BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“MIPASHO” MAANA YAKE NINI? November, 5, 2007

Filed under: Burudani,Sanaa/Maonyesho,Taarab,Tanzania/Zanzibar,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:57 AM

 

Muziki wa mwambao una aina kadha wa kadha.Wataalamu wa muziki wa aina hiyo wanaweza kukuambia mengi kuhusu aina hizo na pia jinsi gani unaweza kuitofautisha kutokana na midundo,mashairi, muonekano wa waimbaji wake nk.

Aina mojawapo iliyojipatia umaarufu sana kipindi cha nyuma kidogo ilikuwa inajulikana kama mipasho”. Neno hili mpaka hivi leo bado tafsiri yake haiko wazi.Jambo moja ambalo lipo wazi ni kwamba kwenye muziki wa mwambao ambao wengi wetu tunaufahamu kwa kifupi tu kama Taarab, majina ya Nasma Khamisi Kidogo (pichani kushoto) na Bi.Khadija Omar Kopa (pichani kulia) ni majina ambayo wapenzi wa muziki huo na watanzania kwa ujumla wanayatambua fika. Kuna wakati “upinzani” baina yao ulikuwa ni kama ule wa Yanga na Simba. Jambo moja ambalo wengi tulikuwa hatujui ni kwamba magwiji hawa wa muziki wa taarabu ni marafiki na kilichokuwa kinatendeka kwenye majukwaa na katika mashairi ilikuwa ni hali halisi ya usanii uliokomaa. Hivi neno “mipasho” lina maana gani?

Advertisements
 

5 Responses to ““MIPASHO” MAANA YAKE NINI?”

 1. Kimori Says:

  Yes, I remmember back in 2000 when I was in Dar.

  One day I boarded a cummuter bus, famously known as “Daladala” from Ubungo heading to Posta, when all of a sudden a driver tuned on a music, which goes like this…”Achia ngazi huo mchuma unaondoka….”, I don’t exactly remember the title of the song!

  It was really a perpetual song and I felt that, it even vanquished the hearts of most of the passengers in a commuter.

  Can you imagine?…The song continued to play even after I reached my destination at Akiba!…I think that is the most significant essence of “Mipasho” and what “Mipasho” is all about!

 2. Dinah Says:

  Hivi maana yake sio “bitching to one another”, awali nilidhani Mipasho ipo Bongo tu…kumbe hata nchi za Magharibi ipo na wengi wenye kupenda “kupashana” ni mashoga na wanawake walio ktk hali ya chini kimaisha Western way……sio kibongo-bongo 😦

  Hivi sasa naona hata vijana wanao-rap wanapashana ila kwa vile wao ni wanaume unadai ni kupigana “madongo” a.k.a kuambiana ukweli.

  Haya Kila la kheri ktk shughuli zenu za kupashana.

 3. asaki Says:

  hakika kila lakheri piga kazi mradi mkono uende kinywani na uvunji sheria ya nchi

 4. Mkereketwa Says:

  hivi hawa imekuwaje wamekaa pamoja???Sio hawa waliokuwa wanaimbana sanamu la michelini au naongopa jamani? Mara taarabu iko huku, mara shepu ya biringani. Hawa watu ni wanafiki jamani. Hapo wamekaa wanachekeana, kesho yake utasikia wameimbana mara oooo, wewe bei ya mtumba, mara ooo wewe wa sh.100 wataka sh.1000 ya nini. Yaani hawa bwana, wamezidi mno uswahili. Ila napenda sana taarabu na hawa ndio magwiji.halohaaaaaallllloooooooooo

 5. Ndumi Says:

  Samahani…ule wimbo wa achia ngazi bibi mchuma unaondoka huo unaitwa nini?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s