BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BALOZI GERTRUDE MONGELLA October, 24, 2007

Filed under: Bunge,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:06 AM

 

Huwezi kuongelea haki za wanawake duniani bila kumtaja Balozi Gertrude Ibengwe Mongela (pichani) Leo hii miongoni mwa wengi anajulikana kama “Mama Beijing”. Hii ni kutokana na yeye kusimamia mkutano maarufu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na wanawake uliofanyikia katika jiji la Beijing nchini China mwezi Septemba mwaka 1995. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo, raia wa Misri, Boutros Boutros Ghali ndiye aliyemkabidhi Balozi Mongela dhamana hiyo.

Leo hii ndiye mwanamke wa pili barani Afrika mwenye madaraka ya juu kabisa ya kuchaguliwa. Wa kwanza ni Raisi wa Liberia, mwanamama Ellen Johnson Sirleaf. Mama Mongela ni raisi wa Bunge la Afrika nafasi ambayo anaishikilia tangu mwezi March mwaka 2004 alipochaguliwa. Bunge la Afrika liliundwa mwaka huo huo wa 2004 na hivyo kumfanya Balozi Mongella kuwa raisi wake wa kwanza. Lakini madaraka na uwajibikaji kwa Gertrude Mongela sio jambo geni hata kidogo. Kama ambavyo utaweza kuona hapo chini kwenye CV yake, Mama Mongella sio tu mpigania haki za wanawake bali pia ni mfano ulio hai kwamba cha msingi sio jinsia bali uwezo binafasi wa mtu. Bila ubishi, Balozi Mongella ni mmojawapo kati “mabalozi” nyeti kabisa tulionao nchini Tanzania.

Balozi Mongella enzi hizo.

Mama Gertrude Mongella alizaliwa katika kisiwa cha Ukerewe (kilichopo ndani ya Ziwa Victoria) mkoani Mwanza mwaka 1945 akiwa ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wanne (watatu ni wanawake na kaka mmoja ambaye ndio wa kwanza kuzaliwa) katika familia yao. Baba yake Patrice Magologozi alikuwa ni mjenzi, fundi seremala na mwanaharakati akikabiliana na siasa za mkoloni. Mama yake Bibi Nambona alikuwa ni mkulima stadi.

Gertrude alikuwa na umri wa miaka 12 tu alipolazimika kukiacha kisiwa cha Ukerewe kuelekea shuleni Maryknoll Nuns(Musoma), shule ambayo ilikuwa chini ya masista wa kanisa katoliki ambao nia yao ilikuwa ni kuelimisha wanawake ili waweze kushiriki ipasavyo katika maendeleo ya nchi ya Tanzania ambayo wakati huo ndio kwanza ilikuwa imejipatia uhuru kutoka kwa waingereza.

Baada ya hapo alijiunga na chuo kikuu cha Dar-es-salaam ambako mwaka 1970 alihitimu na kupata shahada ya kwanza akisomea Elimu(Bachelor of Arts in Education).Baada ya kuhitimu alianza kazi ya kufundisha katika Chuo cha Ualimu Dar-es-salaam ambapo alifundisha kwa takribani miaka minne.Baada ya hapo Balozi Gertrude Mongela alijiingiza kwenye siasa na baadaye mnamo mwaka 1975 kufanikiwa kuingia kwenye lililokuwa Bunge la Afrika Mashariki. Huo ndio ukawa mwanzo wa maisha yake katika siasa ingawa mwenyewe anasema hamu ya kuwa mwanasiasa alikuwa nayo tangu utotoni kutokana na kuvutiwa na alichokuwa akikifanya baba yake.

 

Balozi Mongela akiwa na Boutros B.Ghali makao makuu ya UN, New York mwaka 1995 baada ya mkutano wa kimataifa wa wanawake wa Beijing,China.

 

Huu hapa ni msururu wa vyeo na nafasi mbalimbali ambazo Balozi Gertrude Mongella amewahi kuvitumikia na vingine bado anavitumikia. Kutoka juu ni cheo alichonacho hivi sasa na chini kabisa ni kuanzia alipomaliza shahada yake ya chuo kikuu.

 

2004 -President of Pan-African Parliament
2003 -Goodwill Ambassador – WHO Africa Region
2002 -Leader of OAU Election Observer Team to Zimbabwe Presidential Election
2002 -Member of the Regional reproductive Health Task Force- WHO AfricaRegion
2002 -Member The High Level Advisory Panel (HAP) of Eminent Persons-OAU
2000 -Member of Parliament – Ukerewe Constituency Tanzania
1999 -Member of the Council of “The Future” – UNESCO, Paris
1998 -Member of OAU – Women Committee for Peace and development, Addis Ababa
1997 -Senior Advisor to the Executive Secretary of Economic Commission for Africa (ECA) on Gender Issues.
1996 -President of Advocacy for Women in Africa (AWA)Patroness to the following NGO’s:- TAWALE (Tanzania Association of Women Leaders in Agricultureand environment);- SWAAT (Society for Women and Aids in Africa Tanzania Branch);- TDA (Tanzania Dental Association);- MAWAU (Meaendeleo ya Wanawake Ukeuewe)
1996 -Member of the Board- UN University- Tokyo
1996 -Member of the Board- The Hunger Project- N.Y, USA
1996 -Member of the Board- Agency for Co-operation and Research inDevelopment (ACORD), London
1996 -Member of the Advisory Group to Director general UNESCO; for the follow up of the Beijing Conference in Africa, South of the Sahara
1996 - 1997 UN Under-Secretary and Special Envoy to the Secretary general of theUnited Nations on Women’s Issues and Development
1993 – 1995 UN Assistant Secretary General and Secretary General, fourth WorldConference on Women 1995- Beijing, China
1991 – 1993 Tanzania High Commissioner to India
1990 – 1993 Member of the Trustee- United Nation International Research and Training Institutes for the Advancement of Women (INSTRAW), Santa Domingo
1989 - 1990 Minister Without Portfolio - Government of Tanzania
1989 -Tanzania Representative- Commission on the Status of Women
1985 -Vice-Chairperson- World Conference to review and Appraise the Achievements of the UN decade for Women.
1987 – 1990 Minister without Portfolio- President’s Office
1985 – 1987 Minister of Lands, Tourism and Natural Resources
1982 - 1991 Head - Social Services Department, Government of Tanzania
1982 – 1988 Minister of State- Prime Minister’s Office
1980 – 1993 Member of Parliament- Tanzania
1977 – 1992 Member of central Committee and National Executive Committee of CCM party
1975 – 1982 Member of the Council- University of Dar es Salaam
1975 – 1980 Member of the Board of Directors- Tanzania Rural Development Bank
1978 – 1982 School Inspector
1975 – 1977 Member of the East African Legislative Assembly
1974 – 1978 Curriculum Developer- Institutes of Education, Dar es Salaam
1970 – 1974 Tutor- Dar es Salaam Teachers Training College
1970 -Graduated as teacher from East Africa University College, Dar es Salaam, Tanzania.

 

Balozi Mongella akiwa na Mama Jitto Ram mmoja wa wanawake wanaharakati wa siku nyingi Tanzania.

 

Wakati wa mkutano wa African Women’s Forum uliofanyika nchini Ghana,January mwaka 1997,Mama Mongella akielezea mtizamo wake kwa mtu anayetaka kuwa kiongozi alisema “Kama unataka kuwa kiongozi lazima kwanza uwe na picha kamili ya unachokitaka na unachokisimamia.Lazima usimamie kanuni na maadili. Kanuni na maadili haziwezi kukuangusha kamwe.”.Huyo ndio Balozi Mongella. Unaweza kumsikiliza Balozi Mongella katika mahojiano aliyofanya na jamaa wa The Connection mwaka 2004 kwa kubonyeza hapa.

 

 

Picha kwa msaada wa Muhidin Issa Michuzi na Haki.

Advertisements
 

8 Responses to “BALOZI GERTRUDE MONGELLA”

 1. Mwajuma Says:

  Huyu ndio role model wangu.Asanteni BC na kila la kheri Mama Mongella katika kazi zako.

 2. Dinah Says:

  Mama Mongella mfano mzuri kwa wanawake wengi Tz, inafurahisha kuona mwana mama kushika nafasi za juu ambazo awali ilidhaniwa kuwa ni za wanaume tu.

  Mimi nakutakia kila lililo jema ktk ushughuli zako na Mungu akubariki kwa yote mema uliyoyafanya.

  BC :-)…as u can c huyu mama umaarufu wake kaupata kwa kufanya mambo mengi (ya maana) ktk jamii ya kibongo tena 4 years.

  Kazeni kamba, hii imetulia.

 3. GEORGE Says:

  Hongera sana mama kwani umetutoa kimasomaso Watanzania.Tukiwa nchi za Ughaibuni nasi tunatembea kifua mbele.

 4. Kimori Says:

  A commendable woman!…I would prefer to hear also the other side of her profile, vis-a-vis marital stutus, the kids, etc…BC please do the needful!

 5. happiness Says:

  Hongera sana mama

 6. Reg Miserere Says:

  Dinnah;

  Ni kweli wamama big up!!..

  Na wewe tukuone!!!…

 7. Kathy Schmidt Says:

  Will Gertrude Mongela support great evils?

  What I say here is found in books that anyone can find on the Internet (www.amazon.com or http://www.bn.com) or rare bookstores. Do you realize that many women are supporting a group whose founder spoke highly of the Nazis’ practices and teachings in the 1930s and 1940s, and who wrote books with racists wordings and ugly eugenics practices, such as getting rid of those kids who were deformed or had genetic problems?

  What group and founder are I talking about? Let me give you some idea what this founder wrote in her books (yes, she is a woman). This female founder refers to people who are epileptics, feeble-minded, blind, deaf, mute, etc. as:

  –> “…this dead weight of human waste…” that is “…the terrific cost to the community…”

  This female says, “‘Constructive’ Eugenics…shows us that we are paying for and even submitting to the dictates of an ever increasing, unceasingly spawning class of human beings who never should have been born at all…”

  Lovely, isn’t it?

  And then she refers to these problem people this way:

  –> “Every single case of inherited defect, every malformed child, every congenitally tainted human being brought into this world is of infinite importance to that poor individual; but it is of scarcely less importance to the rest of us and to all of our children who must pay in one way or another for these biological and racial mistakes.”

  She also said that large families should kill some of their children so as to save “resources” for others.

  How about this idea which is similar to the Nazis’ propaganda during the 1930s?

  –> “On its scientific side, Eugenics suggest the reestablishment of the balance between the fertility of the “fit” and the “unfit.” ”

  In one of her publications, a magazine review, persons sympathetic to the Nazis’ practices and even German Nazis themselves wrote articles for her. In other documents, she refers to the supremacy of the white race over the other races. Isn’t great that she wrote side-by-side with those Nazis?

  What are these books and materials to which I refer?

  “The Pivot of Civilization”

  “Woman and the New Race”

  “The Birth Control Review”

  Who is the author of this trash?
  Who is this supporter of the Nazi eugenic practices?

  MARGARET SANGER
  Founder of PLANNED PARENTHOOD

  Do people think that Jewish women are blind to Margaret Sanger’s promotion of racial eugenics? Let me quote something from her that both she and Planned Parenthood standby:

  –> “By education, by persuasion, by appeals to racial ethics and religious motives, the ardent Eugenicist hopes to increase the fertility of the “fit.” ”

  Planned Parenthood refers to her as a Woman of Valor. Do you like that term? Not all of us Jewish women are now blind to what Planned Parenthood is doing to women all over the world. Are you?

  AND note also that the Gay / Lesbian Groups ALL support Planned Parenthood WITHOUT any reservations also!

  a Jewish woman who was deceived and attacked by Planned Parenthood and who also lost relatives in the Holocaust, thanks to Margaret Sanger

 8. annest Says:

  Hongera sana mama Getrude lakini tunataka kukuona ukikuza vipaji vya wanawake wa kitanzania zaidi waalimu ambao wamekua wakitoa watu muhimu sana katika jamii lakini wao hawawi muhimu pia mimi nataka nifike ulipo na niweze kwenda mbali kuliko wewe kwa hiyo usilale mama. Women can make changes belive it or not but that is the truth


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s