BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UNAISHAURI NINI KAMATI YA MISS TANZANIA? December, 5, 2007

Filed under: Fashion,Mahusiano/Jamii,Miss Tanzania,Tanzania/Zanzibar,Urembo — bongocelebrity @ 11:59 AM

 

Pichani ni kamati ya Miss Tanzania ambayo kila mwaka ina jukumu la kuratibu zoezi zima la kumsaka Mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) ambaye huwa ndio mwakilishi wetu katika mashindano ya urembo ya dunia (Miss World) kama haya yaliyomalizika hivi karibuni.

Katika kufuatilia maoni mbalimbali kutoka kwa wasomaji na watembeleaji wetu, ni wazi kwamba wengi mnaamini kwamba yanahitajika marekebisho fulani fulani katika zoezi zima la kumtafuta mrembo wa Tanzania ili kuongeza ushindani katika mashindano ya dunia. Kwa kuzingatia hilo na katika kuitikia maoni ya baadhi yenu,tumeona ni vizuri kama tukawa na kamjadala kidogo kuhusu suala hili.

Bila kuonyesha dharau,kebehi,kashfa,uzushi na bila kuongelea habari binafsi za watu (hapa sio sehemu yake) wala kuleta hoja zisizojenga wala kusaidia kitu chochote,tunakukaribisha kutoa maoni yako.Unashauri nini kifanyike ili kuboresha mashindano hayo?Una ushauri gani kwa kamati ya Miss Tanzania? Kwa nini unadhani mpaka hivi leo bado warembo wetu (kasoro Nancy Sumary mwaka 2005) wanaishia kuwa wasindikizaji na sio washindani? Toa maoni yako.

Maelezo ya Picha:Kutoka kushoto ni Jason Tall (Secretariate member), Prashant Patel (Mwenyekiti wa Kamati) Hashim Lundenga (Mratibu Mkuu na Mkurugenzi wa kampuni ya Lino inayoandaa Miss Tanzania), Dr. Ramesh Shah (mratibu wa majaji) Aidan Ricco (Afisa Habari) na Makoye (Mkuu wa Itifaki)

BC iliwahi kufanya mahojiano ya Hashim Lundenga,Mratibu Mkuu wa kamati ya Miss Tanzania.Unaweza kuyasoma mahojiano hayo kwa kubonyeza hapa.

Picha kwa hisani ya Muhidin Issa Michuzi.

Advertisements
 

46 Responses to “UNAISHAURI NINI KAMATI YA MISS TANZANIA?”

 1. TanzanianDream Says:

  Ivunjwe na lianzishwe shirikisho la Miss Tanzania uongozi uwe chini ya Wizara sio chini ya mtu binafsi kama kampuni yake……..Nimesahau vitu vingine muhimu mtaongezea ila huu ni mtazamo tu…………PERIOD

 2. Karim Says:

  Cha kwanza kabisa ninachokiona hapo ni mfumo dume.Kamati ya Miss Tanzania…wanakamati wote wanaume!Hapo tupu nadhani panakuwa na tatizo kubwa la kijamii.Lazima waingize mwanamke kwenye kamati ili alinde maslahi ya wanawake.

  Kingine ni lazima kuwe na transparency(uwazi) zaidi katika utendaji wao kwani wanafanya kitu cha kitaifa.Wanapata faida kiasi gani?wadhamini wanawapa masharti gani nk.

 3. Tonni Says:

  Karim, nakubaliana na wewe, hasa kuhusu maslahi ya wanawake, mahitaji mengi sana ambayo wanawake wanayaitaji wanaumne wanaweza wasitilie maanani. Kingine ambacho naona ni muhimu zaidi lazima waangalie pia maslahi ya contenstants, sio kuwaacha tu pindi wanapochaguliwa kama miss Tanzania na kwenda kugombania miss word, lazima wawape ajira, na kuwaaendeleza na talents zao kwani contestants wameingiza pesa katika kamati by participating. Lazima wawe responsible for their careers, especially winners.

 4. Dinah Says:

  Naungana na nyote hapo juu na ninapenda kuongeza kwa yeyote watakao take over uendeshaji wa kumpata MissTz kuwa utaratibu wa kumsaka mwakilishi ubadilishwe na usitegemee zaidi Majaji, nikiwa na maana toka ngazi ya kata mapaka kufikia ngazi ya Taifa Wananchi washirikishwe kwa karibu kwani Miss huyo haiwakilishi Kamati/Kampuni yake bali Taifa ambalo ni wananchi.

  Waache ubinafsi na hivyo kupata mshindi halali atakae kubalika kwa wananchi (Kitaifa) bila kuzua mzozo kama huyu aliyepita.

  Kuwe na utaratibu wa kuwa-fund washiriki ktk swala zima la mavazi, urembo (utunzajiwa ngozi, nywele, kucha n.k.) na sio kuwaachia mzigo huo binti hawa wadogo ambao wengi wao ndio kwanza wamemaliza shule au bado wako shuleni(hawana kipato).

  Washiriki (from kata -taifa) wale wasio na uwezo wa kifedha waandaliwe utaratibu wa kujiendeleza kielimu mara baada ya kushiriki.

  Watafute mkalimani(I’m available) ili MissTz ajieleze kwa Lugha yake ambayo itamfanya ajiamini zaidi kuliko kutumia Lugha ya kigeni…..tuige ncho nyingine kama China, Korea, Spain, Chile n.k.

  Naja….

 5. TanzanianDream Says:

  Heheh lkn dada zetu nyie ndo mna kasumba ya lugha…watu wengine Lugha ney lkn anataka aongee hivyo hivyo The Guardian yenyewe hawasomi maskini mwisho wanaishia kuomba maji walainishe makoo…

  However mi siangalii hili la Umiss tu ila kusema ukweli kama mtu anatoka nje ya nchi akipata nafasi ya kufanya mahojiano na media akiongea lugha yake anawakilisha sana sema wenyewe hamjui tu mnabaki kutafuta maneno muda wote kwa lugha ya watu….

  Nway kwa hawa mamiss mi naona hii michezo pia wanatakiwa waangaliwe vizuri japo mivigha haikuwepo enzi zetu lkn bado tulicheza vya kutosha…Fanyeni mbinu waweze kuwa na vipaji vingine vinavyoonekana…..

  NB:Dinah Unaniangusha ni Nchi sio Ncho bwana….Pamoja

 6. Edwin Ndaki Says:

  Hapa BC ndio nilikuwa napasubiri.

  Ngoja nilale kwanza maana saa hizi nite kali maboksi yamenichosha…Asubuhi ninao hao KAMATI YA MISTAZI TANZANIA inayojishughulisha na mambo MISS TANZANIA…

  Kushiriki washiriki wanawake…kamati yoooooooote hata wapamba stage VIDUME…oneni aibu mambo mengene DUNIA YA USAWA Ndega

 7. Edwin Ndaki Says:

  Nalala kidogo nikiamka kesho tu nina nyinyi ze kamati nimwage LECTA najua mnasoma tu BC…

  badaye…chwaaaaaaaaaaaaaaaaaap

 8. Senyandumi Says:

  Mie nilishatoa maoni yangu kabla sijaingia katika BC kule kwa Haki-ngowi,nilisema kwamba kwa vile tumeendelea kuwa wasindikizaji ni bora tukajitoa ili katika mashindano ya dunia tukabaki tunawania umiss Tz tu huku tukijifunza kwanini wenzetu kama Angola wanafanya vizuri mara mbili mfulurizo!?Pia tujikite katika BBA ambako tumekua tukifanya vizuri,sasa miss Tz ajue kuwa next time hakuna kwenda sanya apelekwe MNET aingie katika BBA.Tumechoka kuwa Wadosi sasa.

 9. keso Says:

  Ushauri mmoja tu labda ningesema, inabidi govn’t iangalie vizuri hii issue ya Miss Tanzania. kwa kweli ni pesa nyingi sana tunazilipa kwenda kuona haya mashindano. Hizi pesa zinatumiwaje kusaidia hawa wanao participate?? Kingine ni muhimu sana kama wengine wanavyosema hapo juu, mwanamke anaitajika, kwani warembo wooooote wanakuwa ni wanawake, atleast awekwe mwanamke hata mmoja.. by the way hii kamati imeshakaa hapa kwa muda gani????

 10. Mabig Says:

  Mkalimani mwenyewe kingereza nei, kwani kozi ya kingereza ulimaliza baada ya kwenda likizo ya kunyonyesha dinah, haaaaaaaaaaaaaaaaa. kingereza nawewe umo, sikujua

 11. kijana Says:

  kamati yenyewe ndo hiyo ,inaonyesha kabisa kuwa na sura za kutamani,yatupasa kujua kuwa pia ushiriki wa ma miss sio kuangalia luga tu ila kwa kuwa watu huwa wana tamaa zao na interest zao bas visingizio huwa ni vingi sana hapo ,mie nashauri kuwa kwanza lundenga apigwe chini na kamati yake yote ili wachangue kamati iliosafi na yenye maadili.
  Hamuoni aibu kuwa mashindano yeyenywe ni ya akina dada lakini kamati yenyewe ni waunaume watupu?waungwana kwa mtazamo wenu nyie mnapata picha gani
  Wamejichangua wenyewe ili wafichane siri zao sio so yatupasa kuamka na kukemea hili

 12. Kekue Says:

  He!! Hivi kamati yenyewe ndo hii???? Uuuuuuwiiiiiiii!!! Jameni ili muonekane watu wastaaarabu ebu fanyeni kujiuzulu alafu iundwe kamati nyengine. Unajua wenzetu unapokabidhiwa kitu kifanyie kazi ukishindwa unajiuzulu tena bila kuambiwa lakini wakina sisi du !!!!!!!!! Hivi kwa nini??? WHYYYYYYYYYY!! We are tired of you Lundenga n your felow.

 13. tanwira Says:

  kwanza namshukuru mungu kwa alie gundua na kuwekea nafasi hii ya comment ila mimi kwa muonekano wangu sishauri kitendo kizima eti kamati ibomolewe ila tuu utaratibu na kanuni nyingine zibadilishwe kwani wanaweza badilishwa watu ila kanuni zikawa ni zile zile na ikwawa ni ujinga la msingi tu chakwanza ni lugha ijapokuwa watu hatuoni umuhimu wa kusoma kugha ila kwa kujiuliza ni lugha zipi ni yakwanza kiamataifa lafu kitaifa ya kwanza ni kingereza kwahio mamiss wanaokuwa wanataka kujiunga na umiss lazima kwanza wajue lugha hio kwani wanapoenda kushiriki ugenini inajulikana lugha ni moja wanayouliziwa maswali na kuwasiliana na wenza wao hata miss china hajaongea kichina aliongea lugha ambao wote mtaelewa nini anaulizwa ukija ndani ya nchi iwe kiswahili kinatumika kama semi judgment kuwauliza maswali alafu final waulizwe kwa lugha hio ila ni vizuri ndani ya nchi wakatumia lugha ya kiswahili kama tayari mnawafanyia interview mshajua wanajua lugha basi mjue wanao uwezo wa kuongea,na iwepo taratibu wanapokuwepo kambini basi wawe wanatumia kingereza kama lugha ya mawasilianio ili wapate uzoefu kwani wananchi tujiulize kwanini iliwekwa lugha ya kimataifa ili iwe rahisi kuwasiliana na lugha ya kitaifa namanisha nchi ili iwe rahisi kuwasiliana mnaopinga kingereza inabidi tujiulize je hio ndio silaha ya mtu ashinde kama ni mtanzania lazima atajua kiswahili basi awe na ari ya kujifunza lugha ya pili kwa jili ya kimataifa….
  na la mwisho naomba kwenye kamati nzima ya umiss wawepo na viongozi wanawake huo ni urembo kwanini wanaume wawe wengi na ndio mana mamiss wengi wanajihusisha kimapenzi ili wapate nafasi ya kushinda lakini watakapokuwapo watendaji wanawake ni vema pia na iundwe tume ya kurekebisha tabia baina ya viongozi na wandaaji kwani itasaidiwa kukomesha tabia chafuu zinazojitokeza.binadamu ni kama coin inapande mbili mwenge na kichwa mana anatabia mbili chanya na hasi mtakuwa mmenielewa mikitoa lundega usitegee atakae kaa hapo atakuwa mzuri tuuuu

 14. Igembensabo! Says:

  Eti LINO INTERNATIONAL hivi hiyo kampuni ina kitu gani siwapendi hao waandaaji wa MISS TZ kwani wana mfumo dume na wako kwa ajili ya kuwadhalilisha mabinti zetu…

 15. Jamani ili tuwe makini na swala hili,ni vizuri kushirikiana mawazo na wadau wengine kwa mfano waandaaji wa bongo star search.(Huo ni mfano mmoja tu local na may be uchaguzi wa mshindi wa BBA-Mbona hao wakienda huko wan-compete kwa kishindo?)Vitu vingine vipo wazi tu kwa mfano, ni vema ‘kamati kuu’ya Miss Tanzania ikasisitizwa kuwa na element ya jinsia ya kike pia.Na pia ni vizuri pia kamati husika ikasoma na kuelewa nini maana ya Beauty Pegeant,halafu wakaitengeneza kwa muonekano wa kitanzania bila kusahau somo la exposure kwa makini sana kwa huyo atakaye-winn ili kumtayarisha vizuri kupambana kimataifa.Ubinafsi wa aina yeyote upigwe vita kabisa nikimaanisha kuwa kama majaji watasema hayupo anayeweza kuiwakilisha Tz ktk washiriki waliochaguliwa basi hilo lizingatiwe. Maana yake ni vizuri International judge/s washirikishwe tangu ngazi ya kanda/mikoa (hadi tutakapofahamu vizuri ni jinsi gani tufanye mchujo)Ni hayo tu kwa sasa asante sana.

 16. Mirry Says:

  WATU WENGI WALIO MSUPPORT HUYO DADA KWENDA KWENYE HAYO MASHINDANO WALIFANYAKOSA SANA KWA MTU ASIYENAVIWANGO HATA VYA MISS KARIAKOO (ALIKOTOKA)MIMI BINAFSI HATA MISS KATA NISINGEMPAKA HATA KAMA NINGEPEWA HONGO.
  MMECHANGIA KUMUAIBISHA DADA WA WATU MASIKINI WAKATI MLIJUA KABISA ANA NAFASI YOYOTE KULE HATA ROUND YA KWANZA WALIMPENDELEA INGEKUWA MIMI HATA ROOM ASINGE CHECK IN NINGEMRUDISHA NCHINI KWAO NINGEONA NCHI YAKE WAMEFANYA UTANI KWAMBA HAWAKUWA SERIOUS NA USHINDANI
  TAIFA LETU LIMEPATA AIBU MTAFANYA WATU WAFIKIRIE SISI WATANZANIA WOTE WANAWAKE TUKO HIVYO HIVYO WAKATI MIMI DU MKINIUDHI NITATUMA PICHA YANGUUU HAPA MNIONE NILIVYO BOMBA ANYWAY NATANIA BWANA ILA PLS KAMATI KUWENI SERIOUS HIKI NI KITU CHA WANANCHI NA TAIFA ZIMA

 17. maya65 Says:

  Hii kamati ivunjwe na jukumu la kuchagua mamiss likabidhiwe kwa wizara ya utamaduni na michezo, mimi sioni mantiki yoyote kwa hao wanaume sita eti watupangie nani wa kuwa miss Tanzania….Hebu angalieni upuuzi walioufanya kwenda kutuchagulia miss ambaye hakuwa hata na sifa za umiss na aliyewahi kushindwa huko nyuma,wao walidhani waamuzi wa miss world kule china ni pumba kama wao na matokea yake wameyaona…..huyo miss wao hakuwamo hata katika ishirini bora za mwanzo…wapuuzi nyie!!!!!!

 18. Mwananchi Says:

  Kikubwa hapo ni waingize wanawake wawili ili kupata mtazamo mzuri zaidi. ikiwezekana wachukue hawa mamiss wa zamani kama Hoyce ili kutumia uzoefu wao vizuri

 19. msemakweli Says:

  Mie watz mnanishangaza sana!!!! watu mnawabania watoto wenu,dada zenu,Ma girlfriends wenu mkihishi wakishiki mtawapoteza!!Ndio maana Rais mmoja mstaafu alishawahi kuwashangaa waandishi wa habarina kuambia” YAANI NDIO MNAJUA HABARI HII LEO,NYIE WATU WA AJABU KABISA” Akionyeshwa kukerwa na tabia za kizushi zushi za watz. hata mie najisikia hivyo sasa hivi na suala zima la MISSTZ. kwanza Jamii nzima ibadilike ijue Urembo ni ” industry” kama zingine,Ile perception kila mtu anafirikia kila dada atakayeshiriki MissTZ anakuwa anausishwa na ngono,Ikome Kabisaa!! Ili hivyo “vi YES/NO” viache kuwa “skeptical” then Things will change from there,Lakini tukisubiri msichana fulani akashawishiwa na scouting team ta MissTZ,mtu huyo atabebwa mpaka atakuwa missTz, Vodacom na kamati ya MissTz wanatumia muda na fedha nyingi kuwaandaa hao washikiri,lakini matokeo yake huwa tunayoona pale pale jukwaani,mtu anashindwa kueleza kitu gani kinapatikana kutoka mkoani kwake!!! Ni aibu!!! tukitembea mjini na sehemu mbalimabali tunaona watu wenye vigezo lakini nasikia wanakatazwa kushiri!! na wazazi wao,”viboyfriends” uchwara bcoz hamjiamini au hamuwamini hao mlionao, it is sign of weakeness for most of Tz men,so who will be offended i dont care and i dont mind.Hapo kuna tatizo!!! ambalo kamati ya MissTZ inabebeshwa mzigo wa lawama si zake!!
  hilo kwa kwanza ,la pili hivi lazima washikiri waongee kingereza!! make hapo kuna tatizo,kwenye this year Misstz show tuliona mshiriki alivyolipua watu wote waliokuwepo leaders usiku ule,alipoanza kuongea maneno yake ya kukariri,lakini akawa bubu ghafla baada
  ya kupoteza maneno,ilikuwa ni aibu kwake,kwa taifa hasa ukizingatia Miss world Darego alikuwepo!! Bakita mpo hapo!!! mbona watu wengine wanaongea kilugha na wanakuwa Miss World!!
  USHAURI Kwa kamati ya MissTz
  wajalibu kuongeza na kamati wengine kama MissTz waliopita hasa wale ambao wako outstanding kama Angela damas,K-Lynn,nancy sumari etc

 20. Matty Says:

  Jamani ili tufanilikiwe kwanza hiyo kamati ivunjike soon, kwani wapo hapo tangu 1994 i think na katika kamati yao kuwepo na wanawake wenye msimamo kama Hoyce Temu itakuwa vizuri pia warembo wapewe ajira pindi wamalizapo mashindano, kama alivyosema mchangiaji fulani hapo juu shindano linapofanyika hawa Lino wanapata hela nyingi sana je wanaonufaika nazo ni nani???jibu hapo ni wao lakini wakumbuke bila warembo hakuna hiyo minoti.
  Hivi wadau huyo Lundenga ananini na warembo???mkewe anayokazi maana huyu jamaa anapenda sana totoz ndo maana yupo hapo siku zote….hii haiingii akilini kabisa shindano la wasichana ila waandaaji ni mamen only why?????mi nadhani ni bora haya mashindano yakawa chini ya serikali sababu mrembo anawakilisha nchi na si waandaaji au si kitongoji kama alivyojaza Richa Adhia kwenye autography yake home town Kariakoo, bulshit kabisa huyu mtoto hata Tanzania haikuonekana pale nani anaijua Kariakoo ulimwenguni?? fulk off!!
  Samahani wadau kwa lugha zilizokosa tasfida ila inapain kuona kamati ya kizushi iliyojaa wadosi haina upeo wa kuona mbali tutabaki kuwa wasindikizaji tu.

 21. Kekue Says:

  Mwananchi hiyo kamati itakayoundwa kweli wawepo warembo ambao atleast waliyefanya vizuri kule ili waangalie ni nani wa kumpeleka na cha msingi zaidi kinachofanyika kule na hapa wahakikishe kinafanyika mfano mambo ya talent, vazi la ubunifu lianzie hapa hapa sio wanaenda kuyakuta kule JAMANIIIIIII.

  Alafu wao kina Lundenga cjui wanaangaliaga nini manake wangewashirikisha hawa watoto wangaliwaambia jamani huyu kule hawezi coz wao ndo wanaokuwa kule so they know each n evry thing.

 22. Matty Says:

  Halafu huyo Jason naye kwa madem achana naye, naomba pia,Nancy awekwe kwenye jopo la kamati ya miss Tanzania labda kidogo atawapa ushauri mzuri majaji ni mrembo gani anayestahili sababu ashakuwa na uzoefu.
  Msemakweli nadhani hao wanaowakataza watoto/ndugu zao bado wako 13th century, kuwa mrembo siyo uhuni la hasha mtoto anaweza akawa si miss lakini tabia haisemeki hapa.
  Pili suala la kuona warembo bomba wapo Dar no no no !!!!hilo pia liangaliwe kwa undani maana kuna wasichana wazuri toka mikoani lakini wananyimwa haki sababu tu wanatokea mikoani, jamani hii ni nchi moja hata kama mtu anatoka kusini (sorry ndugu zangu wa maeneo hayo).
  Umefika wakati tusikubali kudanganywa na hawa maanko wa Miss Tanzania, tunataka na maanti wawepo ili waweze kutetea haki za wanawake wawapo kambini na hata baada ya mashindano, Nana uko wapi leo au bado umelala??mwenzio nimeshaamka na nina hasira na hawa maanko.

 23. Lizzie Says:

  Mimi nilikuwa nafikiria kwamba pia kupata watu wenye uzoefu internal and worldwide ni muhimu sanaaa kama TAUSI LIKOKOLA,CECCY MASASI hawa watu sijawahi kuwa meet lakini wanauzoefu kwenye industry ya urembo wao kupata hiyo kazi kila mara lazima waende kwenye audition ili aweke kupata kibarua na ndio wanavohishi kwahiyo wanajua trick na challenge gani itawafanya waweze kuchaguliwa kufanya hiyo kazi na ndio aishi na kulipa bills zake.mwingine Miriam odemba she didnt do very well earlier lakini huyo Asia ambapo ndio world fashion industry ziko huko tele kwahiyo ni mzoefu sanaa tu tofauti na sisi watanzania tunavyofikiria kwasababu hakufanikiwa ile mwanzo.Kingine confidence ulimuona miss Tanzania 2007 alivyokuwa unsure alivyotajwa kucheza ngoma ya asili I could tell the had panic over her,kingine CATWALK ni muhimu sana hii aswa ndio tunahitaji watu hao dada niliyo list hapo juu uzoefu na kuwa flexible,mavazi pia tunajua mtu unatakiwa kubuni lakini inabidi wakae chini madesigner wakibongo wareview video za miss world events za nyuma wapate idea maana watu wanavaa kunguo za madesigner wakubwa wenzetu waliokuwa fani kwa zaid ya 50 years,versage,channel,vera wag na wengineee wengi ALL THE BEST hope wakichukua kila ushauri kido kidogo wa sisi wote tulioandika hapa utasaidia achana na TABIA ZENU WABONGO YAKUTOTAKA USHAURI KAZI NJEMA

 24. kay Says:

  nionavyo mimi ni kwamba ingekuwa kitu cha maana sana kama Lundenga na kamati yake ivunjwe ili iwekwe kamati mpya kwa kuzingatia vipengele muhimu ambavyo vinapaswa vifuatwe,lazima tujiulize tatizo ni nini? na nina uhakika kwamba hata kamati husika inachangia kwa hawa mamiss kufanya vibaya kuanzia kuchaguliwa kwake na baada ya kuchaguliwa sidhani kama kamati inakuwa very close na mshindi kwa kumpa kila aina ya support anayoihitaji especially emotional support. tangu mashindano haya yameanza tunasikia tu Lundeka ndio mwenyekiti wa kamati,hivyo ni wakati sasa wa Lundenga kutoa nafasi kwa watu wegine kufanya kazi ili tuone tofauti. kama mtu anashindwa kila siku ina maana kuna tatizo somewhere,Basi apewe mwingine ili ajaribu kuondoa mapugufu au uozo uliopo.

 25. Lizzie Says:

  najua nimechapia sanaa lakini simnajua boss anapita pita na mimi naogopa nisije fukuzwa kazi bure na MKOLONI

 26. Reubero Says:

  Hi every one,
  Kitu cha MSINGI hayo mashindano yasimamiwe na serikali I mean wizara husika na mambo hayo na sio mtu binafsi,otherwise watu wakwenda kushindana wapo.

 27. Jennas Says:

  Lizzy mbona wamzungumzia Tausi likokola,Watampatia wapi mtu anamipango yake mwenyewe.?
  Kuna watu wako available hapa na wataalam wa urembo na wameshapitia urembo.
  Wewe unadhani hoyce temu alilia bure huyo kabachori alivyotangazwa kuwa mshindi alijua tunaenda kuaibishwa na kutalii kule china.

  Me sikumuona hata round moja eti alipita lakini camera ilikaa vibaya atukuweza kumuona ndiyo kasema lundenga kwenye gazeti moja huo ugoro.

  Huyo kibushuti anadai mbona taifa Stars walishindwa cku zile inamaana analinganisha mpira na mambo ya ulembwende?

  Me nimekasirika aisee ningekuwa mwandishi wa habari ningemtega mtama meno ya sebuleni yamtoke mie.

  Halafu hawa madume wakamatini ukitoa uroda ndiyo unachaguliwa awaangalii kigezo wala nini shenzi kabisa
  Kwanza nasikia miss mwenyewe anamatege.

  Asanteni

 28. Jasmine Says:

  Ushauri wangu ni kama ifuatavo;
  Mabadiliko ni muhimu sana ktk hii kamati hususan suala la kujichanganya na wanawake,decision isiwe ya mtu mmoja tu katika kuchagua mrembo mwakilishi kama ambavyo ilivyo sasa (Lundenga ndio mwenye final say).
  Pia maslahi binafsi kwa warembo (top 10)nini hatma yao baada ya mashindano maana kumpa mtu laki tatu au nne hujamsaidia kitu inabidi wapatiwe careers za kudumu kuheshimu mchango wao ktk mashindano.
  Mwisho kabisa Lundenga aache jeuri na awe anakubali ushauri maana akishauriwa hususan na wananchi huwa anatoa majibu ya nyodo saana ktk vyombo vya habari(kama mlifatilia baada ya kumpata Richa kama Miss Tz alihojiwa na EATV radi, Wallah majibu yake kama unahasira ungeweza kuvunja TV) na hujiona yeye ndo anweza kila kitu hivyo hawezi kuelezwa kitu, wakati huo si ukweli, imefika muda wa yeye kupokea mawazo kutoka kwa wananchi kama changamoto kwake.
  Otherwise yakishindikana hayo yote basi jina libadilike na kuwa MISS LUNDENGA badala ya MISS TANZANIA,kwani kwa kutumia jina la Miss Tanzania tunaaibika watanzania wote pindi kunapotokea mvurundo wa aina yoyote lakini ikiwa yataitwa Miss Lundenga itakuwa ni aibu yake yeye na kamati yake ya Mafisadi wa urembo….ni hayo tu!!!

 29. Jennas Says:

  Nasema hiviiii tunaandamana Lundenga astaafu mana kama nimuda wakutumikia uongozi umeisha embu sasa ajikite kwenye filamu ama kuuza mitumba na sukari za kutoka kwao morogoro.

  Miss gani yule hana kigezo chakwenda kushindana kimataifa mfupi kama miguu ya sofa bwana

  Narudi kwa ushauri zaidi

 30. Matty Says:

  Lizzie hujatulia wewe,kwi kwi kwi!!!!!!mkoloni akikufuma unachati hapa mwambie ukweli hujafurahishwa na kamati nzima ya miss Lundenga na kama atamaindi mimi nitakuunganishia job hapa ofisini kwetu bosi hana noma kabisa.
  Nice talk Jasmine huyo lundenga kang’ang’ania hapo hataki kuondoka na mimi nataka aresign tuone mabadiliko, ukweli ni kwamba tumechoka kupelekwapelekwa tu kila siku tunashika mkia ni lini tutafika ambapo wachina wanafika???

 31. penina mwailunda Says:

  – hv huyu Lundenga kwani ataachia lini hiyo nafasi yake jamani? ametuchosha, kwanza inaonekana kuwa kazeeka, aachie ngazi bwana, inaelekea amesoma shule za zamani, yule mdada hana mvuto hata nusu,

 32. kijana Says:

  Mpakaile kitu imchukue ndo ataachia ,hivi vizee vipenda madaraka vitaisah lini nchi hii,kweli amesiama kwa nguvu kumtete Rich kuw ani Mtanzanai halali ,nyie huwaga hamuonagi aibu jamani,sio mvuto tu hafai na sio mtanzania kwa kweli ,sijui ni nini nchi hii inafanya jamniiiiiiiiiiii

 33. naomy Says:

  yaaaaaaaaan hiyo kamat ivunjwe fasta na iundwe kamat itakayofanya jambo linaloeleweka,.

 34. Mchokozi Says:

  Mimi nashauri Mama GETRUDE RWAKATARE nae aingizwe kwenye hiyo Kamati ili aweze kuwafundisha maadili hao ma Miss wanapokuwa kule Kambini.
  Nawasilisha

 35. kalili Says:

  Naona few people wanasema contestants lazima wajifunze na kuogea English!! To be honest I don’t think that is necessary. Wengi kama wachina, wajapan, spanish wakienda kwenye mashindano yeyote wanaongea lugha zao, na wanatafuta translaters ambao watawatafsiria lugha zao. At the same time wanakuwa wana advertise lugha zao. Kwa ujumla dunia ya sasa, especially kwa sisi ambao tunaishi huku, Marekani, kuongea lugha yako ni ujiko ile mbaya. Watu wana admire sana lugha ya kiswahili. Kwahiyo hata kama hawa contestants wanajua english ushauri wangu wakifika pale juu waongee kiswahili, hii pia itawaasaidia watanzania kupata kazi humo kwenye miss world, tujaribu kuwa pround na lugha yetu. Wanasema English ni lugha ya taifa, kwasababu wengi wanaongea lugha hii, na wale wanaongea lugha nyengine kama kiswahili wakiulizwa”can you speak English” hata kama hawajui wanakimbia “Yes” Kufikiri kuwa wasipoonekana kuwa hawajui english maana yake ni washamba.

  My opinion for this kamati ni kuwa wajaribu sana kudumisha lugha ya kiswahili duniani. Hata kama tukishindwa atleast lugha yetu itakuwa introduced as one of the languages in Miss World. Peace.

 36. wise Says:

  kwanza – kamati yenyewe imepitwa na wakati,nina kubali kwamba lundenga ametoamchango mkubwa sana kufufua tena mashindano hayo.

  pili – kuna tabia ambayo niya kiubinaadamu kabisa ambayo inamtokea mtu yoyte yule akiwa anamajukumu fulani kwa muda mrefu sana baadae inafikia kipindi anaanza kutoka nje ya mwelekeo na hii ni bila ya yeye kujua.watakao jua kama ana potea ni wale wanao mtizama lakini kwa yeye mwenyewe inakuwa ngumu.

  mfano wa makosa yaliyo fanyika sasa.
  kwanza – kamati ya sasa ambayo ilimchagua richa kuwa miss tanzania ili fanya makosa makubwa sana kwasababu unapo mzungumzia mtanzania unamaanisha mtu mweusi hiyo utake usitake bwana michuzi.

  ukiangalia nchi kama angola,kenya,ghana,zambia na zinginezo siwezi kuzimaliza zote,sio kama hawana wahindi au kaladi au wazungu au waarabu lakini unapo zungumzia mwakilishi una maanisha mtu anaye wakilisha majority,hauwezi kuwa mwakilishi wa nchi fulani halafu majority hawafanani na wewe(hauta weza kufanikiwa)na ndio kilicho mtokea richa na wala sio kosa lake ni kosa la kamati hiyo ambayo haiku focus suala hilo nililo liezea hapo.

  bwana michuzi sio suala la ubaguzi,najua kuna wahindi ambao ni raia wa tanzania,kuna wasomali,wazungu kule tangana ukienda kule zanzibar kuna mpaka wachina ambao ni raia wa tanzani(wako pale raha leo wana kampuni ya kutengeza tambi).vile vile bwana michuzi uraia kitu gani(siku hizi hata kwenye internet unapata uraia wa nchi yoyote ikifuatata taratibu zao)lakini ukuzungumzia mwakilishi ni lazima umtoe mtu ambae ni alama ya taifa kumbuka sisi sio marekani maana siku hizi hizi television ndizo zinazotudanganya.

  bwana michuzi richa hawezi kukuwakisha wewe kwenye miss tanzania kwasababu wewe sio muhindi ilo nitakuambia hata mpaka mwaka 2080.na ndio maana majaji kule walimpuuza kwasababu wana akili timamu.

  mfano
  mtu mweusi msichana mrembo,akafaniwa kupata uraia wa india au china,hawezi kuchaguliwa kuwakilisha mataifa hayo,kwa sababu atakuwa hawakilishi majority.utawakilishaje wachina wakati wewe mbantu.ukizungumzia alama ya nchi unazungumzia asili na sio uraia.

  bahati tuliyo poteza
  mwaka huu kama mtu mweusi angetuwakilisha kwenye miss world ile nafasi ya pili ili kuwa ya kwetu kwa sababu kitendo cha mandela kuwepo pale siku ile,ilikuwa lazima mwafrika ashike nafsi tatu za mwanzo (kwa taarifa yenu hakuna mtu yeyote yule anapenda kumwangusha mandela kwa heshima aliyo kuwa nayo duniani)na ndio maana miss angola akawa wa pili.

  mwisho
  kama nilivyosema mwanzo,ni kweli lundenga katoa mchango mkubwa kufufua tena miss tanzania.lakini binaadamu ikifanya jambo fulani kwa muda mrefu baadae unatoka nje ya mwelekeo bila kujijua.na ndio kilicho tokea kwenye uchaguzi wa miss tanzania mwaka huu.

  lakufanya
  wapewe watu wengine ambao wame yaona makosa hayo,waendeshe shughuli hizo za miss tanzania.tukijidanganya tuka waachia hao hao kina lundenga (msije mkashangaa siku moja mwakilishi wetu akawa mchina)

 37. any Says:

  ivi mko serious mashindano yaanzie ngazi za kata? kijijini watu have their issues, umaskini kila kona mara waanze kuangalia kura za maoni nani aende dar kuvaa nguo za beach, wazee watakubali au watafunua nguo kulaani,

 38. Majita Says:

  Hao wazee wakifunua nguo kama ni bibi vizee na wakajua kutembea vizuri jukwaani kisha tukawahoji wakajibu vizuri,kwa busara na tabasamu kidogo baaasi! wao ndo tutawachagua kuwakilisha miss vijiji hivyo.Siiimpo hivyo.

 39. Mwananchi Says:

  Naungana na Wise kuhusu Richa kutokuwa na sifa za kuwakilisha Tanzania, hata kama Kamati ya Lundenga wanataka tuamini tofauti.

  Nafikiri ni vema tukaiga mfano wa watani zetu wa jadi Kenya ambao kwenye Miss World Kenya wana kipengele cha Miss India Kenya.

  Huyu Richa anafaa kuwa Miss India Tanzania

 40. King Says:

  Lundenga, you can truly borrow a leaf from your conterparts in Kenya. The Miss World Kenya committee has a sub-title called MISS INDIA KENYA which is held together with Miss World Kenya.

  Richa should be re-crowned as Miss India Tanzania 2007. And who ever was the 1st Runner-up (assuming she’s not Indian) must be given her righful title of Miss Tanzania 2007.

  Thanks

 41. mweusi Says:

  nasikitika sana serikali haukuchukua hatua yoyote kuhusu uchaguzi wa richa.

  baba wa taifa
  na hakika kama baba wa taifa angekuwepo huyo bwana lundenga angekua kaminywa kimyakimya na wala watu wasingejua yuko wapi.

  hauwezi kumchagua muhindi kutuwakilisha sisi watu weusi,hii hauisiani na ubaguzi wa rangi.

  hakuna kosa kubwa la kitaifa ambalo limesha wai kutokea kama hili.na hata serikali isipo chukua hatua lakini lundenga akae akijua ametuabisha watanzania wote kiujumla.na nina jua sababu kubwa ni hao wahindi wawili ambao wako hapo kwenye kamati ndio waliocheza mchezo wote.

  hivi kweli hakuna watanzania weusi warembo wa kutuwakilisha jamani?

  tatizo msichana mtanzania mweusi hawezi kushinda mpaka atoe rushwa ya ngono.kamati yeyewe imejaa wazee wana magonjwa ya kila aina.

  ushauri
  naomba serikali isimamishe mashindano miss tanzania kusudi tukae upya(tuanzishe mjadala)ni jinsi gani tuendeshe hizi shughuli za urembo,hata kama tutakosa mashindano ya miss world kwa mwaka mmoja sio tatizo lakini tukurudi tuwe na utaratibu mzuri unao eleweka kuliko kutiana aibu.

  na namshukuru yule dada hoyce temu aliliona hilo,lakini watu wote wakamuona mjinga na mbaguzi.

 42. Nana Says:

  Kama wenzangu walivyosema kamati ivunjwe.Mnajua babahemwana Lundenga yeye anamchagua miss kutoka kichwani mwake. Hafikilii watu wengine

 43. Matty Says:

  Nana i miss u ni kweli bora ivunjwe kabisa hatuitaki.

 44. NDAKI Says:

  TANZANIA DREAM NA POPE WAKO WAPI MBONA HAPA SIWASIKII?
  AU LUNDENGA KAWAZIBA MIDOMO?

 45. Deby dada Says:

  Naungana na wote waliotoa ushauri huko juu ila napenda kuongeza kwamba lugha yetu ni ya muhimu ni bora wakatafutwa wakalimani kuliko kutumia lugha ya kigeni, nadhani wote tumeshudia Kikwete alivyoweza kupaisha lugha yetu Kiswahili ni kitamu.

  Pia ni kuhusu hiyo kamati, wanakatiba ya uendeshaji? Why hawafikilii ushiriki wa Mamiss wenyewe? Inaboa sana kuona mijidume inashughulikia mambo ya kike.

  Ushauri

  Iundwe kamati mpya au wachaguliwe viongozi wengine Lundenga jaribu kuwa mdemocrasia kunzisha kitu sio lazima uwe kiongozi unaweza ukawa chini utaheshimika tuu

  Katika kamati mpya izingatie jinsia, na uwakilishi wa mikoa japo kutoka kila kanda hii itaepusha upendeleo kama wa 2007 yule dada wa Tanga alikuwa mzuri sana ila kwasababu mlitaka mtoto wa kariakoo mkatosa.

  MCHOKOZI R U SERIOUS OR?????????

 46. mimi naona hii mambo ya miss tz imezidi longolongo mtu wangu, maana kama rushwa ya ngono ndiyo usiseme!, vimiss vinaachia mambo kwa kwenda mbele!, kina rundenga wanakula tuu.
  Mimi naona iwekewe motisha ya kipekee kama kamati ikishindwa kufikisha miss kumi bora ya miss world watoke wawekwe wengine wanaojua kazi wasiofuata ngono kwa mamiss, nadhani kwa hilo mafanikio tutapata.
  Lundenga na kamati yako acheni kuwaahidi ushindi hewa mamiss kwa ngono.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s