BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“WANA NJENJE” October, 17, 2007

Filed under: Muziki,Sanaa/Maonyesho,Tanzania/Zanzibar,Utamaduni — bongocelebrity @ 3:20 PM

 

Pichani ni mojawapo ya bendi kongwe kabisa nchini Tanzania,The Kilimanjaro Band “Wana Njenje”. Bendi hii ilianzishwa mwaka 1973 mkoani Tanga enzi hizo ikiitwa The Revolutions kabla ya kuhamia jijini Dar-es-salaam mwaka 1979.Jina The Kilimanjaro Band walianza kulitumia mwaka 1989 walipokuwa ziarani nchini Uingereza. Raha kamili ya “mduara” utaipata kwao.

Kwa muda mrefu walikuwa na makazi ya kudumu pale Ambassador Plaza(zamani Gogo Hoteli) mpaka miezi michache iliyopita walipohamia Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay ambapo kila ijumaa wanatoa burudani pale.Mafanikio ya bendi hii yamechangiwa na kujiendesha kama kampuni(The Kilimanjaro Band Company) huku kila mwanamuziki akiwa na hisa na pia kupokea mshahara mwisho wa mwezi kama kampuni za kawaida. Ni mojawapo kati ya bendi chache sana nchini Tanzania ambazo zimedumu kwa muda mrefu namna hiyo bila kusambaratika au kupotea kabisa.

Advertisements