BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SAIDA KESSY-MISS TANZANIA 1997 November, 3, 2007

Filed under: Fashion,Miss Tanzania,Urembo — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Ahadi ni deni.Kama tulivyoahidi wiki iliyopita,tunaendelea kuwakumbusha (kwa picha) baadhi ya warembo wa Tanzania waliowahi kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia miaka ya nyuma.

Pichani ni Saida Kessy, Miss Tanzania 1997.Kabla ya kutwaa taji la Miss Tanzania mwaka huo, Saida alikuwa ametwaa taji la Miss Arusha 1997 na hivyo kuingia katika shindano la Miss Tanzania kama mwakilishi kutoka mkoani Arusha.

Mashindano ya Miss World mwaka huo yalifanyikia huko Baie Lazare, Seychelles (Ushelisheli) tarehe 22 November,1997 na kushuhudia taji la Miss World likienda kwa Diana Hayden kutoka India.

Advertisements
 

26 Responses to “SAIDA KESSY-MISS TANZANIA 1997”

 1. Ally Says:

  dah kweli kitambo!miaka 10 imepita sasa!lkn hv kwa nn hawa dada zetu hz powder zimekua nyingi sana?we mweusi powder kibao duh haya tutafika lkn.

 2. Dinah Says:

  Mwanzo ulikuwa mgumu sana……kama akirudi tena na muonekano huo sidhani kama hata nafasi ya 10 bora atakuwepo.

  Ni mtazamo wangu tu msinitoe macho 🙂

 3. TanzanianDream Says:

  Sanamu ya McDonalds….

 4. Chiki Says:

  Duh! ilikuwaje akashinda mbona anatisha hivyo?? lahaula wallahi!!

 5. lizzie Says:

  du kweli maajabu ya ghomola kweli uwakilishi ulikuwa mgumu kidogo hapa

 6. Yassie Says:

  Sio siri ni hana mvuto, nahisi kuna ujanja ulifanyika haiwezekani kuwa kulikuwa hakuna mrembo wa kuwakilisha taifa mwenye mvuto kwa wakati huo??
  HAVUTII BWANA.

 7. nusrat Says:

  JAMANI MIPODA MINGI YA NINI? KWANI KUJIDODEKA MIPODA NDIO UZURI, HEBU ANGALIA HUYU DADA ANAVYOTISHA JAMANI, UTADHANI MWANACHAMA WA WANNE STARS? DADA PUNGUZA MIPODA, UMECHUSHA SANA, HAPA MWANANGU ANAOGOPA HATA KUANGALIA HII PICHA, JAMANI!!!!

 8. ZeMdau Says:

  Mbona KACHAKAA hivi siku hizi jamani!?!
  Namuonea huruma!

 9. Wilo Says:

  Huyu ni mchezaji wa pekechpekecha nini?

 10. Sekule Says:

  Dah! Kachakaa wapi hajawahi kuwa mzuri,Wala sio poda tu. Hata kama hajapaka poda havutii, kwanza kabisa ni kibiongo, pua kubwa, mdomo umepinda, mwendo wake sio mzuri, miguu kaa sidando pia matenge ya aibu. Naona alipata kuwa Miss Tanzania kwasababu alikuwa wale wa kwanza kwanza kuanza mashindano na wasichana wengi wazuri bado walikuwa wanaona aibu kushindania uzuri. Subutu yake aingie kipindi hiki. Si lolote si chochote.

 11. Debora Says:

  Amakweli kama mtu kama huyu anaweza kutambulisha nchi yetu kwa urembo basi tena, inamaana hatuna warembo Tanzania na hilo nakataa. Binti huyu alibahatika sana. Jamani basi hata ukibahatika basi jitahidi kujifundisha urembo lakini hata kupaka makeup hajui?

 12. stephen Says:

  Jamani mbona anatisha hivyo?? Hiyo poda na nywele ni vipi? Wasichana lipstick nyekundu ni old fashion na ukiipaka akikisha umevaa plain black, red or white. Huyu miss havutii. Je hiyo ni wigi amevaa au? Naona forehead yake imeachana sana hair-line. Kwa kweli kama ni wigi au nywele za kusukia chochote kile hiyo nywele haijawekwa vizuri au ni upepo umesogeza nywele nyuma?? (hahahahahhhhhhhhhhh mashalaaaaaa………..)
  Mimi msichana wangu akitoka saloon kama nywele imekaa jinsi hii nitamrudisha.

 13. Flojoma Says:

  HAHHAHAAHAHA DINAH!!! UMENIUWA MBAVU WASIKUTOE MACHO KINANANI SASA ??

 14. Janey Says:

  Jamani mbona mnamchamba sana mwenzenu. Kila mtu anakasoro yake ndo sababu ma-celebrity wenye hela nchi zilizoendelea wanafanya plastic surgery. Ndio nakubaliana na nyie kwamba sio mzuri hivyo, labda majudge waliomteua walikua wamelewa siku hiyo au wapigania uzuri wenzake siku hiyo walikuwa hata wabovu zaidi, basi ilikuwa bahati yake. Kikubwa aliwakilisha nchi yetu.

 15. kay Says:

  duuuuuuuuu.jamani hata mimi nimeogopa kuangalia mara mbili.hivi huyu mtu hana kioo au ilikuaje???maana kwa status yake hakutakiwa kuzidisha make-up’s hivyo. inaonesha hata urembo haujui alibahatisha tuu.

 16. eddie Says:

  jamani muwe waelewa huyo alikua enzi hizo na pengine alikua mzuri, sasa we sekule kukosoana ndo nini et pua kubwa, ana kibyongo miguu sijui nini,,,,alijiumba? hamjui hapo mnamkosoa mungu? we mwenyewe sekule unayesema hayo hauna kasoro? au kwasababu hatukuoni….. je ulishawahi hata tu kutengeneza kamdoli kakaelekea tu kua kama huyo dada? huko tena unaingilia kazi ya uumbaji wa mungu…kabla hujasema tafakari kwanza sio useme kwasababu unajua kusema au una mdomo,halahala….sekule be careful, whatch ur mouth

 17. Sekuke Says:

  Eddie naona comment yangu with regards to miss huyu imekuudhi sana. Sorry no offence intended. What do you mean eti pengine alikuwa mzuri kwani hiyo picha imechukuliwa 30yrs ago au? na inamaana old people are ugly?? Kama wewe ni mzuri ni mzuri regardless of age. They are so many beatiful old ladies out they you can just tell when they were younger they were’nt just beatiful or sexy they were HOT!Mimi sijasema sina kasoro au mwanamke wangu hana kasoro but the thing is mtu anayewakilisha nchi yetu kama mrembo anatakiwa awe more presentable in anyway, shape and form. This includes intelligency, fluency and everything combined together. Na nina uhakika tunaomabinti ambao they are far better than this lady. What makes you think ukiwa kibiyongo, kiuno kimepinda miguu yote ya kushoto you will look good, and sexy on a bikini?? Or you will walk well kwenye catwalk??Come on!! Get real. She is supposed to be a prentative of our nation when it comes to beaut. Na kama mtu hataki kuwa criticized asijiingizae kwenye limelight. I’m sorry this is just a simple formula and not a rocket science. You dont need to have a PhD to know this fact.

 18. mshua Says:

  E-Bwana Sekule nakubaliana na wewe uzuri hauchakai. Kama hali yake ndo hiyo basi alinusurika sana alipofika kupigania miss world kwani kule alikutana na mabinti bomba. Wakivaa bikini utafikiri wamezaliwa nayo. Stephen kaongelea kuhusu nywele kupulizwa na upepo hapo mchikaji umenivunja mbavu lakini sishangai umefikiria hivyo kwani baada ya kuangalia hiyo picha naona ana kipara.

 19. Tonni Says:

  Huy msichana sio mbaya hivyo jamani, ila hiyo make up yake kwa kweli aliitaji msaada. Ilikuwa 1997, tunaweza kusema wengi walikua wanaogopa kujiingiza kwenye mashindano.

 20. Mchangiaji Says:

  Jamani hivi miaka 10 ni mingi eeh, mbona kachoka hivi!!! Utadhani mnywa gongo! du balaa.

 21. liliy Says:

  Mie nilikua Naomba kama kuna mtu anaye faamu E meil yake kwani mimi nilikua mmoja wawa shiriki ktk mashindano ya miss arusha.au namba ya cm yake Liliyg2003@yahoo.com

 22. Matty Says:

  Beauty does not give up ages!

 23. mimi Says:

  duh!! hivi enzi hizo tulikuwa na sisi tuna malengo ya kupata umiss world jamani??mh inaelekea hizo nywele ndo zilikuwa zimeingia vile….hivi naye alienda nje kushindana?? au tulimpeleka mtu mwingine.ila sio kosa lake jamani ni tekenolojia ndo imebadilika ghafla!!cheers!!!

 24. ERLA Says:

  NI MREMBO NA MSOMI ACHENI MADONGO HAYASAIIDII… KEEP IT UP SAIDA KESSY

 25. Matty Says:

  Erla we nae vipi hiyo MAKE UP UMEIONA IMETULIA?

 26. SHANI Says:

  KILA MARA NYINGI PENYE MAFANIKIO WIVU HAUKOSI.DADA USISIKILIZE MANENO YA WAZUSHI NA WACHAWI.WEWE NI KIVUTIO TOSHA.MTU ASIKWAMBIE KITU.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s