BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

USIKU WA A.Y November, 13, 2007

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Fashion,Muziki — bongocelebrity @ 12:23 AM

 

Mmojawapo wa celebrities wa mwanzo mwanzo kufanya mahojiano na BC alikuwa ni mwanamuziki wa kizazi kipya, AY a.k.a Mzee wa Commercial.Huyu ni mmojawapo wa wale wanamuziki waliokuwa wanaunda kundi la East Coast kabla halijasambaratika mwaka huu.

Mwisho wa East Coast haujawa mwisho wa AY.Hivi sasa anaingia rasmi kwenye “ ujasiriamali”. Ijumaa hii ya tarehe 16/11/2007 ndani ya Club Maisha,AY anatarajia kuua ndege watatu kwa jiwe moja au kwa mpigo.

Siku hiyo AY atazindua rasmi Documentary juu ya maisha yake binafsi na yale ya kimuziki bila kusahau undani ya maisha yake ndani ya mahusiano ya wake ampendaye.Mpaka hivi sasa AY hajawahi kueleza kinagaubaga kuhusiana na hili.Ameahidi kufanya hivyo Ijumaa ndani ya Club Maisha. Documentary imepewa jina la UNDANI WANGU (pichani juu ni cover ya documentary hiyo)

Pili atakuwa anazindua clothing line(viwalo) ambavyo vinakwenda kwa lebo ya “Commercial Wear”.Nguo ni za kiume na pia za kike.AY anasema angependa mashabiki wake siku hiyo wazivae nguo zake na pia kujumuika naye katika usiku huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake. Nguo zinapatikana Zizzou Fashion-Sinza na Dream Wear duka lililopo gorofa ya kwanza ndani ya Millenium Tower.

Pia Mzee wa Commercial atakuwa anazindua rasmi tovuti yake www.ay.co.tz tovuti ambayo ni maalumu kwa mashabiki wake waliopo mbali na wanataka kuwasiliana naye moja kwa moja kupitia mtandao wake huo. Ndani ya tovuti hiyo pia unaweza kusoma mengi juu ya historia yake,tarehe za show zake,picha na video mbalimbali na mambo mengine chungu mbovu.

Baadhi ya wasanii wakali ambao watamsindikiza AY katika usiku huu ni Jua Kali kutoka Kenya, Michael Ross kutoka Uganda, Besta na Juma Nature kutoka Tanzania na wengineo wengi. Wadhamini wa shughuli hii ni Straight Muzik.

Ukitaka kusoma mahojiano tuliyowahi kufanya na AY siku za nyuma bonyeza hapa.

Advertisements
 

8 Responses to “USIKU WA A.Y”

 1. Russian Boy Says:

  Go go go … Tunaitaji New idea ktk kutoka,tumesikia Masoud Kipanya ana Shop Millenium Tower,Naye msela anashop pale,Bongo ni kubwa.kwanini idea zifanane? Pili Tumesikia Hizo TShirt zinaprintiwa Mtaani Pale Sinza Kwa Mfini Boy Near Vatican Hotel.Sasa inakuaje wanapotuongopea Product zina toka Outsiderz????

 2. Dinah Says:

  Kapicha kanono hako! Unatega watu AY!

  Nilisema na nimesema mengi kuhusu wewe. Leo hapa mimi nakupa Pongezi kwa hayo uliyoyafanya. Inafurahisha kuona kuwa wewe umekuja na mtindo tofauti wa kuelezea maisha yako na shughuli zako kwa vitendo(Vid) sio maandishi(makaratasi).

  Hizo nguo za kike ni za ki-miss-miss au na sisi mabonge ummetupendelea?

  Kila la kheri ktk shughuli zako.

 3. maureen Says:

  Big up Ay……na hiyo cover iko bomba…

 4. yaa its true jamaa anajitahidi sana kuhakikisha anafanikiwa na kufika mbali zaidi kupiti fani ya muziki na mengineyo, kusema ukweli wasanii wengi wa bongo wamelala sana, wana mambo mengi ya kufanya ili kujikwamua na ugumu wa maisha lakini wapi, wao wanaamini wakiingia studio akarekodi albamu yake moja, akaipeleka sokoni, akapata shoo mbili tatu hivi , akafanikiwa kununua baloon, basi inaishia hapo na bila kuacha kujiachia kwa kwenda mbele,kumbe kuna kesho inakuja ambayo wao wanatakiwa wajiandae kwa hilo.Mfano mzuri si huyo AY amebaini kesho itakuwa vipi ndio maana amenza leo, basi na tuwaunge mkono na watu kama hawa, ili ifike siku msanii ajivunie mafanikio yake na hata taifa kwa ujumla,asante nawakilisha tu washkaji.

 5. valleshima Says:

  sasa wewe dinah unafikiri anakutega wewe au…nakwambia tena umekosa shabaha,…

 6. […] Check it out! While looking through the blogosphere we stumbled on an interesting post today.Here’s a quick excerptPili atakuwa anazindua clothing line(viwalo) ambavyo vinakwenda kwa lebo ya “Commercial Wear”.Nguo ni za kiume na pia za kike.AY anasema angependa mashabiki wake siku hiyo wazivae nguo zake na pia kujumuika naye katika usiku huo … […]

 7. liven Says:

  big up sana mtu wangu!!
  upo juu nimekukubali.. hiyo kaza hapo ni bomba nbaya wangu!!!
  cheers
  t’chao kip it ril dude!!

 8. Mbatta Says:

  Mwenyewe huyooooooo. U r doing a GOOD JOB. I am so proud of u.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s