Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya urembo (Miss Earth 2007),Angel Kileo, jana alijumuika na warembo wenzake katika kuwania taji la kipaji (Talent). Kama anavyoonekana pichani, Mrembo Angel alionyesha ngoma ya kipekee ambapo alicheza na moto akiwa amevalia nguo asilia ya kaniki. Angel Kileo alifundishwa ngoma hii ya kipekee na Kikundi cha sanaa cha Makumbusho na alifanya mazoezi mazito ili kuweza kumudu ngoma hii. Kutokana na utumiaji wa moto, warembo wenzake wengi pamoja na watazamaji waliogopa moto ule, hata hivyo mrembo huyu alikuwa kati ya wachache waliosifiwa kwa kuonesha vipaji tofauti zaidi ya kucheza ngoma za kiasili au kuimba pekee. Mshindi wa talent atatangazwa tarehe 11 Novemba mwaka huu.
Miss Earth 2007, ambayo ni mashindano yanayobeba kauli mbiu ya urembo kwa sababu maalumu, yanafanyikia huko Manila, Philippines na yanatarajiwa kufikia kilele chake tarehe 11 Novemba 2007 (jumapili ijayo) saa tatu na nusu usiku kwa saa za Manila-Phillippines. Yalianzishwa mwaka 2001.
Kila la kheri bibie.