein ndiye mtabiri wa mwanzo kueneza utabiri wa kila siku katika magazeti mbalimbali ya Afrika Mashariki enzi hizo. Jina lake lilivuma zaidi alipokuwa akitoa utabiri kupitia radio kuhusu mashindano ya mpira kati ya nchi tatu za Africa Mashariki yaliyojulikana kwa jina la Challenge Cup au Gossage Cup.

Advertisements
 

61 Responses to “SHEIKH YAHYA HUSSEIN.”

 1. Kenny Says:

  Kweli kabisa, watu wengi wanamtegemea kwa ajili ya uchawi tuu. utabiri ni cover up..

 2. Moses Jakanyangoe Says:

  Sidhani kama kuna haja ya kuamini kila kitu anachokisema huyu bwana ila kwa vile sisi waswahili tunaamini sana nguvu za giza bado ataendelea kupata wateja! Hakuna ukweli katika haya mambo….watu wanaojua theory of probability wanajua anafanaya kitu gani!

 3. Dinah Says:

  Mh! Kwa jina la Yesu Toka! Ushindwe na ulegee, ukaangukie baharini umezwe na Nyangumi!(joke)

  Kila la kheri ktk shughuli zako Shekhe(niliona mahojiano yako kwenye Luninda mwezi wa 4), naamini ni kipaji kamavilivyo vingine na umejaaliwa na mwenyezi Mungu.

 4. Bob Sankofa Says:

  Kuna kutabiri na kukisia, nadhani Sheikh anafanya hilo la pili zaidi.

  Huwa naangalia sana mahojiano yake pale Channel Ten, huwa naona “ananiuzia chai tu”. Huwezi ukasema “Tarehe fulani ama jua litawaka ama mvua itanyesha” halafu ukauita utabiri, huko ni kukisia na hata mdogo wangu pale nyumbani ana kipaji kikubwa sana cha kukisia.

  Lakini kwa sababu ni namna fulani ya kusukuma siku mbele kwa watu fulani fulani, nampa big-up Sheikh.

 5. Bob hii kali mkuu.Natabiri utafanyika uchaguzi wa uraisi na wabunge mwana 2010.
  Alishatabiri kifo chake?.Anyway nampa shavu

 6. Natabiri Bongo Celebrity wataweka post nyingine baada ya hii!
  Unabisha?
  🙂
  Natania tu , usichukie mpenzi wa watabiri!
  BC wamemaliza kazi .
  Au?:-)

 7. TanzanianDream Says:

  Jamani mbona comment yangu imetolewa? au kisa sikuweka maneno mengi ya kumpamba na kusema “mchawi tu”….Nway kama mtu wa pili alivyosema maana nilikuwa wa kwanza ….Mchawi tu hana lolote

 8. Colin Says:

  Sheikh yahaya ni mtu muhimu sana,profile yake sio tu east africa mpaka mbele huko alishatabiri vitu vikawa kweli.haya mambo yapo jamani someni histry ,encyclopedia inaeleza vizuri sana.Utabiri sio kubahatisha ni calculations (kucheza na namba) wanasema namba ni uchawi mkubwa kuliko kitu kingine.Mi nampabig up kubwa nilishawahi kumtembelea mara mbili hivi ,habahatishi ..Ila anachoniboa ni kutembea peku ndo mana watu wanasema mwanga..

  Big kubwa shekh

 9. babygirl Says:

  Colin umenichekesha mpaka basi na kutembea peku. hivi ni kweli?? mi naomba siku nyingine ukimtembelea muulize kwanini anatembea peku? au mwambie akutabilie akiwa amevaa viatu…lol!!

 10. scholastica Says:

  kama anacheza na namba basi kasoma ipasavyo nampa big up sana cause hiyo shughuli inampa kukaa mjini ila hilo la kukaa bila viatu linanitia wasiwasi ila labda ni mazoea tu naomba atabiri siasa ya nchi hii inapoelekea cause napatwa na wasiwasi sana.big up sheikh kaza buti babu.
  si wabongo wabishi mno.

 11. Dinah Says:

  Hivi kipaji huwa kina mrithi? Kama ndio je Mrithi wake ni nani? Kama hapana mnaomtegemea kiutabiri mtafanyaje?

 12. TanzanianDream Says:

  Naona tumeshamgundua mchawi na wateja wake wanajitokeza…Pamoja

 13. kennedy matioli Says:

  Hebu nisaidie na bahati yangu.Na nataa unitabilie kuhusu maisha yangu na nini natakiwa kufanya kwani maisha yangu huwa nna mtisha yakwamba sikutafika ambapo nataraji maitaji yangu yatatimika.Tafathari nipigie hesabu ya jina langu ili unitumie majibu.Unaweza kunitumia majibu kupitia simu ya rununu 0724038264.Asante kwa mda wako.

 14. Mohamed O. Semiyono Says:

  Nadhani anajaribu zaidi kuelimisha jamii kwa kupitia utabiri wake
  Ispokuwa watu wenge hawaelewi nini anafanya

 15. Amina Feruz Says:

  Jamani waswahili leo utabiri mnauita uchawi, kwa sababu ni utabiri umesemwa kwa kiswahili. Lakini ingekuwa kwa kiingereza mngemsifia sana kuwa ni kazi nzuri, kazi ya utabiri au unajimu inafanywa duniani kote sio Tanzania au Africa tu. Na watu wengi wanawatumia hao wanajimu au watabiri katika mambo yao, kuna wengine wako addicted kabisa hawafanyi kitu mpaka wawaulize wanajimu wao, tena watu maarufu hasa.

  Ni kazi na biashara pia ndio maana hata kwenye website kama ya Yahoo, na msn, kuna kurasa za utabiri au unajimu (HOROSCOPES). Ndio hizo hizo zinatolewa magazetini kama nyota za kondoo, punda, nge na sijui nini. Na Wachina nao wana design zao za nyota kama mbwa, mbuzi, nyoka na kadhalika. Sasa sio kitu cha ajabu au ni kazi ya ajabu hayo mambo ya unajimu.

  Ila ni juu ya mtu kuamua kufuata mambo hayo au kutoyafuata, kusoma horoscopes au kutosoma, wengine wanasoma for fun wengine ndio hivyo tena. Cha msingi ni kujua duniani malengo yako ni nini na wajibu wako kama mwanadamu ni nini.

 16. AGNMWANA Says:

  RAHA RAHA UTAMU, ENDELEYAH MWANAUME, WHY? KWANINI? MBONA WATU WANAHOJI SANA KUHUSU UTABIRI WA SHEIKH, HICHO NI KIPAJI TU, NDIO NI KIPAJI KATIKA UJASILIAMALI, HATA MIMI HUWA NATABIRI, NGOJA NIWAPE UTABIRI WANGU KWA MWAKA 2008 1. UTAKUWA MWAKA AMBAO REDIO NYINGI ZITATANGAZA MATANGAZO YA KONDOMU, BIA, NA VIFO. WATU HAWATACHOKA KUNYWA BIA. RAIS ATAKUWA ANATOA HOTUBA SEHEMU MBALIMBALI ATAKAKO TEMBELEA, HAKUTAKUWA UCHAGUZI MKUU WA RAISI, ANYWAY KATIKA UPANDE WA SOKA, TIMU YA SIMBA ITAENDELEA KUITWA WEKUNDU WA MSIMBAZI. HAYA ATAKAYEBISHA NA ABISHE. KILA MTU ANAYO HAKI YA KUELEZA MAONI NA KUPASHWA HABARI KWA MUJIBU WA KATIBA. WENU KATIKA UTABIRI…..WAKUVWANGAVUNGA

 17. I want to know the telephone number for Sheikh Yahya because I want to ask something

 18. jomaeli Says:

  huyu mzee mi ananitisha

 19. mzee omar lally Says:

  NAMPOGEZA SANA SHEIKH YAYHYA BIN HUSSAIN KWA YOTE ANAYO YAELEZEA KILA MARA. UTABIRI WAKE KWELI HAUNA SHAKA WALA KUTILIWA DOSARI.
  HONGERA SANA TENA SANA SANA,,
  JAMBO MOJA TUU NDIO LANIPA SHAKA NALO NI LA KUHUS ( FIMBO YA AJABU) NATUMAI SHEKHE ATANIELEWA,

  NAMTAKIA DAIMA SWIHA NJEMA NA AENDELEE DAIMA KUTUPA MANUFAA YAKE YA HEKMA NA TAADHIMA,,

 20. tatu Says:

  YOTE TISA KUMI UNAPOSOMA QURUAN TUKUFU TU MIE HOI SIJAONA KUSEMA KWELI YANI NIKIONA TU SHEKHE YAHAYA BIN HUSSEIN ANASOMA QURUAN YANI HUWA NATULIA KAMA MAJI YA MTUNGINI KWA USOMAJI WAKE HADI NATETEMEKA MASHALLAH UMEJAALIWA WIPAJI NA MWENYEZIMUNGU .

  NAKUOMBEA UMRI MREFU.

 21. sam Says:

  Mimi namkubali huy bwana, na hasiye amini basi huyo hana dini make wapagani,wakristo,waislamu,waothodoksi,wahindu, n,k wana amimi majini,wanajua kazi zamungu na shetani sasa iweje wewe husiye jua kazi ya mungu na viumbe vyake umjue yeye….????????????
  by the great samy

 22. ramazani mussa Says:

  asalam alaykoum
  mimi ninatakakujuwa hali yangu ya maisha ni nayo kwa siku hizi na nipite jia gani ili nifaulu maisha mazuri

 23. amida mtamike Says:

  achen kubania watu kila mbuzi atakula kutokana na urefu wa kamba yake big up sheikh

 24. MarthaMe Says:

  simwamini binadamu yoyote namiini Mungu aliyeumba mbingu na dunia…..people wake uo and open ur eyes.

 25. MarthaMe Says:

  simwamini binadamu yoyote namiini Mungu aliyeumba mbingu na dunia…..people wake up and open ur eyes.

 26. Gemini Says:

  Nina matatizo ya uzazi sheikh naomba msaada wako kupitia email address yangu hapo juu, ahsante sana

 27. Ceaser Says:

  Da huyu mzee sio kigagu,bali ni hali flan ya meditation ambayo ata marastafari wanaweza kuipata na kuweka wazi.
  Mzee wangu hicho ni kipaji.kitu ambacho kibaya ni kusema siri za Jah.mfano kutabiri kifo cha mtu,kiama na wapi mtu anakwenda baada ya kufa.
  Mzee wangu,elimu uliyonayo ni yakitabu,na Jah alituambia kupitia prophet Muhamad.kwamba kila kitu cha chini ya jua na maelekezo mengine yapo ndani ya Kitabu cha Mwisho ,ambacho ni Quraan Tukufu.

 28. Karenga Says:

  Ndio naona comments zingine zina mlenga kumshambulia Sheik Yahya Hussein pamoja na kipaji alichopewa na mwenyezi Mungu mwingi wa rehma.Sheikh Yahya Hussein hakamati watu kwa nguvu kwenda kujipatia msaada wa mambo yanayo watatiza hapa duniani,yeye kazi zake ni halali na analipia kodi zote zinazo hitajika na serikali yetu.Yeye hamshurutishi mtu kwenda kwake kwa msaada wa kinyota.Watanzania huu ni wakati wa kujifunza na kwenda na wakati,Sheikh Yahya kafanya jambo kubwa sana kujenga web site kwa ajili ya shughuli zake, naona kaamua kurahisisha mambo, sasa audience yake inazidi kukua kwa kasi sana,tumuombeeni salama katika kazi zake.
  mzee kutoka Ujiji

 29. Mkolonjinji Says:

  Ikiwa kam watu wanaotegemean mwenyezi Mungu. Utabiri kama huu ni shiliki na ALLAH AWEZI KUWAVUMILIA WATU KAMA HAWA SIKU YA KIYAMA.
  KWA HAKIKA ELIMU YA GHAIBU( VITU VILIVYO JIFICHA) IPO KWAEKE (MUNGU) TU
  Ima kwa wale wanaotegemea utabili wa nyota wapo ktk shiri na huo ni ukafiri wa wazi.
  Mtabri yeyeote nwa wano mfuata hawapo katika uongofu (UISLAM) ila ni washirikina.
  nakila mshirikina ajikadirie maisha ktk shimo la moto wa jehamam.

 30. Mkolonjinji Says:

  Acheni kupalilia shiriki. Muaminini Allah. tafadhali contact me Trmlee99@yahoo.com nikutumie kitabu |the right to destroy satanism” utabiri ni part ya satanism religion. wala sio kipaje ambacho UISLAM UNAKIKUBARI. acheni uzushi muogopeni Allah.
  a real muslim never addicts to utabiri.
  “Utabri ni elimu ya shirki na matokeo yake ni motoni”
  Epukeni kutegemea sababu za kitabiri, mtegemeeni Allah huku mkichua hatua za sababu za kisayansi na sio utabri.

  Enyi waislam ujieni uislam wenu . utabiri ni ushirikina.
  Enyi wakristo. hakiak utabiri haupo ktk sifa za uslam.
  utabiri ni ukafiri.

 31. Aliccia Says:

  Bwana Yesu Asifiwe,
  Mimi ni mama wa makamo,natafuta dawa mbadala ya kuzibua mirija ya kizazi na kupevusha mayai,nataka kuzaa na matatizo hayo yamegundulika hospital na siko tayari kufanyiwa upasuaji!!!!
  Tafadhali nisaidie,naomba unitumie majibu kwa email address yangu hapo juu.

  Ubarikiwe sana kwa Jina la Yesu!!!!!!

 32. MZEE KIVUTIO KIKUBWA KWA NCHI YETU SERIKALI IMPE USHIRIKINO NI MTU MUHIMU SANA

 33. hashim Says:

  sheikh yahya mungu akuongoze na akupe mke kijana wa miaka 18 mbichi mtamu mhhhhhhh mzee una mambo wewe.
  wako
  mkojani

 34. fadhila Says:

  habari yako mzee! mimi sina bahati ya kufanikiwa na kitu chochote ambacho kitaniletea manufaa hata mwanaume nikikaa nae antaniacha katika mazingia ya utatanishi nifanyeje na umri unapotea bila mafanikio ya malengo

 35. zaina seif Says:

  Mimi sijawahi kutabiriwa na sheikh yahya, ila nilisha msikia akisoma Quraan. mashaallah, haki ya mungu sheikh huyu akiwa anasoma Quaan tukufu, utasikia madirisha na milango yakigongana kutokana na ile sauti nzuri ya na usomaji wake Quraan tukufu, basi malaika wanagombania madirishani kusikiliza na kuona nani asomae quraan kwa sauti nzuri kama hiyo ! mimi binafsi ninapo msikia sheikh akisoma Quraan mama yangu mzazi huwa natokwa na machozi!

  Hongera sheikh wangu.

 36. issa said AL-ISMAILY Says:

  Namtakia afya njema Sheikh Yahya azidi kutusaidia

 37. RAMAZANI MUSSA Says:

  VIPI HALI YA INCHI YA R D CONGO VITA HUENDELEA ? MIMI NINA HITAJI KUPATA PESA YA KUNUNUA GARI.

 38. sweet bady Says:

  kwakweli haifai kumsema mtu

 39. Willo Says:

  Sheikh Yahya Hussein ni kiboka ya njiakuhusu masuala ya utabiri babu yangu yule si mtu wa mchezo yuko fit sana na anajua afanyalo,mwenzetu macho yake yanaona tusivyoviona sisi wengi.Muachieni babu yangu afanye vitu vyake,je mliishs msikia maalim Hussein pia (huyu ni baba yake sheikh Yahya na kafundisha wengi sana kusoma Holy Qraan pale nyumbani kwake mtaa wa Mafia.Hawa watu wamejaaliwa vipaji vikubwa vikubwa na hakuna mtu atakaye weza kivichukuwa kutoka kwao,wacheni midomo ya kitanzania maana wabongo tunasifa ya kujua matusi na upondaji watu.
  wenu mgosi wa Ndere.

 40. sudika Says:

  hiv mi naomba kujua ki2 kimoja utabiri umekatazwa katika kuran au haujakatazwa?second ni zambi za aina gan ambazo mwenyez munngu amesema hatozisameh mpaka unaingia kaburin?

 41. buddy jamic Says:

  sheikh yahaya ni kiboko wengine wote wanaiga upo juu baba

 42. wardaizoo Says:

  2be honest anatusave sana tu….wanaompinga wana yao!!nadhani kinachohitajika ni imani tu,ata kama unasali kama huna imani ua doing nothing.namfagilia kwa sana coz anawasaidia hata wasioweza kumpa chochote ki2.big up SHEKHE

 43. SALIM ALI Says:

  shk yahy husein ni mushrik nina maana kuwa ni mshirikina kwa waislam wenye kufuata uislma wao ni haraam kujifunza na kuifanyia kazi mambo ya nyota yaani ni nujuu ni mambo ya shetwni mlaanifu aliefukuzwa katika rehema za mwenyezimungu na yeyote atakaemfuata na kuamini maneno yake japo kuwa anaweza kusibu basiatakuwa pale naye katika moto wa jahannam , maana mtume wetu hakuwa mnajimu wala mpiga ramli na mambo ya uchawi hafai kabisha sheke yahya hussein na wala hafai kuitwa shekhe. salim

 44. SALIM ALI Says:

  Acheni kupalilia shiriki. Muaminini Allah. tafadhali contact me Trmlee99@yahoo.com nikutumie kitabu |the right to destroy satanism” utabiri ni part ya satanism religion. wala sio kipaje ambacho UISLAM UNAKIKUBARI. acheni uzushi muogopeni Allah.
  a real muslim never addicts to utabiri.
  “Utabri ni elimu ya shirki na matokeo yake ni motoni”
  Epukeni kutegemea sababu za kitabiri, mtegemeeni Allah huku mkichua hatua za sababu za kisayansi na sio utabri.

  Enyi waislam ujieni uislam wenu . utabiri ni ushirikina.
  Enyi wakristo. hakiak utabiri haupo ktk sifa za uslam.
  utabiri ni ukafiri. nakupongeza sana ndugu yangu kwa waislam wasioijua dini yao wana kokotwa tu na mshirikina

 45. kidoto s kidoto Says:

  naungana na mchaniaji wa mwisho,

  utabiri huendana na majini na ni moja kati ya shirki na muumba wetu anasema hakuna kosa kubwa kwake kama shirk na hasamehe kosa hilo!!
  nachukua fursa hii kumkanya awache mara moja na arudi kwa muumba wake na kama hataki basi akome kuinasibisha elimu yake ya shirki na quraan tukufu na uislam; kwani uislam unakataa mambo hayo na quraan haikubali.

 46. rodman Says:

  sorry naomba website ya Sheikh Yahya Hussein itanisaidia kwa kuwasiliana na shekh

 47. mohamed osman Says:

  please could you kindly give me the contract or information or the name of Sheikh who recovered stolen good in mombasa during the kenya election problem in December

 48. binti-mzuri Says:

  huyu mzee zaidi ya utabiri ni mganga,na am sorry to say this, mchawi. zamani zile,nilikua namjua mama mmoja jirani yangu siku moja aliropokaga eti kaenda kwa huyu sheikh kugangiwa,kisa mumewe alikua anatoka nje ya ndoa.ndo nikashangaa,huyu mtabiri atagangaje,ndo nikapewa ‘habari ndo hiyo’ huyu sio mtabiri tu ila ni mganga na anaweza kukuchawia,kama huyo demu alivyomchawia mume wake. MUNGU tuongoze! hizi dhambi mwe!

 49. Hello Mkolonjinji big up man! u these people they don seem to understand what they’re told! hilo halina ubishi kwamba utabiri huu unaofanywa na hawa mabwana ni njia za shetani tu! Ambao ni ushirikina mtupu lakini kwa bahati mbaya sana nafsi ya mwanadam inapendezwa sana na uovu (mambo ya kishetani) hilo linalofanywa na hawa wanaoitwa wanajimu (astrologists) haliungwi mkono na Quran wala biblia tuache hayo mambo!

 50. Hamida Says:

  Big up sheikh tena nna mpango wakukutembelea mwembechai ndio maana nikapitia habari yako kwanza. Wasiotaka kuku-visit ki vyao vyao. Nahitaji utabiri wa 2009 nakutegemea kwa ushauri

 51. Jose Says:

  Binafsi utabiri wa nyota huwa unanipatia sana sheikh. Kaza buti

 52. Matty Says:

  mwanga tu huyu hakuna nini wala nini!

 53. kulutu Willo Says:

  Mimi ni mmanyema safi na watu wangu wamanyema wengi wanaamini hayo mambo ni kitu cha kawaida kwa wamanyema kuwa na imani kama hizo.Ni vizuri tumuogope m/mungu amekataza sirki kama hizi.Kila mwanadamu ni mtabiri wewe muombe m/mungu na kama siku ni yako utaona mambo yote uliyomuomba yanakwenda sawa,kwa hiyo mchawi wetu mkubwa ni subhana wa taala na sio binadamu au mitume.Mwenyezi mungu amesema kwenye holy qoran “niombeni na nitakusikilizeni”ni hivyo tuu ,simple sana haina haja ya kutegemea watu wengine kuzungumza naye,usitegemee watu wewe nenda moja kwa moja kwake na matokeo yake utayaona.Msisahau kuwa dua zinaambatana na rakaa ,ni lazima kusimamisha sala tano kwanza halafu ndio maombi.Kwa maelezo zaidi kuhusu deen wasiliana namimi through this address karenga@lycos.com hapo tutajadili kwakina kuhusu deen ya kiislam ni hayo kwa leo nawatakieni wote week njema popote mlipo.
  Kulutu Willo
  wasalaam
  Allah knows best!

 54. Abdul Says:

  Hey punguzeni maneno yasiyona mpangilio,Sheikh Yahya Hussein ni bingwa wa utabiri Afrika Mashariki nzima na vitu anavyotabiri vina ukweli mtupu tofauti na hao watabiri wengine ambao wanaongopa bila haya machoni pao yani kazi yao ni wizi mtupu enziii za Mwalimu kulikuwa na watabili wa kweli ambao walitabiri mambo mengi na yalitokea lakini hivi sasa ni wizi mtupu,hata kipindi Kristo anazaliwa wale Mamajusi wa mashariki na magharibi walitabili kuwa kuna Mfalme wa wayaudi amezaliwa nao walienda kumsujudia lakini hivi sasa watu wamejazana kwa waganga wanataka mali na vitu vingi vya anasa wamemsahau Mungu,Sheikh Yahya ni mtabiri basi acheni atabiri atakae amin mwacheni aamin na asiyeamin basi nae mwacheni,ila fahamuni kuwa utabiri sio uchawi.Asanteni wote kama kuna maswali au unahitaji ufahamu zaidi niko kwenye hassbaby@gmail.com

 55. Mkolonjinji Says:

  Naomab niwasalimie kwa salaam ya kiislam,Asalam alikum, (Amani hiwe juu yenu)

  Nawaomba mutembelee website hii http://www.alhidaya.com.
  Utabiri kam wa huyu sheikh ni shirik hivyo yeye ni mshirikina pia. Kila mwenye kumfuata mshirikina ni naye ni mshirikina.

  Allah asema kila mchawi (mshirikina) ajikadirie nafasi ktk moto wa JEHANAM.

  Wote ninyi mnao mshabikia Yahaya ni wafuasi wa shirk. Ninyi na huyo mnaye mfuata nitaingizwa motoni bila wasiwasi. kisha mtashuhudia kwa yakini mpo moto.

  Hivi mnajua nini kuhusu SATANISM? kijitawi chake kidogo MASONS. MNAJUA?

  Siku moja nilikuwa nilifungua TV kipindi kilichokua hewani kilikuwa cha YAHAYA katika maongezi yake alionyesha kuwa Askofu mmoja naye anaendesha kipind star TV (sipendi kumtaja jina lake) Yahaya kaseam kuwa ni FREE MASON. akaongeza akisema kama yeye si FREE MASON aende mahakamani.

  Siku ilifuata yule askofu alijibu kwa kufundisha mtandao wa shetan na akimtuhumu Yahay kuwa ni Mason lakini bila kutaja waziwazi.

  NINI TWAJIFUNZA?
  WOTE HAWA WAWILI NI FREE MASONS. ( WANAFUATA NADHARIA WAZI ZA MFUMO WA SHETANI WAKIJIEGEMEZA KATIKA DINI). YAHAYA AMEJIEGEMEZA KATIKA UISLAM kwa UHAKIKA wa mafundisho ya UISLAM Yahaya si Mwislam. Na huyo Askofu mmiliki wa kanisa amejiegemeza katika Ukristo akitumia Bibilia lakini si Mkristo.

  Wenye akili wameelewa. kama bado unatatizo hapa.
  Unawea kuniandikia nitakutumia kitabu kilicho andikwa kwa lugha ya kiingeleza juu ya SATANISM utawajua hawa.
  Tumia email hii trmlee99@yahoo.com

  Ninashangaa kuona watu wanachangia hoja za kusifu mtu wataiki wawajui mambo wanayo changia.

  Ikiwa wewe ni mwislam acha kushabikia shiriki na washireikina.
  Mwogope Allah.
  Ukiwa wewe ni mkoristo. unahitaji maelekezo zaidi niambie nitakutumia makala zitakazo kusaidia kujua ukweli wa mambo.

  Ukituma email elza wazi nini unahijaji. ucije ukaandika tu nitumie…., nini we unahitaji nini

 56. Mkolonjinji Says:

  HIVI UNAVICHWA VYA NANA GANI? YAHAYA MWENYWE ALIKUBARI KUWA ANATUMIA MAJINI.

  ALLAH AMETUKATAZA CONTACT YEYOTE NA MAJINI. WAPO WATU WANAO SEMEA NA KULETA HOJA ZAO KUWA CONTACT NA MAJINI ZIMERUHUSIWA KTK DINI.

  HOJA ZAO NI DHAIFU. MAFUNDISHO YA UISLAM HAYATUAMBII HIVYO. KOMENI KUUCHAFUA UISLAM KWA SHIRK. HAKUNA DHAMBI KUBWA ZAIDI KULIKO SHIRK.

  ALLAH S.W AMEASEMA ATASAMEHE DHAMBI ZOTE ILA SHIRK.
  MWOGOPENI MUUMBA WENU JAMANI.

 57. imma Says:

  nakupongeza mzeeee kwa kazi unayo fanya

 58. Mariam Says:

  Salaam.
  Sheikh naomba unitabirie mimi nitaolewa na nani? Jina langu kamili lipo kwenye email address yangu.
  Ahsante.

 59. Mariam Says:

  Salaam.
  Sheikh naomba unitabilie mtu atakae nioa. pia naomba namba yako ya simu ya mkononi ili nipate kukuuliza maswali mengine.
  Ahsante.

 60. ramona Says:

  wewe mariam unachekesha sana..subiria mume utakayeletewa na Muumba,wanaume wa kuwavuta kwa uganga sio wazuri.. limbwata litakuishia na utakimbiwa

 61. AMANI KWENU WOTE MLIOCHANGIA MAONI KTK SWALA La YAHAYA HUSSEIN!. Kwakweli tofauti lazima ziwepo kati yetu hii ni kutokana na mitazamo ya watu wenye imani tofauti! Lakini tusiendelee kubisha pasi na kuwa na hoja za msingi wakati tayari mchangiaji ameshatoa maelezo yenye uzito kutoka katika vitabu vitakatifu vya dini! Kwa kweli hata kama utabiri huo utaendana na ukweli lakini lazima tukubali kwamba linalofanywa halipo ktk njia sahihi! Kwani mimi mara nyingi nimeshamsiki Yahaya Hussein akisema kupitia vyombo vya habari kwamba utabiri anaoufanya ni uchawi mkubwa! Husema “HUU NI UCHAWI MKUBWA!” sasa tujiulize uchawi unakubalika ktk jamii yetu? au umepewa nafasi gani ktk vitabu vyetu vya dini! Hata kama anayoyafanya mnayapenda lakini mkubali kwamba hayakubaliki ktk imani za dini ni makosa makubwa! Ni kazi ya shetani! Ni vizuri sana myapime mambo kwa mizani ya mafundisho ya dini na msijiingize ktk malumbano msiyokuwa na elimu nayo bali mnategemea vichwa na mataminio ya nafsi zenu! Nafsi zenu ni zenye kupenda mambo ya anasa na amali zote za shetani ndio maana unaona leo hii wengi hawapo ktk kujibidiisha na mambo ya Mungu bali ni starehe na anasa! Anayoyafanya ni ushetani mtupu! muache ubishi lah mlete hoja zenye kueleweka!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s