BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TUNAPOMKUMBUKA MWALIMU NYERERE. October, 14, 2007

Filed under: Bunge,In Memory/Kumbukumbu,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:06 AM
Tags: , ,

Julius Nyerere

Sote tunaweza kuwa maarufu, tunaweza kuwa chochote tunachotaka . Pamoja na hayo, jambo moja ambalo ni dhahiri itakuwa ni vigumu sana kulifikia ni kuwa maarufu na kuheshimika duniani kote kama ilivyokuwa kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye hivi leo tunakumbuka miaka nane tangu afariki dunia mnamo tarehe kama ya leo mwaka 1999 kule nchini Uingereza katika hospitali ya Mtakatifu Thomas kwa ugonjwa wa saratani ya damu (leukemia).

Serikali ilipotangaza rasmi kwamba Nyerere hatunaye tena, uchungu na simanzi uliikumba nchi nzima na dunia kwa ujumla hususani kwa wale waliokuwa wanamjua Nyerere na kujua alichokuwa akikisimamia na alichokiamini. Bara la Afrika likawa limempoteza kipenzi chake, mtoto wa Afrika ambaye thamani ya mchango wake katika ukombozi wa bara la Afrika haina kipimo. Mpaka anafariki dunia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha amani barani Afrika.Mfano mzuri ni mgogoro wa Burundi aliokuwa akijaribu kuusuluhisha. Mwenyewe aliwahi kutamka kwamba yeye ni mwafrika kwanza na kisha mjamaa.

Mpaka leo hii jina la Nyerere linabakia kuwa kitambulisho chetu kikubwa .Wakati mwingine zaidi hata ya jina la nchi yetu yaani Tanzania.Wapo watu wanaolijua jina la Nyerere na wala wasijue jina la Tanzania au hata Tanganyika. Haishangazi, alikuwa ni mwana wa Afrika kamili. Kadiri siku zinavyopita, taratibu baadhi yetu, hususani vijana wanaoitwa wa kizazi kipya, wanazidi kulisahau jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Viongozi wetu wengi wa sasa( ingawa wakati wa msiba wake waliahidi kumuenzi kwa hali na mali) wanaelekea kusahau kabisa ahadi zao! Wengi wanabakia kumuenzi kwa maneno na sio vitendo.

Lakini je,sote tunafahamu japo kidogo tu historia ya Mwalimu Nyerere? Uwezekano ni kwamba sio wote,hususani vijana wa sasa. Kwa kifupi na kwa msaada wa vyanzo mbalimbali hii hapa historia fupi ya Hayati Baba wa Taifa;

Julius Kambarage Nyerere

Hayati Baba wa Taifa akisisitiza jambo

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13 Aprili mwaka 1922 huko Butiama mkoani Mara, pembezoni mwa ziwa Victoria,kaskazini mwa Tanzania. Baba yake alikuwa ni Chifu katika kabila dogo la Wazanaki.Nyerere alikuwa miongoni wa watoto wanaosemekana kufikia hadi 26. Baba yake, Mzee Burito Nyerere alikuwa na wake wapatao 22.Alianza shule akiwa na umri wa miaka 12 (ilimbidi kutembea kwa zaidi ya kilometa 26 hadi Musoma mjini ili kupata elimu ya msingi). Kipaji cha uelewa shuleni kilimuwezesha kumaliza kozi ya miaka minne ndani ya miaka mitatu tu. Baadaye mnamo mwaka 1937,alijiunga na shule ya sekondari ya serikali ya Tabora kwa masomo ya sekondari. Alibatizwa katika kanisa katoliki akiwa na umri wa miaka 20.

Kipaji chake cha kitaaluma na kiuongozi kilionekana tangu mapema. Kwa msaada wa waliokuwa waalimu wake pale Tabora (ma-father wa kanisa katoliki) baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda kusomea ualimu. Fikra za kimapinduzi na kusaidia waafrika wenzake zilianza kuonekana wazi akiwa Makerere.

Nyumba ya Nyerere

Nyumba aliyojengewa Mwalimu Nyerere na serikali baada ya kustaafu.Ipo Butiama.

Baada ya kumaliza Makerere alirejea Tanzania na kwenda kufundisha (St. Mary’s Secondary School) mkoani Tabora. Mwaka 1949 alipata scholarship kwenda Chuo Kikuu cha Edinburgh kusomea shahada ya pili (Masters) katika historia na uchumi wa kisiasa(History and Political Economy). Alipokuwa masomoni Edinburgh, Nyerere ndipo alipoanza rasmi kuunda mawazo yake ya kiukombozi kufuatia kuanza kujifunza kilichoitwa Fabian Thinking . Mawazo yake ya kuunganisha ujamaa na ujima au maisha ya kijamii ya kiafrika ndipo yalipoanza kujijenga au kujiimarisha.Harakati za kujipatia uhuru kwa nchi ya Ghana zilizokuwa zikiongozwa na Dr.Kwame Nkrumah,anakiri Nyerere katika baadhi ya mahojiano aliyowahi kufanya, zilichangia kuamsha fikra za kujikomboa kutoka mikononi mwa wakoloni. Inasemekana Nyerere ndio alikuwa mtanzania wa kwanza kusomea katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata degree nje ya Afrika. Alihitimu mwaka 1952.

Nyerere na mama Maria

Mwalimu Nyerere na mkewe Mama Maria Nyerere.

Aliporejea nchini Tanzania (enzi hizo bado ikiitwa Tanganyika), alianza kazi ya kufundisha masomo ya Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St.Francis’ (sasa Pugu Sekondari). Wakati huo huo akawa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa TAA(Tanganyika African Association) chama kilichokuwa kimeundwa kusimamia maslahi ya waafrika ingawa tayari kikiwa na vuguvugu la kiukombozi na kisiasa. Hapo ndipo serikali ya kikoloni ilipomlazimisha kuchagua kati ya kufundisha(ualimu) au siasa. Mwenyewe anasema alikuwa amepanga kufundisha kwa angalau miaka mitatu kwanza kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye siasa. Hilo halikuwezekana. Akachagua kuwa mwanasiasa na hivyo kuanza mkakati mzito wa kuviunganisha vyama mbalimbali vilivyokuwa na malengo sawa.

Nyerere was a simple man!

Mwalimu Nyerere ndani ya Butiama.

Kazi ya kuviunganisha vikundi mbalimbali vya kisiasa vilivyokuwa vimeanza kutapakaa nchi nzima haikuwa rahisi. Lakini alifanikiwa kufanya hivyo mwaka 1954 kwa kuundwa kwa TANU(Tanganyika African National Union) na yeye kuchaguliwa kukiongoza.

Humo ndimo alimopumzika Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.Tizama na tafakari kwa makini maneno yaliyoandikwa hapo nje.

Aliingia katika bunge la wakati huo mwaka 1958 kabla hajawa waziri mkuu mwaka 1960. Tarehe 1 May 1961, Tanganyika ilipewa uhuru wa kujitawala na Nyerere akawa waziri mkuu wa kwanza. Uhuru kamili ulipatikana mwaka tarehe 9 December 1961. Mwaka mmoja baadaye (1962) Nyerere akawa Raisi wa kwanza wa Tanganyika ilipokuwa Jamhuri ya Tanganyika.

Nyerere,mama yake na mkewe

Mwalimu Nyerere(katikati),mama yake mzazi(kushoto) na mkewe Maria(kulia).Picha hii ilipigwa Novemba 10,1985 Butiama baada ya Nyerere kustaafu.

Julius Nyerere alimuoa Maria Gabriel Magige (Mama Maria Nyerere) tarehe 24 Januari 1953 na walijaliwa kupata watoto wanane. Alipostaafu nafasi yake ya uraisi mwaka 1985 alirudi kijijini Butiama ambako alibakia kuwa mkulima wa kawaida mpaka kufariki kwake Oktoba 14, 1999. Endelea kupumzika kwa amani Mwalimu.

Tanzania note

Sura ya Nyerere katika noti ya Shs 100 enzi hizo.

R.I.P MWALIMU JULIUS K.NYERERE.

Advertisements
 

22 Responses to “TUNAPOMKUMBUKA MWALIMU NYERERE.”

 1. Moses Jakanyangoe Says:

  There is a friend of mine who by then was working as an engineer ni Friendship Textile (Urafiki), who told me that when the president Mkapa offially broke the news of Mwalimu’s death, in every corner of the factory you could hear loud cries from the people of various ranks even from those who had not known Mwalimu personally…people literally cried loudly!

  Really, he was a great man with great mind to admire!…He will live in our hearts forever!

 2. Kimori Says:

  With tears in my eyes
  I still remember, when I got my form-one joining instruction without a follow-up in a remote area though I lived hundreds of kilometres from the nearest post office

  I still remember that my poor parents were not obliged to pay anything like a school fees or any other expenses whatsoever except the pair of uniforms instructed to be bought,

  I still remember that I had not to carry my own mattress to school,

  I still remember free exercise and text books in the library and how we worked hard without tuitions and photocopy machines,

  I still remember the warrants I used to travel with to and from a boarding secondary school in a far end of the country from where I was born,

  I still remember the train wagons and buses booked for students during the terminal and annual holidays,

  I still remember the unity existed among the school students regardless of the family status, religion, race and social background as I was not aware of the difference between John and Abdallah,

  I still remember how we were proud of our beautiful country and sang a lot of songs of praises,

  I still remember the colouful inter-school sporting events from the primary level to the secondary level, form which many young men and women became champions in out country,

  I still remember a lot!

  Well, time has changed and people too!…all changes are inevitable in any process of development in a society, but let us ask ourselves, are we changing to the positive site of negative side?…The answer is obvious!

  To some of us Mwalimu will always remain in our hearts forever and ever and we have to convey the massage loud and clear to the next generation!

  Our leaders should, therefore, understand that the cost of forgetfulness is too high to be paid by our grandchildren!

 3. TanzanianDream Says:

  Wow….THERE gOES MY hERO mY iDOL….mWALIMU tHE gREAT

 4. Lotte Says:

  Yap! I remember everything like Kimori and wonder whether there was anything wrong with all that! I remember when there were free ex. books (madaftari); all what the office needed was for you to show your old one and sign for a new one. I remember all the songs and our dreams for African Unity and I agree with you Kimori that: “Our leaders should, therefore, understand that the cost of forgetfulness is too high to be paid by our grandchildren!”

  “UPEPARI NI UNYAMA”! Siku zote tutakukumbuka Mwalimu, kwa busara zako na kwa kuongoza kwa mifano!

 5. mohamed Says:

  Kimori ‘pesa mbote’sina cha kusema wala kuongeza HUYO NDIE MWALIMU NYERERE nasi tutahakikisha kuwa ‘Mwalimu will always remain in our hearts forever and ever and we have to convey the message loud and clear to the next generation!safi sana Kimori

 6. Dinah Says:

  Mungu akurehemu Mchonga!

  Sasa wandugu tukimuweka Mwl mioyoni mwetu wale wapenzi wetu, wake/waume/watoto ndugu na marafiki watakaa wapi?

  Mimi nafikiri ni vema kumuenzi kama walivyomuenzi kwa jina “baba wa Taifa”, Uwanja wa ndege sasa ni jina lake, kunamakumbusho kuhusu yeye n.k

  Mimi binafsi sina la kusemakuhusu Mwl nyerere kwani wakati wa Utawala wake nilikuwa mdogo, ninaweza kusifia kuhusu Mwl ni u-“humble” wake, uzungumzaji wake ambao unakufanya uendelee kusikiliza tu na kile kicheko.

  Ila nina uhakika kuwa kuna mabaya mengi tu yalitokea wakati wa Uongozi wake, tusaidiane kuyazungumzia hayo pia sio mema na mzuri tu hakuna mtu perfect sio?

  BC tuletee Rais wa 2 A.H Mwinyi aliyechukua Urais nchi ikiwa “imezubaa”, akaruhusu biashara binafsi na upatikanaji wa pesa wa kizembe(kila mtu alikuwa na mafweza)na uhujumiuchumi ukapotea……:-) 🙂

 7. CASHMOEYHOLLAND Says:

  HAKUNA KAMA NYERERE…KWANI MIAKA YA 1930 TAYARI KAITOA KIMAISHA….WAKATI WAZAZI WENGINE MIAKA HIYO WANALEWA TU CHIBUKU…ONGELA NYERERE…ALLWAYS MISS YOU…RIP..TEACHER…

 8. MAY GOD REST YOUR SOUL.wow siku zinaenda ni kama siku chache tu nilienda msibani msasani.imeshafika miaka 8? mungu akurehem baba wa taifa.

 9. Aboutalib Saleh Says:

  “Kila nafsi itaonja umauti”hii ndio ahadi yake mola kwa wanaadamu….ni miaka 8 sasa tangu baba na muasisi wa taifa hili afariki dunia,ametuwekea misingi bora,tunamshukuru saana,mola ailaze roho yake mahala peme peponi aaamin ….

 10. …Ni vyema sisi sote kama watanzania tukarudisha mioyo ya uzalendo kwa kuipenda nchi yetu na kujali maslahi ya watu wote kama vile ilivyokua miaka fulani ya nyuma….inavyo onekana sasa ni kwamba uzalendo umekufa kila mtu anajali zaidi nafsi yake tu!!

 11. lee Says:

  Naamini kabisaa kama Mwalimu angekuwapo; Kikwete, Lowasa, na hao wa aina hiyo wasingeona ndani!! Ama kweli Mwl aliona mbali 1995! Pumzika pema muzee.

 12. Citizen Says:

  Maisha ya kibepari ni maisha ya uhasama, maisha yenye dhuruma. Binadamu wazima na fahamu zao, huishi kama wanyama wa mwituni ambao maisha yao ya kila siku na ujanja wao wa porini hutegemea urefu wa makucha yao na ukali wa meno yao. UBEPARI NI UNYAMA!!!

 13. Reg Miserere Says:

  Dinnah;

  Ubaya wa mtu uukumbukwe tu ” for future corrections on delivering measurable improvements. Namna nyingine akifariki mtu achana na ubaya wake bwana, au unasemaje??…

 14. kijiwe Says:

  yap Nyerere did what is called “Made you look” to most Tanzanians.Wengi wa wazazi wetu waliweza kujisomea bure and so on.He was very good in making sure hakuna wizi wa kijinga jinga.Then mzee Mwinyi came through with his “Ruksaa” flavour.Yes it was a good one sababu kila mtu aliuchukua mzigo wake mwenyewe.Akaja Mh Mkapa(duh huyu alijaribu kuweka mambo sawa ila his counterpat(if you know what I mean)alimuangusha kwa kuwa kibaka wa hali ya juu.Now we have Mh JK(a.k.a Vasco Da Gama(mzee wa safari za nje).Huyu so far hajafanya lolote tumpe muda ingawa I am a bit sceptical sababu mambo mengi yalikuwa yameshaanza kukamilika.Amekuta ofisi ipo sawa tatizo akaanza kuwa too ambitious na vi promise vyake which i doubt kama atakamilisha even 20% of hizo promise zake na u Vasco DaGama wake.
  So ukweli unabaki palepale kiongozi mzuri Tanzania bado hajazaliwa na kama amezaliwa basi haishi Tanzania.

 15. Mt. Kichaka Says:

  Lee! umesema kweli na waziwazi. Kama Mtu wa watu angekuwa bado hai, basi hawa wauaji, wezi na wala rushwa waliojipanga huko juu wasingeona ndani. Wamuulie john pale Dodoma.
  Tena watatumaliza, Jamani!
  Asante sana Mwalimu kwa malezi yako mema mno.
  Pumzika kwa amani, tutakukuta huko uliko maana jamaa huku wanatuondoa kama mbuzi wa krismas.

 16. Nakumbuka kipindi cha utawala wa awamu ya kwanza.
  shule zote za msingi tulikuwa tunajidai kwa buruga bila kusahau uji wa maziwa.r i p mwalimu

 17. van Says:

  Kimori mi sina jipya ila umenikumbusha mengi aliyoweza kuyafanya baba wa taifa, pia mohamedi napenda kuuliza hivi madaftari ya bure kwani hakuna siku hz?Duuh mi nilikuwa nasoma shule moja hapo TZ ni karibu tu na ofc ya chama tawala miaka ya 1980’s,tukisikia Raisi kipindi kile Mwl. anakuja pale tulikuwa tunaomba kwa mwalimu wa darasa tukamuone, i mean ku-admire his presence,pia ukikutana na msafara wake unapenda asipite haraka ili umuone,ila kwa sasa nasikia watu hawana muda wa kuangalia viongozi, kwa kuchefuka na mambo wanayoyafanya tena utasikia na huyu hajiuzuru?Hii inatufundisha nini ni kwamba wakuu wamesahau majukumu yao.

  Mi napenda nimkumbuke sana mwalimu kwa mengi aliyotufanyia, na kama si juhudi za mwalimu mi ningefika vp huku nilipo.kwani shule zilikuwa bureeee na gharama za maisha zilikuwa chini, ila kwa sasa nasikia wanaichi huko TZ wanalalamika kila kukicha.Jamaini viongozi jitahidini mrejeshe imani kwa wananchi.Kwani “heshima ya ya mtu ni utu na sio pesa na cheo”,nimenukuuu.

 18. pia nami napenda kusema heshima ya mtu ni utu na sio pesa wala cheo chake, pesa cheo ni mungu anavileta kwahiyo kwanza heshima

 19. Prof Buhendwa Eluga Essy Says:

  Nazikumbuka safari zangu kuelekea Butiama kuenda kumuona JKN nikitokea Ufaransa kwa shughuli za PhD yangu katika Elimu ya Siasa. Mara ya mwisho nilimuona ni Kinshasa alipofika na kuniuliza kama naendelea kufanya utafiti juu ya Ujamaa kwani kwa watanzania wengi kuongea kuhusu Ujamaa ilikuwa wakati huo kama kuongea kuhusu “dainosor” (dynosaur)…Kweli ni mtu wa aina pekee na ni wa kujivunia sio Afrika tu bali ulimwenguni. Ujamaa ni imani…

 20. Severin Says:

  Tunakukumbuka na tutakukumbuka kwa mengi Mwalimu. Mungu akupe pumziko la milele na mwanga mwema akuangazie. Tunaamini kiroho bado uko nasi; tuombee watanzania, liombee bara la Afrika.

 21. ERIC Says:

  kweli kabisa kwa sasa hakuna kiongozi mwenye busara kama baba wa taifa si rais wala wabunge nijibuni mlishawahi kusikia nyerere kapigwa mawe au karushiwa jiwe kwenye msafara wake?vipi miaka hii,inadhihirisha kuwa viongozi ni wanafiki wabinafsi wanoko na wasengenyi ndo maana mabalaa kila kukicha sababu ya tamaa ya mali kisa wapepata madaraka.Mi sioni kabisa kama nhi hii inaendelea labda kwa lami na shule zisizo na walimu kuwadanganya kwa kuwalipa mishahara feki,siasa za umbea kama taarabu loh!MUngu aanawaona enyi msiona haya ya kuongoza mnafikiri uongozi ni kukaa kwenye AC naviti vya kuzunguka?au kuvaa suti nakupanda shangingi kama ni hivyo la Nyerere mbona hatukulijua kama la waziri mkuu au Rais kwa nini?Ndo mjue hakuwa na umimi kama nyie Maharamia wa serikali.Na nitasema mpaka siku ya mwisho.
  mpendwaeric@yahoo.com

 22. PUZZO Says:

  R.I.P Mwalimu!!! No One Like U! Katika TZ Ya Leo iliyojaa Maaaffiissaddi!!!!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s