BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MCHUMI, PROF.IBRAHIM LIPUMBA December, 3, 2007

Filed under: Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Ukiongelea wanasiasa wenye taaluma zinazoeleweka nchini Tanzania,sio ajabu mojawapo ya majina yako ya mwanzo mwanzo litakuwepo la Profesa Ibrahim H.Lipumba.(pichani). Lipumba ni Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama Cha Wananchi,CUF.

Alizaliwa tarehe 6 Juni mwaka 1952 katika kijiji cha Ilolangulu,wilaya ya Tabora Vijijini mkoani Tabora,Tanzania. Alianza elimu yake ya msingi (1959-1962) katika shule ya msingi ya Swedish Free Mission Primary School huko Sikonge Tabora. Kuanzia mwaka 1962 mpaka 1966 alikuwa L.A Upper Primary School huko huko Sikonge,Tabora.

Baadaye aliendelea na masomo ya sekondari (1967-1970)-Tabora Boys Secondary School na baadaye (1971-1972) Pugu Secondary School. Mwaka 1973-1976 alikuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam ambapo alipata Shahada ya kwanza (BA Economics). Mwaka 1976-1978 alikuwa tena Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kwa ajili ya Shahada ya pili (MA Economics).Baadaye alielekea Stanford University nchini Marekani (1978-1983) alikosomea Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) kwenye masuala hay ohayo ya Uchumi.

Hii ndio inayomfanya Lipumba kuwa mmojawapo wa wachumi wanaoheshimika barani Afrika kama sio ulimwenguni. Kwa habari zaidi juu Profesa Ibrahim Lipumba na habari za uzoefu wake katika uongozi,nafasi za kazi alizowahi kushikilia,heshima za kitaaluma alizonazo, shughuli za kimataifa alizowahi kufanya nk bonyenza hapa. CV yake unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa.

Picha na Kassim Mbarouk.

Advertisements
 

35 Responses to “MCHUMI, PROF.IBRAHIM LIPUMBA”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Tuachane na politiki…ukweli jamaaa kichwa…CV yake respect….sio hao wengine wasanii tu masela tu…na misemo kila siku.

  Kigumu chama chochote …kigumuuu…

 2. Nerra Says:

  Mdini!

 3. Kamanzi Says:

  si kweli lipumba hana udini katu na kama dunia inatucheka leo ni kwasababu hatujaweza bado kuwatumia maprofesa nguli yaani lipumba na mwandyosa. hao akina wangwe na wengineo hapo udsm ni feki tu

 4. Dinah Says:

  Naona sasa BC mnatafuta namna ya kutuumbua……CV ya Lipumba inatia hasira ukilinganisha na ya “Mzee wa Vita”.

  Is it possible kupata ya Kingunge na Ex-Spika wa Bunge bwana Msekwa oh ei na Lowasa 🙂

 5. Chako Bikoz Says:

  Hawa jamaa wanakuga na CV na Elimu za juu sana lakini kwani huyu jamaa kashafanya nini cha maana wajomba..? mchonga hakuwa na CV kali hivi lakini mavitu yake wote tunayajua, hivyo akina Karume,Mandela na wafanya kweli wengine. Hizi elimu za darasani sidhani kama huwa zinaleta mabadiriko yoyote wajomba au mnasemaje..?

 6. kijana Says:

  Chako acha kabisa ,usizungumze vibaya kuhusu hiki kichwa ,ukweli jamaa ni kichwa sana alichokosea ni kuingia kwenye siasa baada y akuona hawamtumii,ila kama unakumbukumbu safi unafahamu alichokifanya uganda kwenye uchumi,
  Its ama man with full of comfidence and now he is in UN

 7. Miss S. Says:

  Nerra mbona hutoi maelezo ya udini wa Lipumba? Au unataka ku-prove kuwa Weusi ni mbumbumbu kama Watson alivyoripoti kwamba hatuna uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo?

 8. Kimori Says:

  SOCIALISM:
  You have 2 cows and you give one to your neighbor.

  COMMUNISM:
  You have 2 cows; the Government takes both and gives you some milk.

  FASCISM:
  You have 2 cows; the Government takes both and sells you some milk.

  NAZISM:
  You have 2 cows; The Government takes both and shoots you.

  BUREAUCRATISM:
  You have 2 cows; the Government takes both, shoots one, milks the other and pour the milk away…

  TRADITIONAL CAPITALISM:
  You have two cows. You sell one and buy a bull. Your herd multiplies, and
  the economy grows. You sell them and retire on the income.

  AN AMERICAN CORPORATION:
  You have two cows. You sell one, and force the other to produce the milk of
  four cows. Later, you hire a consultant to analyze why the cow dropped dead.

  FRENCH CORPORATION
  You have two cows. You go on strike because you want three cows.

  A JAPANESE CORPORATION:
  You have two cows. You redesign them so they are one-tenth the size of an
  ordinary cow and produce twenty times the milk. You then create a clever cow
  cartoon image called Cowkimon and market them World-Wide.

  A GERMAN CORPORATION:
  You have two cows. You reengineer them so they live for 100 years, eat once a month, and milk themselves.

  AN ITALIAN CORPORATION:
  You have two cows, but you don’t know where they are. You break for lunch.

  A RUSSIAN CORPORATION:
  You have two cows. You count them and learn you have five cows. You count them again and learn you have 42 cows. You count them again and learn you have 2 cows. You stop counting cows and open another bottle of vodka.

  A SWISS CORPORATION:
  You have 5000 cows, none of which belong to you. You charge others for storing them.

  A CHINESE CORPORATION:
  You have two cows. You have 300 people milking them. You claim full employment, high bovine productivity, and arrest the newsman who reported the numbers.

  AN INDIAN CORPORATION:
  You have two cows. You worship them.

  A BRITISH CORPORATION:
  You have two cows. Both are mad.

  A TANZANIA ECONOMY
  You have two cows; you eat them all and beg for one cow.

 9. Subira Says:

  Watu wengine bwana mtu akiwa Mwislamu tu basi mdini wakiulizwa walete evidence za udini wake kimya. Haya sasa tuna interest na hilo suala la udini wengine tunafanya research hizo data zianweza kutusaidia angalau kwa kidogo tu tumejua kumbe tuhuma nyingi ni STEREOTYPES.
  Siasa inatupotezea wataalamu wetu wengi tu ambao wanakuwa hawatumiki ipasavyo, sitaki kutaja vichwa vingine vilivyokimbia Universities kufata siasa au ulaji.
  Na sipendi siasa kwa sababu hiyo tu, ona sasa wanafunzi wa economics wamekosa mwalimu mzuri bila sababu ya msingi pengine na yeye Prof. Lipumba angetupatia wachumi wengine wazuri kuliko yeye ambao ni wanafunzi wake kama angebaki kwenye academic field.

 10. shuwaini Says:

  he is bright and handsome, huwezi mfananisha na Mkapa, mkapa anatishia watoto mtaani.

 11. gasto Says:

  Weee Neera wajibu sasa wananchi hao wanataka ushahidi wa udini wa lipumba uliosoma,usipende kuropoka kwa vitu ulivyokuwa huna ushahidi navyo, shauri yako ipo siku utakuja kuadhirika kwa kuropoka kwako.

 12. Dinah Says:

  Kumbe Lipumba nae handsome? Hahahaha kweli uzuri uko machoni mwa mtazamaji….mwee!

 13. Mchangiaji Says:

  Hizi ndio taratibu na serikali finyu za kitanzania aka Nyerere/Mkapa/Kikwete ,

  Wachumi kutupiliwa mbali, na kuanza kunyanyaswa na serikali zetu, zisizo na fikira na ufanisi.

  Huyu nina uhakika akitua ukerewe, hatoki, lakini masikini tamaa kaweka nyuma. Ali mradi is ahead ya maendeleo ya Tanzania.

  Mpaka tutakapo retain na kuwaenzi wachumi na washauri wetu, ndio tutaanza kuendelea, na hiyo sijui lini ????

  Bongo Celebrity, twakuombeeni mutupe mjadala na fikira za kiuchumi alizotoa professor kwa kuendeleza uchumi wetu Tanzania.

  by Mchangiaji

 14. Mkuu Kimori,
  Nimekubali analysis zako.Mimi huwa najiuliza iweje mhitimu wa shahada ya chuo kikuu,asema hana ajira.

  Somo la Entreprenuership kasoma la nini chuoni?

 15. Mchangiaji,
  Ni vema sana fikira za watu kama Prof Lipumba wanatumia wazungu kuendeleza nchi zao.

  Ni vizuri fikira za watu kama Prof Lipumba zianze kufundishwa mashuleni.

 16. TanzanianDream Says:

  Hehehe wacha niskip maana mada comment zinaweza fika 100 hapa nikiweka shule moja tu…..

 17. shuwaini Says:

  yeap, he is handsome compared to Mkapa and you dina, wakiitwa wazuri huwezi simama!

 18. Matty Says:

  Jamani huyu mchumi yuko bomba wapi???sorry mimi sioni vizuri kama Dina, mbona nasikia bongo handsome ni Jk is it true???

 19. Reg Miserere Says:

  Matty;

  waongo hao mbona hata wewe mwenyewe hsome???

 20. Matty Says:

  Sorry, Reg Miserere mimi si mwanaume hivyo siwezi kuwa handsome pls mimi ni msichana labda uniambie ni beautiful girl nitaleta na mimi picha yangu uone ninavyokimbiza mitaa ya kati.

 21. mabig Says:

  he is handsome, kwa vigezo vya uanaume. watz hatujui mahandsome wakoje, mnaangalia wanaume waliofanana na mama zao ndo mwawaita handsome, hao wala si wazuri na wengi wao ni magay. Kumradhi, JK ana sura ya kigay na hawezi wekwa kwenye list ya handsome, labda huko kijijini kwao Goba. hahahaha!

 22. any Says:

  JK, hihiiiii!

 23. kazuba Says:

  huyo namuamini katika uchumi lakini tanzania ni lazima imtumie wasomi kama hao .

 24. UE Says:

  Tumetawaliwa na sera feki za hawa sisiemu ambazo zinatufanya tuamini kuwa ili tupate maendeleo ni lazima tuichague hiyo na hakuna mwenye uwezo wa kuibadilisha nchi hii asipotoka sisiemu. Hiyo si kweli,mtu kama Kingunge mpaka siku ashindwe kutembea ndio aachie madaraka. Wazee wengi wa sisiemu walioko kwenye system hawana mitazamo mipya, wamezoea kufanya kile walichozoe kukifanya toka miaka hiyo ya 1960’s mpaka leo, tuwaweke pembeni for only 5 yrs halafu tuweke vifaa vipya kama huyu mtaalam then utaona hao waliozoe kula kodi zetu kwa kuishi masaki na kujijazia pdm kila siku kama hawataamka. Lets learn frm our ngrbs kenya!!!

 25. Majita Says:

  Wakati wa utawala wa Mwinyi ni wakati ambao thamani ya hela ya Tanzania ilishuka sana na kati ya vipindi ambapo uchumi uliporomoka kwa kasi ya ajabu.UZURI na UBAYA wa hoja hii ni kuwa ni huyu huyu Pro.Lipumba aliyekuwa mshauri wa Mwinyi wa mambo ya Uchumi.

  Kwa mnao hoji kuhusu handsome ni kweli kwani yeye ni handsome mwenye mwanya wa meno ya chini.Hata hivyo mimi ma-handsome ninaowajua Tanzania ni yule masoud Masoud (Mnamkumbuka wadau??) na Dr. Remmy Ongara.

  Dinnah siku hizi umekuwa mtoto mzuri sana.Zamani ulikuwa unajibu kwa jazba kwelikweli.Nakupa shavu na wewe nipe ulimi

 26. mummy Says:

  huyo Dinah naye kambe mbea tu.

 27. any Says:

  Mbea, mshamba na mpenda ngono, nenda kwenye blog yake utaona anavoongea pumba.

 28. chenga15 Says:

  kimori nakubali falsafa zako m2 wangu,ila lipumba cv yake inatisha lkini hayo ni darasani tu.

 29. Jane Says:

  Mnaomsema Lipumba vibaya mna lenu tofauti lingineeeeeee! Jamaa anatumiwa Ulaya kuwanufaisha wazungu, nyie mtabaki Tanzania masikini, mtumieni jamaa, kichwa hicho.

 30. Mtoto wa Kingoni Says:

  Ndugu zangu, mi nawashangaa sana wale wanaotaka kuhusisha moja kwa moja uprofesa wa huyu bwana na uwezo wake wa kutukwamua watanzani kiuchumi. Kitu ambacho hamkielewi ni kwamba siasa na taaluma ya uchumi ni vitu tofauti sana hasa kama unaziongelea nchi zetu hizi za kimasikini. Kwa muono wangu huyu mtu ni mbinafsi kama kweli anauchungu na watanzania ni vema angebaki Mlimani ajenge kizazi kipya kitakacho weza kuukabili uchumi wa sasa. Maacademicians hawafai kuwa wanasiasa wanatuchanganya na wanajichanganya wenyewe. Siasa hazitaki absolute truth while Taaluma inataka Absolute truth. Si mnaona akina mwandosya, Baregu na wengine wengi wanavyodhalilisha taaluma? Watanzania tukitaka tuendelea tufanye kazi tuache usanii na kusingizia watu. Sifa kubwa ya masikini ni kulaumu sana kuliko kutumia opportunities zilizopo. Shauri yenu mtakufa njaa.

 31. walikh Says:

  Mnacheza, kuna watu wamesoma kuliko yeye huku Ulaya na USA, wala si mkali kama mnavyodhani ndo maana alipoenda USA aliambiwa hawezi kuanza PhD moja kwa moja mpaka afanye Master ingine kwanza, hawezi kusaidia nchi yoyote ya Western na hiyo elimu yake kwa kutoa ushauri kwa maendeleo ya nchi zao sana sana anaweza kupata kazi ya kufundisha undergraduates as a cheap labour, hana lolote, na kuwa rais wa nchi is not a professional job wala hahitaji mtu kuwa msomi wa hali ya juu as all stuffs are being done by other dudes not the president themselves, also nchi nyingi zenye marais waliosoma sana kama mnavyowaita nyinyi wenyewe hasa wa falsafa ya uchumi huwa zinaanguka kiuchumi as most of them are keeping on tryng to implement what economis books says, in reality that is not the way to do things.

 32. KILUNDUMYA ATHUMANI Says:

  KWELI UNATISHA MKUBWA LAKINI KUMBUKA HATA KUWA NA NYUMBA KWENU,UNATIA AIBU WENZIO WANAKUMBUKA KWA KAKA

 33. paku Says:

  tumeona cv ya Prof Lipumba, tunaomba cv ya mgosi makamba maana anajifanya mtu wa dini sana


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s