BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ALI HASSAN MWINYI October, 29, 2007

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:02 AM

Alipoingia madarakani kumpokea aliyekuwa Raisi wa Awamu ya kwanza,Mwalimu Julius Nyerere mnamo tarehe 5 Novemba mwaka 1985, watanzania wachache sana (kama wapo) waliweza kutabiri kwamba miaka kumi baadaye na zaidi baada ya kustaafu rasmi, ataibuka kuwa mmojawapo wa maraisi wa Tanzania ambao watabakia kupendwa na kuheshimika kwa namna ya kipekee kabisa. Tunadiriki kusema “namna ya kipekee” kwa sababu ukweli unabakia kwamba inapofanyika tathmini ya uongozi wake, bado mtu au watu mbalimbali wanakuwa na maoni yao tofauti tofauti kuhusiana na suala hilo. Utoaji huo wa tathmini ni suala ambalo haliwezi kukoma leo wala kesho, ni tukio linaloendea na litakaloendelea, vizazi mpaka vizazi. Huo ndio uzuri au ubaya wa historia na muda (history and time),huwa vina jinsi ya kipekee katika kutoa hukumu zao.

Mpaka anakabidhi madaraka yake ya uraisi kwa raisi wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa mnamo tarehe 23 November mwaka 1995, jina ambalo wengi tulipenda kulitumia ni “Mzee Rukhsa” ingawa kamwe hatukuwahi kusahau kwamba jina lake kamili ni Ali Hassan Mwinyi, Raisi wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Ali Hassan Mwinyi alizaliwa tarehe 8 mwezi wa tano (Mei) mwaka 1923 katika kijiji cha Kivure,wilayani Kisarawe ,mkoa wa Pwani,Tanzania Bara. Kama wengi wa viongozi wetu, Mwinyi naye alizaliwa katika iliyokuwa Tanganyika. Akiwa bado mwenye umri mdogo sana familia yake ilihamia Zanzibar. Kwa maana hiyo Mwinyi ni mzaliwa wa bara aliyekulia na kuendelea kuishi visiwani Zanzibar.

Alianza safari yake kielimu huko visiwani Zanzibar katika shule ya msingi Mangapwani kuanzia mwaka 1933 hadi 1936 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Dole kwa ajili ya elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1937 mpaka mwaka 1942. Baada ya hapo alijiunga na Chuo Cha Ualimu Zanzibar kusomea ualimu kuanzia mwaka 1943 mpaka 1944.

Mwinyi katika picha rasmi ya wakati wa utawala wake.

Kuanzia mwaka 1945 mpaka mwaka 1950 alirejea tena katika shule ya Mangapwani,shule aliyosomea,safari hii akiwa sio mwanafunzi tena bali Mwalimu.Kuanzia mwaka 1950 mpaka 1954 alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo wakati huo huo alikuwa akiongeza elimu yake kwa njia ya posta ambapo alijipatia General Certificate in Education (GCE) na pia alikuwa amejiunga na Durban University Institute of Education, United Kingdom (kwa njia ya posta tena) kusomea stashahada ya ualimu. Baada ya hapo alijiunga tena na Chuo Cha Ualimu Zanzibar kama mkufunzi kuanzia mwaka 1956 mpaka mwaka 1961 huku pia akiendelea kujisomea kwa njia ya posta kutoka Regent Institute kilichopo London nchini Uingereza ambapo alijipatia cheti cha ufundishaji lugha ya kiingereza.

Kuanzia mwaka 1961 mpaka 1962 alijiunga na Hall University, Uingereza katika Tutors’ Attachment Course. Mzee Mwinyi pia ana cheti ya lugha ya kiarabu alichokipatia Cairo nchini Misri kati ya mwaka 1972 na 1974.

Safari yake ya kisiasa aliianza rasmi mwaka 1964 alipojiunga na Afro Shiraz Party (ASP) huko Zanzibar ambapo alikitumikia chama katika ngazi na nafasi mbalimbali. Kati ya mwaka 1964 na 1965 alikuwa ni Katibu Mkuu wa muda katika wizara ya elimu Zanzibar kabla hajateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi katika iliyokuwa Zanzibar State Trading Corporation (ZSTC).Hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1965 na mwaka 1970. Pia katika miaka hiyo hiyo,kuanzia mwaka 1966 mpaka 1970, Mwinyi alikuwa mweka hazina msaidizi katika tawi la ASP la Makadara,Zanzibar. Wakati huo huo pia kati ya mwaka 1964 mpaka 1977 alikuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)

Majukumu mengine aliyokuwa nayo miaka hiyo ni pamoja na uenyekiti wa Zanzibar Censorship Board (1964-1965), Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na pia mwenyekiti wa Baraza la Chakula na Lishe.

Mwinyi (kushoto) akiwa na maraisi wenzake, mstaafu Benjamini Mkapa( kulia) na Raisi wetu wa sasa Jakaya Mrisho Kikwete (katikati)

Kuanzia mwaka 1972 mpaka 1975, Mwinyi alikuwa ni Waziri wa Afya wa Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia 1975 mpaka 1977. Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri cheo alichokitumikia mpaka mwaka 1982 aliporejea nyumbani na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii cheo ambacho alikutumia kwa muda mfupi tu kwani mwaka 1983 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Raisi.

Mwaka 1984, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Raisi wa Zanzibar wakati huo,Alhaj Aboud Jumbe, Mwinyi alichaguliwa kuwa Raisi wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na wakati huo huo Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuanzia mwezi August mwaka huo huo wa 1984 Mwinyi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi cheo alichoendelea nacho mpaka mwaka 1990 baada ya kung’atuka kwa Hayati Mwalimu Nyerere kutoka katika kukiongoza Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Mwinyi (wa pili kutoka kushoto) akishuhudia mchezo wa bao kati ya hayati Mwalimu Nyerere (wa pili kutoka kulia) na mzee mmoja wa Butiama(jina halijulikani).Wengine wanaoshuhudia ni Mama Maria Nyerere(kulia) na kaka yake Nyerere,Chief Burito(wa tatu kutoka kulia).Picha ilipigwa Butiama.

Lakini kabla ya hapo, mwaka 1985,Mwinyi alichaguliwa kuwa Raisi wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kustaafu kwa Mwalimu Nyerere. Mwinyi ni mtaalamu wa lugha ya Kiswahili na pia hupenda michezo hususani jogging. Mwinyi ameoa wake wawili (Sitti Mwinyi na Khadija Mwinyi), ana watoto na wajukuu. Anaishi Msasani jijini Dar-es-salaam.

Advertisements
 

15 Responses to “ALI HASSAN MWINYI”

 1. Kimori Says:

  In my opinion Mwinyi, as a person, is a man of high moral standards, polite, understanding, considerate, just to mention a few traits…..and that is why he is still energetic and looking younger than his real age!

  Despite tha fact that he came into power at the crucial political transition period and couldn’t cope with some changes, he still deserves respect!

  Long live ex-president!

 2. EDWIN NDAKI Says:

  ukitaka kuweka maoni yako..RUKSAAAAAAAAA…

  Kila la kheri A.H Mwinyi…maisha mema yenye ´baraka.

  Anayetaka kuwa maskini ruksaaa..anayetaka kufanikiwa ruksaa….

  mwinye bwana..

 3. Amani M Says:

  Mwinyi is one of the great Tanzanian leader of our time. It is very easy to forget how bad the economic condition was during that time.

  But wisely he managed to move the country to economic stability. One special thing about him is confidence such that he made it look so easy. It wasn’t not easy from no petrol, no food, no foreign exchange, no items in the shops, no freedom of expression, no freedom of travel, et cetera.

  IN SHORT HE STRENGTHEN ECONOMY, GAVE US FREEDOM AND REMOVE FEAR

 4. TanzanianDream Says:

  Embu acheni kudanganya umma jamani…Hiyo Economy ambayo Mwinyi aliileta bongo ni ipi???We had kubadili noti kwa sababu ya inflation..and yet u call that economic strength????lazima nianze kuwa na mashaka na ubongo huo…Simply Mwinyi kutokana na ujinga wa WaTz alitumia mwanya huo kuwafanya wajinga zaidi….Trust me mtu akipata pesa ambayo haina thamani akaishangilia huyo ni zaidi ya Upumbavu…

  Kweli kama nilivyosema vilemba vya ukoka ndo wabongo tunavyopenda kuvishana….Almost kila kitu Mwinyi kashindwa kufanya hata kuinfluence hiyo vyama vingi ameshindwa yeye kama Rais kuitetea Babu akaja kuweka hoja leo unasema alikuwa kiongozi mzuri…Labda lazima kuwe na distinction kati ya kiongozi mzuri na mbaya ili tujue yeye ana lie sehemu gani ila kama Nyerere was in the Good side trust me Mwinyi hayupo hiyo side hata mkilazimisha awepo never will ever be…..

  Kweli Rais mstaafu anahitaji heshima yake ndo most tunachojaribu kufanya lakini heshima sio upumbavu kiasi tuanze kubadili ukweli kuwa kuyumbisha uchumi ni kufanikisha uchumi never in earth ….Otherwise nafurahia tu kuona atleast kuna watu spectacular hutakiwi ku argue nao tho simnyanyapai mtu….PERIOD

 5. maya65 Says:

  wewe hapo juu unapenda kutawaliwa na maraisi wezi, wasio na huruma kwa wananchi wao na ma dictator kama Mkapa!!!!
  sasa mwinyi ubaya gani alioufanya zaidi ya kuwa kipenzi cha watu?
  think twice bro…

 6. Dinah Says:

  Huyu ndio “nyerere” wetu akina sisi tuliokuwa miaka ya 85-95.

  Mzee ruksa alichukua nchi (chaguliwa kuwa Rais) wakati nchi ikiwa ktk Ujamaa, kama ilivyo kwa binaadamu (Mwinyi mmoja wao) unatumia akili na uwezo aliokupa Mungu kurekebisha mambo ili kuishi bila taabu,kufurahi na kuwa na amani.

  Mwinyi huenda alitereza na kufanya makosa kama ilivyo kwa viongozi wote (hata Nyerere alikosea mengi tu, Mkapa pia alitereza), lakini tukihesabu mazuri aliyoyafanya Mwingi hakika yanashinda “makosa”.

  Mwinyi aliruhusu wafanya kazi wa serikali kumiliki Biashara(au kazi nyingine nje ya ofisi), Mwinyi aliruhusu uingizaji wa bidhaa za nje na hatimae tukaanza kupendeza kwa kuvaa viatu vya kufuta 🙂 , mtindo wa Mzee ruksa kuruhusu mambo pia ilituwezesha watanzania kuanza kumiliki Tv, kila mtu akaanza kupendeza kwa kuvaa nguo zilizovaliwa (mitumba), watz waliazna kumiliki nyumba zaidi ya 2 bila kuulizwa umezijenga vipi n.k.

  Upatikanaji wa pesa ulikuwa rahisi sana (huitaji kufanya kazi ngumu kupata manoti), watu tulianza kuwa na magunia ya sukari, mchele, mahindi ndani ya nyumba zetu bila kuwa na hofu kukamatwa….

  Vilevile watanzania tukaweza kwenda kusoma nje tena tunachagua nchi tuzipendazo bila kusubiri Serikali itupeleke “Urusi”.

  Sote tunajifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na mtu aliye juu yetu……kama ambavyo wengi wanaamini kuwa Nyerere was kind “Perfect” hivyo hakukuwana cance ya kujifunza kwa A H Mwinyi nahivyo akaongoza kivyake.

  Sasa watu waliomfuata ndio wanatakiwa kuepuka yaliyofanyika, Mkapa alijitahidi na kama kawaida aliingia Ikulu nchi ikiwa ktk wakati mgumu(pesa haikuwa na thamani)…akajitahidi……Kikwete angalau kaingia Ikulu hali sio mbaya sana ukilingasha alivyoingia Mwinyi.

  Mwinyi alichangia (in his own way) kwa kiasi kikubwa ktk maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania…..alijitahidi.

  Mzee ruksa kila la kheri ktk shughuli zako na maisha yako kwa ujumla.

 7. biwi Says:

  Watanzania wengi watamkumbuka Rais Mwinyi kwa unyenyekevu wake na utaalamu wake katika lugha, wengi tunamkumbuka kwa matamshi yake haswa pale tunapokuwa katika misukosuko na majanga ya kitaifa sauti yake ilizistarehesha roho na moyo ya waathirika na wale wenye hasira pia ikumbukwe ni katika utawala wake tumeweza kuwa wafanyabiashara wa kuingiza bidhaa nchini na haka kademokrasia ka kusema fyoko pia imekuja kipindi chake na matunda yake tunayaona leo kwa kuwa na midahalo na majadiliano ya kusema chochote sio ndani tuu ya vyombo vya habari na pia hadharani .

 8. Dinah Says:

  Nakubaliana na wewee biwi;
  Huyu mzee (Raisi wa 2 wa TZ) alikuwa karibu sana na wananchi…unakumbuka alikuwa na kipindi kwenye Radio kuhusu kiswahili fasaha. Alikuwa akisaidia sana kwa watu wajinga-wajinga(wasiotilia maanani lugha yao) kujua matumizi ya meno ya kiswahili kama inavyopaswa.

  Nakumbuka wakati nilipokuwa mdogo (wakati wa nyerere) ilikuwa mwiko kumzungumzia kiongozi, lakini huyu bwana akaja na ruksa yakusema utakalo ailimradi tu huvunji sheria au kumtusi mtu.

  Mwinyi alikuwa na utaratibu wa kukutana na wanachi mara moja kwa mwezi na vilevile alikuwana utaratibu wa kuhutubia taifa mara moja kwa mwezi.

  Huyu mzee ni muhimu sana ktk historia ya maendeleo ya Tanzania hasa upande wa kusema tutakacho pale tunapojisikia kufanya hivyo bila kuhofia kukamatwa, uhuru ktk biashara za nje na ndani, sekta binafsi,vyama/jumuia zisivyo za kiserikali n.k.

 9. colin Says:

  Hii guys
  hatuwezi kusema kwamba mwinyi ni alikuwa perfect au sio.Kitu muhimu hapa ni kuangalia mazuri na mabaya aloyafanya,kisha tufanye uwiano.Binafsi nampa pongezi mzee mwinyi kwa kipindi chote alichotumikia.alikuwa na weakness zake lakini ukweli unabaki palepale,wakati anaanza kuiongoza nchi 80s ,Tulikuwa na serikali ya kikomusnisti (japokuwa nyerere alikataa kuwa rasmi).Mwinyi alikuwa na kazi ya ziada kutupeleka kwenye semi utandawazi.kuruhusu watu binafsi wafanye biashara(ndo mana hela zikaja mikononi kwa watu).Maisha yakawa rahisi na demokrasia ikaanza kukua,Tukawa na TV na mahitaji muhimu ya binadamu.
  Mzee mwinyi alikuwa kiongozi mwadilifu alotetea maslahi ya taifa ndo mana mzee kifimbo alimwamini.Huwezi ukamlinganisha “ruksa” na huyu Bitoz wa sasa anayeenda na dola laki saba marekani(kwenye brifcase) kwenda kuomba misaada huku akizungukwa na wasaidizi zaidi ya 33.
  Mwinyi aliiheshimu ikulu kama alivyoheshimiwa na mzee kifimbo na kuifanya kama mahali patakatifu .

 10. maya65 Says:

  mhh mr collin hivi ni kweli alikwenda na dola laki saba marekani kwenye brief cace kuomba msaada!!!!!
  haahaahaaaaa kama ni kweli basi wamarekani wakijua hatutapata kitu tena toka US!!!!

 11. gina Says:

  mzee ruksa, tunaomba muendelee kudumisha amani na upendo, bila ubaguzi.

 12. kare Says:

  ruksa, mkumbuke mlikotoka, nchi ni ya watanzania wote.

 13. kijiwe Says:

  e bwana wadau kama kweli huyu bitoz alikwenda na dola laki saba katika briefcase basi nchi imelaaniwa kwa kumchagua

 14. Mama wa Kichagga Says:

  Kila binadamu ana udhaifu wake!

  Mimi binafsi namshukuru mzee Mwinyi kwani aliniwezesha kujua kuwa ati hata kikaragosi mie naweza nunua na kuangalia TV na Music wangu mwenyewe bila kwenda Ulaya!

  Mh. wee acha tu nakumbuka nilikuwa nishachacharika zangu kinoma na vidonda vya tumbo kisa kubana matumizi niweze kupata kitu fulani toka Ulaya. Si rafiki akanitosa akanirudishia hela yangu eti hakuweza kubeba mzigo! Nilisononeka sana. Msemo wa kitabu cha KULI “YANA MWISHO HAYA” GHAFLA MZEE MWINYI akaingia madarakani! Wacha Kariakoo ifurike potelea mbali hata kama vilikuwa havina TBS lakini roho ilipona! Baba Mungu akupe uzima kwani kila maisha ya MTZ uliyagusa kwa namna moja ama nyingine. Tatizo nililoliona ni hawa mafisadi waliutumia mwanya wa siasa yako vibaya. Ndio maana nasema FISADI AFUNGWE MIAKA 30+. Sera zote zikabadilika na mambo yakawa ndio hivyo tena asilimia kama 82% ulifaulu sana.

  Mimi nashukuru sana ktk kipindi cha uongozi wako minong’ono ya upendeleo wa kidini, ukabila, au urafiki haikuwepo ama kabisa.

  NIKIONA PICHA YAKO BABA NINASIKIA FARAJA SANA MOYONI MWANGU.

 15. Ralfa Says:

  Ukweli utabakia palepale kuwa hakuna kizuri kisicho na ubaya. But what we do care most, is how far he has run best compared to whom?
  In my opinion Mzee Mwinyi is a “great man” dispite his weaknesses. Economically he did well to his best due to the fact that it was a transition period from the so called socialism to may be capitalism. I think you can help me, that what is likely to hapen when a certain system is changing anywhere you have experienced.
  Uadilifu wa Mzee Mwinyi katika utawala wake uliomfanya aondoke pasipokuwa na kashfa mbaya, kama vile “kufanya biashara akiwa ikulu” ama kulea “ufisadi” na wizi wa rasilimali za wana nchi wa Tanzania wenye kipato cha chini kabisa unanifanya mie kumheshimu Mzee Ruksa kama kiongozi aliyejali utu, heshima, na mali ndogo walokuwa nayo masikini wa Tz.
  LONG LIVE MZEE RUKSAAA………


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s