BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ONE TO ONE WITH LADY JAYDEE. November, 19, 2007

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Familia,Mapenzi,Muziki,Utamaduni — bongocelebrity @ 12:09 AM

Bila kusita tunaweza kuanza kwa kusema Lady Jaydee(pichani) ni miongoni mwa wanamuziki wa Tanzania ambao hawahitaji utambulisho mrefu sana miongoni mwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya popote walipo nchini Tanzania na duniani kote. Leo hii ukipenda waweza kumuita Jide au Lady Jaydee. Aliwahi pia kuwa na majina mengine lukuki.Unayakumbuka?

 

Pamoja na hayo jina lake rasmi ni Judith Daines Wambura Mbibo.Ukipenda unaweza kumuita Mrs.Gardner G.Habash jina ambalo ana haki zote za kulitumia kwani ameolewa na Gardner,mtangazaji maarufu wa Clouds FM. Judith Wambura alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 15 Juni,1979 kwa Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake.Inasemekana alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba.Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi.Baada ya kumaliza shule,Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujikita kwenye uanamuziki moja kwa moja mwaka 2000.

Baada ya kudumu kwa muda mrefu kama solo artist,mwaka huu Lady Jaydee amefanikiwa kufanya mambo mawili muhimu.Kwanza alianzisha rasmi bendi yake iitwayo Machozi Band na pili kutoa albamu yake ya nne aliyoipa jina Shukrani. Kabla ya hapo alishatoa albamu tatu ambazo ni Machozi(2000),Binti(2003) na Moto(2005).

Leo hii ukitaka kumuona Lady Jaydee kifanya vitu vyake akiwa na bendi yake,Machozi Band, unachotakiwa ni kujongea kila Ijumaa usiku ndani ya ZHONG HUA GARDEN, Regent Estat- Ally Hassan Mwinyi Road jijini Dar-es-salaam. Hutojutia uamuzi wako.

Hivi karibuni tulifanya mahojiano na Lady Jaydee ambapo tuliongelea mambo kadha wa kadha yakiwemo yake binafsi kama mwanandoa,binti maarufu,kazi zake za kimuziki,matarajio yake ya baadaye na mengine mengi.

Ingawa albamu yake ya Shukrani imetoka miezi kadhaa iliyopita,hatukuona haja ya kutoongelea machache juu ya albamu hiyo ambayo kama zilivyo albamu zake zilizopita,hii nayo inasambazwa na GMC Wasanii Promotors ya jijini Dar-es-salaam.Hii ndio albamu yenye wimbo uliotamba sana mwaka huu wa Siku Hazigandi. Bado inapatikana mitaani na madukani kwa wale ambao wangependa kuinunua.Yafuatayo ni mahojiano kamili;

BC: Unaweza kutueleza wewe ni mtu wa aina gani kwa kutumia maneno yasiyozidi matano?

JIDE: Mwanamke mwenye kipaji, uwezo na fikra.

BC: Unakumbuka nini kuhusu maisha yako ulipokuwa binti wa miaka 18? Unadhani umebadilika kwa kiasi gani tangu wakati huo mpaka hivi leo?

JIDE: Kipindi hicho ndio nilikuwa namalizia form four pale Zanaki Girls, nilikuwa natokea katika matamasha ya wanafunzi nikiigiza nyimbo za kina Mc Lyte, Da Brat na wengineo.Nakumbuka nlikuwa rapper zaidi, msela zaidi na mgomvi kwa wastani wangu. Leo hii naangalia nyuma naona nimebadilika sana. Nimekuwa muimbaji zaidi, hata rap siwezi tena, nimeacha usela nimekuwa mwanamke zaidi, nina majukumu ya maisha, nimeacha ugomvi lakini usiingie katika reli yangu. Kwa kweli nimekuwa mkubwa/mtu mzima.

BC: Unakumbuka ilikuwa lini na wapi ambapo ulipanda jukwaani kwa mara ya kwanza kama msanii. Ilikuwaje?

JIDE: Jukwaani nimenza kupanda tangu nikiwa sekondari lakini nakumbuka jukwaa la professional nilipanda kufungua shows ya Chaka Chaka na pia ya Brenda Fassie,wanamuziki kutoka Afrika Kusini ambao walikuja nchini Tanzania katika nyakati tofauti tofauti. Ilikuwa na msisimko tofauti. Nilikuwa muoga sana lakini nakumbuka nilipokelewa vizuri, hadithi za wakubwa zangu kina Bonie Love, Mr C, Ruge, OJ nk wanasema watu walipenda “sauti ya haka katoto”.

 

Lady Jaydee(katikati) ametoka mbali.Pichani ni enzi hizooo akiwa katika pozi na msanii mwenzake wa muziki wa kizazi kipya, Ray C(kushoto) pamoja na mtangazaji,mchota katuni,mbunifu wa mitindo,Masoud Kipanya (kulia)

BC: Hivi karibuni umetoa albamu uliyoipa jina Shukrani jambo ambalo limepelekea watu waanze kujiuliza kama ndio unasema kwaheri katika mambo ya muziki au? Kwanini umeiita albamu yako Shukrani?

JIDE: Nina mapenzi ya kweli na muziki, pia muziki ndio ajira yangu, sina nia ya kuacha. NDIO KWANZA NIMEANZA. Albamu ya Shukrani ni namna ya mimi kucheki nyuma na kusema asante kwa Mola, Wazazi, Wadau wa muziki,wapenzi wa muziki wangu na Watanzania kwa ujumla. Wamepokea kipaji changu na kunikuza katika hatua hii ya kwanza muhimu.

BC: Inakuchukua muda gani kutengeneza albamu kama hii ya “Shukrani”?

JIDE: Muda wa kutengeza albam unatokana na malengo ya msanii. Shukrani nimeitengeza polepole kama kwa miezi kama 11 hivi.

BC: Umewashirikisha wasanii gani katika albamu hii? Ina nyimbo ngapi?

JIDE: Ina nyimbo 12, nimewashirikisha Mad Ice, Nako 2 Nako na Chamilion.

BC: Unaweza kutuambia kidogo kuhusu mlolongo mzima wa kutunga wimbo,kuupa beats na kisha kuuweka kwenye video? Wewe kama msanii unashiriki vipi katika zoezi hilo zima?

JIDE: Nikipata hisia ya wimbo kwanza inakuja melody, halafu naandika tungo kutokana na hisia zangu au stori fulani, kisha nawekesha muda wa studio na mtengenezaji ninayeamini atamudu wimbo nilionao. Tukiwa studio mara nyingi huwa mimi naimba kibwagizo halafu producer anapiga kufuatana na ninavyoimba. Kitu kinatoka.

 

Lady Jaydee akiwa nyumbani kwake.

BC: Mwaka huu umeanzisha bendi ijulikanayo kama Machozi Band na hivyo kuanza kuperform nyimbo zako “live”. Nini kilikusukuma katika kuanzisha bendi hiyo? Unatoa ushauri gani kwa wasanii ambao bado wanatumia ‘playback” katika maonyesho yao?

JIDE: Niliwahi kukutana na Oliver Mutukuzi(mwanamuziki kutoka Zimbabwe anayeheshimika sana barani Afrika na duniani)huko Sauzi mwaka 2002 nadhani. Akanishauri niwe naweka milio ya vyombo live wakati wa kurekodi, nikaanza kufanya hivyo katika albamu ya ‘Binti’ nikaona inapendeza na inadumu zaidi. Basi nikafikiria si vibaya hata onyesho liwe live pia. Basi tangu hapo nliendelea kupiga live japo kwa band za zing zong. Muda ulipofika nikaona niwe na kundi langu mwenyewe. Nashukuru ngoma imekubali na sasa tunapiga gig kila Ijumaa.

Nashauri artists watumie live pale inapobidi, si lazima kila mtu awe na band, lahasha, maana ni gharama sana lakini ni muhimu kwao kujua kutumia band.

 

Usafiri wa Machozi Band.Unaowaona ndio wanaounda kundi zima la Machozi Band likiongozwa na Lady Jaydee mwenyewe.

BC: Tofauti na wanamuziki wengi wa nchi za nje, wanamuziki wengi wa Tanzania tulioongea nao wanasema wanaandika nyimbo zao wao wenyewe.Je wewe pia unaandika nyimbo zako mwenyewe? Kama ndio unadhani hiyo inakusaidiaje kama msanii au binadamu katika kutatua au kuongelea mambo yanayokuhusu wewe au jamii inayokuzunguka?

JIDE: Mimi pia naandika mwenyewe.Nadhani kujua kuandika ni gift ambayo Watanzania tunayo ukifananisha wa artists wa nje. Nakubali pia mtu kuniandikia wimbo japo haijatokea kwa sasa. Nikiandika mwenyewe inanisaidia jambo moja muhimu ‘naakisi ukweli uliopo karibu na jamii ninayoishi’. Hicho ni kitu muhimu katika sanaa.

BC: Baadhi ya nyimbo zako kama vile “Usiusemee Moyo” na “Wanaume Kama Mabinti” zilionekana kama ni nyimbo ulizoziimba kutokana na personal experiences zako.Kuna ukweli wowote katika jambo hili?

JIDE: Wana sanaa wengi wa kweli huwa wanaandika au kuchora au kujigamba kwa kile kilichopo karibu ya jamii yao. Na mimi ni hivyo hivyo. Unaposema ‘personal experience’ si lazima iwe mimi, yaweza kuwa mimi au marafiki zangu au mtanzania kwa jumla. Naangalia jamii kwa jumla nikiwemo mimi.

BC: Kuna muimbaji yeyote wa hapa Tanzania hujafanya nae kazi na ungependa kufanya nae kazi?

JIDE: Nawapenda Khadija Kopa na Babu Njenje, natamani niimbe nao hata kesho.

BC: Style za mavazi yako zimekuwa zikibadilika takribani kila unapotoa albamu mpya. Unaweza kutuambia hiyo inatokana na nini?

JIDE: Inatokana na kukua kirika na kimuziki. Huwezi kuwa yule yule wa jana.

BC: Mavazi ni kitu muhimu sana kwa msanii, unaweza kutuambia mwana mitindo gani unampenda kazi yake hapa Tanzania? Kwanini?

JIDE: Napenda kazi za Mustafa Hasanali.Sababu ni kwamba huyu amemudu vyema kuchanganya vionjo vya mitindo asili ya Tanzania (mfano masai) na ile ya Asia na Magharibi. Hata mimi nilifanya hivyo ktk albamu hii ya ‘Shukrani’.

 

Lady Jaydee katika pozi.

BC: Wewe ni msanii ambaye umeshajizolea tuzo nyingi za muziki mpaka hivi sasa. Katika tuzo zote hizo kuna tuzo yoyote ambayo hukutegemea hata siku moja unaweza kuipata?

JIDE: Ninapofanya wimbo wala siwazi tuzo kabisa.Inapotokea mimi kupewa tuzo yoyote kwa wimbo wangu wowote, kwa kweli inakuwa ni jambo la faraja na huwa nafurahia sana. Nawashukuru wote wanaotoa hizi tuzo. Tanzania, Africa, Ulaya na kote duniani.

BC: Pamoja na mafanikio ambayo umeshayapata katika muziki bado unaonekana kufanya kazi kwa bidii. Je kuna lolote ambalo hujafanikiwa nalo na ambalo pengine ndio chachu yako katika kufanya kazi kwa bidii?

JIDE: Tiger Woods, Zadok, Bill Gates, Reginald Mengi, Oprah n.k wamefanikiwa lakini naona wamo tu jamaa hawaachi kufanya kazi kwa bidii. Sijui kwanini. NA ASIYEFANYA KAZI ASILE, maandiko yanasema. Mimi nataka kula vizuri, kulala vizuri, kuishi vizuri na kumsaidia Mama’angu. Kwa kweli ntafanya kazi kwa bidii, nitafanya kazi ya muziki kwa kuwa nimebarikiwa na Mola kipaji cha kuimba.

 

The Lady.

BC: Wasanii wengi tulioongea nao hawana wawakilishi wao nje ya Tanzania na hususani Marekani,Canada, Uingereza nk. Je wewe unao wawakilishi huko? Kama sio unadhani hilo linachangia vipi katika kupunguza mauzo ya kazi zako na kuutambulisha muziki wako kimataifa zaidi? Una mpango gani?

JIDE: Ni vigumu sana kupata wakala katika mataifa makubwa ya nje sababu nyimbo zetu bado hazina nafasi katika vyombo huko nje kama jinsi nyimbo za nje zinavyopewa nafasi huku nyumbani. Wapenda muziki wana tabia ya kununua wanachokijua na hawawezi kujua nyimbo zetu sababu hazichezwi kwao. Sasa si rahisi kupata wakala maana hujulikani wala huuzi ugenini.

Ningepanda kuwashawishi jamii ya Watanzania wa ughaibuni wawe mawakala wetu, wauziane kihalali muziki wetu na hatimaye tutasogea hatua nyingine kama kupata record deals za kimataifa nk.

BC: Wewe na mume wako Gardner G. Habash ni watu maarufu au celebrities nchini Tanzania. Je umaarufu mlionao unayafanya maisha yenu kama wanandoa kuwa marahisi au magumu? Kivipi?

JIDE: Hakuna jambo rahisi dunia hii. Ndoa yoyote ina ugumu wake, iwe ya watu maarufu au la. Nashukuru Mungu kwani Gardner ananipenda, ananitunza, anathamini familia yangu na kazi yangu.

 

Lady Jaydee akiwa na mume wake,Gardner G.Habash siku ya harusi yao zaidi ya miaka miwili iliyopita.

BC: Wasanii kama kioo cha jamii na mfano wa kuigwa (role models) mara nyingi huwa wanatarajiwa kutoa mchango wa hali na mali kwa jamii zao (giving back to their communities). Wewe kama msanii unalionaje suala hili? Are you giving back to your community?

JIDE: Ni muhimu sana kutoa kwa jamii.Si wasanii tu bali hata makampuni yanayoendesha biashara katika jamii fulani. Ni muhimu warejeshe kitu katika jamii husika. Mimi binafsi najitahidi kushiriki kwa namna mbalimbali katika kutimiza wajibu huo nikiwa kama msanii.Nafanya hivyo kwa kushiriki matamasha mbalimbali yenye muelekeo wa kusaidia wanajamii kwa mfano watoto yatima,waathirika nk.

BC: Nini mipango yako katika miaka mitano ijayo?

JIDE: Kuendelea kuimba zaidi. Nitaendelea kijibidisha katika muziki ifikie siku moja ukitaja ‘muziki wa Afrika’ basi umtaje Lady Jaydee kama ilivyo sasa kwa Miriam Makeba, Oliver Mutukuzi, Brenda Fassie n.k.

Na nikijaaliwa uwezo wa hali na fedha ningependa kuwa na Restaurant maana napenda sana kupika. Nadhani kama nisingekuwa mwana muziki labda ningekuwa mpishi.(kicheko) Mi nnapika ‘maanjam’ mpaka usipoangalia vizuri utaondoka na kidole chako…. Ndo maana bwana atoka mbweta siku hadi siku (kicheko tena).

BC: Lady JayDee asante sana kwa muda wako na mahojiano haya.Tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.

JIDE: Asanteni na nyie pia.Kila la kheri.

Pata burudani,Siku Hazigandi-Lady Jaydee.

 

Advertisements
 

82 Responses to “ONE TO ONE WITH LADY JAYDEE.”

 1. Matilda Says:

  Jide ni m2 wa kuigwa,Napenda kazi yako nakupenda jinsi ulivyo,Napenda unavyoishi na mumeo matatizoyapo ila unakoma si unajua ww ni komando?
  Jamani mtafuteni na Fina Mango mbona hamleti humu uyo dada?Celebrity fanya kazi yako.

 2. Pope Says:

  Huyu dada ana akili hata anavyojibu maswali.
  Binafsi namkubali sana tuu.
  Big Up Dadaa

 3. amina Says:

  napenda nyimbo zake lakini mwenyewe hanivutii…anafanana na kaka yake aliekufa beni wa kijitonyama hana hata uanamke…

 4. hope Says:

  nampenda sana jide sababu nyimbo zake nyingi zina ujumbe hasa kwa jamii na hata ukiangalia albamu zake zote ukizisikiliza ni kama katoa jana maana bado zinatuelimisha big up sanaaaa dada

 5. Dinah Says:

  Kabla sijasoma napenda kwanza kusema…Jide una umbile zuri la kike(unalitunza vema), unaakili,mvumilivu,hulingi(nata/kujisikia), umetulia,sio mlopokaji, unapendeza ukivaa, msafi, huna habari (hujali wasemayo wajinga-wajinga)…..kubwa kabisa unanifurahisha na ubunifu wa mavazi yako.

 6. Dume Says:

  We Amina acha maneno yako kama hakuvutii kwani amekwambia anatafuta mchumba? au anataka kugombea umiss?
  we mwenyewe ukoje kwanza?

  Jide mzuri bwana.

 7. eddie Says:

  i do lv this lady na napenda sana wimbo wake wa si wema, shes good bright and quite. namtakia mafanikio mema na jide always put god first. mwaaaahh

 8. Angelina Says:

  kazi zako nzuuuri sana.kaza buti mamaake.

 9. Ally Says:

  Kazi nzuri kuhusu akili kilamtu anzo za kumtosha mwenyewe muhim acha kuvuta bangi jide.

 10. Jabir Says:

  Kaza,buti jide,watu wanashindwa kuelewa kwamba muziki wako pamoja na wewe mwenyewe mpo Kibiashara, unajua washabiki wako wanapenda nini toka kwako kuanzia muonekano wako n.k.Unatafuta Charanga By all means hapa mjini kila mtu ana njia yake ya kuhakikisha anakula vizuri,kulala vizuri ,kuwasaidia wazee wake n.k.Wewe anakufurahisha au hawakufurahishi hiyo sii juu yake kwani at the end of the day haumpelekei mkate Nyumbani kwake. upo kwenye Biashara na Biashara ni Matangazo.Si mmemuona Richard sasa ni Milionea kwa uppuzi tu aliokuwa anaufanya BIG BROTHER wewe unafikiri kama kusingekuwa na zawadi Nono kama ile angefanya ule uchafu Big Brother.Lakini kwasababu ya pesa ndio maana watu wanakuwa machangu,majambazi,mafisadi n.k.
  Jabir

 11. MaryAnn Says:

  I like dat girl very much,,,she so cute(african qn) but i wuold like to advice her something …..acha kuvaa naked clothes coz iz not good at all…

  much love Jdee

 12. mbuche Says:

  mimi binafsi namshauri jay dee awe na web site yake ili ajitangaze zaidi kama wafanyavyo wanamuziki wengine.Nyimbo zake ni nzuri sana keep it up baby na muweke mungu mbele atakufikisha kule unakotaka.

 13. lizzie Says:

  All the best jay dee ur very stunning and talented

 14. lizzie Says:

  sipendi muziki wako but I like u personal

 15. frank Says:

  guys, tanzania tuna hazina kama hii??? i dont believe it.. tujaribuni sana the next african music queen atoke kwetu. naami huyu mtoto anaweza. nani anayeweza kupata record deal kwa jide? pls come forward we will support this talent to the end.. frank niko Japan

 16. amani Says:

  sio vibaya kufanana na kaka yako au dada yako au baba yako au mama yako au yoyote kutoka ukoo wako. ndio ubinadamu. labda angekuwa mtu kafanana na punda ana miguu minne hapo ndio ningeshituka. jide una mwili mzuri, huzeeki, hivi unakula nini??? bongo celeb muulize jd atujibu tafadhali

 17. chriss Says:

  nasikia ana majumba huko bongo kimara. michuzi giv us a photo ya crib. chriss in UK

 18. veronica Says:

  una bahati kubebwa na mumeo. kila saa mko wote. sisi wengine ni shida tu sababu wanaume wako busy na simu zao nusu saa, kama ulivoimbaga ktk ule ‘usijigaaambeee’. siri ni nini? tupe na sisi kwa njia ya mwimbo

 19. halima Says:

  hupendezi na huyo mume wetu.

 20. halima white Says:

  kumbe ray c mshamba tangu zamani. hiyo nguo ya vipi hapo juu? lol, ujage mwanza tukufundisha mwanawane

 21. mwita Says:

  bibie ana kipaji na bwana ana kipaji pia. sijui mtoto itakuwaje. hivi ni kweli kua jdee alifanya kazi ya kuuza sigara huko znz? tujulishe

 22. Lady Mere Says:

  i love the songs, whenever i hear her voice, i sit down and listen to the words, they are so true and compasionate to me..i sometimes cry, as some are too emotional…i love her personality! you go girl..waache waosha vinywa wana muda wa kupoteza wakati wee unasonga mbele! Kweli wimbo wa “siku hazigandi”umeenda kwa walengwa! I like all the albums she made, keep it ma girl, my prayers are with you!!Dont forget to put God first, thats very important.

 23. Pussycat Says:

  I like the lyrics and the beats..beats zina sound more like south african.

 24. CASHMONEYHOLLAND Says:

  MBONA KUNA WATU MNAMAHINDI MTU AKIWA ANJITAHIDI.HUYU MREMBO AMEJITAHIDI HAPO ALIPO,NA KAZI ZAKE ZINAOEKANA.SASA KAMA KAFANANA NA KAKA YAKE KUNA KOSA GANI NA NI DAMU MOJA.KUBANIANA NOMA.SEMA WATU TUNAMMAIND MJINGA ALIYE CHUKUA JIKO JUMLA….KWANI HANA NJAA HUYO MWANADADA.

 25. Jabir Says:

  Wewe Mary Ann nilishasema hapo juu kwamba huyo yupo Kibiashara na Biashara yake inalipa kwa kuvaa hivyo.Sasa unasema ….”acha kuvaa naked clothes” Biashara yeyote ni matangazo na hayo ndio matangazo yenyewe na wateja wake wanapenda mambo hayo.Ndio maana wanalipa pesa kuingia kumuona anavyoimba,anavyocheza n.k.Kwa hivyo anavyovaa hana tofauti na wale dada poa wanaozurura usiku tofauti ni kwamba ukaaji wake uchi unaonekana kukubalika na jamii kwa kisingizio cha Uanamuziki,kama ilivyo kwa Dada zetu wanaoitwa Ma Miss.Au kama ilivyo kwa stage show wa kiume kuvaa vizuri Suti n.k wakati dada zetu wanavalishwa nguo za ajabu kwa kisingizio kila kazi ina nguo zake na hizo ndio nguo mujarab kwa wao kuvaa ili kuvutia wanaume WAKWARE-MIDENDA INAWATOKA kwa kuona minenguo ya akina AISHA MADINDA n.k/Wote wapo kazini wanatafuta Pesa by All Means.
  Jabir.

 26. koku Says:

  nakufagilia sana mama maana kazi zako kwanza zimetulia na umetulia unajua unachokifanya wanaokuponda wote ni wasiopenda maendeleo yako cha muhimu usiwajali mama komaa na kazi.

  mimi binafsi nakuzimikia vibaya sana.
  koku.

 27. LWABULINDA JOSEPH Says:

  Hongera binti machozi
  kazi yako nzuri kaza buti ufikie malengo yako

 28. koku Says:

  achana nao mama nakukubali kwa kazi zako zimekwenda shule na nimependa jinsi unavyojibu maswali kweli kichwa chako kimetulia na unajua unachokifanya, ongera sana.

  ushauri wangu usifuate maneno ya watu kwani maneno ni sumu.

  koku.
  kokutangilila_k@yahoo.com

 29. Dume Says:

  Hapa sasa ndio unaweza sema kuna Hatters sio kwa yule mwehu. Na we Julie unamkazania aje huko NAmibia kwenye CAmera 25 Kamchapa mtu Finger je mko wawili na huko mbali NAmibia si atakunanihiii kabisa!!! mkoromeeni kakudhalilisheni yule sio kukazania ujinga tuuu
  sore natoka nje ya mada bwana BC ila wanakera hawa!!

  MAMA JIDEEEEE BIG UP MPWA WANGU. MTU AKIKULETEA MLETE HAPA TUMGECHE

 30. jojo Says:

  Kaza buti JIDE wote wanasema mabaya juu yako hawana lolote ni wivu unawasumbua,kuimba unafunika uzuri unao na GADNER NI WAKO vilevile watabaki hawaamini

 31. janeth Says:

  halafu watu wengine bwana!
  Hiyo ni chuki binafsi,yeye ni mimbaji kakwambia anataka kugombea u miss? asipokuvutia sura we inakuhusu nini? Ujue kuwa una makengeza vitu vizuri na vibaya hujui kutofautisha! Mi mnaniudhi!!!!!!!!!!!!!!!!!

 32. janeth Says:

  halafu watu wengine bwana!
  Hiyo ni chuki binafsi,yeye ni mimbaji kakwambia anataka kugombea u miss? asipokuvutia sura we inakuhusu nini? Ujue kuwa una makengeza vitu vizuri na vibaya hujui kutofautisha! Mi mnaniudhi!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Big up Jide. nakukubali 100%

 33. Mama Jr Says:

  She is talented..kilichowakilishwa hapa ni kipaji..na if u talk about Tz talent kwenye muziki wa kizazi kipya na historia yake Jide utamtaja..big up dada..we halima unaesema mume wenu mbona picha yako hatujaiona mkiwa wote..Wambura mama stay focussed..u’re doing great..inshaallah hollywood utafika one day.

 34. Emmy. Says:

  Pumbafu zako. Shenzy taip. We Amina umekosa cha kuandika ndo maana umeweka huo ubazazi wako. Kama kafanana na kaka yake we inakuhusu nini? We mwenyewe hapo sura lako booooovu. Hivi amina unaundugu na kima. Miguu yako ya kushoto. Utalingana na jide saa ngapi. Keep it up my sister achana na huyo sokwe anaesema huna mvuto. Kwanza hakulishi wala hakuvishi.

 35. Upendo Says:

  We amina acha mambo yako. Uanamke wake ulipo anajua Gadner. We haukuhusu.

 36. Iky babu Says:

  Oh. unaimba sana, nyimbo zako ni babu kubwa hongera sana, usikate tamaa na maneno ya watu, kwenye mafanikio yoyote hakukosi majungu.

 37. rose Says:

  Amina :mnyonge mnyogeni haki yake mpeni. hakuna mtu anapenda kuzaliwa na kasoro ambazo wengine mnaziona kama angekuwa ameiumba mwenyewe kama nguo anapopeleka kwa fundi ni sawa. kila mtu ni mfano wa mungu kwahiyo unamkosa muumba? kuswali huendi hujui kama kuna mugu? acha mambo yasiakuwa na umuhimu, gadner amemuona miss word kwake ndo maana akaamua kufunga na ndoa. wewe osha kinywa mpaka mwisho wa dunia hii huwezi kubadilisha kitu.
  Halima Mwanza: penzi ni kiti cha basi ukishuka wenzio wanakaa shida ni gani? huyo mwenye mume kweli keshafunga ndoa ingine wewe unachongaaa sana nin??????????? ACHA TABIA ZA KISHAMBA.
  Imbaa jide kila mtu na maisha yake na wala asikutishe huyo mshamba wa mwanza.

 38. Emmy[mza] Says:

  Sio vizuri kumfananisha mwenzio na ndugu yake aliekwisha aga dunia. Uwe na imani ya kibinadamu we amina hivi umesahau kuwa kila nafsi itaonja mauti. Pumbavu zako we amina. Nahisi hukuzaliwa bali ulitapikwa. Kwa kuwa ulitapikwa nafikiri hautaonja mauti. B Nyang’au wewe.

 39. renee Says:

  jide ur de best of de best.it shows itself!much love

 40. bdo Says:

  veronica Says: November 19, 2007 at 11:48 am
  una bahati kubebwa na mumeo. kila saa mko wote. sisi wengine ni shida tu sababu wanaume wako busy na simu zao nusu saa, kama ulivoimbaga ktk ule ‘usijigaaambeee’. siri ni nini? tupe na sisi kwa njia ya mwimbo

  “please vero..anyway ni maoni yako, hamchelewi kunyakua kama mwewe, big up dada yangu JD coz huwezi fanya kazi while frastruted, ikiwezekana mbane zaidi gadner for your success…@

 41. Jabir Says:

  Amembeba kwa ajili ya Picha tu,unafikiri anambeba kila siku ,Siku nyingine wanalala mzungu wa nne.Jide mwenyewe amekwambia Ugomvi zilikua zake siku nyingine huwa anajikumbusha,hawezi kuacha kabisa.Nakumbuka siku moja aliwahi kumtuma Dudu Baya akampige Dada moja klabu moja ambaye alimuhisi anamchukulia mwandani wake(Kabla Hajaolewa)-jide matata Sana.
  Jabir

 42. Grace Kombe - Arusha Says:

  Kweli ni mwanamke mwenye kipaji, fikra na uwezo…Ongeza bidii ktk kazi!

 43. Yusuph Says:

  From the day niliyoanza kumsikia Jay d nilimkubali,nakumbuka toka katika ile album ya 1 iliyojumuisha watu tofauti kama Fina,Ml Chris,Jimmy na wengine.Ukija kwenye album ya machozi ilikuwa bonge la album la Rn’B usipime.Akaja na Binti ndio kabisa istoshe ktk album ya Moto mle ndo aliuwasha moto si wa kitoto yote tisa kumi ni hii album ya shukrani yani ndio usiipimie kabisa manake kama kawaida yake hana historia ya kutoa nyimbo mbaya na kama mnunuaji wa album zake nna jeuri ya kusena hutadiriki kuforward coz kila nyimbo ni tight.Mwisho wa siku ndio maana akipeleka sokoni anauza si kitoto manake ni mkali,yuko serious na kazi yaje na anajua anafanya nini.Jay dee we mkali manake hata majina ya album zako yanaleta maana Shukrani za moto wa binti machozi.I wish 1 day nipate nafasi ya kupiga naye stori hata kwa dakika kadhaa,Jay dee eeehh we mkali,ukitaka kuamini sikilizeni wimbo wake wa NISHIKE MKONO ambao umetoka mtaamini jinsi Jay dee alivyo kmkali na ladha aliyonayo
  Am out

 44. LWABULINDA JOSEPH Says:

  JIDE NYIMBO ZAKO KWENYE VCD NITAZIPATAJE ‘ORIGINAL’ NIPO MWISHO WA RELI KIGOMA HUKU TUNAPATA FEKI

 45. glory Says:

  namkubali, sauti ina mvuto, nyimbo zina ujumbe na beats zimetulia. ila naomba kumuuliza swali akiweza anijibu. kwenye binti alisema iweje mwanaume akuzuge maisha yakuzingue kwenye shukrani kibao penzi anadai tutamkuta kaburini akikosa penzi. anaongeleaje hili?

 46. lim Says:

  Always when I look at you, i get confidence with my life.napata nguvu kwani naona wewe ni mpiganaji na unafanikiwa. i’m not mwana muziki, ila natumia motto yako kupambana na maisha yangu, and I can see the good sign,
  I real like you, I dont care about what do people say, I like u!!

 47. queen Says:

  mamaa jide unatisha.keep it up

 48. Louisa Says:

  Jide unakubalika katika jamii, kaza uzi huo huo usisikilize ya watu wasiopenda mtu apate, mtu mwema siku zote atakupa ushauri mzuri na sio kukuponda,uyo mwita asema wewe ulikuwa unauza sigara mwanza je yeye anaevaa mashati meupe na kufanya kazi benki mbona hata baiskeli hana!!!!!

 49. Kimori Says:

  One day I happened to listen and see her in a close range, when she sang a National Anthem as an openning song to one of the nights in the closure of the Business Forum abroard….I was really impressed. As the forum comprised of people from different nationalities, one of them whispered to me…, “Your National Anthem is one of the best in the world”. I think he meant also that Jide’s voice was the best!

 50. Flojoma Says:

  JAMANI MM SIJUI NIANZIE WAPI KWANZA KABISA NAMPA HONGERA SANA SWEET BABY JIDE YAANI WEWE NDIO MWANAMKE KATI YA WANAWAKE WANAOJUA KUPAMBANA. KUNAUSEMI UNASEMA HWAT PEOPLE THINK ABOUT U IS NONE OF UR BUSINESS. KWAHIYO WEWE WANYAKAZI DADA WANAOSEMA IPO SIKU WATALALA NAKUSAHAU. MM NAMPENDA SANA JIDE AMA KWA HAKIKA ANAKOGA NYOYO ZA WENGI, WE LOVE U BABY GIRL.MM NAMUUNGA MKONO ROSE KWAMBA PENZI NI KITI CHA BASI KWA HIYO WANAO BWATA WAACHE GARDINA ALIMUONA YEYEACHENI WIVU.

 51. Flojoma Says:

  JEDE MUNGU AKUBARIKI UZIDI KUNG’AAA MAMA. YAANI MM HAKUNA KANDA AMBAYO SINA ZOTE KWA SABABU NAJUA NIKIKOSA MOJA TUU NIMEKOSA VINGI . PIA KAMA KAWA DADA SIKU HAZIGANDI BIGA MZIGO MAISHA NI KARATA NA UMEWEZA KUICHEZA

 52. mashoo Says:

  wewe ni mwanamke jasiri na unajua jinsi ya kuishi,mana muziki na ndoa vyote unavimudu,hongera dada kila mara ninavyokuona napata ujasiri na kufuata mfano wa maisha yako,kujiamini na kuamua.la maana usimsahau Muumba wako na kila mara hakikisha hukai nae mbali.goodluck girl

 53. Reg Miserere Says:

  Amina; sina uhakika kama uko sawa.

  Unaweza kunishawishi kama uko sawa?

  JD…huyu ni mmoja wa ”ya kwao yamewashinda”… Achana naye…Big up!!!…

 54. norasco c.nyimbo Says:

  HUYO DADA AMINA ANA MATATIZO.HAIWEZEKANI ASEME KWAMBA HANA HATA UANAMKE.TUWE WASTAARABU MBONA KUNA WANAWAKE WAPO KAMA WANAUME ITAKUWA KUFANANA BWANA.JAY DEE KIFAA BWANA NAMZIMIA MPAKA KUFA.KWANZA WEWE AMINA TUTUMIE PICHA YAKO PENGINE WEWE NDIO HATA 2000 BORA HAUPO.KWAHEERI.

 55. Reg Miserere Says:

  Geti la Milembe Dodoma walinzi hakuna?

  Amina;

  Mlitoroka wangapi siku hiyo???

  Kama hukuwahi kutoroka milembe muombe msamaha JD na watanzania wote kwa ujumla.

  Napita tu….Baadae kidogo..

 56. Jasmine Says:

  Huyu AMINA hamumjui?? ni dada anaetafuta umaarufu kwa gharama za kipumbavu hivyo asiwaumize kichwa, kwanza mtaani kwao wanamwita jamvi la wageni!! sasa huo ndio uanamke??
  BIG UP JIDE, UR THE ONE AND ONLY FEMALE MUSICIAN IN MY HEART!!

 57. mum Says:

  Nakupenda sana DJ na napenda music wako sana tu.

  kazana kufanya kazi zako.

  wish u all the best

  mum

 58. Kakwimba Says:

  Jide u ar de best musician that’s why people keep talking’bout u.
  we never develop without people like dada Amina de ar here to challenge and to bother da wisemen/women we cant fight dem bt we can teach dem a lesson.

  Keep it up Jide.

 59. Mama wa Kichagga Says:

  JD,

  Nitakosa fadhila nisipokusemea neno! Nakupenda wewe binafsi, kazi yako na hata uvumilivu wako kwa ujumla maana mengi yalisemwa juu yako ila hukuterereka.

  Kwa harakaharaaka naweza sema Amina kakosea! Uzuri wa mtu hutofautiana toka kwa watu mbalimbali. Wengine uzuri ni nywele, wengine kifua, miguu, kiuono, macho, akili za kuchambua mambo,ukarimu, ucheshi, kipaji nk. Sasa mwanamke mwenzangu Amina JD hana hata moja hapa kwa Gardner?

  Ni ukweli usiofichika Gardener akikupima wewe na JD maksi zako ni kidogo na ndio maana akaamua kufunga naye ndoa na sio wewe. Nakushauri subiri wa kwako kuliko kukaa na kulaumu na kukosoa kwani haitakusaidia.

  – Gardner wee kiboko, na umepata kitu cha uhakika hakikisha unakipa support ili nyumba yenu iwe YA MFANO.

  PICHA YENU NZURI SANA NIMEIPENDA BIG UP ALL OF YOU

 60. Mie Says:

  –NANUKUU–
  Kwa harakaharaaka naweza sema Amina kakosea! Uzuri wa mtu hutofautiana toka kwa watu mbalimbali. Wengine uzuri ni nywele, wengine kifua, miguu, kiuono, macho, akili za kuchambua mambo,ukarimu, ucheshi, kipaji nk. Sasa mwanamke mwenzangu Amina JD hana hata moja hapa kwa Gardner?

  Ni ukweli usiofichika Gardener akikupima wewe na JD maksi zako ni kidogo na ndio maana akaamua kufunga naye ndoa na sio wewe.

  –MWISHO WA KUNUKUU–

  mama wa Kichaga una utu. I always love ur comments, inaonesha unawatendea haki wahusika

  Hakuna mwanamuziki nanayempenda kushinda JD hapa Tanzania, sio muziki wake tu, hata maisha yake amepita katika mambo magumu na amevumilia mengi, anafanya kazi kwa bidii, ananivutia jinsi alivyo na muziki wake, she is natural na pia mbona hamjazungumzia kuhusu studio yake, ana studio ya muziki inaitwa JUG.

  Sio kama wanamuziki wengine wana sifa mbaya na hawapendi kubadilika. Hata kama alifanya mabaya hapo zamani ……….kumjua sana undani, zi wapi tena nafasi?…………..kilamtu anadhambi, hakuna aliyemsafi

  Mrs Gardner wewe ni mfano wa kuigwa.

 61. mkereketwa Says:

  Mimi nasikiliza NJALO kila siku iendayo kwa mungu. Yaani hadi wazungu huku nao wanaujua siku hizi maana nikiuweka huwa nafungulia sauti hado mwisho. I like Jide sana tu. And Jide, when I come back tu TZ nitakutoa out for dinner wewe na mumeo mkiniruhusu.

 62. Mama wa Kichagga Says:

  Mie,

  Asante kwa mchango wako na uzalendo wako. Hakuna jambo zuri duniani kama KUTAMBUA MCHANGO WA MWENZIO AMA KWA KIMOMBO “appreciation”. BIG UP MAN/GAL

  KIND OF YOU! & GOOD LUCK. Tuendelee kuifanya dunia kuwa mahala pazuri pa kuishi.

 63. Mie Says:

  Thanks mama wa kichagga, i real appreciate for your kind approval. Sikukuu njema kwenu woteee! na wale waliopata bahati ya kuwa na nyimbo za JIDE ni vizuri kusiliza. kuna msg.

 64. NYUNZA Says:

  DADA JIDE,Keep it up.Naupenda saaana wimbo wako wa HARUSI.Ukweli unakipaji cha kuimba.

 65. Brenda Says:

  I lyk ur songs zimetulia..pia interview iko bomba…keep it up

 66. Suzy Says:

  Binadamu hawana jema hata kidogo, huo ni wivu usio na maendeleo…. Pia namshangaa Amina inawezekana alikuwa anampenda Gardner amechemsha huyo ni kuachana naye kabisa. Jd wee songa mbele hiyo ni bahati uliopewa na Mungu.

 67. lightness Says:

  My dear uko juu….una shine
  acha wseme tu mama Gkwani kawaida yao kujihesabia haki na kusema wengine!!!
  Ndio maisha
  Wewe ni mzuri sana kwani uzuri inategemea na kila mtu anavyo uelewa……
  Mimi nakuombea undelee kuwa juu.. kwani kila binadamu ana mapungufu, hakuna aliye kam malaika
  Kila la kheri dada mimi nakukubali sanaa

 68. Upendo Furaha Amani Says:

  Lady Jai-Dee;
  Ninakufagilia Dada yangu; Nyimbo zako zinaigusa jamii. Ukweli kwangu ni zaidi hasa wimbo huu wa SIKU HAZIGANDI unanigusa sana. Kweli kila mtu ana dhambi hakuna aliye msafi. Hata kama nikiwa katika wakati mgumu huwa naimbaga wimbo huu.
  Nakutakia kila la heri dada yangu. Mungu akuongezee, na akuwezeshe uweze songa mbele zaidi na zaidi.

 69. jomaeli Says:

  nyie mnaomtetea jide kujipendekeza tu

 70. Anna Says:

  MMh jomaeli unawivu si kitoto, kumsifia mtu sio kujipendekeza jifunze kiswahili vizuri.

  JIDE NAFAGILIA SANA NYIMBO ZAKO YANI NIKISIKIA WIMBO WAKO HATAKAMA NILIKUA NA MIHASIRA BASI NAJIKUTA NATABASAMU MWENYEWE.. BIG UP KWASANA

 71. Simon Siwango Says:

  Mwacheni Afanye muziki ye katoka, Ni tajiri sasa kwa ajili ya music. Endelea mama muziki wako uko juu…..

 72. VICTORIA Says:

  Congrats all,,for ur wedding day

 73. miss sinza Says:

  rose number 37 comment yako imenikuna wallahi

 74. zawadi Says:

  yotee mlosema mlotenda nasahau nasonga mbele mangapi ii yameswemwa magap nimeona….bg up mrs gadner

 75. Mswahilina Says:

  Dada yangu Judith Wabura,
  Wimbo wako wa siku hazigandi kweli umenigusa sana, Ninasemwa sana na niliokuwa ninawaamini, hawataki kwangu yatokee mazuri.
  Ama kweli, ninasonga mbele maana siku hazigandi.

 76. Emily Says:

  Jamani mbona huyo amina mnasema hivyo kwani si kila mtu ana haki ya kusema anavyoona na kufikiri.Hii ni nchi huru kwa watu huru.Cha zaidi mpeni nafasi amina kama anaona jide havutii amfanyie makeup basii..teh teh

 77. Evelyne Says:

  Dada Jide nakuzimii mno yaani wee acha tu, albamu zako zote ziko bomba, kaza buti dada safari bado ndefu hakuna matamu yasiyokuwa na chungu. Walimwengu kusema wamezoea wanachonga sana juu yako achana nao! wanataka umkose muumba wako achana nao!!!!!!!

  “Mliosema, mliotenda mangapi nimeona bado nasonga mbele” ujumbe huu ni kibomu tosha kwa watu kama amina. “Kila mtu anadhambi usijihesabie haki kwani hakuna aliyemsafi” amina muombe Mungu msamaha kwani umeukosoa uumbaji wake, kwani maandiko yanasema sisi sote tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu au wewe ni mpagani???????????????????????

  Big up sana dada Jide uko bomba, Gadner yuko bomba na Mungu atawajalia mtapata watoto ma miss Universy.

  Eve.

 78. abdul Says:

  i’m so love u’r work now days on side of the songs u just brings well and quite good fleva to us endelea kutupaladha zako u’r personality is sonice hivyo BIG UP MTU WANGU.

 79. Casto A. Mwinuka Says:

  I real appreciate u man. Keep it up.

 80. Casto A. Mwinuka Says:

  I want u to knw tht hakuna mwanamke ninayemfeel zaidi yako in this Bongo. Love u Jide.

 81. Tamu Says:

  u r my role mode JD
  una sauti ya kumtoa nyoka pangoni na zaidi uvaaji wako unaishi utakavyo sio watakavyo.

  u mfano wakuigwa na wanawake wote.

  keep it up Mummy
  we all support u

 82. anonymas Says:

  Mimi binafasi namfagilia sana huyu binti na ni mshabiki wake mkubwa na kila anapotoa album huwa nahakikisha napata copy yake kwasababu huwa anaumiza kichwa chake kutunga mashairi ambayo mara nyingi huwa yanabeba ujumbe mzito pongezi kwa hilo pili nimekuwa niki m-admire huyu binti alivo na msimamo katika maisha yake amekuwa akizungumzwa vbaya mara nyingi na vyombo vya habari na watu wanaodai ni wakaribu na yeye. Cha ajabu haonyeshi kutetereka amekuwa akitete kwa nguvu zote ndoa na fani yake Pia Garner hongera mkeo ulie nae ni mtulivu mwenye kpaji na anaejiheshimu sana kulinganisha na umri wake mwisho bc mtuwekee picha ya nyumba ya nguli huyu kwa mtandao aweze kuwapa changamoto vjana wenzakee


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s