BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MTUME JAPO NJIWA! November, 9, 2007

Filed under: Burudani,Muziki,Taarab,Tanzania/Zanzibar,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:41 AM

Ijumaa nyingine imewadia.Leo unapanga kufanya nini?Unapanga kwenda wapi kujiliwaza baada ya wiki nzima ya mihangaiko ya hapa na pale kimaisha?Ni wazi kwamba siku hazifanani na kama alivyosema Lady JayDee,siku pia hazigandi.Ni muhimu kupata muda wa kupumzika japo siku moja kwa wiki.Inaweza ikawa sio ijumaa jioni kama ambavyo wengi tumezoea.Inaweza kuwa siku yoyote ya wiki, ni uamuzi wako.

Wakati mipango hiyo ikiendelea,baadhi yenu mmekuwa mkiuliza mbona muziki wa mwambao haupewi nafasi ndani ya BC?Msitie shaka kwani BC haina sera za upendeleo na kwa maana hiyi leo hatuna budi kutimiza haja hiyo ya wapenzi wa muziki wa mwambao.Huu ni muziki ambao huuwezi kuutenganisha na Tanzania hata kidogo.Anayetuburudisha hivi leo ni Patricia Hillary na kibao chake maarufu cha Njiwa.Kama uko mbali na wale uwapendao,wale wakufaao maishani,mtume japo njiwa akupelekee zako salamu.Ijumaa Njema!

Advertisements
 

5 Responses to “MTUME JAPO NJIWA!”

 1. Bob Sankofa Says:

  Leo ni fainali za kumtafuta malkia wa Ngwasuma pale Diamond Jubilee, mimi na timu yangu ya http://www.mwenyemacho.com tutakuwa pale kushuhudia mmoja kati ya madada 10 akiondoka na gari la shilingi milioni kumi.

  BC iko mbali nasi kimwili lakini kihabari iko nasi karibu kuliko maelezo. Tunamtuma njiwa kwa timu nzima ya BC, njiwa anakuja na salamu za pongezi kwa kazi nzuri mnayofanya amabyo si tu kuhabarisha umma wa Waswahili bali kuwa hifadhi njema ya kumbukumbu ya yaliyowahi kujiri katika jamii ya Waswahili. Nikisema Kiswahili namaanisha yeyote anayeongea lugha hiyo si lazima Mtanzania 🙂

  Ewe njiwa muvuzisha salamu kwa timu yote ya BC fasta!

 2. Dinah Says:

  :-)) Bob

  Hii ni classic taarabu na inasikilizika!

 3. Ally Says:

  Yap!ni classic taarab.Naomba utuletee na zile za huzuni kwa sie wafiwa,kifo cha baba na kifo cha mama,utufarijishe BC,plz plz

 4. DUNDA GALDEN Says:

  MARADHI YA NYUMBANI
  HAHAH HAPO PIA SI HABA KWANI NJIWA ALIE KUSUDIWA PALE NI MSHENGA KAMA SIKOSEI NAMKUMBUKA JIRANI YANGU MMOJA ALIPOKUWA MSHENGA BASI MATOKEO YAKE MCHUMBA AKAMCHUKUWA YEYE NA KWA BUSALA ZA ALIEMTUMA AKAMTAKIA KILA LA KHERI MPAKA SASA JAMAA ANA WATOTO WANNE HICHO KISA CHA KWELI KABISA ENZI CHA KISA HIKI UKIPIGWA MWIMBO HUU……
  THINKS ALOT BC HOME IS HOME SASA INABIDI MUWE NJIWA MICHUZI MPE Hi MASUDI WA KIPANYA. JIKHO MAN MAEMBE MACO SAWE NA MSACHO BEAST WA PALE DUNDA GALDEN
  TELL THEM CHAFOSA NEVER DIE

 5. Thinks Dunda Galden ujumbe umefika Maco sawe Big Up BC
  lini unaludi?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s