BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

THREE LITTLE BIRDS October, 26, 2007

Filed under: Bunge,Maisha,Muziki,Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 12:09 AM

Ni wazi kwamba wiki moja iliyopita na hii tunayoelekea kuimaliza zimekuwa na ugumu wa aina yake. Kwanza zilikuwa ni habari za kuuawa kikatili mwanamuziki wa miondoko ya reggae kutoka Afrika Kusini,Lucky Dube na kisha habari za ajali mbaya ya gari iliyosababisha kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Salome Joseph Mbatia, dereva wake (jina bado hatujalipata) na utingo wa fuso iliyogongana naye aliyekuwa anaitwa Castory Kilagwa (22).

Kwa ujumla habari za namna hii huleta simanzi na majonzi makubwa. Katika wakati huu mgumu kwa ndugu,jamaa na marafiki wote waliofikwa na misiba huku pia tukikumbuka kwamba wapo watu wengi wengine ambao nao pia wamepoteza ndugu,jamaa na marafiki (ingawa kutokana na nafasi zao katika jamii habari zao hatuzisikii kama hizi za wengine), BC inapenda kuwapa pole wafiwa wote na pia wote mnaokabiliwa na matatizo mengine yoyote ya kimaisha.

Sasa kwa sababu leo ni ijumaa na kama kawaida yetu huwa tunapata mdundo, wimbo wa leo unaitwa Three Little Birds kutoka kwa Mfalme wa Reggae duniani,Hayati Bob Marley.Wimbo huu ndio ulikuwa wimbo rasmi wakati wa mazishi ya yake. Bonyeza umsikie Bob akikukumbusha kwamba Usihofu sana, kila kitu kitakuwa sawa.Maneno ya wimbo unaweza kuyapata hapa. Ijumaa Njema.

Advertisements
 

3 Responses to “THREE LITTLE BIRDS”

 1. Wesley Malilo Says:

  Perfect song for the occassion.R.I.P Mama Mbatia and all others.Bob was a genius king.

 2. EDWIN NDAKI Says:

  Hakika siku moja kila kitu kitakuwa juu ya mstari…

  Nuff peace an love…

  Rest in Peace Mama Mbatia..

  Pole Junior Mbatia,familia nzima na watanzania kwa ujumla.

  Kuwa strong mdogo wangu ndio kazi yangu.Tulimpenda mama,Mungu kampenda zaidi.Tupo pamoja mdogo wangu

  Bwana alitoa,bwana ametwaa,jina la bwana linabrikiwe…
  AMINA

 3. DUNDA GALDEN Says:

  POLENI SANA FAMILIA JOHN MASSAWE WA PALE MOSHI KWA KUONDOKEWA NA MZEE WENU NYINYI MLIMPENDA LAKINI MUNGU ALIMPENDA ZAID MUWE NA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIZITO NA MUNGU AWAPE MOYO WA IMANI
  AMIN


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s