BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MWAKA UNAWEZEKANA KUWA WA SHETANI? November, 10, 2007

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Maisha,Muziki — bongocelebrity @ 12:30 AM

 

 

Miaka inatofautiana.Ulivyokuwa mwaka uliopita sivyo utakavyokuwa mwaka huu.Huo ni ukweli usiopingika. Lakini je,inawezekana kwamba mwaka fulani ukawa “Mwaka wa Shetani”?. Amani Temba,maarufu kama Mheshimiwa Temba,msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wanaume TMK(Original) katika wimbo wake “Mwaka wa Shetani” anaelekea kusema inawezekana mwaka fulani ukawa wa shetani.Kila unachotaka kufanya hakitimii,kila mpango unavurugika.Wewe unasemaje?Kuna kitu kama Mwaka wa Shetani?

Usikilize wimbo wenyewe kwa kubonyeza hapa.

Pichani ni Mh.Temba akiwa jukwaani kuuelezea mwaka wa shetani.

Photo credit:MichuziJR.

Advertisements
 

5 Responses to “MWAKA UNAWEZEKANA KUWA WA SHETANI?”

 1. Bob Sankofa Says:

  Watu na nchi yao bwana, kaka uzalendo hadi shingoni. Poa sana hii.

 2. Na haujaisha bado.Takribani bado siku 50 ataendelea kutesa.

 3. Dinah Says:

  MH. Temba kazi nzuri.

  Kuna kitu kama mwaka wa shetani?
  Well, inategemea na unavyoamini. Kile unachoamini na kukili ndio kitakachokua au tokea.

  Piga kazi, kuwa mbunifu, ongeza bidii,usikate tamaa na mambo yataenda poa tu.

  Mf: Unasumbuliwa na homa za hapa na pale na kikohozi. Ukaamua kwenda kupima ukakutwa una NGOMA….kwa mshituko ukalia nakususa (kushindwa kula wala kwenda viwanja) huku moyoni ukikili kuwa hutopona tena (homa na kikohozi) basi ujue ndio safari hiyo (kifo) lakini ukikili kuwa utapona (maradhi hayo) na unafanya jitihada za kula vema, kunywa na kufuata masharti ya Dk basi unaendelea kuwepo.

  Unatakiwa kufikiria chanya na sio hasi ili kufikia malengo yako na wakati huohuo kutambua kuwa “kutesa ni kwa zamu” kila mtu anahaki ya kuwa juu nakufurahia akishangaa anashuka na wewe unachukua nafasi sio?

  Maish ani kupanda na kushuka msimuachie mwanya shetani kwa kukili kuwa mwaka wake huu unless hamna imani za kidini.

  J’mosi njema 🙂

 4. kaboka Says:

  du kumbe winter imeshaanza bongo,si mchezo.kweli huu mwaka wa shetani

 5. liven Says:

  eeeebwana mh.temba !! upo juu ila kaza buti wangu


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s