BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NATURE ASHINDA TUZO ZA CHANNEL O! October, 13, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:59 PM

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature ambaye kama mtakumbuka BongoCelebrity iliandika juu ya kuchaguliwa kwake kuwania tuzo za kituo cha televisheni cha Channel O zijulikanazo kama Channel O Spirit of Africa Music Video Awards, ameshinda!

Juma Nature ambaye alihudhuria utoaji wa tuzo hizo zilizofanyikia katika ukumbi wa jiji la Johanesburg (Johanesburg City Hall) nchini Afrika Kusini hivi karibuni , ameshinda kwa upande wa video bora kutoka Afrika Mashariki kutokana na wimbo wake Mugambo.Matokeo kamili unaweza kuyasoma katika tovuti ya Channel O.

Katika mazungumzo mafupi tuliyofanya naye baada ya kurejea toka Afrika Kusini na ushindi, Nature amewashukuru watanzania wote waliompigia kura ili ashinde.Amewataka wote kuendelea na moyo huo huo kwani sio tu kwamba wanasaidia kukua kwa muziki wa kizazi kipya bali pia kuzidi kuitangaza Tanzania katika medani za kimataifa.

Wimbo Mugambo ulirekodiwa katika studio za Bongo Records na video ikatengenezwa na Visual Lab iliyo chini ya uongozi wa Adam Juma. BongoCelebrity inampongeza Juma Nature na wote walioshirikiana naye kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha ushindi huu. Siku za nyuma tuliwahi kufanya mahojiano na Juma Nature ambayo unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Advertisements