BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PAPA KUZURU TANZANIA October, 19, 2007

Filed under: Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 3:27 PM
Tags: , , , ,

 

Pichani ni kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu, Papa Benedict wa 16 na raisi Jakaya Mrisho Kikwete walipokutana kwenye makazi ya kiongozi huyo huko Vatican hivi karibuni . Kuna habari kwamba Papa Benedict amekubali mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete kuitembelea Tanzania katika ziara yake anayotarajia kuifanya hivi karibuni katika nchi za bara la Afrika. Pata undani wa habari hii kwa kubonyeza hapa.

Advertisements
 

R.I.P LUCKY DUBE

Filed under: Breaking News,Developing News,Muziki — bongocelebrity @ 8:30 AM

Mwanamziki wa mtindo wa reggae kutoka Afrika Kusini, Lucky Dube , ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi usiku wa kuamkia jana huko katika kitongoji cha Rosettenville, Johannesburg nchini Afrika Kusini.Polisi wa jijini Johanesburg wanasema majambazi hao walikusudia kuliiba gari la mwanamziki huyo.

 

Lucky Dube alikuwa amerekodi zaidi ya Album ishirini na kuzuru karibu pembe zote duniani akiimba nyimbo zenye ujumbe wa kijamii . Watanzania watamkumbuka kwa ziara kadhaa alizowahi kufanya nchini Tanzania na pia muziki wake uliokuwa na ujumbe wa amani na kimapinduzi.R.I.P Lucky. Soma habari hii zaidi hapa. (more…)

 

MWISHO MWAMPAMBA

Filed under: Tanzania/Zanzibar,Television — bongocelebrity @ 12:04 AM
Tags: ,

 

Pichani ni Mwisho Mwampamba aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa I lililofanyika miaka minne iliyopita. Mwisho alifikia hatua ya fainali kabla ya kuzidiwa kete kidogo na kimwana Mzambia Cherise Makabale ambaye ndiye aliibuka mshindi.

Mwisho alizaliwa Mkoani Mbeya, mwaka 1980 kisha akakulia na kupata elimu yake mkoani Morogoro. Alipata elimu yake ya msingi huko Morogoro International School na hatimaye kuhitimu kidato cha sita katika shule ya Sekondari Forest, huko huko Morogoro.BongoCelebrity iko mbioni kufanya mahojiano rasmi na Mwisho a.k.a Mr.Morogoro.Stay tuned!

 

MAYAULA MAYONI

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:01 AM
Tags: , ,

Kama masihara vile,ni Ijumaa tena. Wakati wa kushusha pumzi, kulainisha koo, kupata muda adimu wa familia bila kusahau kufanya tafakuri jinsi wiki ilivyokwenda. Wimbo wa leo ni Mbongou kutoka kwa Mayaula Mayoni, mwanamuziki kutoka DRC ambaye aliishi Tanzania kwa muda mrefu tu. Hivi sasa amerudi DRC na habari za uhakika zinapasha kwamba yuko hoi kitandani akisumbuliwa na maradhi ya kupooza. Wale ambao wanakumbuka disco la pale Tazara Club enzi zile wataukumbuka zaidi wimbo huu.Pata burudani.