BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

R.I.P “SHAKA ZULU”. November, 6, 2007

Filed under: Filamu/Movie,In Memory/Kumbukumbu,Maisha — bongocelebrity @ 1:05 PM

 

Ukimtaja kwa jina la Henry Cele watu wengi watapata shida kidogo kutambua unamuongelea nani.Lakini ukimtaja kama “jamaa aliyeigiza kama Shaka Zulu” katika filamu maarufu ya Shaka Zulu kila mpenda filamu atakuambia “ahaa…yule”.Filamu hiyo ambayo ilikuwa inaelezea historia ya mfalme Shaka Zulu wa huko kusini mwa Afrika ni mojawapo ya filamu ambazo zipo kwenye lile kundi la “all time favourite movies ever made”.

Habari za kusikitisha ni kwamba muigizaji huyo aliaga dunia ijumaa iliyopita ya tarehe 2 Novemba huko Durban,Afrika Kusini katika hospitali ya Mtakatifu Augustine alipokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki mbili akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua. Amefariki akiwa na umri wa miaka 58.

Henry Cele au maarufu kama Shaka Zulu alizaliwa huko Durban mnamo mwaka 1949. Mwanzoni mwa maisha yake alikuwa ni mcheza soka wa kulipwa akiwa mlinda mlango kabla hajaingia kwenye masuala ya uigizaji. Kutokana na umahiri wake kama mlinda mlango (golikipa),wenzake walipenda kumuita “Black Cat” yaani paka mweusi. Hii ilitokana pia na weusi wake ambao ni ule unaoitwa “weusi tii”.

 

Ingawa katika maisha yake kama muigizaji filamu ameshiriki katika filamu mbalimbali kama vile Point of Impact ya mwaka 1993 na The Last Samurai ya mwaka 1990, filamu ya Shaka Zulu ndio atayokumbukwa nayo milele. Filamu hiyo aliyocheza na waigizaji maarufu kama Edward Fox na Christopher Lee.Kama hujawahi kuiona filamu ya Shaka Zulu, pata kipande kidogo katika video hii ya youtube;

Mpaka anafariki dunia inasemekana Henry Cele alikuwa amekuwa kama “chizi” hivi akipiga watu na kutukana watu ovyo. Mauti yamemfika huku akiwa amefungwa minyororo ili kumzuia asidhuru watu. Mke wake, Jenny Hollander, alikuwa pembeni ya kitanda chake hospitalini wakati mauti inamfika.Mkewe huyo amemuelezea kama mtu mpenda watu na aliyethamini sana kuishi karibu na watu wake na kuwasaidia.

Henry Cele alikuwa na watoto wanne ambao aliwazaa wakati wa ndoa yake ya kwanza. Hakubahatika kupata mtoto na Jenny Hollander ingawa walikuwa wameoana kwa zaidi ya miaka kumi.Anatarajiwa kuzikwa huko kijijini kwao Kwamashu,Durban wiki hii.R.I.P Henry Cele.

Advertisements
 

9 Responses to “R.I.P “SHAKA ZULU”.”

 1. Dinah Says:

  Dah! watu muhimu mbona wanazidi kupungua tu…tunabaki na maguluguja tu.

  RIP Cele.

 2. lilian Says:

  kifo cha huyu jamaa kimenisikitisha sana. one of my favourite movie is Shaka Zulu, on top of that he is one of my favourite actor in general. Mambo mengi muhimu yamo katika hii movie, hasa jinsi wazungu walivyoingia na kutawala kiakili wazee wetu wa enzi hizo, mpaka kuja kuwa watumwa wao, most of all how smart Shaka was, even though mwishoni alishindwa nguvu. He did the best job potraying Shaka, I was conviced that he was the really Shaka. His death felt like loosing Shaka all over again. RIP. You’ left a mark in me and lot of people.

 3. hombiz Says:

  Nimesikitishwa sana na kifo cha msanii huyu mahiri. Kwakweli sinema yake ninayoifahamu ni moja tu, nayo ni Shaka Zulu. Aliigiza wa ustadi mkubwa sana. Wala hakubahatisha. Yaani mtu yoyote aliyekwishaiona sinema ile, sidhani kama atapingana na kauli yangu. Na kwa ambaye bado hajaiona hii sinema, basi ningemshauli akaione ili aweze kutoa tathmini binafsi.
  MOLA amrehemu Henry Cele a.k.a Shaka Zulu, apumzike kwa amani, AMINA.

 4. veronica Says:

  natoa pole sana kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na funs wake wote inauma pale anapotutoka mtu muhimu na hasa hawa vioo wa jamii
  RIP Cele

 5. Bob Sankofa Says:

  Cele pia aliwahi kucheza filamu ya SIMBA WA TSAVO kama mnaikumbuka wadau. Alicheza kama kibarua mjenga reli ya Kenya kipindi cha ukoloni.

  Katika kazi zake zote naiheshimu zaidi triology ya SHAKA.

  R.I.P Mzee.

 6. Walter Says:

  Nilimpenda mcheza filamu huyu, kwa kweli filamu zake zinafundisha mengi ya asili ya kiafrika.

  Mwenyezi Mungu amempenda zaidi, tumwombee apunzike kwa amani.

  Amen

 7. jnjr Says:

  RIP man of action…….AMEN

 8. Mama wa Kichagga Says:

  I’M SORRY TO HEAR THAT HENRY CELE “SHAKA ZULU” HAS DIED. IT HAPPENS THAT HE BECAME ONE OF MY HEROS WELL OVER 30 YRS AGO AFTER AFTER I WATCHED HIS MOVIE “SHAKA ZULU”.

  HE WAS AND STILL IS I AM SURE MUCH LOVED BY THE PEOPLE IN AFRICA AND OTHER CONTINENTS THROUGH HIS OUTSTANDING WORK (ACTOR).

  MY SYMPATHIES TO HIS FAMILY AND OTHERS WHO WERE CLOSE TO HIM. R.I.P.

 9. Andrew Says:

  Hello Africa World!!!
  Shaka Zulu soundtrack needed for all time!!
  Pls


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s