BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

57! October, 12, 2007

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:46 PM
Tags: ,

Jumapili iliyopita Raisi Jakaya Mrisho Kikwete alisheherekea miaka 57 ya kuzaliwa.Alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1950 katika katika kijiji cha Msoga kilichopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani katika iliyokuwa inaitwa Tanganyika. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Msoga kati ya mwaka 1958 na 1961.Baada ya hapo alihamia shule ya kati(middle school) Lugoba kati ya mwaka 1962 mpaka 1965. Baada ya hapo akajiunga na shule ya sekondari Kibaha kwa ajili ya O’level.Hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1966 mpaka 1969. Baada ya hapo akaelekea shule ya sekondari Tanga kwa ajili ya A’Level. Mwaka 1972 mpaka 1975 alikuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam akisomea Uchumi.

 

Pichani Raisi Jakaya Mrisho Kikwete, akikata keki kusheherekea hiyo siku yake ya kuzaliwa katika hafla iliyofanyikia kwenye makazi yake,Ikulu jijini Dar-es-salam. Kutoka Kushoto ni watoto wa raisi Ridhwan, Rashid Chodo,Mohamed (mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ambaye ni yatima anayelelewa na raisi nyumbani kwake), Lulu na Khalfan Kikwete.

Picha kwa hisani ya Yahya Charahani.

Advertisements
 

SALAMU KUTOKA KWA ALLY REHMTULLAH

Filed under: Eid Mubarak,Fashion,Fashion Designer — bongocelebrity @ 9:03 AM

 

NEEMA

Filed under: Eid Mubarak,Muziki,Tanzania/Zanzibar,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ni Ijumaa tena. Kama kawaida leo ni siku ya midundo kidogo. Leo si wengine bali Orchestra Mlimani Park na wimbo Neema ukiwa ni utunzi wake Cosmas Thobias Chidumule. BongoCelebrity inapenda kuchukua nafasi hii pia kuwatakia watanzania wote, popote walipo mwisho mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na hivyo EID MUBARAK!