Msanii kutoka Mombasa-kenya Mwanaisha Abdallah Mohamed a.k.a Nyota Ndogo alipowarusha wabongo na kibao chake kilichotokea kupendwa na kutamba sana kiitwacho Watu na Viatu (bonyeza hapo kuangalia video ya wimbo huo) ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza,jijini Dar hivi karibuni. Nyota ndogo katika wimbo wake huo anasema duniani kuna watu na viatu,kuna watu wana roho mbaya sana,waepuke.Ni kweli?Ukiitazama vizuri picha hii unaweza kuona sura za baadhi ya bongo celebrities.Unaweza kuwatambua?
Advertisements
Mimi nimemtambua bwana CREW 🙂
Hii picha imetoka vema sana….kama sio Bongo vile.
keep up girl
hata mimi nimemtambua celebrity mmoja..anaitwa Dinah.
Yule kuleeee mwisho kavaa nguo…nooo nakutania m2 wangu….
Nampenda sana Nyota ndogo hasa baada ya kubahatika kusikiliza mahojiano yake mwaka 2002, aliyofanya na mtangazaji Godwin Gondwe aliyekuwa anatangaza Radio One stereo, kuhusu historia ya maisha yake.
Kapitia kwingi sana ukijumuisha alishawahi kuajiriwa kama “housegirl” na akiwa na majukumu mengi na changamoto alizopitia.
Nilimpenda jinsi alivyokuwa muwazi tofauti na baadhi ya wasanii wakiwa wanahojiwa na niwatu wa kupiga changa la macho tu.wengine wanaandikiwa mashairi hata kuwashukuru waliowaandikia wanakilia kujisifu tu.
Mwingine ni binti msanii maaarufu alikuwa na ugomvi na waandishi kuhusu umri wake.Ila naona siku hizi kaamua kuweka umri wake hadharani sijui kaamua kuguess au kashauriwa atachangua ANA ANA DO kupata umri wake…
Al in al ..hongera NYOTA NDOGO ambayo leo hii inatoa nuru kubwa kuangaza ka jua.
Wasalaaam…
Dinah na wadau wengine wa BC.
Mnaonaje ilo vazi la Nyota Ndogo..plz comment nikusikie..nimetumia lugha ya malkia kuweka msisitizo
Kavaa vizuri na bado anavutia,tofauti na watu wengine wanafikiri kukaa nusu uchi ndio kuvutia watazamaji.bado anaweza kuhifadhi sehemu nyeti za mwili wako na bado watu watakupenda.Watu wanachotaka ni mziki wako,je ni mzuri,unachezeka,wanapata ujumbe. ni hayo tu.
John
‘WATU NA VIATU’ Ni wimbo bora kwangu
umesheheni hekima tupu natambua mchango wako kwa jamii. Nakutakia mafanikio katika maisha yako keep it up baby
mmh! mbona hao wote wa mbele ni watoto wa joseph kusaga??? clouds members,check wanavyojishaua vimbelefront hovyooooooooooh!