BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MH.SALOME MBATIA HATUNAYE TENA! October, 24, 2007

Filed under: Breaking News,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:39 PM

Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi punde zinapasha kwamba aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mheshimiwa Salome Joseph Mbatia (pichani), amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Kibena karibu na Songea. Habari zinazidi kupasha kwamba dereva wake naye amefariki kufuatia ajali hiyo. Mheshimiwa Salome Mbatia alikuwa ni mbunge kupitia viti maalumu. Amefariki akiwa na umri wa miaka 55.

 

 

 

Marehemu Salome Mbatia (kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu UN, Dr.Asha Rose Migiro enzi hizo wote wakiwa wabunge kabla Migiro hajateuliwa kushika wadhifa alionao hivi sasa.Hii ilikuwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Habari zaidi zitazidi kuwajieni kadiri tutakavyoendelea kuzipata.

Advertisements
 

BALOZI GERTRUDE MONGELLA

Filed under: Bunge,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:06 AM

 

Huwezi kuongelea haki za wanawake duniani bila kumtaja Balozi Gertrude Ibengwe Mongela (pichani) Leo hii miongoni mwa wengi anajulikana kama “Mama Beijing”. Hii ni kutokana na yeye kusimamia mkutano maarufu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na wanawake uliofanyikia katika jiji la Beijing nchini China mwezi Septemba mwaka 1995. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo, raia wa Misri, Boutros Boutros Ghali ndiye aliyemkabidhi Balozi Mongela dhamana hiyo.

Leo hii ndiye mwanamke wa pili barani Afrika mwenye madaraka ya juu kabisa ya kuchaguliwa. Wa kwanza ni Raisi wa Liberia, mwanamama Ellen Johnson Sirleaf. Mama Mongela ni raisi wa Bunge la Afrika nafasi ambayo anaishikilia tangu mwezi March mwaka 2004 alipochaguliwa. Bunge la Afrika liliundwa mwaka huo huo wa 2004 na hivyo kumfanya Balozi Mongella kuwa raisi wake wa kwanza. Lakini madaraka na uwajibikaji kwa Gertrude Mongela sio jambo geni hata kidogo. Kama ambavyo utaweza kuona hapo chini kwenye CV yake, Mama Mongella sio tu mpigania haki za wanawake bali pia ni mfano ulio hai kwamba cha msingi sio jinsia bali uwezo binafasi wa mtu. Bila ubishi, Balozi Mongella ni mmojawapo kati “mabalozi” nyeti kabisa tulionao nchini Tanzania. (more…)