BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SANAA BAGAMOYO October, 22, 2007

Filed under: Burudani,Sanaa/Maonyesho,Tamasha,Utamaduni — bongocelebrity @ 3:20 PM

 

Tamasha la Sanaa na Utamaduni linalofanyika chini ya uaandaaji na usimamizi wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo kila mwaka ni mojawapo ya matukio muhimu sana kwa wapenzi wa sanaa na utamaduni. Mwaka huu ni mwaka wa 26 tangu kuanzishwa kwa Tamasha hilo. Mwaka huu limepewa kauli mbiu “Sanaa Katika Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini” na limeanza leo 22 Octoba 2007 na litaendelea mpaka tarehe 27 Octoba 2007 litakapofungwa rasmi. (more…)

Advertisements
 

“SERIKALI ITUUNGE MKONO”-STEVE KANUMBA

Filed under: Filamu/Movie,Sanaa/Maonyesho,Television,Utamaduni — bongocelebrity @ 12:06 AM

Filamu za kitanzania zina historia ndefu tofauti na wengi wanavyofikiria. Kama mtakumbuka (kwa waliokuwepo enzi hizo) kuliwahi kuwepo na filamu kama vile Fimbo ya Mnyonge (1974), Harusi ya Mariam(1983) na Yomba Yomba(1983) na nyinginezo ambazo ziliwahi kutamba sana enzi hizo. Baadaye idara ya filamu ikapotea kabla ya kupigwa kikumbo na sanaa ya maigizo(wataalamu wanasema kuna tofauti kubwa kati ya maigizo na filamu). Lakini hivi karibuni enzi za filamu za kitanzania zimerudi,tena kwa kasi. Kama kulivyo na Hollywood(Los Angeles,USA),Nollywood(Lagos,Nigeria) na Bollywood(Mumbai,India), hivi leo inasemekana kuna Bongowood(Dar-es-salaam,Tanzania).

 

Mmoja kati ya waigizaji wengi wa filamu nchini Tanzania ambao wanasaidia kuzirudisha enzi hizo ni kijana Steven Charles Kanumba. Kwa wafuatiliaji wa filamu za kitanzania, hili jina na sura(pichani) sio geni hata kidogo.Lakini Kanumba ametokea wapi na anaelekea wapi?

Yeye mwenyewe anapasha kwamba alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 8 January mwaka 1984.Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Bugoyi huko huko Shinyanga. Baadaye alijiunga na shule ya sekondari Mwadui ambapo alisoma kwa miaka miwili tu kabla ya kuhamia katika shule ya Dar-es-salaam Christian Seminary alipomaliza elimu yake ya awali ya sekondari. Baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari Jitegemee kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

Ingawa alianza kuigiza tangu utotoni, safari yake katika fani hii aliianza rasmi mwaka 2002 alipojiunga na kundi maarufu la sanaa za maigizo la Kaole. Hivi karibuni tulifanya naye mahojiano ambapo tulizungumza naye mengi kuhusu kazi yake ya uigizaji na maisha yake kwa ujumla. Tulipomuuliza kuhusu habari iliyokuwa imetawala kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania miezi michache iliyopita kuhusiana na uhusiano wake na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu na pia “beef” kati yake na msanii mwenzake aitwaye Frank inayosemekana kusababishwa na wao wawili kumgombea mrembo huyo,hakusita kutupatia majibu yake. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)