BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DANSI ILIPOKUWA DANSI! November, 14, 2007

Filed under: Historia,Muziki,Utamaduni,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:15 AM

 

Mojawapo ya bendi ambazo ziliwahi kutingisha sana nchini Tanzania ni ile iliyoitwa DDC Mlimani Park Orchestra.Pichani ni baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo miaka hiyo.Hii ilikuwa ni wakati wa mojawapo ya ziara zao za kimataifa.

Bendi ambayo ilianzishwa mwaka 1978,mwanzoni ilijulikana kama Mlimani Park Orchestra ikiwa kama “resident band” pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar-es-salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services. Mmiliki huyo wa mwanzo alipofilisika mnamo mwaka 1983,bendi ikachukuliwa na Dar-es-salaam Development Corporation (DDC) na hivyo mwanzo wa kujulikana kama DDC Mlimani Park Orchestra.Baadhi ya wanamuziki waanzilishi wa Mlimani Park Orchestra ni kama vile Abel Balthazar,Muhiddin Maalim Gurumo,Cosmas Tobias Chidumule,Joseph Mulenga na Michael Enoch kabla Bitchuka hajajiunga nao baadaye.

Kuna mtu anaweza kutusaidia kuitaja hii line-up nzima ya DDC Mlimani Park Orchestra kama wanavyoonekana pichani?F.M.Tungaraza,Fresh Jumbe,Muhidin Issa Michuzi,Ebby Mkandara,Freddy Macha,mpo?

Advertisements
 

18 Responses to “DANSI ILIPOKUWA DANSI!”

 1. sinzia Says:

  Asante kwa kutupa flash-back pic…mimi nilikuwa bado mdogo enzi za picha hiyo…hivyo sitaweza watambuwa wote..lakini ni jambo lililowazi kuwa aliyechuchumaa kushoto kwako mwenye suti na tai shingoni(AMEJISHIKA KIDEVU) ni Hassan Rehani Bichuka. Ni mwanamziki aliyekuwa anajulikana sana…na kwa kiswahili cha sikuhizi tungeweza sema aliwafunika wengine katika ile Band. Good job BC

 2. Fresh Says:

  WALIOSIMAMA NYUMA TOKA KUSHOTO NI:
  Marehemu Machaku Salum (Aliyekuwa katibu wa bendi/Trumpet) , Marehemu Michael Bilali (Lead guitar), Huruka Uvuruge (Rhythm guitar), Juma Town (Alto Saxphone), Hamisi Milambo (Trumpet), Henry Mkanyia (Lead guitar), Abdala dogodogo (Bass) na Habib Abasi Mgalusi “Jeff” au “Jeffasto” (Drums).
  MSTARI WA MBELE WALIOCHUCHUMAA TOKA KUSHOTO:
  Hassan Bitchuka (Muimbaji), Joseph Bernad (Tenor Saxphone), Mashaka Shabani (Percussion/Drums) na Maxmillian “Max” Bushoke (Muimbaji).

 3. Dinah Says:

  Dah! watu mmetoka mbali wakati huo jeans ikitwa dengriz maalumu kwa wafungwa.

  F.M.Tungaraza,Fresh Jumbe,Muhidin Issa Michuzi,Ebby Mkandara,Freddy Macha.

  Ei? hawa ndio vingwangwa wa enzi zenu sio (vijana wa enzi hizo)mbona mimi mmenisahau wajameni? 🙂

 4. Editor Says:

  Fresh,
  Shukrani sana kwa kutusaidia na hiyo line-up ya “Sikinde”.Stay blessed.

  Dinah,samahani kwa kukusahau kwenye “list”.!!Next time.

 5. Mi Chichemi!:-) Asante BC!

 6. f m tungaraza Says:

  Jeff,

  Feresh kamaliza kila kitu.

  Piga, kata ngwala, piga mtama,kata funua,binua, piga ngeta, kaba, kwaruza na kucha, uma na meno, tia konde, piga kelbu au fumbata, galagaza, buluza, tia pingu, au sweka selo lakini nikikuporochoka tu kama ni saa saba unusu mchana na nipo Helsinki, Finland nitawasha redio niikamate Capital FM, nisikilize “..Africaaa rise and shineee!!” toka redio SABC (South African Broadcasting Company). Kipindi hiki ndicho kipindi cha redio kinachonisogeza karibu na bara zima la Afrika kila siku za juma niwapo Finland.

  Mwaka jana nilikuwa nasikiliza mahojiano makali kati ya mtangazaji wa SABC na ofisa mmoja wa Naijeria. Yalipoisha yale mahojiano nikamsikia yule mtangazaji wa SABC akisema “..from South African Broadcasting Company, it is me Maxmillian Bushoke..” Wallahi sikuamini masikio yangu! Nikanyanyua simu nikamkong’otea Muhidin Michuzi. Nikamwambia niliyosikia toka redioni dakika chache zilizopita. Muhidin akaniambia “..Ndiyo yeye Max Bushoke yupo SABC siku hizi..” Tukazungumza mengine zaidi kidogo tukaagana. Naam, Max sasa kaungana na safu ya kina Francis Chanduona, Duncan Mkandawile, na Bwana Njelanje kule SABC zamani Redio RSA.

  Tafadhali kama unaweza naomba utuletee mahojiano na Max Bushoke ili tupate unono wa nini kilijiri mpaka ikawa toka “Nginde” hadi SABC.

 7. Michuzi Says:

  Asante kaka Fresh kwa kutupa line-up japo ungengoja siku mbili tatu ili tuone ni wangapi wanakumbuka listi hiyo ya maauaji. Inasikitisha kuona hapo Michaeol ‘King’ Enoch Ticha wa ma Ticha hakwenda safari hiyo japo asilimia 75 ya muziki wa Sikinde enzi hizo uliwekwa bashraf na yeye.

 8. f m tungaraza Says:

  Jeff,

  Feresh kamaliza kila kitu.

  Piga, kata ngwala, piga mtama, binua, kata, funua piga ngeta, kaba, kwaruza na kucha, uma na meno, tia konde, piga kelbu au fumbata, galagaza, buluza, tia pingu, au sweka selo lakini nikikuporochoka tu kama ni saa saba unusu mchana na nipo Helsinki, Finland nitawasha redio niikamate Capital FM, nisikilize “..Africaaa rise and shineee!!” toka redio SABC (South African Broadcasting Company). Kipindi hiki ndicho kipindi cha redio kinachonisogeza karibu na bara zima la Afrika kila siku za juma niwapo Finland.

  Mwaka jana nilikuwa nasikiliza mahojiano makali kati ya mtangazaji wa SABC na ofisa mmoja wa Naijeria. Yalipoisha yale mahojiano nikamsikia yule mtangazaji wa SABC akisema “..from South African Broadcasting Company, it is me Maxmillian Bushoke..” Wallahi sikuamini masikio yangu! Nikanyanyua simu nikamkong’otea Muhidin Michuzi. Nikamwambia niliyosikia toka redioni dakika chache zilizopita. Muhidin akaniambia “..Ndiyo yeye Max Bushoke yupo SABC siku hizi..” Tukazungumza mengine zaidi kidogo tukaagana. Naam, Max sasa kaungana na safu ya kina Francis Chanduona, Duncan Mkandawile, na Bwana Njelanje kule SABC zamani Redio RSA.

  Tafadhali kama unaweza naomba utuletee mahojiano na Max Bushoke ili tupate unono wa nini kilijiri mpaka ikawa toka “Nginde” hadi SABC.

 9. Ally Says:

  Fresh nimekukubali wangu!!una miaka mingapi wewe?halafu unaonekana mpaka leo hiyo miziki yao ndio mipigo yako!!Big up bro

 10. Ally Says:

  Halafu umetaja na ani zao ss yaani kuonyesha kiasi gani umezama mpiga dram mpiga guitar mpiga tumba dah kaka heshima nyingi sana.

 11. Ally Says:

  Mbona huyu wa 2 toka kushoto waliochuchumaa kamajenerali ulimwengu au mi sioni vzr wadau nambieni vzr kaka fresh sio ulimwengu kweli huyu!!!!!!!!!

 12. Fresh Says:

  Michuzi,

  Kweli ningesubiri kidogo, samahani bro. Hata hivyo niliona niwajibike tu baada ya BC kuomba msaada. Nadhani Mzee King Michael Enoch ticha hakuenda safari hiyo kwa sababu alikuwa ni mgonjwamgonjwa kwa siku nyingi tu.

  Ally

  Asante kwa kunikubali. Hao jamaa nawajuwa pamoja na vyombo wapigavyo kwasababu ukimuondoa Mashaka (ambae nilipiga naye Dar International na nikamuwacha huko), waliobaki wote hao (pamoja na wengine ambao hawapo kwenye picha) nilikuwa nao sikinde kwenye siku zangu za mwishomwisho kabla sijaondoka bongo mwaka 1990. Na hiyo picha nadhani walipiga baada ya mwaka 91 mara baada ya mimi kuondoka.
  Kwa umri mimi nilikuwa ndiye mdogo wa wote hao kasoro Abdala dogodogo tu. Kwasasahivi miziki yangu imebadilika kidogo na si kama hiyo tuliyokuwa tukipiga nilipokuwa nao.
  Huyo jamaa (kwenye picha) ni kweli kabisa anafanana na Jenerali Ulimwengu, lakini ni Joseph Bernad mpiga sax.

 13. Ally Says:

  Sawa mkubwa upo wapi ss?na bado unafanya mziki?maana kama 90 umeondoka bongo kitambo!!

 14. Dinah Says:

  Freshjumbe.com 🙂

 15. bdo Says:

  Bro.Jeff big up kwa line up yako, nimekubali ngoma huchezwa na mwenyewe… ila naomba kumnukuu ‘mdau FM Tungaraza’ kuhusuhu max Bushoke,kuwa…

  “..from South African Broadcasting Company, it is me Maxmillian Bushoke..” Wallahi sikuamini masikio yangu! Nikanyanyua simu nikamkong’otea Muhidin Michuzi. Nikamwambia niliyosikia toka redioni dakika chache zilizopita. Muhidin akaniambia “..Ndiyo yeye Max Bushoke yupo SABC siku hizi..” ……….mwisho wa kunukuu.

  naomba kuuliza
  1.Je huko SABC, Max Bushoke ni Mtangazaji au ilikuwa mgeni akihojiwa studio?
  2.Au najichanganya mwenyewe!kuwa nadhani ‘cosmass chidumule ndiye mtangazaji huko RSA? please i remain to be guided

 16. james Says:

  sina chakuongeza za ya alivyo andika mdau namba 2 fresh kwani hakuna kosa hata mmoja

 17. james Says:

  kumbe mdau namba2 ni fresh jumbe ndio maana amewatambuwa wote kwani baadae alijumuka nao hao wana sikinde na wimbo wake wa kwanza ndani ya ngide ni mv mapenzi namba2 nakumbuka kwa mara ya kwanza ameuwimba wimbo huu ddc magomeni kondoa nakufangilia mzee mwenzangu waa waah!

 18. phareed Says:

  thanks bc kwa kutukumbusha mambo ya enzi, yaani hapo mziki ulikua si mchezo, mimi namzimia sana fresh jumbe jee naweza vipi kupata nyimbo zake zote alizowahi kushiriki na benditofauti pia na bendi yake?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s