BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NATURE ASHINDA TUZO ZA CHANNEL O! October, 13, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:59 PM

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature ambaye kama mtakumbuka BongoCelebrity iliandika juu ya kuchaguliwa kwake kuwania tuzo za kituo cha televisheni cha Channel O zijulikanazo kama Channel O Spirit of Africa Music Video Awards, ameshinda!

Juma Nature ambaye alihudhuria utoaji wa tuzo hizo zilizofanyikia katika ukumbi wa jiji la Johanesburg (Johanesburg City Hall) nchini Afrika Kusini hivi karibuni , ameshinda kwa upande wa video bora kutoka Afrika Mashariki kutokana na wimbo wake Mugambo.Matokeo kamili unaweza kuyasoma katika tovuti ya Channel O.

Katika mazungumzo mafupi tuliyofanya naye baada ya kurejea toka Afrika Kusini na ushindi, Nature amewashukuru watanzania wote waliompigia kura ili ashinde.Amewataka wote kuendelea na moyo huo huo kwani sio tu kwamba wanasaidia kukua kwa muziki wa kizazi kipya bali pia kuzidi kuitangaza Tanzania katika medani za kimataifa.

Wimbo Mugambo ulirekodiwa katika studio za Bongo Records na video ikatengenezwa na Visual Lab iliyo chini ya uongozi wa Adam Juma. BongoCelebrity inampongeza Juma Nature na wote walioshirikiana naye kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha ushindi huu. Siku za nyuma tuliwahi kufanya mahojiano na Juma Nature ambayo unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Advertisements
 

14 Responses to “NATURE ASHINDA TUZO ZA CHANNEL O!”

 1. Dinah Says:

  Mimi napenda mpangilio wa meno yake 🙂

  Hongera JN kwa ushindi huo.

 2. jull Says:

  SHEIKH YAHAYA ALITABIRI USHINDI WAKE

 3. Kasyome Says:

  Hongera sana Necha!
  Yaani huyu jamaa alipotangazwa tu kwa mara ya kwanza kwamba anawania hii tuzo niliamini angeshinda tu!Kwa nini?Msikilize!!!!!!

 4. TanzanianDream Says:

  Duuh Wabongo bwana wanafki mno eti nilijua atashinda mbona hukujua atashinda MTV Europe?au ulijua halafu akashindwa?

  Nway huyu jamaa ndo msanii mwenye mganga hodari kwa wasanii wa Fleva labda anashindana na bwana Mheshimiwa kwa kuwa na mganga hodari…

 5. Big Willy Says:

  Big up sana mtoto wa kiumeni mwendo huohuo kaka kaza buti aminiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mlume

 6. kinono Says:

  Lakini wanamuziki wa kibongo kwa nini wengi wanakuwa wachafu?

 7. mohamed Says:

  Hongea mgoshi!

 8. emanuely lwilla a.k.a CHOMA P Says:

  BIG UP KAKA KAZA MWENDO ILAINAKUBIDI UBADILIKE KAKA SI UNAJUA MWANZO MGUMU SIKU ZOTE M2WANGU SAIZI KILICHO BAKI CHEKI LIFE LAKO KAKA SIUNAJUHA MAJUKUMU.SINA MENGI KAKA

 9. speed Says:

  T/dream nmeshindwa kukuvumilia kwakweli,ninachofanya ni kukukanya ndugu la sivyo utaishia kubaya,watu wakiamua kukasaka uwape ushahidi watakupata tu hata ujifiche vipi…ohooo!!!!!11

  anyway,msitu wa vina…ohi ohi oi oi..sana tu mtu wangu…endelea ziba ziba vilimi limi vya watu mpk waje wakupigie magoti mtu mzima.

  kikubwa nimemiss michano yako style za “hili game”,otherwise kwa bongo uko juu.

  Hongera sana mtu mzima….

 10. beutness Says:

  mi simfagilii hata kidogo, aache unafiki umbeya na majungu.

 11. […] kusema blogu zina nguvu kubwa sana katika kubadili upepo wa matokeo ya kitu fulani. Kwanza ilikuwa Juma Nature juzijuzi pale kwenye tuzo za muziki za Channel O, akanyakua ile kitu. Halafu leo usiku, baada ya […]

 12. […] kusema blogu zina nguvu kubwa sana katika kubadili upepo wa matokeo ya kitu fulani. Kwanza ilikuwa Juma Nature juzijuzi pale kwenye tuzo za muziki za Channel O, akanyakua ile kitu kwa nguvu ya kura ya wadau. […]


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s